Wednesday, 25 June 2014

Super Eagles ya Nigeria ndiyo timu ya kwanza kutoka Afrika kufuzu kwa raundi ya pili ya kombe la dunia.


Mabingwa hao wa Afrika walifuzu kama washindi wa pili katika kundi F licha ya kushindwa mabao 3-2 na Argentina katika ya mwisho ya makundi.
Nigeria iliingia katika mechi hiyo ikifahamu fika kuwa iwapo Iran itailaza Bosnia basi wao walifaa kuilaza Argentina.
Hata hivyo Bosnia haikuchelea iliizaba Iran 3-1 na kupunguza shinikizo kwa vijana wa Stephen Keshi .Nyota wa Argentina Lionel Messi alifunga mabao mawili na kuwasaidia kuibana Nigeria.Mshambulizi huyo wa Barcelona alifunga bao la kwanza, lakini Ahmed Musa akasawazishia Nigeria chini ya sekunde 80.
Messi alifunga tena kupitia mkwaju wa adhabu na kufanya mambo kuwa 2-1 kabla ya mapumziko, lakini Musa akasawazisha tena.Marcos Rojo alifunga bao la ushindi kwa Argentina na kuifanya timu yake kumaliza kileleni mwa kundi F kwa kushinda mechi zote tatu walizocheza, huku Nigeria ikifuzu katika nafasi ya pili kwa alama 4 baada ya Iran kushindwa kunyakua alama kutoka kwa Bosnia-Hercegovina.Ilichukua dakika 3 tu kabla ya bao la kwanza kufungwa baada ya Messi kukutana na pasi yake Angel Di Maria.
Waargentina hawakuwa wamekamilisha kusherehekea kabla ya Nigeria kusawazisha.Kiungo cha kati Michel Babatunde alimmegea pasi safi Musa aliyefunga bao hilo la kusawazisha .Ilikuwa mara ya kwanza kwa historia ya Kombe la Dunia kwa timu mbili zinazochuana kufunga katika dakika tano za kwanza.
Nigeria sasa itachuana Ufaransa katika mkondo wa pili huku

NGASSA AULA AFRIKA KUSINI, FREE STATE STARS WAFIKA BEI, WAHAHA KUMNG’OA YANGA SC.


MSHAMBULIAJI wa Yanga SC, Mrisho Khlafan Ngassa amefuzu majaribio baada ya siku moja tu katika klabu ya Free State Stars ya Afrika Kusini, ambayo sasa inafanya utaratibu wa kumnunua.
Ngassa aliondoka jana asubuhi Dar es Salaam na jioni ya jana akafanya mazoezi na klabu hiyo na moja kwa moja akakubalika.
BIN ZUBEIRY inafahamu hivi sasa Free State Stars imeanza mawasiliano na uongozi wa Yanga juu kumnunua mchezaji huyo hodari.

Akizungumza kutoka Afrika Kusini leo, Ngassa amesema; “Nilidhani yatakuwa majaribio ya muda mrefu, lakini nimefika tu baada ya kufanya nao mazoezi mara moja, wakasema wewe si wa kujaribiwa, umekuja hapa kusajiliwa,”amesema Ngassa.
Ngassa alikwenda mwenyewe Afrika Kusini kwa gharama zake baada ya kuambiwa klabu hiyo inatafuta winga.
“Kuna rafiki yangu aliniambia hii timu inatafuta winga, akaniambia ananiunganishia mpango wa kwenda majaribio na nijiamini nitafuzu, nikakubali nimekuja na mambo safi,”alisema.
Ngassa amesema kwamba kwa sasa Free State wanawasiliana na Yanga SC juu ya mpango wa kumhamishia huko. “Naipenda sana Yanga, nimecheza pale kwa moyo wangu wote, lakini naomba tu wawe wepesi kuniruhusu kuja kujiendeleza huku,”amesema.
Free State imetuma barua Yanga SC kutoa ofa ya bei wanayotaka kumnunua Ngassa na sasa inasubiri majibu kwa ajili ya hatua zaidi.
Ngassa ameshindwa kwenda na timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kambini Botswana kwa ajili ya mpango huo wa kuhamia Afrika Kusini.
Stars imeondoka alfajiri ya leo kwa ndege ya shirika la Afrika Kusini kwenda Gaborone, Botswana ambapo kitapiga kambi ya wiki mbili.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imeweka kambi hiyo chini ya Kocha Mart Nooij ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi yake ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika (AFCON) dhidi ya Msumbiji (Mambas) itakayochezwa Julai 20 mwaka huu Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mechi hiyo itachezeshwa na waamuzi kutoka Misri wakiongozwa na Mahmoud Ashor wakati Kamishna atakuwa Felix Tangawarima kutoka Zimbabwe.

Sekretarieti ya Ajira Yazipa Rungu Serikali za Mitaa.


Serikali za mitaa zitaruhusiwa kuanza kuajiri watumishi wa baadhi ya kada za chini katika mwaka wa fedha wa 2014/2015.Akihojiwa katika Maonyesho ya Wiki yaUtumishi wa Umma kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam, Msemaji wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa
Umma, Riziki Abraham, alithibitisha kuwa Sekretarieti hiyo itakasimu sehemu ya madaraka yake ya kuendesha mchakato wajira serikalini kwa serikali za mitaa.
"Sekretarieti ya Ajira imeandaa mpango wa kukasimisha madaraka yake ya kuendesha mchakato wa ajira serikalini kwa baadhi ya kada za chini (operation staff) kwenye mamlaka za Serikali za Mitaa na mchakato huo utaanza mwaka wa fedha 2014/15" alisema.Pia, alisema katika kila nafasi ya kazi inayotangazwa kwa hiyo haizingatii GPA (kiwango cha ufaulu kwa masomo yote ). Alieleza kuwa zipokada, ambazo GPA inazingatiwa ;na zipo
kada ambazo kinachoangaliwa ni ufaulu tu wa kawaida na sifa zilizoainishwa."Zipo baadhi ya kada ambazo masharti yake ni pamoja na kuwa na GPA ya kiwangofulani. Kada ambazo ni lazima GPA kuangaliwa ni kama vile kada za wakufunzi wa vyuo mbalimbali. Kazi nyingine hazina
masharti ya GPA, kinachoangaliwa ni ufaulu tu na sifa zilizoainishwa katika tangazo la nafasi za kazi kulingana na kada husika",alisema Riziki.Alitaja moja ya matatizo wanayopata waombaji wa kazi kuwa ni kupotelewa na vyeti vya kitaaluma. Alisema waombaji wa kazi ambao wamepata tatizo hilo, wanachopaswa kufanya ni kuripoti kwenye mamlaka husika, alikokuwa amepata cheti hicho ili apewe mwongozo wa kufanya na kutangaza kupotelewa kwa cheti au vyeti kwenye chombo cha habari (gazeti)."Ikithibitika hivyo mamlaka husika kwa mfano Baraza la Mitihani wana utaratibu wa kuwasiliana na Sekretarieti ya Ajira kwa kutoa majina ya watu waliopoteza vyeti nahatimaye huruhusiwa kufanya usaili"
alisema.

MWIGULU NCHEMBA BLOG: VIDEO:N/WAZIRI FEDHA MH:MWIGULU NCHEMBA AKIHITIMIS...

MWIGULU NCHEMBA BLOG: VIDEO:N/WAZIRI FEDHA MH:MWIGULU NCHEMBA AKIHITIMIS...

Italia nje ya kombe la dunia

Uruguay ilifunga bao la ushindi katika dakika za mwisho na kuwabandua washindi mara nne wa kombe la dunia Italia .
Hata hivyo habari kuu kutoka katika mechi hii ilikuwa ni kashfa nyingine ya tukio la Luiz Suarez ‘kung’ata’
Uruguay sasa itacheza dhidi ya Colombia au Ivory Coast jijini Maracana siku ya Jumamosi katika raundi ya pili ya Kombe la Dunia, lakini utata unatarajiwa kuibuka kabla ya siku hiyo.
Italia walitoka uwanjani wakiwa na ghadhabu kutokana na waliyoshuhudia kabla yao kuondolewa katika kombe la Dunia la pili bila kupita kutoka mechi za makundi- kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 1966.
Kocha wa Italia Cesare Prendelli alisema kabla ya mchezo kuwa ilikuwa “mechi muhimu sana katika taaluma yake kandanda” na baada ya kushindwa akapendekeza kujiuzulu.
Mechi hii ilikuwa na hamaki na hasira ndani na nje ya uwanja.
Baloteli hakuvuma katika mechi hii

Mara kwa mara wasaididizi wa refari walilazimika kuzuia zogo kati ya timu hizo mbili, kipenga cha refarii kikatiza mchezo mara nyingi na wachezaji wakachukua muda mrefu wakisukumana walipokuwa wakikimbia na mpira miguuni.
Italia ilikuwa ikihitaji sare tu ili kufuzu. Katika mfumo wa 3-5-2, Italia walikosa mshikamano, mbio na walihatarisha lango lao kila wakati. Lakini iwapo mfumo wao ulitekelezwa ili kuzuia ushambulizi wa Uruguay, mfumo huo ulisaidia.
Andrea Pirlo alimlazimu mlindalango wa Uruguay Fernando Muslera kuondoa mkwaju wake uliotokana na mpira wa adhabu na kuugongesha mlingoti, huku mshambulizi Ciro Immobile akipiga mkwaju nje ya lango.
Edinson Cavani alitaka kuzawadiwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 50 baada ya kuangushwa na Andrea Barzagli, lakini refarii akapuuzilia mbali.
Refarii huyo raiya wa Mexico hata hivyo angebadili mchezo muda mfupi baadae wakati alipomwonyesha Marchisio kadi nyekundu baada ya kiungo huyo wa kati wa Juventus kumchezea vibaya Arevalo katikati mwa uwanja.
Marchisio alinyanyua mguu na kumgonga kiungo huyo wa Uruguay gotini.
Chiellini akimwonesha refarii alikongatwa na Suarez

Suarez alikaribia kufunga bao alipopiga mkwaju wa chini kwa chini ambao Buffon aliudaka .
Utata zaidi ulizuka wakati Suarez na Chiellini walipokumbana katika maeneo ya penalti zikiwa zimesalia dakika tisa kwa mechi kukamilika.
Beki huyo wa Italia alilalamika wakati huo huo kwa refarii kwamba alikuwa ameng’atwa na akajaribu kumwonyesha alama.
Wakati wachezaji wa Italia walipokuwa wakiendelea kulalamika, Uruguay wakapata kona.
Suarez alipiga pasi nzuri naye Godin akafunga bao hilo la ushindi.
Itali walijaribu kila wawezalo ili kupata bao, hadi mlindalango Buffon kujaribu kutafuta bao kutokana na kona waliyopata waitaliano dakika za mwisho, lakini upande wake Oscar Tabarez ukawadhibiti.
Hata hivyo huenda mechi hii isikumbukwe sana. Macho yote, kwa mara nyingine yatamwelekea Suarez.

Tuesday, 17 June 2014

dj sek: NAFASI ZA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO ZATANGAZWA MUDA...

dj sek: NAFASI ZA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO ZATANGAZWA MUDA...:           Nafasi za kujiunga na kidato cha nne mwaka 2014  kwa wanafunzi waliomaliza mwaka jana zimetangazwa rasmi muda huu jijini d...