ZOEZI la usajili linaonekana kuupasua kichwa uongozi mpya wa
klabu ya Simba kutokana na kuwepo kwa mkanganyiko mkubwa juu na nani
asajiliwe katika kikosi hicho.
Simba tayari imewasajili mabeki Mohammed Hussein
‘Tshabalala’, Joram Mgeveke na makipa Hussein Shariff ‘Casillas’ na
Peter Manyika Junior ikiwa ni jitahada zake za mwanzo za kuboresha
kikosi hicho.
Kwa sasa viongozi wa Kamati ya Usajili ya Simba
wanahaha ndani na nje ya nchi kuangalia uwezekano wa kuongeza nyota
kadhaa katika kikosi cha timu hiyo. Ifuatayo ni orodha ya wachezaji 10
wanaoweza kuvaa jezi za Simba msimu ujao na ambao wamekuwa wakiupasua
kichwa uongozi mpya.
1. Jean-Claude Iranzi
Ni straika wa APR ya Rwanda yuko kwenye rada za
viongozi wa Kamati ya Usajili ya Simba ikiwa ni jitihada za kumwongezea
nguvu Mrundi Amissi Tambwe katika upachikaji wa mabao klabuni hapo.
Iranzi alizungumza na Mwanaspoti na kukiri kufanya mazungumzo ya awali
na uongozi wa Simba hivyo huenda tukamwona kwenye jezi ya wekundu hao
msimu ujao,ingawa bado viongozi wa juu wanabishana.
2. Paul Kiongera
Rais wa Simba, Evans Aveva katikati ya wiki
iliyopita alikwea pipa hadi nchini Kenya kwenda kufanya mazungumzo na
mshambuliaji huyo wa KCB ya nchini humo baada ya jitihada za Kamati ya
Usajili kufeli. Awali Kamati ya Usajili ya Simba ilifanya makubaliano na
Kiongera na kukubaliana kumlipa dola 15000 (Sh 24.3 milioni) kama ada
ya usajili lakini mmoja wa vigogo hao wa Simba alikurupuka na kujikuta
akipandisha dau hilo hadi dola 25000 (Sh 32.3).
Habari kutoka ndani Simba zinadai kuwa Aveva
ameshafanikiwa kumalizana na Kiongera na atatua nchini muda wowote
kuanzia leo ili kusaini mkataba na wekundu hao.
3. Pierre Kwizera
Kiungo Pierre Kwizera anayekipiga timu ya Afad
Abidjan ya Ivory Coast aliwasili nchini alfajiri ya Jumamosi iliyopita
na kufanya mazungumzo na viongozi wa Kamati ya Usajili ya Simba na
kufikia makubaliano ya awali. Baada ya kufikia makubaliano hayo Pierre
tayari amerejea nchini Ivory Coast kwenda kumalizana na klabu yake hiyo
ya awali kwaajili ya kukamilisha dili hilo la kuhamia Simba. Ujio wa
Pierre unaweza kuua dili la Iranzi kutokana na nafasi za wachezaji wa
kigeni klabuni hapo kusalia mbili pekee. Nafasi ya pili itajazwa na
Kiongera.
4. Elius Maguri
Baada ya Simba kushindwa kukamilisha dili la
usajili wa mchezaji yoyote kutoka klabu ya Mbeya City, sasa wamehamishia
rada zao kwa mpachika mabao wa Ruvu Shooting, Elius Maguri.
Mshambuliaji huyo ambaye alimaliza msimu uliopita akiwa na mabao 14
huenda akaongezwa msimbazi ili aongeze nguvu katika kikosi hicho
kilichomaliza katika nafasi ya nne msimu uliopita. Taarifa zaidi zinadai
kuwa Simba imeshamalizana na mchezaji huyo na kazi imeabaki kumalizana
n
5. Saady Kipanga
6. Edward Charles
7. Jabir Aziz ‘Stima’
8. Deus Kaseke
9. Haruna Moshi ‘Bobani’
10. Shaaban Kisiga
5. Saady Kipanga
Licha ya Klabu ya Mbeya City kugoma kuwauzia Simba
mchezaji yoyote, Kipanga bado ana mapenzi ya kutua Simba na tayari
ameshafanya makubaliano na baadhi ya viongozi wa kamati ya Usajili. Dili
la Kipanga linaonekana kuwa gumu kutokana na Mbeya City kuwa na msimamo
mkali hivyo endapo uhamisho wa Elius Maguli utafanikiwa dili la Kipanga
linaweza kuwekwa kapuni.
6. Edward Charles
BEKI ngongoti wa JKT Ruvu, Edward Charles amekuwa
kwenye rada za Simba kwa muda mrefu sana na huenda wiki hii viongozi wa
Kamati ya Usajili wa klabu hiyo ukamalizana na mchezaji huyo. Taarifa za
ndani kutoka Simba zinaeleza kuwa dili hilo limekwamishwa na wakala wa
Charles ambaye ni Mjomba wake kutaka Simba itoe Sh 25 milioni wakati
Simba wako tayari kutoka Sh 18 milioni pamoja na kulipa fidia ya mkataba
wake wa mwaka mmoja uliosalia Ruvu.
7. Jabir Aziz ‘Stima’
Taarifa za ndani kutoka Kamati ya Usajili ya Simba
zinadai kuwa kuna uwezekano kiungo wa zamani wa klabu hiyo, Jabir Aziz
‘Stima’ aliyetemwa na Azam akarejeshwa klabuni hapo. Dili la Stima
linaonekana kukwamishwa na dili jingine la Michael Mgimwa ambaye tayari
ameanza mazoezi na klabu hiyo. Awali baadhi ya viongozi wa Kamati ya
Usajili walimtaka Stima akafanye mazoezi na klabu hiyo ili kocha mkuu wa
timu hiyo Zdravko Logarusic aweze kuuona uwezo wake lakini mchezaji
huyo aligoma na kutaka kupewa mkataba kwanza.
8. Deus Kaseke
Simba bado haijakata tamaa ya kumnasa kiungo
mshambuliaji wa Mbeya City, Deus Kaseke ambaye amewekewa ugumu na klabu
yake. Kocha Logarusic aliingia matatani na uongozi wa klabu hiyo
wikiendi iliyopita baada ya kuutaka uongozi wa klabu hiyo kumsajili
Kaseke pamoja na wenzake wanne kutoka Mbeya City. Taarifa za ndani zaidi
kutoka Simba zinadai kuwa Logarusic anaukubali sana uwezo wa Kaseke.
9. Haruna Moshi ‘Bobani’
Kamati ya usajili ya Simba imekumbwa na mpasuko
mkubwa baada ya baadhi ya vigogo wa kamati hiyo kuibua upya uwezekano wa
kumrejesha kiungo wa zamani wa timu hiyo, Haruna Moshi ‘Bobani’. Awali
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe alisema
hawawezi kumrejesha Bobani kutokana na nidhamu yake mbaya lakini
inasemekana kuwa baadhi ya wajumbe wanampigia chepuo mchezaji huyo kwa
madai kuwa kiwango chake bado kinaridhisha.
10. Shaaban Kisiga
Uchovu! Kamati ya Usajili ya Simba imeonekana
kuchoka baada ya baadhi ya wajumbe wake kupendekeza kusajiliwa kwa
Kiungo Shaban Kisiga. Kiungo huyo kwa sasa ni mchezaji huru baada ya
kutemwa na Mtibwa Sugar aliyoichezea msimu uliopita. Hivyo katika majira
haya ya usajili usishangae kusikia Kisiga amesajili kuichezea Simba kwa
mara ya pili.