Pages - Menu

Pages

Wednesday, 14 August 2013

SAKATA LA AZAM TV VS YANGA



SAKATA LA AZAM TV VS YANGA: SERIKALI YAAMUA YANGA NA KAMATI YA LIGI KUPITIA UPYA MKATABA - AZAM MEDIA NA YANGA KUFANYA MKUTANO WA KUJADILI MASLAHI YA WANA JANGWANI

Hatimaye mkutano ulioitishwa na serikali kupitia wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo kusuluhisha mgogoro wamkataba wa mauzo ya haki za matangazo ya Television uliowashirikisha kamati ya ligi kuu ya soka Tanzania bara, klabu ya Yanga na Azam Media umemalizika hivi punde huku maamuzi kadhaa yakifikiwa.

Kwa mujibu wa chanzo cha habaricha mtandao huu, klabu ya Yanga imeibuka kidedea kwenye madai yake ya kupinga utaratibu mzima wa mkataba huo baina ya kamati ya ligi naAzamMedia.

Hii inakuja baada maamuzi yamkutano huo kuamuru kwambavipengele vya mkataba huokupitiwa upya na klabu ya Yanga na Kamati ya Ligi na vile ambavyo vitaonekana kuwa na matatizo virekebishwe.

Pia imeamuliwa kwamba Yanga SC itakaa kikao na Azam Media kuzungumzia mambo mbalimbali ambayo Yanga imeonekana kuwa na shaka nayo kuhusu

Azampamoja na maslahi ya Yanga kupitia dili hilo la ununuaji wa haki za matangazo ya TV ya mechi za ligiuliofanywa na Azam Media.

No comments:

Post a Comment