Wednesday 30 October 2013

Kikao cha Baraza la Madiwani la Hamshauri ya Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza leo kimetawaliwa na vurugu

Kikao cha Baraza la Madiwani la Hamshauri ya Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza leo kimetawaliwa na vurugu na mabishano hali iliyopelekea kuvunjika kwa kikao hicho.

Vurugu na kurushiana maneno makali, zilianza baada ya Meya wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Henry Matata lipotoa amri ya kuwafukuza kwenye kikao madiwani wawili kutoka chama cha Demokrasi na maendeleo (CHADEMA).

Miaka 35 jela kwa njama ya kumuua Mandela


Mike du Toit aliongoza kundi la kibaguzi la Boeremag kuwashambulia waafrika weusi na kupanga kumuua Mandela

Kiongozi wa njama ya waliokuwa wanaharakati wa kibaguzi nchini Afrika Kusini kumuua Nelson Mandela na kuwafukuza waafrika weusi kutoka nchini humo, amefungwa jela kwa miaka 35. Hii ni kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari nchini humo.
Kiongozi huyo aliyekuwa mhadhiri wa huo kikuu Mike du Toit alipatikana na hatia mwaka jana kwa kosa la uhaini, kwa kukiokongoza kikundi hicho katika kupanga njama ya kumuua Mandela. Kesi yake ilisikilizwa kwa miaka 9.
Aliongoza kundi la wapiganaji wa Boeremag, wabaguzi wakuu wa kizungu nchini humo.
Mnamo mwaka 2002 wapiganaji hao walijaribu kuipindua serikali iliyokuwa inaongozwa na chama tawala cha ANC.
Wanachama wengine 20 wa Boeremag waliopatikana na hatia kwa kosa la uhaini, walihukumiwa jela kwa kati ya miaka mitano na 35 katika mahakama moja mjini Pretoria.
Mnamo mwezi Julai mwaka 2012 du Toit alipatikana na hatia ya mashambulizi ya mabomu katika mtaa wa mabanda wa Soweto mjini Johannesburg mwaka 2002.
Alikuwa mtu wa kwanza kuwahi kupatikana na hatia ya kosa la uhaini nchini Afrika Kusini tangu kumalizika kwa utawala wa kibaguzi mwaka 1994.
Wadadisi wanasema kuwa huku swala la ubaguzi likiendelea kuwa changamoto nchini Afrika Kusini makundi yenye itikadi kali za kibaguzi kama Boeremag, hayana ushawishi mkubwa.

Arsenal nje ya kombe la Capital One


Arsenal nje ya kombe la Capital One

Katika mashindano ya Capital one huko uingereza Arsenal ambao wako kileleni mwa ligi kuu ya uingereza waligaragazwa bila huruma na Chelsea kwa mabao mawili kwa bila. Lakini Chlesea walipokuwa wakiwatesa the Arsenal nyumbani kwao Manchester United waliwachapa Norwich kwa mabao manne kwa bila.

 Hii inafanya Man u Kushinda mara sita mfulululizo, bila shaka na kumpa Moyes matumaini ya kufanya vizuri katika ligii ya Uingereza halikadhalika kombe hilo la Capital one.

 Na katika kile kinachonekana kuwa wanasoka wa afrika wameshuka katika chati ni kiungo wa kati Yaya Toure pekee kutoka Ivory Coast ambaye yumo katika orodha ya wachezaji 23 walioteuliwa kuwaniwa tuzo ya mchezaji bora wa Fifa mwaka huo.

Kwa sasa wachezaji nyota wa zamani kama Didier Drogba, Samuel Eto'o na Michael Essien wanaonekana kufifia.
Na Yaya Toure yuko nchini Kenya katika juhudi za kupiga vita biashara haramu ya pembe za ndovu.
Toure saa ni balozi wa shirika la mazingira duniani UNEP. Mchezaji huyo mshidi mara mbili barani Afrika alifurahi katika hotuba yake kukubali wadhifa huo mpya.

US:Nia ya viongozi ndio sababu ya udukuzi


               Mkrugenzi wa upelelezi nchini Marekani James Clapper

 Mkuu wa ujasusi nchini Marekani, James Clapper amesema kuwa nia ya baadhi ya viongozi wa kimataifa ndio moja ya sababu kuu ya Marekani kufanya upelelezi.
Mkurugenzi wa shirika la kitaifa la upelelezi, James Clapper, katika kutetea sababu yao ya kuwapeleleza viongozi wa kimataifa , alisema kuwa juhudi kama hizo ni muhimu sana katika sera ya upelelezi ya Marekani.
Lakini aliambia kamati ya waakilishi wa bunge kuhusu upelelezi, kuwa Marekani haipelelezi mataifa ya kigeni kwa undani na kiholela.
Bwana Clapper alikuwa anajibu tuhuma dhidi ya Marekani kufuatia ripoti za udukuzi dhidi ya viongozi wa kimataifa na ambao ni washirika wakuu wa taifa hilo.
"Nia ya viongozi ndio moja ya sababu kuu ya kwa nini tunafanya upelelezi na kuutathmini,'' alisema Clapper akiongeza kuwa washirika wa kimataifa a Marekani pia huchunguza maafisa wa Marekani na mashirika mengine kama sehemu ya mipangilio ya serikali.
Alisema kuvuja kwa taarifa kuhusu shughuli za upelelezi wa Marekani dhidi ya mataifa mengine imeharibia nchi hiyo sifa yake na kuwa alitarajia taarifa zaidi kutolewa.
Rais Obama anasema kuwa anataka kubadili namna nchi hiyo inavyokusanya ujasusi wake.
Lakini alisema hakuna nchi nyengine iliyo na uwezo wa kukusanya upelelezi kama Marekani na kuwa kulikuwa na makosa yaliofanyika ambayo ni ya kibinadamu au yaliyotokana na hitilafu za kimitambo.
Mwandishi wa BBC Jonny Dymond mjini Washington alisema kuwa ikiwa mtu yeyote alikuwa anatarajia kuombwa radhi na Marekani basi ajue kuwa hilo haliwezi kufanyika.

11 wauawa kwenye ajali ya treni Nairobi

Watu 11 wamethibitishwa kufariki katika ajali iliyohusisha treni na basi iliyokuwa imewabeba watu wakielekea kazini katika mtaa wa Umoja viungani mwa mji wa Nairobi.
Basi hiyo inayoaminika kuwa na watu 34 iligongwa na treni kwenye njia ya reli kuelekea mjini. Kwa mujibu wa shirika la Red Cross, idadi ya majeruhi imefika 34 na wamepelekwa katika hospitali kuu ya Kenyatta.
Baadhi ya waliojeruhiwa wanasemekana kuwa katika hali mbaya.
Walioshuhudia ajali hiyo wanasema kuwa basi hilo lilisukumwa umbali wa mita hamsini baada ya kugongwa kwa upande.
Inaarifiwa watu sita walifariki papo hapo na wengine wawili kufariki baadaye kutokana na majeraha waliyoyapata.
Wengine wengi wamejeruhiwa kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu.
Mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP aliyeshuhudia ajali hiyo alisema kuwa basi iliharibiwa vibaya baada ya kugongwa kwa upande na treni ihiyo ilikuwa inasafiri kwa kasi kubwa.
Ajali hiyo imetokea asubuhi wakati wa msongamano wa watu na magari huku watu wengi wakiwa katika haraka kuu kuelekea kazini

Dalili za mwanamke anayetembea nje ya ndoa au nje ya mpenzie

Kuna dalili nyingi ambazo zinajitokeza, lakini ukiona zaidi ya dalili mbili zinajitokeza kuna uwezekano mkubwa wa kitu kinachoendelea nje ya mahusiano yenu au ndoa yenu.

Maumbile

Viungo vya uzazi
Viungo vya mahusiano vya mwanamke kwa kawaida bila kuwa na matumizi ya mara kwa mara au muda mrefu husinyaa misuli yake, lakini inapotokea kuonekana mnapokutana amekuwa ni sawa na mlango wa kuingilia tembo wakati ulipokutana naye mara ya mwisho au mazoea ya kukutana alionekana kuwa na sawa ule mlango wa tundu la sindano lisilopenyeka kirahisi. Ujue anamahusiano nje yako.
Matiti
Kwa kawaida maembe huwa laini yanaposhikwashikwa, na pale yasiposukuwasukwa huwa magumu, na itokeapo huna mahusiano labda kwa safari au malezi ya mtoto na vinginevyo na kisha kukuta hali hiyo ujue kuna big baby anayetumia.
 

Mitindo na mazoea ya mahusiano
Pale inapojitokeza madai yasiyo ya kawaida kufanywa na kwamba bila hivyo hajisikii vizuri, jambo ambalo hakuzoea, na inapotokea anaonekana kama mzoefu wa mtindo huo, ni dalili tosha kwamba kuna anayemzoesha hayo huko aendako.


Watoto wadogo husaidia kutoa siri
Kumchongea mama kwa baba ingawa anachoongea huwezi kuelewa
Inapotokea kama ana mtoto basi baba anaporudi utaona hata kama ni mtoto wa umri wa miaka miwili na nusu and up anaonekana kuongea mambo ya kukueleza baba kwa mkupuo uanapofika tu kana kwamba anamchongea mama yake jambo ambalo halijazoeleka, mtoto anapoongea hivyo utamwona mama yake anamwangalia kwa makini sana ujue kuna kitu mtoto anakiona kisicho cha kawaida kinachofanywa na mamake.
Kushtuka na kulia amwonapo mtu anayehusiana na mamake pengine kabla haya akumwogopa
Kwa kawaida mtoto mdogo anaposhuhudia mtu asiye baba yake akifanya mambo hayo kwa mama yake anafikiri anamwadhibu, na kwa kawaida kama ni mtu wa karibu anapotembelea nyumbani utashtukia mtoto analia sana anapomwona mtu huyo humwogopa na kumkimbia, kitu ambacho si cha kawaida kwake, pengine anaweza akamfananisha na mtu anayemwona mara nyingi katika shuhguli hiyo, hata hivyo watoto makini sana kwa kunasa sura ya mtu kwa kawaida hawakosei.

Kutopenda kuondoka na mtoto
Inapotokea mtoto kuonyesha dalili hizo mama anaanza kuwa na mazoea ya kutopenda kutoka na mtoto anapoenda matembezini au shopping, hii ina maana kuendelea kuwa na mtoto pengine anavuruga malengo yake na watu wake. Ikumbukwe kwamba kabla hakuona shida kuondoka na mtoto ko kote aendako.

Kanisani au msikitini
Pamoja na kuwa na mazoea ya kwenda kanisani na kuwa mcha Mungu, inatokea hasa kwa wakristo wakatoliki au waanglikana wenye mazoea ya kushiriki komunyo anaanza kutoshiriki bila sababu za msingi. Baada ya hapo anaanza kutoshiriki ibada na moja kwa moja dhamiri inakufa kabisa hahudhurii kanisani, ni dalili tosha kwamba dhamiri inamshtaki na hivyo ameona bora kuendelea kujiburuza matopeni.

Kuondoka bila kuaga aendako
Kwa kawaida watu wanaoishi pamoja wanakawaida ya kuagana wapi mwenzake anaenda na iwapo inapotokea tatizo rahisi kufuatilia maelekezo aliyotoa kwamba wapi anaenda. Lakini ghafla utaona hapendi kabisa kuaga na pengine anakuwa na kawaida ya kuondoka ghafla kabisa na ukimwuliza anakuwa mkali na anakuambia tu naenda mahala nitarudi na hataki kumchukua mtoto. Ujue kuna kitu kinachoendlea huko aendako.

Zamu za kazi za usiku hasa manesi na wanajeshi
Wenye zamu za usiku inaweza kutokea maelezo ya overtime za mara kwa mara usiku. Ukivinjari maeneo ya kazi kutembelea kuona kama yupo kazini au la utakuta kama ana gari haionekana eneo la kazi. Jaribu kuulizia uongozi unaona wanashangaa kwamba mbona yuko off duty. Hapo kuna kinachoendelea juu ya paa la nyumba nyingine.

Vurugu nyumbani
Ugomvi usioisha wa mara kwa mara, pengine unaweza kushangaa hata sababu haieleweki na anazua jambo tu la ugonvi ujue kuna kitu kinamwasha anamkumbuka mshikaji wake wa huku nje ujuavyo waswahili husema vya wizi vitamu zaidi kuliwa kuliko vya mazoea.

Dalili baada ya kutoka kufanya ufuska
Anaonekana kuwa mchovu.


  • Anapiga miayo mirefu ya uchovu tofauti na miayo ya njaa.
  • Anatembea kwa kujivuta hasa miguu inaonekana kukosa nguvu ilivyo kawaida.
  • Anakuwa na wasiwasi na kujaribu kukusoma kama unaelewa kinachoendelea.
  • Anapenda kwenda kulala mapema hata kama hana uchovu wa kazi.
  • Hapendi majadiliano au maongezi ya kawaida.
  • Dalili tosha kwamba kuna kazi nzito ameifanya huko alikotoka kwa kuona dalili hizo hapo juu.

Uchovu wa sex huambatana na ulegevu wa macho kama una mpenzi siku ukishafanya nae afu mwangalie machoni atakuwa kachoka na macho yamemlegea !!
MWANAUME AFANYEJE NA HALI HIYO
Baadhi ya wanaume hupaparikia hali hiyo na kuzua ugonvi wa ajabu kwa mwenzake anayefanya ngono zembe nje ya mahusiano yao. Usionyeshe dalili za kufahamu kinachoendelea usije kumshtusha, bora tulia kwanza.

Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha hilo litokee kama ifuatavyo:

  • Kutokuwa pamoja kwa muda mrefu kwa sababu ya kikazi, masomo au uhamiaji
  • Ugomvi ambao humfanya mwingine asijisikie vema kwa mwenzake
  • Dalili za kuambikizwa magonjwa pengine hufanya mwingine aogope kuhusiana naye kama ilishawahi kutokea
  • Kutoridhishwa kwa mwenzake pengine kabla ya ndoa au mahusiano alikuwa na mwingine aliyemzoesha zaidi ya ufanyavyo.
  • Mazingira ya kazi afanyayo humletea vichocheo vya kufanya ngono zaidi hasa kwa manesi wanafinyama miili ya watu kila siku makazini na hivyo huwaamsha kufanya ufuska.
  • Self control inapokusekana hasa elimu ya saikolojia ambayo ndiyo kinga madhubuhi ya kujilinda.
  • Kuiga na kufanyia mazoea tunayosoma na kujadiliana mitandaoni ndiyo yanayoamsha silika ya kufanya ufuska.
  • Nk


Mwanaume mwenye akili timamu haoni sababu ya kugombana na mtu ambaye kwa utashi ana akili yake ameamua kufanya afanyavyo na pengine kufikia hatua ya kutomjali mtoto wake kama anaye.

Pengine utulivu wa mwanaume kwa kutoonyesha dalili wazi anazoona na viashiria kadhaa inaweza kusaidia kujua mengi zaidi kwa sababu mwanamke baada ya kufanya siri muda mrefu na kufikiri mwanaume hajui anaanza kutokuwa na wasiwasi na pengine kuamua kumwacha mumewe nyumbani na kwenda kulala na wanaume nje, hilo hutokea mara nyingi kwa visingizio mbalimbali kama shopping, zamu ya kazi overtime, kutembelea binamu nk.

Utaona anajifungia chumbani kwamba analala kumbe anawasiliana na hawara zake kwa simu kisha anakurupuka ghafula kutoka kwa kusema naenda mahala nitarudi, na ujua vya wili just two hours zinatosha.

Jambo la msingi mwanaume tulia na tunza kichwa na kama una familia peleka nguvu zako kulea familia yako. Kwa kawaida mambo haya mwenyewe ataumia siku yake na kujutia, na pengine mwanaume jihadhari kwani kama ulishapata dalili awali ya mambo yasiyo kawaida basi usije shtukia yamekukuta maana akishazoeana na hao wa nje pengine hawatakuwa na haja ya matumizi ya kuvaa socks.

MTOTO WA WAZIRI LUKUVI AJERUHIWA KWA TUHUMA ZA UJANGILI

 
MTOTO wa kaka wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Uratibu na Bunge, Willium Lukuvi, aitwaye Tomm Malenga, ambaye ni katibu wake, amejeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kuhusishwa na ujangili.
Habari zilizopatikana mjini hapa, juzi Jumapili, Oktoba 27, mwaka huu, zinasema akiwa ofisini kwake siku hiyo, Tomm alifuatwa na maofisa wa Wanyama Pori kwa kile kilichotajwa kuwa anahusika na ujangili.
“Walifika na kumkamata kisha wakaanza kumpiga, tena palepale ofisini kwa Lukuvi. Amevunjika vidole vya mguu na mkono wake mmoja hauko sawa baada ya kipigo hicho,” alisema mtoa habari wetu.
Tomm hakupatikana ili kuzungumzia sakata hilo lakini waziri Lukuvi alifafanua baada ya kuzungumza na mwandishi wetu ambapo alisema kilichofanyika anakijua na kwamba ni njama za wabaya wake.
“Sikiliza bwana, licha ya Tomm kuwa msaidizi wangu wa jimboni ni mtoto wa marehemu kaka yangu. Wanasema eti ametajwa kwenye ujangili; sasa kutajwa tu, unawezaje kwenda kumchukua mtu ofisini kwake, tena kwa kumpiga? Huo siyo utawala wa kisheria,” alisema waziri Lukuvi.
Alisema, mtu aliyemtaja Tomm ni Gedi ambaye alikuwa wa kwanza kukamatwa kwa ujangili na akasema amekuwa akishirikiana na mwanaye.
“Ukweli ni kwamba huyo Gedi ana usongo na mimi, kwani huwa ananipinga tangu mwaka 1995. Aliwahi kugombea udiwani, tukagundua kuwa ni Msomali, tukamfuta. Nadhani anatumia mwaya huo kunichafu mimi na familia yangu,” alisema Lukuvi.

Tuesday 29 October 2013

Kapt Komba ajitoa mhanga, asema Lowassa Rais 2015


Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kapteni Mstaafu, John Komba amevunja ukimya na kutamka wazi kuwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ndiye chaguo lake na atakuwa Rais ajaye uchaguzi wa 2015.
Komba anakuwa mtu wa pili kumtaja Lowassa hadharani kuwa anafaa kwa rais 2015.
Itakumbukwa Mbunge wa Viti Maalumu, Beatrice Shelukindo (CCM) naye alivunja ukimya baada ya kutangaza kumuunga mkono Lowassa kumrithi Rais Kikwete.
Shelukindo alitoa kauli hiyo wakati akiwasalimia wakazi wa Monduli baada ya kukaribishwa kuchangia ujenzi wa Hosteli ya KKKT, kwenye sherehe za kukaribisha Mwaka Mpya zilizofanyika nyumbani kwa Lowassa na kuhudhuriwa na makada kadhaa wa CCM.
Akizungumza na Mwananchi katika mahojiano maalumu jana, Komba ambaye ni Kiongozi wa Kundi la Uhamasishaji cha CCM Tanzania One Theatre (TOT Plus), alisema mtazamo wake kwa mtu anayefaa kumrithi Rais Jakaya Kikwete ni Lowassa.
Komba aliyeingia kwenye siasa kutokana na msukumo wa mama yake aliyekuwa msaidizi wa Bibi Titi Mohamed, alisema anazo sababu kuu tano za kumkubali Lowassa kuwa Rais na atasimama popote kumtetea.
“Nakuambia Lowassa ndiye anafaa kuwa Rais... unafikiri kuna mwingine. Nina sababu zangu tatu,” alisema Komba na kuhoji:
“Wewe unakwenda kwenye harambee, nani leo hii anaweza kusaidia kuchangia kwa fedha nyingi na zote hizo ni kwa maendeleo yanayokusudiwa kama siyo Lowassa?”
alisema Komba ambaye ni mahiri katika kuinadi CCM, katika kampeni mbalimbali za udiwani, ubunge na urais.Juu ya kuwa atakuwa katika wakati mgumu endapo anayempigia debe hatokuwa, Komba alisema: “Mimi sikwambii ni nani, lakini wapo Mawaziri waliomkana, lakini leo hii wapo kwenye Serikali hii hii ya Rais Kikwete.
“Mimi nasema Lowassa, na kama akipita sawa nitaburudiiika kwelikweli, lakini kama akiteuliwa mwingine, mimi nitakuwa naye...nitamwimbia hadi mwisho. Kazi yangu si unaijua, nitampigia debe kwa kuwa si mtu wa mtu mmoja, ni uteuzi wa wanaCCM ule si wa Komba.” alisema.
Mbali na kumnadi Lowassa, Komba alisifu uimara wa chama chake kuwa kinaimarika siku hadi siku na ndicho kinachotoa viongozi wa kweli na hata wananchi wanakikubali.

KUNDI LA BONGO MOVIE LIMEAMUA KUMTENGA WEMA SEPETU KWAKTOKUSHIKI KATIKA MSIBA WA BABA YAKE. SOMA KILICHO SABABISHA

Katika hali isiyotarajiwa katika wasanii wanaounda kundi la Bongo Movie ambalo linaundwa na baadhi ya wasanii wa filamu Swahiliwood wamejikuta wakijitenga kushiriki msiba wa baba mzazi wa msanii mwenzao Wema Isack Sepetu, baada ya kuundwa zengwe na mmoja wa watu wenye ushawishi katika kundi hilo, Wema akiongea kwa huzuni amesema kuwa hata wale waliofika jana katika msiba huo hawakufika kwa ajili ya kumfariji bali walifika kwa ajili ya kumsanifu. 

  utafiti uliofanwa ulibaini hilo kwa kuwapigia simu baadhi ya wasanii wanaotoka katika kundi hilo nao bila kusita kwa masharti ya kutotajwa majina walitiririka kwa kusema kuwa ni kweli uongozi wa kundi hilo umetoa agizo watu wasishiriki kutokana na tabia ya msanii huyo kutoshiriki katika misiba ya wasanii wenzake.
“Ni kweli hilo lipo na lina ukweli kwa njia moja au nyingine Wema bwana huwa hashiriki katika misiba ya wasanii wenzake, kuna mtu muhimu sana na ana sauti katika kundi la Bongo Movie amesema kuwa katika misiba iliyotokea ameshiriki misiba miwili tu, wa marehemu Sharo na Kanumba kwa sababu alikuwa mtu wake,”anasema kijana huyo.
Hili si jambo la kulifurahia kwa wasanii kwani halijengi bali linaleta mgawanyiko wa moja kwa moja, msanii mwingine alikiri kuwa Wema anabagua kushiriki misiba kwani wakati amefariki marehemu John Maganga alipigiwa simu ili ashiriki katika msiba lakini alisema yupo Location, hivyo wasanii wenzake wanamtenga ili aone umuhimu wa kushiriki misiba ya wenzake.

Jana jioni nyumbani hakukuwa na wasanii zaidi ya mtangazaji wa kipindi cha Take One Zamaradi Mketema akiwa na Rais wa shirikisho la wasanii Simon Mwakifwamba na waombolezaji wengine, huku baadhi ya wasanii wakifika pale na kuondoka jambo ambalo Wema alilitafsiri kama walifika pale kutoa lawama ili asiwaone kama hawajafika lakinihawakuwa na dhamira ya kweli mioyoni mwao.

MATOKEO YA WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI SASA YATAANZA KUPANGWA KWA MFUMO WA COURSE WORK.(CONTINUOUS ASSESSMENT)


Kamishna wa Elimu Profesa Eustella Bhalalusesa ameliambia gazeti la Habari Leo kuwa Serikali itabadili mfumo wa upangaji alama za ufaulu wa mitihani ya Sekondari ili kazi anazofanya mwanafunzi shuleni, zitumike katika kumpatia alama ya ufaulu katika mtihani wa mwisho, mfumo unaolandana na ule unaotumika katika Vyuo Vikuu..

Tayari Serikali imetuma dokezo, ambalo lipo katika tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa wadau wa elimu ili kupata maoni yao kabla ya kuanzisha mfumo huo. 

Dodoso hilo limeeleza kuwa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995, imeelekeza kwamba katika kuamua kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi wa elimu ya sekondari, Alama za Tathmini Endelevu ya Mwanafunzi zitachangia asilimia hamsini na mtihani wa mwisho utachangia asilimia hamsini pia.

Mathalani, kwa mtihani wenye alama za jumla ya 100, mwanafunzi akipata alama 50 kupitia kazi za shule, atatakiwa kutafuta alama 50 katika mtihani wa mwisho.

Kwa kutumia mfumo huu, mwanafunzi atakuwa anakwenda kufanya mtihani akiwa tayari anajua alama za mchango wa kazi shuleni (continuous assessment) na kuwa na hakika ya anachotakiwa kukipata wakati anakwenda kufanya katika mtihani:

“Hatutaki kuona mwanafunzi hanufaiki na kile alichokivuna akiwa shule. Mfano mfumo wa sasa mwanafunzi aliyepata alama F ni aliyepata alama kati ya 0-34.
"Lakini hapo kuna wanafunzi ambao wamezidiana kwa mfano aliyepata alama 20, hawezi kuwa sawa na aliyepata 0 ingawa wote wanawekwa kundi la F,” alifafanua Profesa Bhalalusesa.

“Hata hivyo, kumekuwa na mitizamo na mapendekezo tofauti katika muundo na matumizi ya Alama za Tathmini Endelevu ya Mwanafunzi. Mfumo huu hata hivyo hautumiki kwa wanafunzi wa kujitegemea,” lilieleza dokezo hilo.

-Habarileo

Sera ya ujasusi yaikaba koo Marekani


Chansela Angela Merkel wa Ujerumani na Rais Barack Obama wa Marekani

Shinikizo linazidi kuongezeka dhidi ya Ikulu ya Marekani kuelezea ukusanyaji wa taarifa za kijasusi za Marekani na kwa nini Rais Barack Obama anaonekana kutofahamu ukubwa wa tatizo hili.
Mkuu wa Shirika la Ujasusi na maafisa kadha watafika mbele ya Baraza la Wawakilishi kutoa maelezo kufuatia kadhia hiyo.

Na mwenyekiti wa kamati ya usalama ya Baraza la Seneti ametaka kupitiwa upya kwa mpango mzima wa Marekani wa ukusanyaji wa taarifa za kijasusi.
Rais Obama ameelezea hadharani nia yake ya kuchunguza shughuli za kijasusi huku kukiwa na madai ya kuzichunguza kijasusi nchi marafiki duniani.
Ujumbe wa Umoja wa Ulaya, uliopo mjini Washington umeelezea mvutano huo kuhusu ukusanyaji wa taarifa za kiintelijensia kuwa ni kuvunjika kwa kuaminiana kati ya Marekani na washirika wake.
Jumatatu bwana Carney, msemaji wa Rais Barack Obama, aliwaambia waandishi wa habari kuwa utawala wa Marekani unatambua umuhimu wa kujizuia zaidi katika kukusanya taarifa za kijasusi.
"Kuna mabadiliko yasiyo ya kawaida... Kwa namna tunavyotuma na kukusanya taarifa", anasema Jay Carney.
Amesema Marekani haitumii uwezo wake wa kukusanya taarifa za kiintelijensia kwa madhumuni ya kuimarisha maslahi yake ya kiuchumi, na kwamba Rais Obama amedhamiria kuhakikisha kuwa tunakusanya taarifa si tu kwa sababu tunaweza kufanya hivyo, lakini kwa sababu tunalazimika, kwa sababu tunazihitaji taarifa hizo kwa usalama wetu.
"pia tunataka kuhakikisha kuwa taarifa zetu za kiintelijensia zinafanya kazi kubwa ya kukidhi malengo yetu ya sera ya nje na usalama wa taifa, na kwamba tunapima hatari na faida ya shughuli zetu hiz. Anasema Bwana Carney.
Bwana Carney na Bwana Obama hawajazungumzia lolote kuhusu tuhuma halisi kwamba Marekani imekuwa ikifuatilia taarifa za kijasusi kutoka kwa washirika wake kimataifa, ikiwa ni pamoja na kurekodi mazungumzo ya simu ya maafisa wa nje.

Al Ahly kukutana na Orlando Pirates


Klabu ya soka ya Misri, Al-Ahly iko kifua mbele katika kutetea ubingwa wao wa ligi ya klabu bingwa Afrika baada ya kuicharaza klabu ya Cameroon ya Coton Sport katika penalty ili kuweza kufika fainali.
Klabu hiyo ya Cairo ilishinda kwa ujumla wa mabao sita saba kwenye mechi iliyochezwa katika eneo la El-Gouna baada ya mechi ukamilia kwa sare ya bao maoja kwa moja.

Matokeo sawa na hayo yalishuhudiwa kwenye mechi ya mkondo wa kwanza, iliyomalizika kwa mabao mawili kwa mawili.
Ahly itakutana na Orlando Pirates wa Afrika Kusini katika fainali itakayokuwa na mikondo miwili mwezi ujao.
Abdullah Al Saied aliingiza bao baada ya dakika tatu ya kuanza kwa mchezo na kuipa Misri mwanzo mzuri wa mechi , na kisha kuingiza bao lengine.
Ahly, ambayo haikushiriki mechi tatu za kimataifa, iliyohusisha mechi ya Misri ambayo ilishindwa vibaya sana na Ghana, ilipata nafasi nzuri za kuendeleza ushindi wao wakati wa kipindi cha kwanza cha mchuano.
Mchezaji Alexis Yougouda alifanikiwa kuingiza bao lake la saba
Wakati wa mchuano huo, Mohamed Aboutrika alikosa bao lake la kwanza lakini wachezaji wenzake walifanikiwa kuingiza mabao baadaye.
Mechi hiyo ilichezwa bila ya mashabiki baada ya kupigwa marufuku kushuhudia mechi za klabu yao, kutokana na ghasia za hivi karibuni.
Kocha wao Mohamed Youssef pia alilazimika kujionea mechi akiwa nje ya uwanja baada ya kuondolewa uwanjani wakati wa mkondo wa kwanza wa mecih hizo mjini Garoua wiki mbili zilizopita.
Ahly wameshinda ubingwa wa ligi hiyo mara saba awali, na kuifanya kuwa klabu yenye kufanikiwa zaidi barani Afrika.

Kumekucha Azam TV

UONGOZI wa Azam TV unatarajiwa kufanya uzinduzi rasmi mwezi ujao jijini Dar es Salaam huku ukijinasibu kutoa huduma ya kiwango cha juu kwa bei nafuu ili kuwanufaisha wananchi.
Hayo yalibainishwa na Mtendaji Mkuu wa Azam TV, Rhys Torrington, wakati akizungumza na waandishi wa habari waliofanya ziara katika ofisi za Azam Media jijini Dar es Salaam.
Torrington alisema wamejipanga kutoa huduma bora yenye kiwango cha kimataifa ambako wanatarajia kufanya uzinduzi rasmi Novemba mwaka huu.
Alisema, kati kati ya Novemba, wataanza kuuza ving’amuzi vya Azam TV ambako itawawezesha watazamaji kujionea zaidi ya Chaneli 30.
Alibainisha kuwa, ving’amuzi vya Azam TV vitapatikana kwa sh 95,000 na dishi lake huku huduma ya kufungiwa majumbani ikiwa ni bure.
“Mteja akishafungiwa huduma za Azam TV, malipo ya mwezi yatakuwa ni sh 12,500 tu na mteja atapata chaneli zaidi ya 50 katika king’amuzi cha Azam TV, ingawaje kwa kuanzia tutaanza na chaneli 30,” alisema Torrington.
Aliongeza kuwa, Azam TV itakuwa na Azam 1 itakayokuwa na habari za Afrika na zaidi za Kiswahili huku Azam 2 itakayokuwa ya kimataifa na baadhi vipindi vya Kiswahili na sinema za Kitanzania kwa saa 24.
Azam TV inayomiliki haki za kurusha mechi za Ligi Kuu ya Vodacom hivi sasa inarusha mechi hizo kupitia TBC1, huku ikitarajiwa kuanza kuzionesha yenyewe moja kwa moja mzunguko wa pili kwa ubora zaidi.

Mapunda amng’oa Kaseja Taifa Stars

KOCHA wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Kim Poulsen, amemwita kipa wa zamani wa timu hiyo, Ivo Mapunda, katika kikosi cha pili cha timu hiyo kwa ajili ya michuano ya Chalenji itakayofanyika mwezi ujao mjini Nairobi, Kenya.
Mapunda anayecheza soka ya kulipwa katika Klabu ya Gor Mahia ya Kenya, anamweka nje kipa namba moja wa Taifa Stars, Juma Kasema, ambaye tangu amalize mkataba wake na Simba amekuwa hana timu ya kuchezea.
Kipa huyo ameitwa katika kikosi cha pili cha Stars kilichopewa jina la Future Young Taifa Stars, kitakachoingia kambini Novemba 9, kinachojumuisha nyota 30, wakiwamo wawili kutoka timu ngeni katika Ligi Kuu ya Bara, Mbeya City ya Mbeya, ambapo watakaofanya vizuri watapandishwa hadi kikosi cha Stars.
Nyota waliomo kwenye kikosi hicho ambacho Novemba 13 kitacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Taifa Stars; Makipa: Aishi Manula (Azam), Hussein Shariff (Mtibwa Sugar) na Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya).
Mabeki: David Luhende (Yanga), Hassan Mwasapili na John Kabanda (Mbeya City), Himid Mao , Said Morad, Wazir Salum na Ismail Gambo (Azam), Issa Rashid, Miraji Adam (Simba), Kessy Khamis (Mtibwa Sugar), Michael Pius (Ruvu Shooting) na Mohamed Hussein (Kagera Sugar).
Viungo: Amri Kiemba, Ramadhani Singano, Haruna Chanongo, Jonas Mkude na William Luccian (Simba), Farid Mussa, Khamis Mcha (Azam), , Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Simon Msuva (Yanga), Washambuliaji: Elias Maguli (Ruvu Shooting), Hussein Javu (Yanga), Joseph Kimwaga (Azam), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Mwagane Yeya na Paul Nonga (Mbeya City).
Kim alisema kuelekea mechi hiyo ya kirafiki, Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaingia kambini Novemba 12 kabla ya siku itakayofuata kucheza na Future Young Taifa Stars kuelekea michuano ya Kombe la Chalenji.
Baada ya mechi hiyo, kambi ya Future Young Taifa Stars itavunjwa na kubaki Stars itakayoondoka Novemba 14 kwenda Arusha kwa kambi na kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa kabla ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ajili ya michuano ya Kombe la Chalenji itakayopigwa kuanzia Novemba 27 - Desemba 12.
Nyota 16 wa Taifa Stars na timu zao kwenye mabano ambao wataingia kambini Novemba 12, ni Ally Mustafa (Yanga), Mwadini Ali (Azam), Aggrey Morris (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (AC Cannes, Ufaransa) na Nadir Haroub (Yanga).
Erasto Nyoni (Azam), Vincent Barnabas (Mtibwa Sugar), Salum Abubakar (Azam), Mwinyi Kazimoto (Markhiya, Qatar), Frank Domayo (Yanga), Athuman Idd (Yanga), Mrisho Ngasa (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC) na John Bocco (Azam).
Wachezaji wengine kumi kutoka Future Young Taifa Stars baadaye wataongezwa katika kikosi kitakachounda timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) kwa ajili ya michuano ya Kombe la Chalenji.

Yaya Toure azuru Kenya


Mchezaji maarufu wa timu ya Manchester City Yaya Toure, amewasili mjini Nairobi Kenya kwa uzinduzi wa muungano mpya wa kukabiliana na uwindaji haramu kwa ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mazingira (UNEP).
Muungano huo umeanzishwa ili kukabiliana na uwindaji haramu wa wanyama pori haswa Ndovu ambao wanakabiliwa na tisho la kudidimia kutokana na uwindaji haramu barani Afrika.

Toure, mshindi wa tuzo la mchezaji soka bora zaidi Mwafrika kwa miaka miwili mfululizo, 2011 na 2012 ataeleza kwanini amekubali kushirikiana na muungano huo kupambana dhidi ya uwindaji haramu na nini hasa jukumu lake.
Anatarajiwa kuongea na waandishi wa habari katika makao makuu ya Umoja wa mataifa katika mtaa w akifahari wa Gigiri, Nairobi.
Wengine watakao zungumza ni Achim Steiner mkurugenzi mkuu wa shirika la UNEP pampja na mkurugenzi wa shirikisho la kandanda la kenya Sam Nyamwea.

Watumishi wa umma kulipwa kulingana na elimu

SERIKALI imepanga kutengeneza miongozo itakayowapanga watumishi wa umma katika makundi mbalimbali kwa ajili ya kulipwa kulingana na elimu yao.
Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Mtendaji wa Bodi ya Mishahara na Maslahi wa Ofisi ya Rais, Tamika Mwakahesya, baada ya kuapishwa na Rais Jakaka Kikwete kushika wadhifa huo.
Mwakahesya alisema hiyo itakuwa kazi yake ya kwanza ikifuatiwa na utafiti kuhusu vyanzo vya makusanyo nchini ambavyo vinawezesha watumishi wa umma waweze kulipwa.
“Kutokana na hali halisi ya uchumi ulivyo nchini na hasa ikizingatiwa kwamba mishahara ya watumishi inahitaji makusanyo inanipasa niangalie vyanzo vya makusanyo yetu kabla ya kuongeza au kupunguza mishahara,” alisema. Mwakahesya ambaye kabla ya wadhifa huo alikuwa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Wizara ya Kazi na Ajira, aliwataka watumishi wa umma kutofanya kazi kwa mazoea bali wafanye kwa tija, ili kipato chao kiweze kuboreshwa.
Naye Daniel Ole Njoolay ambaye aliapishwa na Rais Kikwete kuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria na nchi zilizo Magharibi mwa Afrika alisema atatumia nafasi aliyoteuliwa kuzishauri nchi kuja kuwekeza na kutalii.
“Namshukuru Mheshimiwa Rais kwa kunikumbuka …wakati nastaafu ukuu wa mkoa wa Rukwa mwaka 2011 aliniahidi kunipangia kazi nyingine, sasa amenipangia hivyo nitafanya kazi bila kuchoka,” alisema.
Katika hafla ya kuwaapisha viongozi, Rais Kikwete pia alimwapisha Bashir Mrindoko kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji na Raphael Daluti kuwa Naibu Katibu Mkuu katika wizara hiyo.

‘Wawekezaji wamepewa fedha zetu’

WAKATI Rais Jakaya Kikwete na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, wakiwabeza Watanzania kuwa hawana uwezo wa kifedha kuwekeza katika utafiti wa gesi na mafuta, mwanasheria maarufu nchini, Mabere Marando, ametoboa siri za vyanzo vya fedha za wawekezaji wa nje wanaopigiwa debe na serikali.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya stendi ya Kibiti wilayani Rufiji juzi, Marando alisema wawekezaji wengi kutoka nje hawaji na fedha mifukoni, badala yake wanatumia mabenki ya hapa nchini kujipatia mitaji hiyo, jambo alilodai kuwa linaweza kufanywa na wawekezaji wazawa.
Marando ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Makamu Mwenyekiti wa chama Kanda ya Pwani, alisema serikali imeshindwa kuwasaidia wazawa kwa kuwachukulia dhamana ya kukopa mitaji mikubwa kama inavyofanywa na nchi nyingine.
Kwamba badala ya kuwawezesha imegeuka kuwasimanga na kuwabeza kuwa hawana uwezo wa kifedha wa kampuni zao kushiriki katika michakato hiyo ya kupewa vitalu vya utafiti wa gesi na mafuta. Alisema hali hiyo ni makusudi ya serikali ya CCM kuwazuia Watanzania kutumia fursa zilizopo na badala yake inakimbiza fursa hiyo kwa wageni.
“Niliposikia rais akitoa kuli hiyo niliumia sana lakini nikaja kutambua kuwa huyu mtu hakuwahi kupigika katika maisha ya tabu na wala hajawahi kufanya biashara kwa maana hao wageni aliokuwa nao juzi wengi wao wakiwa wanataka vitalu, mimi nimewaandalia nyaraka za kukopa katika mabenki yetu nchini,” alisema.
Marando aliongeza kuwa mmoja wa waombaji hao wa uwekezaji katika vitalu vya gesi, ameweka leseni ya kampuni yake kama dhamana katika moja ya benki hapa nchini ili aweze kupata mkopo, jambo aliloeleza kuwa linaweza kufanywa na Watanzania wengi wenye dhamana za kutosha.
Aliongeza kuwa sera ya CHADEMA ni kuwapa kipaumbele wazawa badala ya wageni katika kumiliki vyanzo vya rasilimali hali aliyoeleza kuwa ni tofauti na serikali ya CCM.
Marando alisisitiza kuwa makubaliano ya uwekezaji wa eneo lolote nchini unapaswa uanzie kwa mwekezaji kukubaliana na mmiliki wa eneo analotaka kuwekeza tofauti na ilivyo sasa kwa serikali kuamua bila kuwashirikisha wananchi.
Alitolea mifano uamuzi wa serikali kushindwa kuwashirikisha wananchi katika hatua za awali ni matokea ya migongano ya mara kwa mara baina ya wawekezaji na wananchi wa maeneo husika.

Mwigamba: Sikupigana na Mbowe • CHADEMA yadai kompyuta yake ina siri zitakazogusa wengi

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Arusha ambaye amesimamishwa uongozi kwa tuhuma za usaliti, Samson Mwigamba, amesema kuwa hakupigana na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe, kama ilivyodaiwa na baadhi ya magazeti.
Mwigamba alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa kuelezea kile kilichojiri mwishoni mwa wiki hadi akapigwa na baadhi ya wajumbe wa kikao, wakimtuhumu kwamba aliandika taarifa za uongo kwenye mtandao wa kijamii wa Jamii Forums akizungumzia masuala ya uongozi ndani ya chama.
Mwigamba alisema kuwa hata wakati akivutana na walinzi wa chama Mbowe hakuwa ndani ya chumba cha mkutano, hivyo akadai kuwa anashangazwa na wale waliosambaza taarifa hizo kwamba alipigana na kiongozi huyo ambaye pia ni Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.
Aliwataja wale aliodai walimpiga kuwa ni Katibu wa Bavicha Wilaya ya Arusha, Noel OLovaroya, walinzi wa chama pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, kwamba alijaribu bila mafanikio kumpiga na kitofali ambapo alikikwepa kwa kujiangusha chini na kujigonga kisogoni.
“Wakati vurugu zikianza Mbowe hakuwa ukumbini, nilimuona akija Lema na Olevaroya, ambapo Lema alishikwa kabla hajanifikia huku Olevaroya akiruka juu ya meza na kuja kunipiga ngumi, mimi kwa kujitetea ilibidi nimpige ngumi kabla hatujaamuliwa,” alisema.
Mwigamba alimtuhumu Lema kuwa amekuwa akimtishia kumuua kwa kipindi kirefu, ambapo siku ya tukio alirudia kauli hiyo kabla hajaenda kuchukua kitofali na kujaribu kumpiga nacho ambapo alikikwepa.
Alisema kuwa tayari alishatoa taarifa polisi na kupewa kumbukumbu: AR/RB/1759/2013 aliyoifungua Februari 12, mwaka huu, baada ya kuwa anapokea vitisho vya kuuawa kutoka kwa Lema kupitia simu yake ya kiganjani.
Kuhusu kusimamishwa uongozi, Mwigamba alisema kuwa ametii licha ya kuwa kikao kilichomsimamisha hakina mamlaka kisheria, huku akiweka wazi kuwa hayuko tayari kukihama chama hicho, kwani bado anaamini ndicho chenye uwezo wa kuleta mabadiliko nchini.
Hata hivyo, tuhuma za Mwigamba zilikanushwa na Katibu wa CHADEMA wa mkoa, Amani Golugwa, akisema ni uongo dhidi ya Lema, kwani kwenye taarifa yake aliyowasilisha juzi kwenye kikao cha uongozi wa kanda alimsifu mbunge huyo kwamba ameongoza harakati mbalimbali za ujenzi wa chama kwa mafanikio makubwa, zikiwamo kampeni za ushindi wa kata nne zilizofanya uchaguzi mdogo hivi karibuni.
“Kwa kipindi chote ambacho amekuwa hayuko kazini Lema amekuwa akimsaidia hata kukamilisha ujenzi wa nyumba yake maeneo ya Sokon 1, hata anavyokwenda kwenye kesi zake Dar es Salaam ni Lema amekuwa akimsaidia gharama.
“Hicho alichokizungumza kwenye mkutano wake juu ya malalamiko ndiyo anatudhihirishia kuwa amekuwa nyoka na mnafiki ndani ya kundi letu,” alifafanua katibu huyo huku akisema hakuna malalamiko yoyote juu ya suala hilo ndani ya chama.
Golugwa aliongeza kuwa baada ya kupitia kompyuta ya Mwigamba wamebaini mambo mengi machafu na ya hatari kwa mustakabali wa chama ambayo yanawagusa watu wengi.
Hata hivyo hakutaka kuingia kwa undani wala kuyafafanua akisema yatakisaidia chama katika uchunguzi wake zaidi, na kwamba tayari kikao cha Baraza la mkoa kimeshakaa na kimemwandikia Mwigamba barua ya ajieleze ni kwa nini asivuliwe uongozi ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kulifikisha suala hilo mbele ya kikao cha Kamati Kuu ya Taifa.

Utata wagubika muswada wa kura ya maoni


Kuna uwezekano wa kuzuka mvutano mkali kwenye Mkutano wa 13 wa Bunge unaoanza leo mjini Dodoma kutokana na utata wa maandalizi ya Muswada wa Sheria ya Kura ya Maoni unaotakiwa kuwasilishwa.
Mijadala ya miswada miwili, ambayo inahusiana na mchakato wa kupata Katiba Mpya ndiyo inatazamiwa kuwasha moto katika Bunge hili.
Miswada inayosubiriwa kwa hamu ni pamoja na ule wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na ule wa Sheria ya Kura ya Maoni.
Maandalizi ya Muswada wa Kura ya Maoni huenda yakazua zogo bungeni kutokana na kuwapo malalamiko kuwa upande wa Zanzibar haukushirikishwa kikamilifu.
Pia inasemekana Kamati ya Haki, Sheria na Utawala haijakaa kupitia muswada huo na pia haijakutana na wadau mbalimbali.
Mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo, aliiambia Mwananchi kuwa hawajaupitia muswada huo baada ya kufanyiwa marekebisho.
Akizungumzia suala hilo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu wa Bunge), William Lukuvi alisema muswada huo uliondolewa kwa ajili ya kufanyiwa marekebisho ambayo alieleza kuwa tayari yameshafanyika.
“Muswada sio kama uliondolewa bila kujadiliwa, ulijadiliwa na baadaye tulikubaliana ufanyiwe marekebisho ambayo tayari yameshafanyika. Wiki hii tutauwasilisha tena mbele ya Kamati,” alisema Lukuvi.
Alipotafutwa Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, Pindi Chana kueleza kama Kamati hiyo ilikutana na upande wa Zanzibar alisema, “Siwezi kuzungumzia suala la miswada na gazeti lenu (Mwananchi), sitaki kueleza lolote, kama unataka maelezo mtafute Katibu wa Bunge au Spika,” alisema na kukata simu.
Muswada huo unaeleza kuwa kura ya maoni inatakiwa kupigwa Tanzania Bara na Zanzibar, jambo ambalo lilipingwa na upande wa Zanzibar kwa madai kuwa nao wana sheria kama hiyo na kwamba masuala ya kura ya maoni siyo ya Muungano
Muswada wa Sheria ya Marekebisho
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Mkurugenzi wa Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa wa Bunge, Deogratias Egidio alisema kuwa pamoja na miswada hiyo miwili pia kutakuwa na miswada zaidi
Egidio alisema muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba unatarajiwa kurudishwa bungeni baada ya kuombewa hati ya dharura.
Alikiri kuwa bado walikuwa hawajapelekewa, lakini wanategemea wakati wowote utapelekwa bungeni.
Muswada wa magazeti
Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali unatazamiwa kuwa moto kwani utalenga kurekebisha sheria mbalimbali ikiwamo Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976.
Wabunge tayari wamepigia kelele marekebisho hayo na Chadema wametoa tamko rasmi kuupinga.
Katika ya marekebisho ya muswada huo ni kupendekezwa kuongezwa faini kutoka Sh150,000 hadi Sh5 milioni kwa magazeti yatakayoandika habari za uchochezi, huku kipengele cha kufungiwa kwa magazeti kikiachwa kama kilivyo.

GWAJIMA TAJIRI NO. 1



Utafiti huo umefanywa kwa kutembelea makanisa makubwa ya kiroho ya jijini Dar es Salaam na kuomba kuzungumza na viongozi wake ambapo Gwajima alitoa ushirikiano kwa asilimia mia moja kuliko wengine.
MAKANISA YALIYOTEMBELEWA
Makanisa yaliyotembelewa na majina ya viongozi wake kwenye mabano ni pamoja na Full Gospel Bible Fellowship (Askofu Zachary Kakobe), Living Water Center ‘Makuti Kawe’ (Mtume Onesmo Ndegi), Kanisa la Maombezi ‘GRC’ (Lusekelo Anthony ‘Mzee wa Upako’), Mikocheni B Assemblies of God (Mama Rwakatare) na Kanisa la Efatha (Nabii na Mtume Josephat Mwingira).
KWA NINI GWAJIMA NI NAMBA MOJA?
Anakuwa namba moja kwa sababu alianika mali zake na kipato chake kingine bila kushikwa na kigugumizi. Gwajima alisema anamiliki gari la kifahari aina ya Hummer 2 ambalo gharama ya manunuzi mpaka kufika Tanzania ni wastani wa shilingi milioni 250.
AWANUNULIA WACHUNGAJI MAGARI
Baadhi ya magari aliyoyakumbuka ni Subaru Forester (sokoni linauzwa shilingi milioni 17), Mitsubishi Pajero (shilingi milioni 16), Toyota Spacio new model (milioni 20) na Toyota Harrier Lexus (milioni 35).
ANAMILIKI JUMBA LA GHOROFA NNE
Mchungaji huyo alikwenda mbele zaidi kwa kuanika maisha yake ambapo alisema awali alikuwa akiishi kwenye  nyumba ya kupanga iliyopo Mbezi Beach, Dar lakini kwa sasa amehamia katika nyumba yake mpya ya ghorofa nne, mbili zikiwa hazijakamilika. Nyumba hiyo ipo Mbezi Beach.
ANA MABASI 20 KWA AJILI YA KUSAFIRISHIA WAUMINI WAKE
Gwajima: “Pia nimeweza kwa neema ya Mungu kununua mabasi ishirini. Haya ni kwa ajili ya kusafirishia waumini wa kanisa langu wakati wa kuja kwenye ibada na kurudi makwao.”
Alisema mabasi hayo ambayo hakuyataja majina na wala yenyewe hayajaandikwa majina mbele akidai ni ‘oda’ maalum, kila moja alilinunua kwa shilingi milioni 120.
SAFARI YA ULAYA NA MAREKANI KILA MWAKA HUMWINGIZIA SHILINGI MILIONI 192
Akizungumzia kipato, Gwajima alisema mbali na sadaka ambazo huendeleza kanisa, yeye mwenyewe kila mwaka huwa na safari ya Marekani kwenda kufundisha Injili  kama mwalimu.
“Pia nimekuwa nikijipatia fedha kutokana na kazi ya ualimu ambapo kila mwaka mara moja huwa nakwenda nchi za Ulaya na Marekani kufundisha kwa siku 60. Katika siku hizo huwa nalipwa dola za Marekani 2,000 kwa siku,” (kama shilingi milioni 3.2).
Kwa hesabu hiyo, kwa siku sitini Mchungaji Gwajima hukamata shilingi milioni 192 na kurudi nazo Tanzania.
ATAMBA KUWA NA WAUMINI WENGI KULIKO WENZAKE
Gwajima alisema kwa sasa kanisa lake limepanuka ambapo alitamba kuwapa Neno waumini wapatao 70,000 kwa siku hivyo yu mbioni kuanzisha makanisa  mengine  mikoa yote ya Tanzania.
Kiongozi huyo alifafanua kuwa amefanikiwa kuwa na waumini wengi kuliko makanisa mengine kutokana na huduma nzuri anayotoa kwa waumini na jamii kwa jumla.
“Nimefanikiwa kuwa na waumini wengi kuliko wengine kwa sababu nahubiri Neno tu, sirushiani maneno na makanisa mengine.
“Sisi (yeye na wachungaji wake) hatuna utamaduni wa kuwashambulia wachungaji wenzetu. Wao hata wakitusema vipi, sisi tunakaa kimya kwani kujibishana kunaleta mgawanyiko,” alisema Gwajima.
MZEE WA UPAKO
Uwazi lilifika kwa Mzee wa Upako, Ubungo Kibangu, Dar lakini ilikuwa ngumu kumuona, wasaidizi wake wakisema ana huduma ya kiroho.
Hata hivyo, kwa kutumia kumbukumbu za nyuma ambapo mtumishi huyo wa Mungu aliwahi kuhubiria waumini wake (ikaandikwa kwenye Uwazi) akitaja utajiri alionao na mahubiri hayo kurushwa na Channel Ten, alisema:
“Mimi ndiye Mzee wa Upako, nikitoka nje nakuta magari yangu sita, nachagua leo niendeshe hili au lile. Najiambia hapana hili nililiendesha jana, nachukua lingine.”
ATAJA MAGARI ALIYONAYO
Katika mahubiri hayo, Mzee wa Upako aliyataja magari hayo kuwa ni Mercedes Benz, Land Rover Discovery, Range Rover Sport, BMW X5, Ford Escape na Range Rover Vogue.
Aidha, mtumishi huyo wa Mungu aliendelea kutamba kuwa nyumbani mwake kuna viyoyozi  (AC) na kubainisha kwamba huwa akitoka kwenye gari lenye kiyoyozi anaingia katika nyumba yenye kiyoyozi.
Kiongozi huyo ana kanisa kubwa la ghorofa Ubungo Kibangu na mabasi makubwa matano ambayo hutumika kuwasafirishia waumini wake kutoka Barabara ya Mandela hadi kanisani kwake.
KWA WACHUNGAJI WENGINE, UWAZI LAAMBULIA PATUPU
Kwa wachungaji wengine wa kiroho, mwandishi wetu alipigwa danadana za nenda rudi, nenda rudi lakini kwa muda wote huo hakuweza kuonana na viongozi wake ili na wao wafungukie utajiri wao licha ya kwamba badhi yao unajulikana.
Uwazi lilipenda kusikia kutoka kwenye vinywa vyao na si kwa kuambiwa na watu wengine au kuhisi.
Kwa Askofu Kakobe, nako hali ilikuwa hivyohivyo ingawa siku za nyuma aliwahi kunukuliwa akisema kwamba yeye siyo tajiri.
Akizungumza na Uwazi hivi karibuni kwenye ofisi za kanisa lake, Kawe, Dar, Mchungaji Gwajima alisema hivi karibuni aliwanunulia wachungaji wake 30 magari ya kutembelea. Alisema fedha hizo alizitoa mfukoni mwake.

HIVI NDIVYO KURA ZA UCHAGUZI WA TFF ZILIVYOKUWA


Rais
Jamal Malinzi- 73~ 57.9%
Athuman Nyamlani- 52~ 41.2%
Makamu wa Rais
Iman Madega- 06
Ramadhan Nassib- 52
Wallece Karia- 67
Kanda 13 Dsm
Wilfred Kidau- 04
Muhsin Balhabou- 60
Omary Abdulkadir 10
Kanda 12 Kilimanjaro
Davis Mosha- 54
Khalid Mohamed- 69
Kanda 11 Pwani
Farid Baraka- 14
Geofrey Nyange- 78
Juma Pinto- 26
Riziki Majala- 05
Twahil Njoki- 02
Kanda 10 Dodoma
Hussein Mwamba- 63
Stewart Masima- 58
Charles Komba- 04
Kanda 9 Lindi
Athuman Kambi- 84
Francis Ndulane- 30
Zafarani Demoder 11
Kanda 8 Ruvuma
James Mhagama-93
Stanley Lugenge- 31
Kanda 7 Iringa
Ayoub Nyenzi- 59
David Lugenge- 08
John Kiteve- 12
Lusekelo Mwanjala- 46
Kanda 6 Rukwa
Ayoub Nyaulingo- 52
Blassy Kiondo- 73
Kanda 5 Kigoma
Ahmeid Mgoi- 92
Yusuf Kitumbo- 28
Kanda 4 Arusha
Ally Mtumwa- 19
Alley Mbise- 51
Omari Ally- 53
Kanda 3 Shinyanga
Epaphra Swai- 63
Mbasha Matutu- 61
Kanda 2 Mara
Jumbe Magati- 11
Mugisha Galibona- 24
Samuel Nyalla- 39
Vedastus Lufano- 51
Kanda 1 Geita
Kalilo Samson- 102
Views: 329

HUKUMU YA WALIOTAKA KUMUUA NYERERE 1983


                                                 Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

                                 Walioshitakiwa kwa uhaini mwaka 1983 walikuwa wengi.
Ilielezwa mbele ya jaji aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, Nassor Mzavas kwamba washitakiwa walikuwa 19.
Miongoni mwao alikuwepo Thomas Lugangira au ‘Uncle Tom’ au ‘Uncle Check bob.’
Wenzake walikuwa ni Hatibu Gandi au ‘Hatty Mac Ghee’, Kapteni Mohammed Tamim, Kapteni Mbogoro,  Kapteni Christopher Kadege,  Luteni Badru Rwechungura Kajaja na Kapteni Mapunda.
Wengine walikuwa ni Banyikwa na mkewe, Christopher Ngaiza, Zacharia Hans Pope , Kapteni Rodrick Rosham Robert  na wengine kibao ambao jumla yao walikuwa 19.
Wakati kesi inaendelea Lugangira na Hatty Mc Ghee walipanga njama na kufanikiwa kutoroka kutoka katika Gereza la Keko, Dar.
Ilidaiwa kuwa walitorokea nchini Kenya. Baada ya kufika Kenya, Lugangira akatorokea Uingereza. Hatty Mc Ghee alikamatwa na kurudishwa Tanzania kwa kubadilishana na mtu mmoja aliyekuwa akitakiwa Kenya aliyetajwa kwa jina la Private Hezekiah Ochuka ilidaiwa kuwa alifanya ‘madudu’ huko Kenya.
Mc Ghee aliporejeshwa nchini aliunganishwa na wenzake na kesi ikapamba moto.
Toleo lililopita nilieleza jinsi Komandoo Tamim alivyouawa wakati wa kurupushani za kumkamata pale Kinondoni Mkwajuni.
Lakini hata mahakamani wakati wa kutoa ushahidi juu ya komandoo huyo  mwana usalama mmoja aliyekuwa akiitwa Mr X alisema walijaribu kumkamata lakini akawatoroka kwa kuruka ukuta wa nyumba aliyokuwa akiishi.
Akasema wakati wakimkimbiza Komandoo Tamim alidandia gari moja pick up iliyokuwa imebeba masanduku ya bia na kuanza kuwarushia wana usalama waliokuwa wakimkimbiza, hivyo akapigwa risasi na kufa.
Kesi hiyo ya uhaini ilikuwa inasisimua sana haswa maswali ya wakili wa utetezi aliyekuwa akiitwa Murtaza Lakha. Mawakili wengine wa utetezi ninaowakumbuka kwa jina moja moja ni Mucadam, Jadeja na Tarimo.
Upande wa serikali ulikuwa unaongozwa na Wakili William Sekule, pia alikuwepo Johnson Mwanyika.
Wakili Sekule alileta mashahidi kadhaa ambao walisumbuliwa sana na mawakili wa utetezi haswa Murtaza Lakha.
Jaji Mnzavas alitoa hukumu Desemba 28, 1985 ambapo washitakiwa wengine aliwafunga kifungo cha maisha na wengine walifungwa miaka kadhaa lakini Banyikwa na Ngaiza waliachiwa huru.

Kinana azima mapinduzi UVCCM


Mwenyekiti Sadifa acheza sakakasi kukwepa kung’olewa, amteua hasimu wake kisiasa, Makonda na wengine watatu kuongoza
Dodoma. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alilazimika kuzima mapinduzi yaliyokuwa yamepangwa kuwang’oa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana ya chama hicho (UVCCM), Sadifa Juma Khamis na makamu wake, Mboni Muhita.
Jana Kinana akifungua mkutano wa Baraza Kuu la jumuiya hiyo, aliweka bayana kuwa mkutano huo haukuwa kwa ajili ya “kuibomoa UVCCM, bali kuijenga”, kauli ambayo inatajwa kuwa iliwavunja nguvu wajumbe waliokuwa wamepanga kuanzisha harakati za kuwatoa madarakani viongozi hao.
Habari zaidi kutoka Dodoma zilisema kauli ya Kinana iliongeza nguvu harakati za kujinasua za Sadifa ambaye usiku wa kuamkia jana, alikesha akifanya vikao vya kuwaomba radhi wenyeviti wa UVCCM wa mikoa na baadaye wajumbe wote wa Baraza Kuu.
“Hatua hiyo nadhani imemsaidia sana maana wenzake ndani ya umoja huo hawaridhiki na jinsi mambo yanavyokwenda, pamoja na uongozi wake. Wanaona kama hakidhi standards (viwango) zao,” kilisema chanzo chetu kutoka ndani ya mkutano huo.
Hii ni mara ya pili kwa Katibu Mkuu huyo kumwokoa Sadifa, kwani Septemba mwaka huu, alilazimika kuingilia kati mgogoro ambao uliibuka katika kikao cha Baraza Kuu la jumuiya hiyo Visiwani Zanzibar baada ya wajumbe kutaka kumwajibisha kwa madai kwamba alikiuka kanuni za uteuzi wa wakuu wa idara za UVCCM.
Pamoja na kauli elekezi ya Kinana, Sadifa ambaye pia ni Mbunge  wa Donge, Zanzibar alilazimika kucheza sarakasi zilizomwezesha kuzima mapinduzi yaliyokuwa yameandaliwa dhidi yake. Mwenyekiti huyo aliongoza kikao cha Baraza Kuu kwa saa tatu na kukamilisha ajenda zilizokuwa zimepangwa, ikiwa ni pamoja na kuwaidhinisha wakuu wapya wa idara za jumuiya hiyo,  kisha aliahirisha mkutano huo mara tu baada ya kuibuliwa kwa hoja ya kutaka kumjadili.
Habari zilizolifikia gazeti hili jana jioni zilisema, Mwenyekiti wa UVCCM, Mkoa wa Mbeya, Amani Kajuna ndiye aliyeibua hoja ya kutaka Sadifa ajadiliwe kutokana na kile alichosema kuwa kiongozi huyo ameifanya jumuiya hiyo kushindwa kutekeleza wajibu wake ipasavyo.
“Kama tunataka kusonga mbele katika jumuiya yetu, lazima tuhakikishe kwamba tunaisafisha nyumba yetu ili tukitoka hapa wote tuwe tunazungumza lugha moja. Kwa hiyo napendekeza mwenyekiti atoke nje ili tumjadili,” chanzo chetu kilimnukuu Kajuna.
Habari zaidi zilidai mapendekezo hayo ni kama yaliungwa mkono na baadhi ya wajumbe, akiwamo Mwenyekiti wa UVCCM wa Mkoa wa Dodoma, Henry Msunga ambaye alisimama na kusema: “Hiyo ni hoja ya msingi sana”.
Hata hivyo, wakati wajumbe wengine wengi wakiwa wameinua mikono yao juu wakitaka kuchangia pendekezo hilo, Sadifa alisimama na kuanza kuzungumza huku akiomba msamaha kwa upungufu wa kiuongozi unaojitokeza na katika hali isiyotarajiwa aliahirisha rasmi mkutano huo.
Kajuna na Msunga kwa nyakati tofauti jana, walilithibitishia gazeti hili kuwapo kwa matukio hayo, lakini walikataa kuyazungumzia kwa undani huku wakisema kuwa bado wana fursa katika vikao vijavyo kwa ajili ya kurekebisha mambo ndani ya jumuiya hiyo.
“Mimi bado nina imani na jumuiya yetu, maana watendaji ambao tumewapitisha leo (jana) ninaamini watafanya kazi nzuri. Sisi viongozi wa mikoa tuko vizuri na tuna wanachama wengi, kwa hiyo jumuiya itaendelea kuwa imara,” alisema Kajuna.
Kwa upande wake, Msunga alisema: “Baada ya hoja kuibuliwa kweli mimi niliiona ni ya msingi sana, ila nimeridhika na maelezo kwamba mkutano ulikuwa na ajenda maalumu kwa hiyo ninachoamini ni kwamba fursa bado ipo, tutakapokutana tena tutakuwa na nafasi ya kurekebisha kasoro zinazojitokeza”.
Jitihada za kumtafuta Sadifa hazikufanikiwa jana, baada ya gazeti hili kuambiwa kuwa alikuwa kwenye kikao cha Kamati ya Utekelezaji ya jumuiya hiyo, kilichokutana jana usiku.
Chimbuko la mapinduzi
Mpango huo wa mapinduzi ulikuwa ni mwendelezo wa fukuto lililoanzia katika Mkutano Maalumu wa Baraza Kuu lililofanyika Zanzibar mapema Septemba mwaka huu, wakati wajumbe walipowakataa wakuu wa idara za UVCCM kwamba hawakuwa halali kutokana na uteuzi wao kutofuata taratibu na kanuni za jumuiya hiyo.
Mapema jana kabla ya kuzuka kwa hoja za kutaka kumjadili Sadifa, baraza hilo liliwapitisha wakuu wa idara wapya watatu akiwamo hasimu wa kisiasa wa mwenyekiti huyo wa UVCCM, Paul Makonda ambaye sasa ataongoza Idara ya Chipukizi na Uhamasishaji.
Makonda mara baada ya kushindwa katika Uchaguzi Mkuu wa jumuiya hiyo mwishoni mwa mwaka jana alipokuwa akiwania nafasi ya makamu mwenyekiti, aliteuliwa kuwa mjumbe wa Baraza Kuu lakini aliikataa nafasi hiyo.
Hatua hiyo ilimgharimu katika kikao cha Baraza Kuu la UVCCM, Februari mwaka huu, wakati alipokwenda Dodoma kwa mwaliko wa kuhudhuria kikao hicho, lakini baada ya kuchukua posho, alitimuliwa kwa maelezo kwamba aliwahi kukataa nafasi hiyo.
Taarifa ambazo gazeti hili lilizipata na kuthibitishwa na Katibu Mkuu wa UVCCM, Sixtus Mapunda zilisema wengine walioteuliwa na kuidhinishwa na Kikao cha Baraza Kuu ni Zainabu Katimba atakayeongoza Idara ya Oganaizesheni na Omari Suleiman ambaye amepewa Idara ya Fedha na Uchumi.
Sadifa ambaye pia ni Mbunge wa Donge aliwahi kulalamika juu ya kuwapo kwa kundi la vijana ambao wamekuwa wakimpiga vita sambamba na kuingilia utendaji wa kazi zake za kila siku kinyume cha katiba ya jumuiya hiyo.

Chanzo MWANANCHI

MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISITU IMEMUACHIA HURU ALIYEKUWA WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA RAISI, ARCADO NTAGAZWA


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imewaachia huru Waziri wa zamani, Arcado Ntagazwa na wenzake waliokuwa na kesi na kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu zenye thamani ya sh milioni 74.9, baada ya kuwaona hawana hatia na hawakutenda kosa hilo.

Sambamba na hilo, mahakama hiyo imemshauri mlalamikaji katika kesi hiyo ambaye ni Noel Severe kufungua kesi ya madai kama walivyofanya hivi karibuni, ambapo walifungua kesi ya madai dhidi ya Ntagazwa.

Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Gene Dudu, alisema kuwa kesi hiyo ya jinai namba 108/2012 aliyoitolea hukumu jana, haikupaswa kuwa jinai bali ya madai.

Akisoma hukumu hiyo, saa tano asubuhi, Dudu alisema upande wa Jamhuri uliokuwa ukiwakilishwa na Wakili wa Serikali, Charles Anindo, katika harakati zake za kutaka kuthibitisha kesi yake ulileta mashahidi watano wakati upande wa washitakiwa waliokuwa wanatetewa na wakili wa kujtegemea, Alex Mshumbusi, ulileta mashahidi wanne, ambao ni washitakiwa wenyewe na shahidi mmoja.

Hakimu Dudu alisema mahakama yake ilipata fursa ya kuchambua ushahidi wa pande zote mbili na mwisho wa siku ikabakiwa na swali moja la kujiuliza kuwa, je, ni kweli washitakiwa hao walitenda kosa kinyume cha kifungu cha 320 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002?

Aliongeza kuwa kwa mujibu wa kifungu hicho ni lazima mtuhumiwa awe ametoa taarifa za uongo kwa mlalamikaji ili ajipatie kitu fulani kwa njia hiyo ya uongo na awe na nia ovu wakati akitaka kujipatia mali hizo.

“Lakini kwa mujibu wa ushahidi uliopo mahakamani, imeonesha wazi kabisa Ntagazwa na mshitakiwa wa pili ambao ni wajumbe wa bodi wa taasisi ya Ford walitoa oda kwa Kampuni ya Visual Storm ambayo Mkurugenzi wake ni Severe, ya kuomba watengenezewe fulana 5,000 na kapelo Korea 5,000, ambapo walifanya hivyo baada ya kikao cha bodi kutenga bajeti ya kutengenezwa kwa mavazi hayo.

“Mavazi hayo yaligawiwa bure kwa umma siku ya kumbukumbu ya kifo cha hayati Julius Nyerere, wakiwa na lengo la kutokomeza ufisadi wakati wa kumuenzi kiongozi huyo, kwa ahadi kuwa wangelipa ndani ya mwezi mmoja,” alisema Dudu.

Alisema hoja ya kwamba mshitakiwa wa tatu ambaye ni mtoto wa Ntagazwa, Dk. Webhale Ntagazwa, kuwa ndiye alitoa oda ya kuchapwa kwa fulana na kofia hizo, hakustahili kushitakiwa kwa kosa hilo kwa sababu Ford ni taasisi na si mali ya mshitakiwa.

Dudu alisema utetezi wa washitakiwa unaonesha waliandika barua kwa wafadhili wakiomba fedha za kuweza kufanikisha mradi wao wa kutaka kumuenzi Nyerere siku ya kumbukumbu ya kifo chake Oktoba 14, na wafadhili hao waliwakubalia waendelee na taratibu za kuchapisha fulana na kwamba watatoa fedha za kulipia.

Lakini kabla ya tamasha kufanyika, Ntagazwa na wenzake walishtukia fulana zao hizo zikibadilishwa nembo na kuonekana ni za Chama Cha Jamii (CCJ), hali iliyosababisha mfadhili aliyewaahidi fedha kujitoa akidai hawafadhili vyama.

“Mahakama hii imeona habari hiyo iliyochapishwa kwenye gazeti la Mtanzania, ambapo hata washitakiwa waliandika barua kwa IGP Said Mwema kulalamika fulana na kofia zao kuhujumiwa, hivyo kusababisha washitakiwa wajikute wakishindwa kulipia gharama za uchapishaji kwa kampuni ya Severe baada ya mfadhili wao kujitoa,” alisema.

Baada ya hakimu huyo kusoma hukumu, Ntagazwa aliangua kilio nje ya mahakama akisema: “Yaani kumuenzi Nyerere ndiko kulikosababisha nifunguliwe kosa la jinai? Tena polisi walivyo na roho mbaya na katili siku wanakuja kunikamata nyumbani walinikamata uchi wa mnyama nikiwa bafuni naoga kwa sababu nimehamia CHADEMA.

Pamoja na Ntagazwa, washitakiwa wengine ni mtoto wake, Dk. Webhale Ntagazwa na mshitakiwa wa kwanza ni Senetor Mirelya (60).

Aprili 23, mwaka 2012, ilidaiwa mahakamani hapo na wakili wa Serikali, Ladislaus Komanya, kuwa Oktoba 22 mwaka 2009 huko Msasani Mikoroshini, washitakiwa hao kwa nia ovu walijipatia fulana 5,000 na kofia 5,000 zenye thamani ya sh milioni 74.9 kutoka kwa Noel Severe, kwa makubaliano kuwa wangemlipa katika kipindi cha mwezi mmoja tangu walipochukua vifaa hivyo lakini walishindwa.

-Tanzania daim

MAPIGANO DHIDI YA WAASI WA M23 HUKO CONGO YAPAMBA MOTO

 
Mapigano mapya yamezuka jana Jumamosi(26.10.2013) kati ya majeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na waasi katika siku ya pili ya machafuko ambayo yamesababisha miito ya utulivu kutoka kwa jumuiya ya kimataifa .

Mapigano ya hivi karibuni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo yamezuka siku ya Ijumaa, chini ya wiki moja baada ya serikali mjini Kinshasa na waasi wa kundi la M23 kutangaza kuwa mazungumzo ya amani mjini Kampala yamevunjika.

Jeshi la serikali jioni ya Jumamosi lilisema kuwa limeukamata mji wa Kibumba , mji ulioko kilometa 25 kaskazini ya eneo mji wa mashariki mwa nchi hiyo wa Goma ambao unatoa njia kuelekea katika eneo la waasi upande wa kaskazini.

"Kibumba uko chini ya udhibiti wa jeshi la serikali FARDC kuanzia leo," afisa mwandamizi wa jeshi ameliambia shirika la habari la AFP mjini Goma. Waasi hawakuweza kupatikana mara moja kuzungumzia tamko hilo.

Upande mwingine wa mapigano umeanza ghasia siku ya Jumamosi wakati jeshi liliposhambulia maeneo ya kundi la M23 katika jimbo la Mabenga, kiasi ya kilometa 80 kaskazini mwa goma na karibu na mpaka na Uganda.(P.T)


Jeshi "limeanzisha mashambulizi katika barabara ya Mabenga kuelekea Kahunga. Linatumia wanajeshi, vifaru na makombora", afisa mwingine wa jeshi amesema, akizungumza kwa masharti ya kutotajwa jina.

Waasi wamethibitisha kuwa mapigano yamesambaa hadi katika eneo la kaskazini.

Mapigano yasambaa

"Mapigano yanaongezeka katika maeneo yote," kiongozi wa kisiasa wa M23 Bertrand Bisimwa amesema katika tovuti ya kundi hilo.

Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika mzozo huo, Mary Robinson na Martin Kobler, wametoa taarifa wakielezea wasi wasi wao mkubwa kuhusiana na mapigano hayo mapya.

"Tunatoa wito kwa pande zote kuonyesha hali ya uvumilivu na kuanza tena majadiliano mjini Kampala," wamesema. Marekani imesema kuwa imesitushwa na ripoti za kuongezeka kwa mapigano, licha ya miito ya kimataifa kwa pande hizo kuonesha hali ya kuvumiliana.

"Tunawasi wasi mkubwa juu ya ripoti za mapigano ya mpakani, " katika jimbo la Kivu ya kaskazini, msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni Jen Psaki amesema katika taarifa, akizitaka pande zinazopigana, "kuacha vitendo vitakavyozidisha hali hiyo".

Taarifa ya Psaki imezitaka pande hizo kurejea katika majadiliano, " ili kuondoa vikwazo vilivyobaki kuelekea kutiwa saini kwa makubaliano ya mwisho, na ya msingi, ambayo yataleta usitishaji wa kudumu wa mapigano na kuwawajibisha wake ambao wamefanya uhalifu mkubwa".

Jumuiya ya kimataifa yaonya

Mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya Catherine Ashton pia ametoa wito, "kwa wahusika wote katika eneo hilo kuzuwia kuongezeka zaidi kwa hali hiyo na kuufanya mzozo huo wa kimataifa".

Athari zilizoripotiwa ndani ya mpaka wa Rwanda kutokana na matukio ya hivi karibuni yanapaswa kufanyiwa uchunguzi kwa pamoja," amesema Ashton.

Waasi wanadai kuwa jeshi la serikali lilishambulia maeneo yao mapema siku ya Ijumaa, lakini jeshi la serikali linasisitiza kuwa lilishambuliwa kwanza, madai ambayo yanaungwa mkono na duru kutoka ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MONUSCO.

Wakati huo huo jeshi la serikali ya Congo limesema limepata mafanikio makubwa dhidi ya waasi wa M23 katika siku ya pili ya mapigano makali jana Jumamosi na kuitaka nchi jirani ya Rwanda kusaidia kuwanyang'anya silaha waasi.

Picha:Jinsi wanawake wa Kenya Ambavyo Hawana Aibu Wakiwa Club

girl 
There was a story about this sometime ago talking about how these girls went gaga in a club, no one gave the true story saying it was at a time they had told their folks they were going to a vigil. At a time in life ladies feel they have their lives to themselves, and only God
can help save them from the social vices that trail such freedoms.

Monday 28 October 2013

Ivo Mapunda aitwa kikosi cha ‘Future Young Taifa Stars’

Ivo Mapunda aitwa kikosi cha ‘Future Young Taifa Stars’ Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 30 wa timu ya pili (Future Young Taifa Stars) kitakachoingia kambini Novemba 9 mwaka huu ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Chalenji.

Kipa Ivo Mapunda wa Gor Mahia ya Kenya ni miongoni mwa wachezaji walioitwa na Kim kwenye kikosi hicho ambacho hukitumia kuangalia uwezo wa wachezaji kabla ya kuwajumuisha kwenye timu ya wakubwa.

Kikosi hicho kamili ambacho Novemba 13 kitacheza mechi ya kirafiki na Taifa Stars kinaundwa na; makipa Aishi Manula (Azam), Hussein Shariff (Mtibwa Sugar) na Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya).

Mabeki ni David Luhende (Yanga), Hassan Mwasapili (Mbeya City), Himid Mao (Azam), Issa Rashid (Simba), Ismail Gambo (Azam), John Kabanda (Mbeya City), Kessy Khamis (Mtibwa Sugar), Michael Pius (Ruvu Shooting), Miraji Adam (Simba), Mohamed Hussein (Kagera Sugar), Said Moradi (Azam) na Waziri Salum (Azam).

Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Farid Mussa (Azam), Haruni Chanongo (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Jonas Mkude (Simba), Khamis Mcha (Azam), Ramadhan Singano (Simba), Simon Msuva (Yanga), William Lucian (Simba).

Washambuliaji ni Elias Maguli (Ruvu Shooting), Hussein Javu (Yanga), Joseph Kimwaga (Azam), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Mwagane Yeya (Mbeya City) na Paul Nonga (Mbeya City).

Kim amesema kikosi cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager chenyewe kitaingia kambini Novemba 12 jijini Dar es Salaam ambapo siku inayofuata ndipo kitakapocheza mechi na Future Young Taifa Stars.

Baada ya mechi hiyo, kambi ya Future Young Taifa Stars itavunjwa wakati Taifa Stars itaondoka Novemba 14 mwaka huu kwenda Arusha ambapo itaweka kambi na kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa kabla ya kwenda Nairobi, Kenya kwenye michuano ya Kombe la Chalenji itakayofanyika kuanzia Novemba 27 hadi Desemba 12 mwaka huu.

Wachezaji 16 wa kikosi cha Taifa Stars kitakachoingia kambini Novemba 12 mwaka huu kinaundwa na Ally Mustafa (Yanga), Mwadini Ali (Azam), Aggrey Morris (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (AC Cannes, Ufaransa) na Nadir Haroub (Yanga).

Erasto Nyoni (Azam), Vincent Barnabas (Mtibwa Sugar), Salum Abubakar (Azam), Mwinyi Kazimoto (Markhiya, Qatar), Frank Domayo (Yanga), Athuman Idd (Yanga), Mrisho Ngasa (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC) na John Bocco (Azam).

Wachezaji wengine kumi kutoka Future Young Taifa Stars baadaye wataongezwa katika kikosi kitakachounda timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) kwa ajili ya michuano ya Kombe la Chalenji.

Uwoya awapasha wanao mwandama


MSANII wa filamu za Bongo aliyetangaza kuikacha kazi hiyo , Irene Uwoya, amesema mali anazomiliki amezinunua kwa pesa zake alizopata wakati akiwa mwigizaji pamoja na zile zinazotokana na biashara zake nyingine.
Ameongeza kuwa ameamua kuweka wazi ukweli huo kutokana na maneno yaliyozagaa kuwa magari anayomiliki amenunuliwa na wanaume ‘wanaomweka mjini’.
“Kwa nini watu hawataki kukubali kuwa kazi ya uigizaji inalipa, yaani sisi tukinunua magari tumehongwa? Yaani wa kuhongwa ni sisi tu na si tasnia nyingine?” alihoji Uwoya.
Aidha Uwoya alisema kuwa kazi ya filamu ukijua kuitumia vizuri kwa kujiwekea malengo na kuitumia vizuri kila senti unayoipata, unaweza kupata mafanikio makubwa.
“Tunaigiza sehemu nyingine ambazo hutaki hata mwanao aone, hii siyo kazi rahisi maana yake ni kwamba kama ukiipatia unaweza kujikuta unaingiza pesa kila siku kwani mwaka mzima uko kazini,” alisema.

BABA YAKE DIAMOND PLATINUMZ AFURAHIA UAMUZI WA MWANAE KURUDIANA NA WEMA ASEMA PENNY HANA NYOTA YA KUWA NA MWANAE..!!

 
Baba mzazi wa Diamond, Abdul Jumaa


Akizungumza na mwanahabari wetu juzikati, Baba Diamond alisema alifurahishwa mno na hatua ya mwanaye kurudiana na Wema kwani ndiye mwanamke anayejielewa na ana nyota kali tofauti na warembo wengine aliowahi kuwa nao.

Wema ni mwanamke mwenye nyota kali sana na anapendwa na wengi. Siyo kama hao akina sijui Penny (Penniel Mungilwa).

“Hana majivuno hata mimi nilisema mwanzoni walipoachana kuwa Diamond alipoteza bahati lakini sasa naamini atafika mbali zaidi kwani kama siyo kuachana kwao, Diamond angekuwa mbali,” alisema.

Hata hivyo, alimtaka Diamond kutulia na Wema kwani ndiye mwanamke sahihi kwake na aepuke kutangatanga kwani atashindwa kufanya mambo ya maana yatakayomuwezesha kuwa juu zaidi ya hapo alipo kwa sasa.
Hivi karibuni Diamond alithibitisha kurudiana na Wema wakiwa China lakini alipotua Bongo akaendelea na uhusiano wake na Penny hivyo kuwaacha mashabiki wake njiapanda.



TB JOSHUA ATABIRI KUWA RAISI WA MOJA YA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI ATATEKWA NA KULIPULIWA

Mchungaji Maarufu kutoka Nigeria Ambae hutabiri mambo mbalimbali na kweli yakatokea  TB Joshua ametoa utabiri mpya ambao unahusisha Africa Mashariki .

Ameonyeshwa rais mmoja Africa Mashariki atatekwa na ameonyeshwa watu wakiwa club wanacheza then wanalipukiwa na nchi iyo ni jirani na Kenya, Angalizo, amesema siyo kenya tena,je itakuwa nchi gani?

Misa ya jana jumapili ndo kasema, na amesema ataendelea kuomba ili jumatano na alhamisi ijayo aonyeshwe ni rais gani na nchi gani.

Malinzi atoa msamaha kwa wote waliofungiwa.

Jamal Emil Malinzi ndiye Rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Malinzi ameshinda wadhifa huo katika uchaguzi wa Kamati ya Utendaji ya TFF uliofanyika juzi (Oktoba 27 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.

Aliibuka na ushindi wa kura 73 dhidi ya mpinzani wake pekee Athuman Jumanne Nyamlani aliyepata kura 52. Nafasi ya Makamu wa Rais imetwaliwa na Wallace Peter Karia aliyepata kura 67 na kuwashinda Ramadhan Omari Nassib kura 52 huku Imani Omari Madega akipata kura sita.

Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa, Rais Malinzi ametaka ushirikiano kutoka kwa wadau wote akiwemo mpinzani wake Nyamlani katika kuhakikisha mpira wa miguu nchini unasonga mbele.

Pia ametoa msamaha kwa watu wote waliokuwa wamefungiwa kuanzia ngazi ya wilaya, mkoa na TFF. Msamaha huo hauwahusu wale waliofungiwa kwa makosa ya rushwa au kupanga matokeo. Vilevile msamaha huo hauhusu adhabu zilizotolewa katika ngazi ya klabu.

Rais Malinzi pia amevunja kamati zote za TFF ambapo ataziunda upya kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji.

Kwa upande wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji walioshinda ni Kalilo Samson (Kanda namba 1- Geita na Kagera) aliyepata kura 102 za ndiyo na 17 za hapana. Kanda namba 2- Mara na Mwanza, mshindi ni Vedastus Lufano aliyepata kura 51 dhidi ya Jumbe Odessa Magati (11), Mugisha Galibona (24), na Samwel Nyalla (39).

Epaphra Swai ndiye mshindi wa Kanda namba 3- Shinyanga na Simiyu kwa kura 63 dhidi ya Mbasha Matutu aliyepata 61. Kanda namba 4- Arusha na Manyara mshindi ni  Omali Walii Ali aliyepata kura 53 dhidi Elley Mbise (51), Ally Mtumwa (19).

Kanda namba 4- Kigoma na Tabora, mshindi ni Ahmed Idd Mgoyi aliyepata kura 92 dhidi ya 28 za Hamisi Yusuf Kitumbo.

Ayubu Nyaulingo na Blassy Mghube Kiondo ameshinda Kanda namba 6- Katavi na Rukwa kwa kura 73 dhidi ya Ayubu Nyaulingo aliyepata 52. Ayoub Shaibu Nyenzi ndiye mshindi wa Kanda namba 7- Iringa na Mbeya kwa kupata kura 59 na kuwapiku David Samson Lugenge (8), John Exavery Kiteve (12) na Lusekelo Elias Mwanjala (46).

Kanda namba 8- Njombe na Ruvuma inawakilishwa na James Patrick Mhagama aliyepata kura 93 dhidi ya 31 za Kapteni mstaafu Stanley William Lugenge. Athuman Kingombe Kambi ndiye mshindi wa Kanda namba 9- Lindi na Mtwara kwa kura 84 akiwazidi Francis Kumba Ndulane (30) na Zafarani Mzee Damoder (11).

Hussein Zuberi Mwamba ametetea ujumbe wa Kanda namba 10- Dodoma na Singida kwa kura 63 akiwapiku Stewart Masima (58) na Charles Komba (4). Geofrey Irick Nyange ameshinda Kanda namba 11- Morogoro na Pwani akipata kura 78 dhidi ya Juma Pinto (26), Farid Nahdi (14), Riziki Juma Majala (5) na Twahil Twaha Njoki (2).

Kanda namba 12- Kilimanjaro na Pwani, Khalid Abdallah Mohamed ndiye aliyeibuka kidedea kwa kura 69 dhidi ya 54 za mpinzani wake Davis Elisa Mosha.  Kidao Wilfred Mzigama ameshinda Kanda namba 13- Dar es Salaam kwa kupata kura 60 dhidi ya wapinzani wake Muhsin Said Balhabou (50), Omar Isack Abdulkadir (10) na Alex Crispine Kamuzelya (4).