MECHI ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya
Yanga na Al Ahly kutoka Misri iliyochezwa
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni
mwa wiki imeingiza sh. 448,414,000.
Mapato hayo yametokana na watazamaji
50,202 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa viingilio vya sh. 7,000, sh. 13,000, sh.
25,000 na sh. 35,000. Yanga ilishinda mechi
hiyo kwa bao 1-0.
Mgawo wa mapato hayo ulikuwa kama
ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)
ni sh. 68,402,135.59, gharama za kuchapa tiketi ni sh. 10,343,219, waamuzi na kamishna
sh. 14,665,930 na matangazo sh. 15,679,000. Uwanja sh. 50,898,557.31, gharama za
mchezo sh. 33,932,371.54, Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF)/Shirikisho la Mpira
wa Miguu Afrika (CAF) sh. 33,932,371.54
wakati Yanga ilipata mgawo wa sh.220,560,415.01.
No comments:
Post a Comment