Thursday, 27 March 2014

AHSANTE BENCHI LA UFUNDI LA YANGA MNANIFANYA NIJISIKIE FAHARI HUKU MTAANI!

Ni kazi ngumu sana kuwafundisha mastaa wa bongo wachezaji hawa hujaa viburi na majivuno. . Wengi hawajitumi mazoezini , mara kadhaa huondoka kambini kwa sababu kibao hawahofu kitu wanajua tu wana namba kikosini hata kocha akibana basi viongozi watampanga tu au hata wapenzi wa klabu hiyo watapiiga makelele kulazimisha mchezaji husika apangwe. . Vimeshuhudiwa vitendo vingi vya utovu wa nidhamu mchezaji anaenda kwao akifika huko hapokei simu ya kiongozi au kubadilisha line kabisa! ! Kiongozi hajui mchezaji anarudi lini mashabiki/waandishi wakiuliza kiongozi hujibu "nimempigia sana simu lakini haikupokelewa ni siku ya 3 sasa tumsubiri tu atarudi" na isitoshe timu inakuwa mashindanoni..
Ernie Brandts alishindwa kabisa kudhibiti vitendo vya nidhamu kwa wachezaji wetu mbali na hivyo hata upendo baina yao wengiwao haukuwepo ikapelekea wachezaji kibao kushuka viwango vyao. .nna uhakika Hussein Njavu wa Ernie Brandts angetemwa msimu ujao alishapotea tayari, Said Bahanuzi, Jeryson Tegete, saleh Dilunga , Oscar Joshua , Juma Abdul na hata Simon Msuva hawa wangepotea mnamkumbuka Nadir Haroub alivochuja? Wengi tukipendekeza atemwe na Brandts akatusikia alikuwa na mawazo kama yetu Canavaro akaanza kupigwa benchi kulia akicheza Juma Abdul, kati Twite na Yondani kushoto Luhende. .
Tulijaza vipaji vingi katika timu yetu lakini hakuwepo kiongozi mzuri wa kuviunganisha matokeo yake timu ikawa inapata hasara tu. . Wachezaji wanaongoza 3 - 0 wanaona wamemaliza kazi wanatuliza mpira kwa makalio kisa washangiliwe matokeo yake kipindi cha pili zinarudi na almanusura tupigwe la 4! Wanatoka uwanjani kesho wamesahau ukiwauliza wanakwambia mpira unadunda mpira ni dakika 90. . Mashabiki tunaumia sana nakumbuka ile siku niliumia kuzidi!
Viongozi wakakaa chini na kulifumua benchi zima la ufundi, wakaorodhesha sifa za kocha atakayetufaa wakagundua lazima awe ameanda umri yaani awe mzee wachezaji wasipate muda wa kushindana naye bali wamuogope kama babu yao au baba yao. . Awe na busara za kiutu uzima! Ndipo tukamuajiri Hans van pluijm kisha wakampa nguvu ya maamuzi kocha pamoja na ukurugenzi wa benchi la ufundi Kisha msaidizi akawa Mkwasa kocha mzawa mwenye elimu ya ukocha na uzoefu na soka la Tanzania! Sasa Yanga ni mshike mshike hakuna wachezaji wenye uhakika na namba! Frank Domayo kampoteza chuji hadi kwenye benchi hayupo, Juma Abdul anaitendea haki namba ya Twite ajirekebishe kukaba, morali na kurusha mipira tu, Niyonzima mchezaji aliyekuwa tegemeo kaumwa alivopona yupo fit lakini Hassan Dilunga anataka kucheza picha la Domayo kwa chuji, Oscar Joshua ashampeleka benchi Luhende, Hussein Javu ambaye hata benchi hakuwepo sasa hivi ashampeleka mtu benchi, Tegete kapewa hiyo nafasi jana mpira ukamkataa Javu akaingia akilini akijua hii timu sasa ni mshike mshike! Kiiza, kavumbagu hatarini. . Jana tunaongoza goli 3 lakini kocha wetu Babu hakutulia kwenye benchi Dakika zote hakuonekana kuridhishwa na idadi hiyo aliwahamasisha wachezaji wetu kusaka ushindi zaidi! Nidhamu imekuwa juu, viwango vya wachezaji vimekua sasa timu inacheza!
AHSANTE BENCHI LA UFUNDI MNANIFANYA NIJISIKIE FAHARI HUKU MTAANI!
ASUBUHI NJEMA MWANAJANGWANI
 wachezaji hawa hujaa viburi na majivuno. . Wengi hawajitumi mazoezini , mara kadhaa huondoka kambini kwa sababu kibao hawahofu kitu wanajua tu wana namba kikosini hata kocha akibana basi viongozi watampanga tu au hata wapenzi wa klabu hiyo watapiiga makelele kulazimisha mchezaji husika apangwe. . Vimeshuhudiwa vitendo vingi vya utovu wa nidhamu mchezaji anaenda kwao akifika huko hapokei simu ya kiongozi au kubadilisha line kabisa! ! Kiongozi hajui mchezaji anarudi lini mashabiki/waandishi wakiuliza kiongozi hujibu "nimempigia sana simu lakini haikupokelewa ni siku ya 3 sasa tumsubiri tu atarudi" na isitoshe timu inakuwa mashindanoni..
Ernie Brandts alishindwa kabisa kudhibiti vitendo vya nidhamu kwa wachezaji wetu mbali na hivyo hata upendo baina yao wengiwao haukuwepo ikapelekea wachezaji kibao kushuka viwango vyao. .nna uhakika Hussein Njavu wa Ernie Brandts angetemwa msimu ujao alishapotea tayari, Said Bahanuzi, Jeryson Tegete, saleh Dilunga , Oscar Joshua , Juma Abdul na hata Simon Msuva hawa wangepotea mnamkumbuka Nadir Haroub alivochuja? Wengi tukipendekeza atemwe na Brandts akatusikia alikuwa na mawazo kama yetu Canavaro akaanza kupigwa benchi kulia akicheza Juma Abdul, kati Twite na Yondani kushoto Luhende. .
Tulijaza vipaji vingi katika timu yetu lakini hakuwepo kiongozi mzuri wa kuviunganisha matokeo yake timu ikawa inapata hasara tu. . Wachezaji wanaongoza 3 - 0 wanaona wamemaliza kazi wanatuliza mpira kwa makalio kisa washangiliwe matokeo yake kipindi cha pili zinarudi na almanusura tupigwe la 4! Wanatoka uwanjani kesho wamesahau ukiwauliza wanakwambia mpira unadunda mpira ni dakika 90. . Mashabiki tunaumia sana nakumbuka ile siku niliumia kuzidi!
Viongozi wakakaa chini na kulifumua benchi zima la ufundi, wakaorodhesha sifa za kocha atakayetufaa wakagundua lazima awe ameanda umri yaani awe mzee wachezaji wasipate muda wa kushindana naye bali wamuogope kama babu yao au baba yao. . Awe na busara za kiutu uzima! Ndipo tukamuajiri Hans van pluijm kisha wakampa nguvu ya maamuzi kocha pamoja na ukurugenzi wa benchi la ufundi Kisha msaidizi akawa Mkwasa kocha mzawa mwenye elimu ya ukocha na uzoefu na soka la Tanzania! Sasa Yanga ni mshike mshike hakuna wachezaji wenye uhakika na namba! Frank Domayo kampoteza chuji hadi kwenye benchi hayupo, Juma Abdul anaitendea haki namba ya Twite ajirekebishe kukaba, morali na kurusha mipira tu, Niyonzima mchezaji aliyekuwa tegemeo kaumwa alivopona yupo fit lakini Hassan Dilunga anataka kucheza picha la Domayo kwa chuji, Oscar Joshua ashampeleka benchi Luhende, Hussein Javu ambaye hata benchi hakuwepo sasa hivi ashampeleka mtu benchi, Tegete kapewa hiyo nafasi jana mpira ukamkataa Javu akaingia akilini akijua hii timu sasa ni mshike mshike! Kiiza, kavumbagu hatarini. . Jana tunaongoza goli 3 lakini kocha wetu Babu hakutulia kwenye benchi Dakika zote hakuonekana kuridhishwa na idadi hiyo aliwahamasisha wachezaji wetu kusaka ushindi zaidi! Nidhamu imekuwa juu, viwango vya wachezaji vimekua sasa timu inacheza!
AHSANTE BENCHI LA UFUNDI MNANIFANYA NIJISIKIE FAHARI HUKU MTAANI!
ASUBUHI NJEMA MWANAJANGWANI

No comments:

Post a Comment