Friday, 28 March 2014

SIKIA HII YA RASIM YA KATIBA MPYA TANZANIA

Lesson moja kubwa sana kwa WaTanzania ni kwamba tusiwe watu wa ku-react after the fact bse mara chache sana husaidia, hasa kwa michakato inayohusu Sheria. Muda wa kuamka ndiyo huu; tuwe na tabia ya kufuatilia mambo, hasa contemporary issues.
Kinachotokea kuhusu mchakato wa Katiba Mpya ni matokeo ya Sheria dhaifu, zinazotungwa kwa haraka haraka bila nia thabiti na maandalizi ya kutosha; na ambazo punde tena zinapindishwa ku-accomodate malengo Fulani.
Wakati kina Lissu wanapambana na Sheria ya Marekebisho ya Katiba, most of us tulimuona kama mtu m-bishi m-bishi tu wa Chadema. Hatukuelewa kwamba maandalizi ya kinachotokea leo yalianza wakati wa kutunga Sheria ile. Kama tungekuwa vigilant tungepinga, kwa mfano Sheria kubadilishwa ili kuwazuia wajumbe wa Tume ya Katiba kuwa wajumbe wa Bunge; kilichofuata ni Judge Warioba kutangulizwa, kisha Rasimu karibu yote (ikiwemo ukomo wa Uongozi, Rais kupunguziwa Madaraka, Haki za Binadamu) kubomolewa kwa mifano ambayo inayotakiwa kujadiliwa kwa umakini. Kwa mfano; Boris Yeltsin hakupanda katika kifaru sababu wanajeshi hawakulipwa mishahara, au kulikuwa na ugomvi kati ya Serikali Kuu ya USSR na Serikali Shirikishi zilizozaliwa kama za Russia. Yeltsin alipanda katika kifaru ili kuungana na wanajeshi wa Serikali Kuu ya USSR waliokuwa wakipinga jaribio la kumpindua Mikhail Gorbachev, Rais wa Shirikisho la USSR kutoka kwa wahafidhina waliopinga mabadiliko ya Sera ya Perestroika yaliyounda, pamoja na mambo mengine mengi ya Kidemokrasia, Serikali kadhaa shirikishi, katika USSR kama vile Russia na Ukraine na Estonia na Belarus. Tena huu ndiyo mfano mzuri kabisa wa namna Jeshi linavyoweza kulinda Katiba ya Nchi bila kujali chochote.
USSR ilibomoka sababu ilijengwa katika muungano wa kimaficho na wa lazima (ingawa leo hii kila siku Belarus na visehemu kadhaa katika nchi nyingine kama Crimea Abkhazia zinabembeleza kujiunga Russia), kama ilivyokuwa kwa Somalia na Somaliland na Puntland au Ethiopia na Eritrea au Czech Republic na Slovakia au Serbia, Croatia, Montenegro, Slovenia, Bosnia+ Herzegovina hatimaye Kosovo.
Comoro iliathiriwa sana na mapinduzi ya mara kwa mara ya Mfaransa Bob Denard kwa maslahi yake, na ya France; mpaka pale France ilipoamua enough is enough, na kumfunga jela. Makovu yale ndiyo yaliyoendelea kuyumbisha Comoro, kiasi kwamba Visiwa Shirikishi vilikuwa vinasumbua mara kwa mara. Mapinduzi yaliyotulizwa na majeshi ya nje yamewahi tokea hata katika nchi zisizo na muungano kama Congo Brazaville na Mali.
Nchi kama Switzerland inaundwa na confederations ya Cantons, na Rais huchaguliwa kila mwaka mmoja toka Cantons hizo, labda aliyepo apendwe na kuendelea mwaka mwingine au zaidi; na kuna madaraka ya Cantons, na ya Serikali Kuu. South Africa kuna Mawaziri Wakuu wa Majimbo, na wana nguvu hasa tu; na bado Rais wa nchi ndo Supreme. Cha msingi ni Katiba imara. UK; Baadhi ya Waskochi na Wa-Irish Kaskazini na wa-Welsh wanawachukia Wa-English mno; but Katiba ndo inawabana, pamoja na kwamba wana mabunge yao na madaraka Fulani, the bucks stops in London Kwa Serikali ya Shirikisho. Wapo wanaopinga Utawala wa Kifalme, lakini kila mwaka wanawasilisha mamilioni ya Pauni kwake bse misingi ya Katiba ni imara. Quebec na Canada hata lugha ni tofauti, but Muungano wao uko katika misingi ya Katiba imara na unadunda ingawa kila mara Quebec wanajaribu kujitoa, wanashindwa katika Kura ya Maoni; Katiba inasema lazima kujitoa kuungwe mkono na asilimia kadhaa. Germany; kila Jimbo lina Waziri Mkuu very powerful, na ni kama nchi tu, lakini Serikali Kuu ya Muungano ndo kila kitu. Nigeria pia kuna Majimbo yenye hadhi na tabia kama za nchi, na yana rasilimali kama mafuta, na Governors ni very powerful; lakini pamoja na matatizo kadhaa (ambayo hayajasababishwa na muundo wa Muungano, bali na hulka za watawala), Muungano unadumu. Kina Biafra walipojaribu kujitenga, hata wanajeshi baadhi toka huko huko Biafra walimpinga Gen. Ojukwu.
Kuweka, kwa mfano, kwamba Elimu ni haki ya kila Mtanzania haimfanyi mtu kuwa na haki ya kwenda Mahakamani kudai laptops au lunch shuleni, kama ambavyo haki ya kumiliki mali katika Katiba ya sasa haimfanyi mtu kuwa na haki ya kudai apewe ardhi ya kijiji isiyotumika. Kinacholindwa ni kutonyimwa Elimu wakati Serikali ina uwezo, au kubaguliwa katika haki hiyo.
Kuwa wa Kwanza kuweka term limits katika Ubunge siyo tatizo, tunaangalia mahitaji yetu ni yapi na kwa nini wananchi walitaka hayo; mbona tulikuwa moja ya watu wa kwanza Duniani kukataa kuweka vipengele vya Haki za Binadamu katika Katiba yetu mpaka 1984 ili kusaidia programmes za ajabu kama Africanization, then miaka michache baadae tunaajiri consultants kibao wazungu nk. Recalls ni utaratibu wa kawaida tu wa Kikatiba kama watu wanaona mapungufu katika utendaji wa Mbunge wao. Cha msingi ni kuweka vipengele vinavyodhibiti haki ya Recall;mfano, unaweka angalizo kwamba Mbunge au Muwakilishi akiwa mgonjwa au akiwa Rumande kabla ya Hatia hakuna recall mpaka upite muda Fulani. Na pia Recall siyo automatic, lazima kuwe na threshold Fulani ya kisheria, mfano 51% ya wapiga kura wa Jimbo.
Katiba lazima ianishe wazi kwamba Mahakama za Nchi husika zina mipaka Fulani, na Mahakama za Rufaa na Supreme Court zina un-limited powers kuhusu masuala Fulani. Siyo mambo ya sasa ya Zanzibar kubadilisha Katiba yao na kusema mashauri ya haki za binadamu au Katiba yatasikilizwa na Majaji watatu wa Mahakama ya Zanzibar na uamuzi wao ndiyo wa Mwisho; tayari unaua maana ya Mahakama ya Rufani ya Tanzania.
Rasimu haina tatizo, tatizo lililopo ni uoga wa mabadiliko kama waliokuwa nao wale wahafidhina waliotaka kumpindua Gorbachev.
Haya; tusisahau pia kwamba Kura ya Maoni itaendeshwa na Tume Ya Taifa ya Uchaguzi, na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Zanzibar; kwa kutumia madftari yale yale ya wapiga Kura. Sasa kama hatukujiandikisha, ni tatizo kubwa. Na uboreshaji kabla ya Kura ya maoni ni ndoto, hasa ukizingatia maslahi yanayoonekana sasa. Na tunaziamini kiasi gani Tume hizi zinazolalamikiwa kila mara? Of course swali litakuja kwamba ni nani sasa asimamie Kura ya Maoni; Sheria ingeweza tu kuunda chombo HURU kisicho na doa kama walivyofanya Kenya.

Na Peter Kibatala

No comments:

Post a Comment