Monday, 14 April 2014

MAPYA YAIBUKA NDEGE ILIYOPOTEA, RUBANI ALIPIGA SIMU ANGANI.

Rubani msaidizi wa ndege iliyopotea namba MH370 alipiga simu yake ya mkononi wakati ndege ikiruka chini chini kupita pwani ya magharibi mwa Malaysia.

Wachunguzi wamegundua kwamba simu hiyo ilipigwa kutoka kwenye simu ya mkononi ya Fariq Abdul Hamid wakati Boeing 777 ikiruka chini chini karibu na kisiwa cha Penang, kaskazini mwa pwani ya magharibi ya Malaysia.
Gazeti la The New Straits Times limeripoti leo kwamba ilifahamika ndege hiyo, ilikiwa na watu 239 ndani yake, ilikuwa ikiruka chini chini kiasi cha minara ya mawasiliano iliyokuwa karibu kuweza kunasa ishara za Fariq.
Simu hiyo ilikatika ghafla, hata hivyo imefahamika kwamba mawasiliano yalirushwa na kituo kidogo cha mawasiliano kilichopo kwenye jimbo la Penang.
Gazeti hilo lilisemwa kwamba haikuweza kujulikana mara moja Fariq alikuwa akimpigia nani 'kutokana na chanzo cha habari kutotaka kuweka bayana taarifa zaidi za uchunguzi.'

Liliongeza: "Mnara wa kampuni ya mawasiliano ulinasa simu hiyo aliyokuwa akijaribu kupiga.
"Kuhusu kwanini simu hiyo ilikatika, inawezekana sababu ndege hiyo ilikuwa ikienda kwa kasi mbali na mnara huo na haikuweza kupata mawasiliano kwenye mnara unaofuatia," gazeti hilo lilisema, likinukuu vyanzo vya habari.
Gazeti hilo liliongeza kwamba imebainika pia kwamba mawasiliano ya mwisho ya Fariq yalikuwa kupitia WhatsApp na kwamba yalifanyika majira ya Saa 5:30 usiku wa Machi 7, muda mfupi kabla hajapanda ndege hiyo kuanza safari ya masaa sita kwenda Beijing, China.
The New Straits Times lilisema lilielezwa kwamba ukaguzi wa kumbukumbu kwenye simu ya Fariq ulionesha kwamba mtu wa mwisho kabisa kuongea naye ilikuwa 'mtu wake wa kawaida (namba iliyokuwa ikijirudia rudia katika orodha ya simu zake alizopiga).'
Simu hiyo ya mwisho, lilisema gazeti hilo, ilipigwa sio zaidi ya masaa mawili kabla ya ndege hiyo kuruka saa 6:41 usiku wa Machi8 kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kuala Lumpur.
Vyanzo tofauti vililieleza gazeti hilo kwamba ukaguzi kwenye simu ya Fariq ulionesha kwamba mahusiano na simu hiyo aliyopiga simu hiyo ya mwisho kabla ya kupanda ndege hiyo yalikuwa 'adilifu'.
"Hii ni matokeo ya kawaida kwa simu hiyo kuwa imezimwa.
"Wakati fulani, hatahivyo, wakati ndege hiyo ikiwa angani, kati ya Igari na eneo hilo karibu na Penang (muda mfupi kabla ya ndege hiyo kupotea kwenye rada), laini hiyo 'iliunganishwa tena'."
Gazeti hilo lilisema kwamba uunganishwaji haumaanishi kwamba lazima simu hiyo kwamba ilipigwa. Inawezekana pia ni matokeo ya simu hiyo kuwa imewashwa tena.
Jana ilionekana kama kisanduku cheusi kinaweza kuwa kimepatikana chini katika Bahari ya Hindi.
Kituo cha redio cha 6PR kilituma ujumbe katika twitter ugunduzi huo, kikimnukuu mtaalamu wa anga Geoffrey Thomas, ambaye alibainisha kinasa taarifa hicho cha ndege hiyo hatimaye kimepatikana zaidi ya mwezi mmoja baada ya Boeing 777 kupotea.
Waziri Mkuu wa Australia Tony Abbott, ambaye yuko nchini China, alisema watafutaji wana 'uhakika' ishara hizo zilizopatikana zilikuwa kutoka kwenye kisanduku cheusi kutoka kwenye ndege ya MH370.
"Hakika sitaki kusema taarifa zaidi ya hapo kwa wakati huu... kama ishara ya heshima kwa watu wa China na familia zao."

No comments:

Post a Comment