Pages - Menu

Pages

Sunday, 11 August 2013

Kozi ya makamishna, waamuzi leo


Kozi ya makamishna, waamuzi leo


SEMINA kwa ajili ya makamishna wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), na Ligi Daraja la Kwanza (FDL), pamoja na mtihani wa utimamu wa mwili kwa waamuzi wote wa daraja la kwanza (Class I), wanaotaka kuchezesha VPL msimu wa 2013/2014 inatarajiwa kuanza katika vituo vya Dar es Salaam na Mwanza, leo.
Boniface Wambura ambaye ni Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), alisema jana kwamba mafunzo hayo yatakayomalizika Agosti 14 mwaka huu, yatakuwa chini ya wakufunzi Leslie Liunda, Joan Minja na Riziki Majala kwa kituo cha Dar es Salaam, wakati Mwanza watakuwepo Alfred Rwiza na Omari Kasinde.
Wambura alisema kwa Dar es Salaam mafunzo hayo yatafanyika Uwanja wa Taifa wakati Mwanza yatakuwa CCM Kirumba.
Alibainisha kuwa Mwanza kutakuwa na makamishna na waamuzi kutoka mikoa ya Geita, Kagera, Katavi, Kigoma, Manyara, Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Singida na Tabora huku Dar es Salaam ikihusisha mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Kilimanjaro, Lindi, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Njombe, Pwani, Ruvuma na Tanga.
Aliongeza kuwa washiriki wote wanatakiwa kufuata utaratibu huo wa vituo walivyopangiwa na si vinginevyo.

No comments:

Post a Comment