Wednesday 16 July 2014

VAN GAAL AWASILI MAN UNITED KWA NDEGE BINAFSI TAYARI KUANZA KAZI OLD TRAFFORD



 KOCHA Louis van Gaal ametua mjini Manchester tayari kuanza kazi katika ofisi mpya, Old Trafford.
Mwalimu huyo wa Manchester United alitua kwa ndege binafsi Jijini humo majira ya Saa 2.40 leo asubuhi na moja kwa moja kupelekwa makao makuu ya klabu, Carrington.
Atasalamiana na wakuu mbalimbali wa klabu hiyo kabla ya kuzungushwa kwenye Uwanja wa mazoezi na kisha kutambulishwa kwa wachezaji.

 Atapata fursa ya kuanza kujenga uhusiano na wachezaji baada ya kuongoza mazoezi kidogo kwa mara ya kwanza na
United inatarajiwa kumtambulisha rasmi kwa umma kesho katika Mkutanno na Waandishi wa Habari.
Mara baada ya kutambulishwa kocha huyo mwenye umri wa miaka 62 atapaa tena na kikosi chake kwenda ziara ya Marekani ambako watacheza mechi nne.
Kocha huyo wa zamani wa Bayern Munich anaamini hana sababu ya kupumzika kwa sasa baada ya kuiongoza kwa mara ya mwisho Uholanzi katika Kombe la Dunia, zaidi ya kuanza kazi kwa mwajiri mpya.
Uholanzi ilimaliza katika nafasi ya tatu kwenye Kombe la Dunia baada ya kuwafunga wenyeji, Brazil mabao 3-0 wakitoka kutolewa kwa penalti na Argentina katika Nusu Fainali.

 La Galaxy, Roma, Real Madrid na Inter Milan ndiyo timu ambazo zitamenyana na United na kumpa Mholanzi huyo fursa ya kukitathmini kikosi chake kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya England baada ya msimu mbaya uliopita chini ya kocha aliyemtangulia, David Moyes.
Van Gaal anatarajiwa kuchukua maamuzi zaidi ya kikosi hicho, pamoja na kuwakaribisha wachezaji wapy, Ander Herrera na Luke Shaw.
Chris Smalling, Tom Cleverley, Javier Hernandez, Shinji Kagawa, Darren Fletcher, na Ashley Young wote watasubiri kujua hatima yao kama watabaki Old Trafford. Robin van Persie yupo kwenye likizo ya wiki tatu baada ya Kombe la Dunia

No comments:

Post a Comment