Wednesday 25 June 2014

Super Eagles ya Nigeria ndiyo timu ya kwanza kutoka Afrika kufuzu kwa raundi ya pili ya kombe la dunia.


Mabingwa hao wa Afrika walifuzu kama washindi wa pili katika kundi F licha ya kushindwa mabao 3-2 na Argentina katika ya mwisho ya makundi.
Nigeria iliingia katika mechi hiyo ikifahamu fika kuwa iwapo Iran itailaza Bosnia basi wao walifaa kuilaza Argentina.
Hata hivyo Bosnia haikuchelea iliizaba Iran 3-1 na kupunguza shinikizo kwa vijana wa Stephen Keshi .Nyota wa Argentina Lionel Messi alifunga mabao mawili na kuwasaidia kuibana Nigeria.Mshambulizi huyo wa Barcelona alifunga bao la kwanza, lakini Ahmed Musa akasawazishia Nigeria chini ya sekunde 80.
Messi alifunga tena kupitia mkwaju wa adhabu na kufanya mambo kuwa 2-1 kabla ya mapumziko, lakini Musa akasawazisha tena.Marcos Rojo alifunga bao la ushindi kwa Argentina na kuifanya timu yake kumaliza kileleni mwa kundi F kwa kushinda mechi zote tatu walizocheza, huku Nigeria ikifuzu katika nafasi ya pili kwa alama 4 baada ya Iran kushindwa kunyakua alama kutoka kwa Bosnia-Hercegovina.Ilichukua dakika 3 tu kabla ya bao la kwanza kufungwa baada ya Messi kukutana na pasi yake Angel Di Maria.
Waargentina hawakuwa wamekamilisha kusherehekea kabla ya Nigeria kusawazisha.Kiungo cha kati Michel Babatunde alimmegea pasi safi Musa aliyefunga bao hilo la kusawazisha .Ilikuwa mara ya kwanza kwa historia ya Kombe la Dunia kwa timu mbili zinazochuana kufunga katika dakika tano za kwanza.
Nigeria sasa itachuana Ufaransa katika mkondo wa pili huku

NGASSA AULA AFRIKA KUSINI, FREE STATE STARS WAFIKA BEI, WAHAHA KUMNG’OA YANGA SC.


MSHAMBULIAJI wa Yanga SC, Mrisho Khlafan Ngassa amefuzu majaribio baada ya siku moja tu katika klabu ya Free State Stars ya Afrika Kusini, ambayo sasa inafanya utaratibu wa kumnunua.
Ngassa aliondoka jana asubuhi Dar es Salaam na jioni ya jana akafanya mazoezi na klabu hiyo na moja kwa moja akakubalika.
BIN ZUBEIRY inafahamu hivi sasa Free State Stars imeanza mawasiliano na uongozi wa Yanga juu kumnunua mchezaji huyo hodari.

Akizungumza kutoka Afrika Kusini leo, Ngassa amesema; “Nilidhani yatakuwa majaribio ya muda mrefu, lakini nimefika tu baada ya kufanya nao mazoezi mara moja, wakasema wewe si wa kujaribiwa, umekuja hapa kusajiliwa,”amesema Ngassa.
Ngassa alikwenda mwenyewe Afrika Kusini kwa gharama zake baada ya kuambiwa klabu hiyo inatafuta winga.
“Kuna rafiki yangu aliniambia hii timu inatafuta winga, akaniambia ananiunganishia mpango wa kwenda majaribio na nijiamini nitafuzu, nikakubali nimekuja na mambo safi,”alisema.
Ngassa amesema kwamba kwa sasa Free State wanawasiliana na Yanga SC juu ya mpango wa kumhamishia huko. “Naipenda sana Yanga, nimecheza pale kwa moyo wangu wote, lakini naomba tu wawe wepesi kuniruhusu kuja kujiendeleza huku,”amesema.
Free State imetuma barua Yanga SC kutoa ofa ya bei wanayotaka kumnunua Ngassa na sasa inasubiri majibu kwa ajili ya hatua zaidi.
Ngassa ameshindwa kwenda na timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kambini Botswana kwa ajili ya mpango huo wa kuhamia Afrika Kusini.
Stars imeondoka alfajiri ya leo kwa ndege ya shirika la Afrika Kusini kwenda Gaborone, Botswana ambapo kitapiga kambi ya wiki mbili.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imeweka kambi hiyo chini ya Kocha Mart Nooij ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi yake ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika (AFCON) dhidi ya Msumbiji (Mambas) itakayochezwa Julai 20 mwaka huu Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mechi hiyo itachezeshwa na waamuzi kutoka Misri wakiongozwa na Mahmoud Ashor wakati Kamishna atakuwa Felix Tangawarima kutoka Zimbabwe.

Sekretarieti ya Ajira Yazipa Rungu Serikali za Mitaa.


Serikali za mitaa zitaruhusiwa kuanza kuajiri watumishi wa baadhi ya kada za chini katika mwaka wa fedha wa 2014/2015.Akihojiwa katika Maonyesho ya Wiki yaUtumishi wa Umma kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam, Msemaji wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa
Umma, Riziki Abraham, alithibitisha kuwa Sekretarieti hiyo itakasimu sehemu ya madaraka yake ya kuendesha mchakato wajira serikalini kwa serikali za mitaa.
"Sekretarieti ya Ajira imeandaa mpango wa kukasimisha madaraka yake ya kuendesha mchakato wa ajira serikalini kwa baadhi ya kada za chini (operation staff) kwenye mamlaka za Serikali za Mitaa na mchakato huo utaanza mwaka wa fedha 2014/15" alisema.Pia, alisema katika kila nafasi ya kazi inayotangazwa kwa hiyo haizingatii GPA (kiwango cha ufaulu kwa masomo yote ). Alieleza kuwa zipokada, ambazo GPA inazingatiwa ;na zipo
kada ambazo kinachoangaliwa ni ufaulu tu wa kawaida na sifa zilizoainishwa."Zipo baadhi ya kada ambazo masharti yake ni pamoja na kuwa na GPA ya kiwangofulani. Kada ambazo ni lazima GPA kuangaliwa ni kama vile kada za wakufunzi wa vyuo mbalimbali. Kazi nyingine hazina
masharti ya GPA, kinachoangaliwa ni ufaulu tu na sifa zilizoainishwa katika tangazo la nafasi za kazi kulingana na kada husika",alisema Riziki.Alitaja moja ya matatizo wanayopata waombaji wa kazi kuwa ni kupotelewa na vyeti vya kitaaluma. Alisema waombaji wa kazi ambao wamepata tatizo hilo, wanachopaswa kufanya ni kuripoti kwenye mamlaka husika, alikokuwa amepata cheti hicho ili apewe mwongozo wa kufanya na kutangaza kupotelewa kwa cheti au vyeti kwenye chombo cha habari (gazeti)."Ikithibitika hivyo mamlaka husika kwa mfano Baraza la Mitihani wana utaratibu wa kuwasiliana na Sekretarieti ya Ajira kwa kutoa majina ya watu waliopoteza vyeti nahatimaye huruhusiwa kufanya usaili"
alisema.

MWIGULU NCHEMBA BLOG: VIDEO:N/WAZIRI FEDHA MH:MWIGULU NCHEMBA AKIHITIMIS...

MWIGULU NCHEMBA BLOG: VIDEO:N/WAZIRI FEDHA MH:MWIGULU NCHEMBA AKIHITIMIS...

Italia nje ya kombe la dunia

Uruguay ilifunga bao la ushindi katika dakika za mwisho na kuwabandua washindi mara nne wa kombe la dunia Italia .
Hata hivyo habari kuu kutoka katika mechi hii ilikuwa ni kashfa nyingine ya tukio la Luiz Suarez ‘kung’ata’
Uruguay sasa itacheza dhidi ya Colombia au Ivory Coast jijini Maracana siku ya Jumamosi katika raundi ya pili ya Kombe la Dunia, lakini utata unatarajiwa kuibuka kabla ya siku hiyo.
Italia walitoka uwanjani wakiwa na ghadhabu kutokana na waliyoshuhudia kabla yao kuondolewa katika kombe la Dunia la pili bila kupita kutoka mechi za makundi- kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 1966.
Kocha wa Italia Cesare Prendelli alisema kabla ya mchezo kuwa ilikuwa “mechi muhimu sana katika taaluma yake kandanda” na baada ya kushindwa akapendekeza kujiuzulu.
Mechi hii ilikuwa na hamaki na hasira ndani na nje ya uwanja.
Baloteli hakuvuma katika mechi hii

Mara kwa mara wasaididizi wa refari walilazimika kuzuia zogo kati ya timu hizo mbili, kipenga cha refarii kikatiza mchezo mara nyingi na wachezaji wakachukua muda mrefu wakisukumana walipokuwa wakikimbia na mpira miguuni.
Italia ilikuwa ikihitaji sare tu ili kufuzu. Katika mfumo wa 3-5-2, Italia walikosa mshikamano, mbio na walihatarisha lango lao kila wakati. Lakini iwapo mfumo wao ulitekelezwa ili kuzuia ushambulizi wa Uruguay, mfumo huo ulisaidia.
Andrea Pirlo alimlazimu mlindalango wa Uruguay Fernando Muslera kuondoa mkwaju wake uliotokana na mpira wa adhabu na kuugongesha mlingoti, huku mshambulizi Ciro Immobile akipiga mkwaju nje ya lango.
Edinson Cavani alitaka kuzawadiwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 50 baada ya kuangushwa na Andrea Barzagli, lakini refarii akapuuzilia mbali.
Refarii huyo raiya wa Mexico hata hivyo angebadili mchezo muda mfupi baadae wakati alipomwonyesha Marchisio kadi nyekundu baada ya kiungo huyo wa kati wa Juventus kumchezea vibaya Arevalo katikati mwa uwanja.
Marchisio alinyanyua mguu na kumgonga kiungo huyo wa Uruguay gotini.
Chiellini akimwonesha refarii alikongatwa na Suarez

Suarez alikaribia kufunga bao alipopiga mkwaju wa chini kwa chini ambao Buffon aliudaka .
Utata zaidi ulizuka wakati Suarez na Chiellini walipokumbana katika maeneo ya penalti zikiwa zimesalia dakika tisa kwa mechi kukamilika.
Beki huyo wa Italia alilalamika wakati huo huo kwa refarii kwamba alikuwa ameng’atwa na akajaribu kumwonyesha alama.
Wakati wachezaji wa Italia walipokuwa wakiendelea kulalamika, Uruguay wakapata kona.
Suarez alipiga pasi nzuri naye Godin akafunga bao hilo la ushindi.
Itali walijaribu kila wawezalo ili kupata bao, hadi mlindalango Buffon kujaribu kutafuta bao kutokana na kona waliyopata waitaliano dakika za mwisho, lakini upande wake Oscar Tabarez ukawadhibiti.
Hata hivyo huenda mechi hii isikumbukwe sana. Macho yote, kwa mara nyingine yatamwelekea Suarez.

Tuesday 17 June 2014

dj sek: NAFASI ZA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO ZATANGAZWA MUDA...

dj sek: NAFASI ZA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO ZATANGAZWA MUDA...:           Nafasi za kujiunga na kidato cha nne mwaka 2014  kwa wanafunzi waliomaliza mwaka jana zimetangazwa rasmi muda huu jijini d...

WIZI SIMBA NA YANGA HUU HAPA

Jamii ya wanayanga inampenda sana mtu huyu kwa sababu yuko tayari hata kufilisika kwa ajili ya Yanga. Ni wazi Yanga ikibeba ubingwa yeye hufarijika sana kwa sababu yeye ni Yanga na Yanga ni yeye! Kinachonipa kizunguzungu kuhusu mtu huyu ni kufanya mkakati Yanga ifungwe mabao mengi na Simba ili kiongozi fulani afukuzwe! Kumbe kwa mtu huyu nani anaongoza Yanga ni jambo lenye umuhimu mkubwa mno linapolinganishwa na mafanikio ya timu! Cha kusisimua anapewa hadhi kubwa mtu huyo kwa jinsi alivyopanga "kumuondoa kiongozi wa YANGA ANAYOIPENDA SANA" kwa kipigo kikubwa kwa YANGA ANAYOIPENDA SANA!
Jamii ya wanasimba inawapenda sana watu hawa kwa sababu wako tayari hata kufilisika kwa ajili ya Simba. Ni wazi Simba ikibeba ubingwa wao hufarijika sana kwa sababu wao ni Simba na Simba ni wao! Kinachonipa kizunguzungu kuhusu watu hawa ni kufanya mkakati Simba ifungwe fungwe mechi nyingi za ligi kuu, ikiwezekana ishuke daraja ili kiongozi fulani aonekane hafai! Kumbe kwa watu hawa nani anaongoza Simba ni jambo lenye umuhimu mkubwa mno linapolinganishwa na mafanikio ya timu! Waafrika bwana, tuko zaidi ya bogus! Jamani Yanga na Simba, siku hizi hakuna mapinduzi, hata mkimhujumu kiongozi kwa kuifanya TIMU MNAYOIPENDA SANA IHARIBU VIBAYA SANA kiongozi huyo mtakuwa naye tu mpaka amalize muda wake. Mtapigwa weeeeeee lakini yupo tu.
Naiona mikakati hii dhidi ya viongozi wanaochukiwa ndani ya Yanga na Simba kama mume kukorofishana na mkewe KIPENZI halafu anawatafuta wahuni, anawalipa pesa nyingi wambake mkewe KIPENZI kisha kumwambia "umelala na wahuni vichochoroni,umepoteza sifa za kuwa mke wangu". Sijui hii imekaaje hii.

Monday 16 June 2014

Wiki mbili baada ya kuitwaa rasmi Ikulu ya Malawi, Rais mpya wa nchi hiyo, Profesa Peter Mutharika anatarajiwa kufunga ndoa na Gertrude Maseko Jumamosi ijayo, baada ya kuishi maisha ya ukapera kwa zaidi ya miaka 30.




Mutharika, mdogo wa Rais wa Pili wa Malawi, Bingu wa Mutharika ambaye kwa sasa ni marehemu, alikuwa mume wa Christophine G. Mutharika, raia wa Visiwa vya Carribean na kubahatika kuzaa naye watoto watatu, Monique, Moyenda na Mahopela ambao wote ni wanasheria mahiri kwa sasa nchini Marekani.

Hata hivyo, Mutharika alimpoteza mkewe huyo kwa ugonjwa wa kansa mwaka 1990, hivyo kumfanya asioe kwa muda mrefu, huku akijikita zaidi katika kazi zake za uwakili kwa zaidi ya miaka 40 nchini Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu ya Malawi iliyosainiwa na Mwandishi wa Habari wa Rais, Chikondi Juma imeeleza kuwa ndoa ya Rais Mutharika na Maseko itafungwa Jumamosi ya Juni 21 mwaka huu katika Kanisa la Mtakatifu Michael na Malaika Wote, jijini Blantyre.

Harusi hiyo inafanyika huku Wamalawi wakifanya chereko za kuwasili kwa mara ya kwanza nchini Malawi kwa mabinti wa rais huyo, Monique na Moyenda, siku chache baada ya uchaguzi uliomwingiza Ikulu baba yao akiwa Rais wa Tano wa nchi hiyo.

Taarifa hiyo ya Ikulu imeongeza kuwa, Maseko ambaye alikuwa mbunge wa jimbo la Balaka Kaskazini kwa tiketi ya chama cha Democratic Progress (DPP) cha Mutharika, ni mwandani wa muda mrefu wa Rais mpya na kwamba alikuwa sambamba naye katika kampeni za uchaguzi mkuu uliofanyika Mei 20, mwaka huu na kuhitimisha utawala wa miaka miwili na ushee wa Rais Joyce Banda.

“Baada ya shughuli za kanisani, chereko zitahamia katika familia ya Mutharika iliyopo Ndata katika Wilaya ya Thyolo,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Tukio la kuoa na kuwasili kwa watoto wake, kumeelezwa kumaliza uvumi uliokuwa umeenezwa na wapinzani wake kisiasa kuwa, Mutharika hakuwa mwanamume aliyekamilika.

Uvumi huo ulijibiwa na Katibu Mkuu wa DPP, Chimwemwe Chipungu mara baada ya kuwapokea mabinti hao kwenye Uwanja wa Ndege wa Lilongwe wakitokea Marekani, akisema: “Watu walikuwa na hofu kama Rais Mutharika ana watoto. Ni uvumi wa kijinga. Waliokuwa wakieneza uvumi huo sasa watapata aibu. Rais wetu ana watoto na ni baba wa familia.”

Na Rais Mutharika mwenyewe, wakati wa kampeni aliyasigina maneno ya wapinzani wake kwa kusema ana watoto wenye afya njema, akili timamu na wanasheria maarufu Marekani, mmoja akiwa Profesa katika moja ya vyuo vikuu vya huko.

“Ukiachana na watoto, pia nina wajukuu kadhaa,” alisema Mutharika mwenye umri wa miaka 74 sasa ambaye akiwa mwanazuoni katika masuala ya sheria, aliwahi kufundisha katika vyuo kadhaa, kikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) katika miaka ya 1970.

Kabla ya kuutwaa urais wa Malawi, Profesa Mutharika aliyebobea katika masuala ya sheria ambaye pia ni mwanasiasa mzoefu na mashuhuri, ameshika nyadhifa za uwaziri katika wizara mbalimbali zikiwamo Wizara ya Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, nafasi aliyoishika hadi anaingia katika uchaguzi mkuu hivi karibuni.

WAJUA WANAWAKE WANAVYOSHAMBULIWA NA U.T.I


WAJUA WANAWAKE WANAVYOSHAMBULIWA NA U.T.I 

U.T.I kirefu chake ni Urinary Tract Infection ni maambukizi ya bakteria mbalimbali wanaoshambulia  mfumo wa mkojo, yaani kwenye figo (kidney), kibofu cha mkojo na mifereji inayotoa mkojo (urethra)
Mifereji inayotoa mkojo kwenye figo (ureter) na mfereji unaotoa mkojo nje, mara nyingi bakteria hushambulia sehemu za chini za mfumo wa mkojo yaani urinary bladder na kitaalamu kuitwa bladder infection.
Bakteria hao baada ya kumuingia binadamu hupona mara moja  pindi mgonjwa anapoanza dozi lakini kama wadudu hawa hawatatibiwa vizuri wanaweza kupanda na kushambulia figo na mshipa unaounga sehemu hiyo uitwao renal pelvis na kuleta madhara makubwa, hivyo kusababisha ugonjwa wa figo.

Kuna wadudu wanaotoka kwenye utumbo mkubwa wa binadamu ambao kila binadamu anaishi nao, hawa husaidia kulinda mwili na kitaalamu hujulikana kama  normal flora na huwa ni askari wa mwili.
Vijidudu hivyo hushuka hadi kwenye mlango wa  haja kubwa na kuenea mpaka sehemu za siri. Kama wataingia kwenye mfumo wa mkojo hushambulia sehemu hizo kwani wadudu  hao wanakuwa hawajazoea mazingira ya sehemu za mkojo.

WANAWAKE WANAVYOSHAMBULIWA NA UTI

Mara nyingi wanawake  ndiyo wanaoshambuliwa kirahisi na bakteria wa UTI  kutokana na maumbile yao ya sehemu za siri.
Sababu kubwa ya kushambuliwa kirahisi ni kwa kuwa wanakuwa na mfereji mfupi wa kutoa nje mkojo (shot urethra).
Sababu nyingine inayosababisha UTI ni kutokumywa maji kwa wingi, hivyo kushindwa kwenda haja ndogo mara kwa mara.
Kama mtu ana ugonjwa wa mawe kwenye figo (kidney stone) pia kwa wanaume  wenye ugonjwa wa kuvimba tezi la manii (enlarged prostate), wana uwezekano wa kukumbwa na maradhi haya. U.T.I kirefu chake ni Urinary Tract Infection ni maambukizi ya bakteria mbalimbali wanaoshambulia mfumo wa mkojo, yaani kwenye figo (kidney), kibofu cha mkojo na mifereji inayotoa mkojo (urethra)
Mifereji inayotoa mkojo kwenye figo (ureter) na mfereji unaotoa mkojo nje, mara nyingi bakteria hushambulia sehemu za chini za mfumo wa mkojo yaani urinary bladder na kitaalamu kuitwa bladder infection.
Bakteria hao baada ya kumuingia binadamu hupona mara moja pindi mgonjwa anapoanza dozi lakini kama wadudu hawa hawatatibiwa vizuri wanaweza kupanda na kushambulia figo na mshipa unaounga sehemu hiyo uitwao renal pelvis na kuleta madhara makubwa, hivyo kusababisha ugonjwa wa figo.
Kuna wadudu wanaotoka kwenye utumbo mkubwa wa binadamu ambao kila binadamu anaishi nao, hawa husaidia kulinda mwili na kitaalamu hujulikana kama normal flora na huwa ni askari wa mwili.
Vijidudu hivyo hushuka hadi kwenye mlango wa haja kubwa na kuenea mpaka sehemu za siri. Kama wataingia kwenye mfumo wa mkojo hushambulia sehemu hizo kwani wadudu hao wanakuwa hawajazoea mazingira ya sehemu za mkojo.
WANAWAKE WANAVYOSHAMBULIWA NA UTI
Mara nyingi wanawake ndiyo wanaoshambuliwa kirahisi na bakteria wa UTI kutokana na maumbile yao ya sehemu za siri.
Sababu kubwa ya kushambuliwa kirahisi ni kwa kuwa wanakuwa na mfereji mfupi wa kutoa nje mkojo (shot urethra).
Sababu nyingine inayosababisha UTI ni kutokumywa maji kwa wingi, hivyo kushindwa kwenda haja ndogo mara kwa mara.
Kama mtu ana ugonjwa wa mawe kwenye figo (kidney stone) pia kwa wanaume wenye ugonjwa wa kuvimba tezi la manii (enlarged prostate), wana uwezekano wa kukumbwa na maradhi haya.

Maximo hawezi kuwa mwarobaini wa Yanga.


MIAKA miwili iliyopita, Chama cha Soka Afrika Kusini (SAFA) kilimwajiri Gordon Igesund kuwa Kocha mkuu wa Bafana Bafana kwa mkataba wa miaka miwili na kukabidhiwa majukumu makubwa mawili.

Jukumu la kwanza lilikuwa ni kuhakikisha timu yake inatinga katika hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) iliyofanyika hapo Bondeni mwaka 2013.

Jukumu la pili ilikuwa ni kuisaidia timu kufuzu Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 zinazoendelea sasa nchini Brazil.

Kwa bahati mbaya sana, Bafana Bafana iliishia hatua ya robo fainali ya mashindano ya Afcon 2013, pia ilishindwa kukata tiketi ya Kombe la Dunia 2014. Kwa mtaji huo, Kocha Igesund alishindwa kutimiza yale yote ambayo aliagizwa na waajiri wake.

Wiki iliyopita, SAFA imetangaza kuwa haitamuongeza mkataba Igesund mara mkataba wake wa sasa utakapomalizika mwishoni mwa mwezi huu. Sababu za uamuzi huo ni kuwa Kocha huyo aliyeaminiwa sana na Wasauzi wakati alipoajiriwa, ameshindwa kutimiza kwa ukamilifu majukumu aliyopewa na waajiri wake.

Turejee nyumbani. Timu ya soka ya Yanga imetangaza kusudio la kumwajiri Marcio Maximo kuwa kocha mkuu kuanzia msimu ujao. Kusudio hilo limepokelewa kwa vifijo na wapenzi wa klabu hiyo kubwa nchini.

Maximo anaaminika na Wanayanga kuwa atakuwa mwarobaini wa timu kuleta vikombe vingi Jangwani. Anaaminika na Wanayanga kuwa atasaidia kupandisha kiwango cha uchezaji kwa timu hiyo ili kufikia kiwango halisi cha kimataifa kama jinsi alivyofanya kwa Taifa Stars enzi zake.

Pia, anaaminika kuwa atarejesha mshikamano wa Wanayanga wote na mapenzi makubwa kwa timu yao kama alivyofanya wakati akiifundisha Stars. Hayo ndiyo matarajio makubwa ya wapenzi na mashabiki wa timu hiyo wanaoungojea kwa hamu ujio wa Maximo kama kweli atakuja.

Swali moja ambalo nimekuwa nikijiuliza mara baada ya Yanga kuja na kusudio hilo ni kwamba, hivi kweli Yanga imewahi kuwa na tatizo la makocha? Hivi ni kweli kuwa kufanya vibaya kwa Yanga kwenye michuano ya kitaifa na kimataifa kunatokana na tatizo la kocha au ni matatizo mengine?

Tangu Yanga ianze kubadili makocha kuanzia kwa Srejodevic Milutin ‘Micho’, Sam Timbe, Dusan Kondic, Tom Saintfiet, Ernest Brandts na wengineo, sijawahi kuona kocha aliyekuwa kimeo kiasi cha kutakiwa kutimuliwa kazi haraka. Makocha wote walikuwa na uwezo mkubwa na historia nzuri, ingawa wote waliishia kutimuliwa mapema.

Sababu kubwa ni kwamba, makocha wote hawa waliingia Yanga bila kupewa hadidu za rejea na matokeo yake wametimuliwa bila kuwa na makosa yoyote. Makocha hawa walitakiwa kukabidhiwa majukumu kama SAFA walivyomkabidhi Igesund. Kushindwa kwao kutekeleza majukumu waliyopewa, ingekuwa ndiyo tiketi yao ya kutimuliwa kazi, labda itokee huruma ya mwajiri wako. Lakini haikuwa hivyo kwa Yanga!

Makocha wengi wa Yanga wametimuliwa kutokana na ama kuwa wakweli kupita kiasi, na wengine kwa kushindwa tu kuifunga Simba. Brandts alitimuliwa huku timu yake ikiongoza ligi, kisha akaajiriwa kocha aliyeishusha timu na kumaliza ligi ikiwa nafasi ya pili. Hapo ni kocha yupi bora kati ya Brandts aliyetimuliwa na huyo aliyemrithi? Nauliza tu.

Maximo anakuja kwa staili ile ile ya watangulizi wake. Kutokana na hali hiyo na kwa mfumo wa uongozi wa sasa, hata wakija akina Maximo kumi, Yanga itabaki kuwa Wahapahapa tu!


Mwanaspoti

Kamati kuu ya Uchaguzi Simba yamuondoa Wambura katika mbio za kugombea Urais wa Simba SC.

Kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club, ilifanya mkutano wake kawaida tarehe 15 Juni 2014 kujadili mambo mbalimbali ambayo yanayohusu uchaguzi mkuu wa Simba Sports Club ambao umepangwa kufanyika tarehe tarehe 29 Juni 2014. Kamati ya Uchaguzi ya Simba sports Club inapenda kuujulisha umma, hususan wapenzi wa Simba Sports Club mambo yafuatayo:

1. Kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club, kwa mujibu wa Ibara ya 10(6) ya Kanuni za uchaguzi za TFF toleo la mwaka 2013, ndiyo chombo pekee chenye mamlaka ya kutangaza, kubadilisha, kusimamisha au kufuta tarehe ya Uchaguzi ya Simba Sports Club. Kwakuwa Kamati haijafanya hivyo, wala hakuna mdau yoyote aliyeleta hoja ya kusimamisha uchaguzi, tunawajulisha kuwa uchaguzi wa Simba Sports Club upo pale pale kama ambayo Kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club ilivyopanga. Maandalizi ya uchaguzi huo yanaendelea vema na Uchaguzi utafanyika tarehe 29 Juni 2014 kama ilivyopangwa hapo awali.

2. Kamati imesikia kupitia vyombo vya habari kuwa TFF imesimamisha uchaguzi wa Simba Sports Club mpaka hapo Kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club itakapoteua Kamati ya Maadili. Kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club inapenda kusema yafuatayo:

i. Mamlaka ya kusimamisha uchaguzi ni kazi ya Kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club kwa mujibu wa ibara 10 (6) ya Kanuni za Uchaguzi, 2013
ii. Kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club ilipoanza mchakato wa uchaguzi ilitoa tamko kuwa: “kwasababu Simba Sports Club haina kanuni za Uchaguzi, Kamati ya Rufaa ya uchaguzi, wala Kamati za Maadili kwa mujibu wa ibara za 16 (e) na (f) ya Katiba ya Simba Mwaka 2014, vyombo husika vya TFF vitatumika”. Kulikuwa hakuna pingamizi toka kwa mtu yoyote juu ya kauli hiyo, ikiwemo TFF.
iii. Tarehe 26 Mei 2013, Rais wa TFF aliialika Kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club katika chakula cha mchana. Katika mkutano huo, kauli ya aya (ii) hapo juu ilirejewa na Kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club ilikabidhi rasmi mchakato mzima wa uchaguzi na kutoa ufafanuzi kuwa kamati husika za TFF zitahusika, jambo ambalo halikupingwa na TFF.
iv. TFF iliruhusu Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF kusikiliza Rufaa za uchaguzi za Simba, hivyo basi haiwezi kuzuia Kamati zake nyingine kusikiliza Masuala ya kimaadili. “Estopel” inawazuia TFF kufanya hivyo sasa.
v. Wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club, isipokuwa watatu tu, ni wagombea katika uchaguzi huu. Na hao watoto tayari wapo kwenye Kambi za Kampeni za uchaguzi hii ambazo zipo bayana kabisa. Kuiagiza Kamati ya Utendaji ya Simba iunde Kamati ya Maadili kusikiliza kesi za maadili dhidi yao wenyewe ni kukiuka msingi wa haki ya asili (natural justice). Ni dhahiri kuwa haki haiwezi kutendeka kwa wajumbe wa kamati ya utendaji ya Simba Sports Sports Club, ambao ni watuhumiwa katika masuala ya maadili, wachague majaji wa kuwahukumu. Hapo haki haitatendeka.

Ifahamike kuwa, baada ya Kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club kuteua Kamati ya uchaguzi ya Simba Sports Club, Kamati hiyo haina mamlaka tena ya kujadili, kuingilia au kuteua chombo kingine kufanya shughuli zinazohusu uchaguzi ukizingatia kuwa wajumbe wake ni wagombea.

vi. Katika Uchaguzi Mkuu wa TFF wa Mwaka 2013, ambao ulimuingiza Jamal Malinzi Madarakani, FIFA walikuja, wakongea na pande zote na hatimaye, walisema kuwa; “tunapendekeza kuwa uchaguzi mkuu usimame ili kuunda kamati mbalimbali”. Mapendekezo hayo yalipokelewa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Bw. Deo Lyato, na hatimaye ni Kamati ya Uchaguzi ya TFF ndio iliyotangaza kusimamisha Uchaguzi na sio Sepp Blatter.

vii. Kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club ni Kamati huru ambayo haipaswi kuingiliwa na Chombo chochote kile. Ili kulinda uhuru huo, tunalazimika kukanusha matamshi ya TFF kuhusu kusitisha Uchaguzi Mkuu wa Simba Sports Club.

3. Malalamiko ya Kimaadili Kupelekwa FIFA.
Kwa mujibu wa Ibara ya 11 (9) ya Kanuni za Uchaguzi za TFF, 2013, inatoa mamlaka kwa Kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club kupeleka masuala ya maadili katika kamati ya maadili ya TFF. Tarehe 9 Juni 2014, Kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club ilipeleka Masuala ya Maadili katika Kamati ya Maadili ya TFF. Kwakuwa TFF imekataa kusikiliza masuala ya maadili ambayo yanakiuka Kanuni za maadili, Katiba za Simba, TFF na FIFA, Kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club, itapeleka Masuala ya Maadili FIFA ili haki itendeke.

4. Kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club ilijadili kuhusu vitendo vya wagombea kupiga kampeni kabla ya muda wa kampeni ulioruhusiwa. Kwa mujibu wa Mchakato wa Uchaguzi ya Simba Sports Club, muda wa kampeni unaanza tarehe 24 -28 Juni 2014. Hapo awali kamati ilibaini kuwa wagombea wawili wa nafasi ya urais; Michael Richard Wambura na Evans Aveva walifanya vitendo vya kampeni siku ya kuchukua na kurejesha fomu za kugombea. Tarehe 25 Mei 2014, Kamati iliwapa ONYO KALI la maandishi wagombea hao na kuwataarifu kuwa hatua kali zaidi zitachukuliwa dhidi yao, ikiwemo kuondolewa katika kinyang’anyiro cha uchaguzi.

Baada ya Kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club kumuondoa Bw. Michael Richard Wambura katika kinyang’anyiro cha uchaguzi Mkuu wa SImba Sports Club, Bw. Wambura aliitisha Mkutano na waandishi wa habari, aliitukana Kam
ati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club, na kutoa matamshi ambayo ni Kampeni.

Baadaya ya Kamati ya Rufaa ya uchaguzi ya TFF kumrejesha Bw. Wambura katika Kinyang’anyiro cha Uchaguzi Mkuu wa Simba, Bw. Wambura aliitisha tena mkutano wa waandishi wa habari, aliisifu kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF, kwa mara kwanza aliisifu Kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club na kutoa matamshi ambayo ni wazi kuwa ni kampeni. Baadhi ya Matamshi aliyoyatoa kupitia vyombo vya habari ni kama ifuatavyo:

i. “Simba Sports Club inahitaji zaidi wadhamini na sio wafadhili”
ii. “Wafadhili kazi yao in kutoa fedha mfuko wa kushoto na kuepeleka mfuko wa kulia”
iii. “Simba ilikuwa na viwanja vitatu lakini kimoja kimeuzwa na wajanja na vimebaki viwili tu”
Kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club ilitafakari matamshi hayo, na kubaini kuwa hiyo ni kampeni ya waziwazi wakati muda wa kampeni bado haujaanza.
Kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club ililipa jambo ili uzito wa kipekee kwasababu Mkosaji amekuwa na tabia ya kurudia kosa hilo hata baada ya kupewe onyo la maandishi.

HIVYO BASI:
Kwa mujibu wa mamlaka ya kikanuni, hususan Ibara za: 6 (1) (a) – (g); 6 (1) (L) na 14(3) za Kanuni za uchaguzi za TFF – 2013, Bw. Michael Richard Wambura anaondolewa Katika Kinyang’anyiro cha Uchaguzi wa Simba Sports Club, 2013, kwa kosa la kurudia kufanya kampeni kabla ya muda wa kampeni ambao umepengwa,".

JUA JINSI YA KUMTAMBUA MPENZI ALIYEKUSALITI MUDA MFUPI ULIOPITA.

RATIBA YA GHAFLA

Rafiki zangu, ukishaanza kuwa na wasiwasi na mpenzi wako kwamba huenda anataka kukusaliti, jambo la kwanza kabisa unalotakiwa kukumbuka ni sehemu aliyokuambia amepitia/anakwenda kama ilikuwa katika mipango yake au amefanya safari ya kushtukiza.
Hii ni dalili ya kwanza kabla hata hamjakutana nyumbani; “Sorry baby, kuna sehemu napitia mara moja, nitachelewa kidogo kurudi nyumbani,” kauli kama hii iangalie sana.
Mwingine anaweza kupiga simu na kusema: “Mume wangu, bosi ametupa ofa ya dina wafanyakazi wote, kwa hiyo nitachelewa kurudi nyumbani, samahani sana dear.”
Kauli hizo mbili ni alama ya kwanza katika kushibisha hoja yako ya kusalitiwa kama ni kweli atakuwa amefanya hivyo. Kumbuka kwamba, si lazima kila anayesema amepata dharura amesaliti.

ANAKWEPA KUWASILIANA

Mtu huyo ambaye ameshatoa taarifa kwamba amepata dharura, utashangaa hataki kuwasiliana na wewe. Pengine ukimpigia simu, anaweza asipokee na kama akipokea anaweza kukujibu: “Nitakupigia baadaye, samahani sipo sehemu nzuri.”
Unaweza kumwandikia meseji lakini pia asijibu. Wapo wengine vichwa ngumu zaidi, ambao wao kuacha kupokea simu na kujibu meseji si vitu muhimu sana, wanazima kabisa! Ukiona dalili hii, basi ujue unasalitiwa.

UCHANGAMFU KUPITILIZA

Pamoja na mambo hayo hapo juu, lakini mwenzi huyu akirejea nyumbani, huwa mchangamfu kupitiliza. Ana maneno mengi, anaanzisha mijadala ya ghafla na kuifunga mwenyewe. Atajifanya anataka kufanya mambo mengi kwa ajili yako.
Ahadi zake zinakuwa nyingi za ghafla na nyingi zipo wazi kabisa kwamba si rahisi kuzitekeleza. Alama hii ni kati ya zile 10 zinathibitisha kwamba ndani ya saa 24 umeibiwa mali yako.

UPOLE KUPITILIZA

Kinyume cha uchangamfu ni upole, kama mwenzi wako ametoka kimapenzi na patina mwingine kwa ile hofu yake moyoni, anaweza kuwa mpole kupitiliza. Anafanya hivyo kwa lengo la kutafuta huruma.
Hana sababu ya kuwa mpole, lakini anaweza kutumia ngao hiyo, ili maswali utakayomuuliza yawe kuhusu upole na ukimya wake, usahau mambo ya kuhisi kuwa umesalitiwa. Hata hivyo, majibu yake yanaweza kuwa ya mkato sana: “Sijisikii vizuri, siku yangu haikuwa nzuri kabisa leo. Kuna mtu nimetibuana naye ofisini, amenichanganya kabisa.”
Alama hii ni moja ya sababu zitakazokufanya uendelee kumchunguza katika hatua zinazofuata ili mwisho ugundue kuwa umesalitiwa au ni wasiwasi wako tu.

UGONJWA WA GHAFLA

Katika kukwepa usumbufu wa maswali mengi, mwingine huamua kujifanya anaumwa. Atarudi akiwa mkimya kuliko kawaida, ukimwuliza atakujibu kuwa anaumwa. Kama mpenzi wake, anajua wazi kuwa hutakuwa na muda wa kuanza kuhisi usaliti badala yake utamjali na kuuliza hali yake.
Mgonjwa huyu kwa kawaida huwa haumwi magonjwa siriasi, sana sana atakuambia hajisikii vizuri, kichwa kinamgonga au moyo unaenda mbio. Ukizungumza kuhusu suala la hospitali atakataa akidai hana hali mbaya sana. Mara nyingi hupenda kukimbilia kitandani, akitaka kupumzika.
Anafanya hivyo kwa sababu anakwepa aibu ya kukutanisha uso wake na wako. Ukitaka kwenda kumnunulia dawa za maumivu atakujibu: “Nimeshameza panadol baby.” Mwenzi wa aina hii unatakiwa umtilie mashaka, maana inawezekana ametoka kufanya kitu kibaya.

MAJIBU TATA

Mpenzi ambaye ametoka kukusaliti huwa hapendi kuulizwa maswali mengi, ukimwuliza majibu yake huwa tatanishi sana. Kwa kuwa ameshasingizia kwamba anaumwa, hivyo atafika na kulala moja kwa moja.
Ukitaka kujua zaidi kuhusu kuugua kwake au dharura aliyoipata iliyosababisha achelewe kurudi nyumbani, hukosa majibu yanayoeleweka. Wakati mwingine anaweza kujisahau na kukupa jibu ambalo linapingana na maelezo yake ya awali. Ukiona hivyo ujue kuna namna.

HATAKI FARAGHA

Kwa kuwa tayari ameshatoka kwa mtu mwingine, huhofia sana kukutana na wewe faragha. Kama tulivyoona katika vipengele vilivyopita, hutengeneza mazingira ya kukufanya msikutane kimwili, hofu yake ikiwa ni kukuficha usigundue mchezo wake mchafu.
Kisingizio cha kuumwa, bila shaka ni kikubwa na kitakufanya ushindwe kuwa na mhemko wa kimahaba, lakini kurudi nyumbani akiwa amekunja ndita au mpole kupitiliza, tafsiri yake ni wewe kuogopa au kuhamisha hisia zako kutoka kwenye mapenzi na kuanza kumfikiria yeye kama yeye.
Kwa vyovyote vile, kama ni mwenzi wako wa muda mrefu, zipo alama nyingi zitakazoweza kukufanya ujue kuwa ametoka nje, kwanza ni vyema kumkazania kukutana naye faragha. Hata kama atasingizia anaumwa, ng’ang’ania kukutana naye, maana hapa ndipo penye ukweli mkubwa zaidi.
Mchunguze anavyokupokea, halafu pima uwajibikaji wake. Huwa mvivu na asiyetaka kutoa ushirikiano. Anaweza kuishia kulalamika kuwa hajisikii vizuri na kusisitiza mhairishe zoezi hilo.
Mpenzi msomaji, njia unayopita kila siku unaijua. Sehemu yenye makorongo unaifahamu, yenye matuta pia utatambua, hata yenye makorongo yenye maji yaliyosimama pia unaijua vyema, sasa ukikutana na tofauti yoyote katika barabara unayoitumia siku zote, maana yake tingatinga limepita.

ANAKWEPA KUSOGELEWA

Akifika tu nyumbani, atahakikisha hupati nafasi ya kuwa naye karibu. Hataki kabisa kusogelewa. Hapo anakimbia vitu vitatu;
Kwanza kabisa, inawezekana huko alipotoka alitumia manukato tofauti na aliyotoka nayo nyumbani asubuhi.
Pili, manukato ya sabuni mpya aliyotumia, anaogopa usiyasikie, tatu, kila mtu ana harufu yake, unapokaa na mtu kwa ukaribu hasa faragha kwa saa mbili au zaidi, kila mmoja huhama na harufu ya mwenzake.
Kwa kuwa wewe unaitambua vyema harufu ya mpenzi wako, atahofia kukusogelea maana utashtukia. Mwisho kabisa, hata kama atakuwa amekwepa yote hayo, labda hajaoga, hajatumia manukato mengine, bado utaweza kumkamata kwa harufu ya manukato, sabuni au mafuta aliyotumia mtu aliyekuwa naye.
Kukwepa kukusogelea, tafsiri yake ni kwamba hataki usikie harufu ya tofauti kutoka kwake, maana anajua alichokifanya. Jiulize, kama kila siku huwa mnapokeana kwa mabusu na kukumbatiana, kwanini safari hii anakukwepa?

ANAKIMBILIA BAFUNI

Akifanikiwa kukuzuga katika kipengele kilichopita, basi safari yake huishia bafuni. Ataenda haraka na hatataka kwenda na wewe maana kuna kitu anajaribu kukuficha. Wengi wanaamini (kuna ukweli kwa asilimia chache) baada ya kuoga wanaweza kupoteza ushahidi wa kutoka nje ya ndoa/wapenzi wao.
Utakapomruhusu aoge, kwanza atatumia sabuni ya siku zote, ambayo anaweza kuitumia kwa wingi awezavyo ili kuficha ushahidi. Atajisafisha zaidi nyeti zake ili usijue kilichotokea muda mfupi.
Akitoka bafuni lazima atakimbilia kwenye meza ya kujipambia kisha hapo atajimiminia manukato ili kuzima kabisa ushahidi ambao ungeweza kumuumbua. Jiulize, kama kila siku huwa mnaoga pamoja, kwanini amekuja ghafla na kukimbilia bafuni bila wewe?

WASIWASI MWINGI

Atakuwa mwenye wasiwasi mwingi sana, hata kama akikubali kukutana na wewe faragha, ushirikiano huwa hafifu. Mwoga kupitiliza na muda wote huwa anahisi kwamba hatakufikisha salama safari yako.
Wasiwasi wake hauishii hapo, hata kupeana mikono tu na kukutanisha macho, kutakuonesha jinsi alivyo na wasiwasi. Si kama anapenda hali hiyo, ila anazidiwa na hisia za usaliti kwa kuwa anajua alichokifanya muda mfupi uliopita.

Kama utavifuatilia vipengele hivyo kwa makini, ni rahisi sana kumkamata mwizi wako. Acha papara, chunguza taratibu, ukiona angalau kuna nusu ya hizi nili zokupa hapo juu, ujue wazi kuwa unaibiwa tu.

Yafuatayo baadhi ya mambo ambayo unapaswa kuyafanya baada ya kubaini kuwa mpenzi wako amekusaliti.


Kubaliana na kilichotokea


Kama keshakusaliti ni tukio ambao limeshatokea na haliwezi kufutika. Kubali kuwa umetendwa, huzunika lakini mwisho liache lipite ili uweze kujipanga upya.

Usijilaumu

Wapo ambao wakishasalitiwa hujuta kukubali kuingia kwenye uhusiano na watu waliowatenda. Utamsikia mtu akisema “najuta kumkubalia awe mpenzi wangu”. Kujilaumu kwa namna hiyo hukutakiwi kwani kutakufanya uzidi kunyong’onyea.

Jitoe

Jifanye kama vile aliyesalitiwa siyo wewe bali ni rafiki yako kisha jiulize ungemshaurije? Ushauri ambao ungempa basi uchukue kisha uufanyie kazi.

Pima ulivyoathirika

Je, kitendo cha mpenzi wako kukusaliti kimekukosesha imani juu yake? Kama ni hivyo, unadhani una sababu ya kuendelea kuwa naye au unahisi madhara aliyokupatia huwezi kumvumilia?

Mweleze ukweli

Kwa vyovyote utakavyoamua ni lazima umweleze ukweli juu namna alivyokuumiza kwa usaliti wake. Hata kama utampa nafasi nyingine lazima ajue jinsi alivyokuumiza ili iwe changamoto kwake.

Chunguza kwa nini kakusaliti

Usiliache likapita hivi hivi, unatakiwa kujua sababu ya yeye kukusaliti. Je, kuna ambacho anakikosa kwako au ni tamaa zake tu? Jibu utakalolipata litakusaidia katika maisha yako ya kimapenzi.

Usikubali akulainishe

Huenda huyo mpenzi wako ni msanii na anaweza kukulainisha kwa maneno ambayo yanaweza kukufanya ukalichukulia tukio hilo kiurahisi. Kuwa na msimamo na eleza hisia zako kwa uwazi.

Amua kusuka au kunyoa

Likishatokea hilo jaribu kuzungumza na moyo wako. Uamuzi wa kuendelea kuwa naye au kumuacha uuchukue bila shinikizo. Hata kama kakuumiza, kama unadhani unaweza kumpa nafasi nyingine mpe ili usije ukajuta baadaye kwa kumkosa lakini kama unaona moyo wako unamkataa, muache.

Msamehe

Kwa uamuzi wowote utakaochukua ni lazima uwe tayari kumsamehe ili kuliondoa dukuduku lako rohoni. Kutokumsamehe kunaweza kukufanya ukawa unaumia kila wakati na kukosa amani.

Iwe fundisho kwako

Chukulia tukio hilo kama fundisho kwako. Huenda wewe ndiye uliyechangia kusalitiwa, kama ni hivyo badilika ili yasije yakakukuta kama hayo utakapokuwa na mwingine. Pia kama kusalitiwa kumetokana na kutoridhika kwa mpenzi wako, kuwa makini wakati wa kuchagua mwingine wa kuwa naye.

HUYU NDIYE BILIONEA WA KITANZANIA BAKHRESA SOMA HISTORIA YAKE.

Katika makala haya tutakuletea uchambuzi wa wajasiliamali wenye mafanikio Afrika Mashariki historia yao kimaisha, kiwango chao cha elimu tabia binafsi, maadili na kanuni wanazozishikilia, nidhamu, utajili
wanaomiliki, mahusiano na maisha ya kifamilia. Vilevile tutaangalia namna walivyo jenga biashara imara, namna wanavyokabiliana na changa moto mbalimbali, mchango wao katika jamii, mawazo, maoni na ushauri wao kwa wajasiliamali wanaochipukia.Katika toleo hili tunakuletea mjasiliamali mwenye mafanikio afrika ya mashariki ambaye alianza na biashara ya mabaki ya mazao ya baharini, kushona viatu, biashara ya viazi na baadae mgahawa. Leo hii ni milionea anayemiliki rasilimali mbalimbali za viwanda, pamoja na vyombo vya usafiri ndani na nje ya nchi. M jasiliamali huyu si mwingine bali ni Said Salim Awadh BakhresaSaid Salim Bakhresa alizaliwa mwaka 1949 mjini Zanzibar, alisoma elimu ya msingi hadi alipofikia umri wa miaka 14 ambapo aliacha shule kutokana na maisha ya familia kuwa magumu hivyo kujiingiza katika biashara ili aweze kuhudumia familia katika mahitaji kama chakula baada ya baba yake kukabiliwa na madeni. K atika miaka ya 1960, wakati Tanzania ilipokuwa nchi ya kijamaa na Kenya ikifuata siasa za kibepari, Bakhresa aliweza kununua mabaki ya mazao ya baharini kama, mifupa na magamba ya viumbe wa baharini na kuyauza Mombasa. Kutokana na tofauti ya kifedha iliyokuwapo wakati huo, aliweza kununua ngozi za viatu kutoka Kenya na kuzitumia kushonea viatu hapa Tanzania.Badae alifanya biashara ya viazi, mikate na ice cream. K atika miaka ya 1970,s Bakhresa alifungua na kuendesha biashara ya mgahawa. M gahawa huu alinunua kutoka kwa mgeni wa kihindi ukiwa na jina la AZAM,jina ambalo analitumia kama nembo(brand) ya bidhaa zake kwa sasa. K atika miaka ya 1990 s alinza uwekezaji katika v! iwanda. Kwa sasa kiasi kikubwa cha mchele na bidhaa za nafaka zinatoka katika kampuni ya Bakhresa Group iliyopo kipawa (flour Mill) .Nchi jirani ya Rwanda kwa mfano, inategemea tani 120,000 za unga wa wangano kwa mwaka kutoka kwa kampuni ya Bakhresa.
Said Salim Awadh Bakhresa ni mwenykiti wa makampuni ya Bakhresa Group, ni Mtanzania anayemilki viwanda vingi vinavyozalisha bidhaa za vyakula zinazouzika ndani na nje ya nchi. P ia kokote jijini Dar-es- salaam na mikoani, bidhaa za AZAM utasikia zikitajwa. Azam ni nembo(brand) ya bidhaa zinazotengenezwa kupitia makampuni ya Bakhresa, Azam ni neno la kihindi linalomaananisha ukubwa. Bakhresa amejijengea jina kibiashara kwani si ajabu kusikia watu wakisema, Amka na Azam, shinda na Azam au sheherekea na Azam. Tafasili yake ni kwamba katika maisha yetu ya kila siku, tunatumia bidhaa za Azam kwa kiasi kikubwa sana. Asubuhi tuamkapo tunapata kifungua kinywa kwa vitafunwa vya Azam. M chana tunakula ugali, wali, au chips na tunakunywa maji na juice kutoka Azam. J ioni kama utakula tambi au kunywa soda n.k . u naweza kujikuta bado unatumia bidhaa za Azam. Hivyo ndivyo wimbo wa bidhaa za Azam unavyo imbwa katika maisha ya Watanzania kila siku.
Kulingana na jarida la forbes Bakhresa ndiye anayeaminika kuwa tajiri namba moja nchini Tanzania, akishikilia nafasi ya 30 ya matajiri Afrika. M apato yake kwa mwaka ni zaidi ya dola za Kimarekani $520 milioni. Bakhresa ana wafanyakazi zaidi ya 2,000 wenye ajira rasmi.
Bakhresa ni mtu mashuhuri katika harakati za mapinduzi na maendeleo ya viwanda Tanzania Bara na Visiwani. jasiliamali huyu ameweza kujizolea sifa kemkem ndani na nje ya nchi, si tu kutokana na wingi wa bidhaa zake bali pia ni kutokana na bidhaa zake kukidhi viwango vya ubora kimataifa.
Mjasiliamali huyu amejijengea umaarufu mkubwa katika biashara kwa takribani miongo mitatu sasa. Ameweza kujenga timu imara ambayo inasimamiwa na wakurugenzi makini ambao ni watoto wake mwenyewe. Bakhresa Group ina matawi katika nchi sita ambazo ni,. Rwanda, Burundi, Uganda, Malawi, Zambia na Msumbiji. Amejikita zaidi katika usindikaji wa vyakula. Ana viwanda vya kusaga unga wa ngano na mahindi, viwanda vya ukoboaji wa mchele, uandaaji wa vyakula kama mikate,chapatti, vinywaji kama maji (Uhai) , juisi za matunda na soda, pamoja na ice cream. Pia ana kiwanda cha vifungashio vya bidhaa mbalimbali, biashara ya mafuta ya magari na mitambo. Vilevile anazo boti za usafilishaji abiria ambazo hufanya safari zake katika Bahar i ya Hindi. H ali kadhalika, anafanya biashara ya usafirishaji mizigo (azam logistics). Katika michezo ,Bakhresa anamiliki timu ya mpira wa miguu ijulikanayo kwa jina la Azam Footbal Club ambayo imefikia kiwango cha kucheza ligi kuu Tanzania bara.

Unapomzungumzia Said Salim Bakhresa unamzungumzia mtu wa aina yake katika Tanzania, ni mtu anayesemkana kusimamia maono yake na kuhakikisha yanatimilika kikamilifu. Anauzoefu mkubwa katika usimamizi wa biashara , ni mtu anaye fanya tafiti juu ya maendeleo ya viwanda na masoko katika kutambua mahitaji ya watu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.
Anatumia mbinu mbalimbali katika kuhakikisha bidhaa zake zinaliteka soko la ndani na la nje ya nchi. Licha ya kutangaza bidhaa zake kupitia redio na televisheni, anapata fursa ya kujitangaza kupitia timu yake ya mpira wa miguu anayoimiliki(Azam Football Club) hivyo anatangaza bidhaa zake kupitia michezo. Vilevile anawatumia wachuuzi au Machinga katika kutangaza bidhaa zake mfano Ice cream. Pamoja na mafanikio makubwa aliyonayo , mfano kumiliki na kuendesha biashara mbalimbali ndani na nje ya nchi , bado kuna vikwazo na changamoto mbalimbali anazokabiliana nazo ili kufikia malengo yake. Kwa mfano sera za biashara zisizo simamiwa vizuri katika ushindani wa masoko, gharama za teknolojia katika uzalishaji n.k.
Katika suala zima la kupanga , kudhubutu na kufanya ni vitu vya msingi katika kufikia mafanikio. B akhresa ni mtu anayehamasisha Watanzania wasiogope kujifunza kwa vitendo, kwani wengi huhofia changamoto zinazoweza kusababisha, anguko katika biashara lakini mjasiliamali anapaswa kujiamini katika mawazo yake na kujiwekea mipango mathubuti. Ka zi ya ujasiliamali inahitaji ubunifu kwa kiasi kikubwa katika kuweza kubaini na kuibua fursa zilizopo na hata kuweza kukabiliana na changamoto zake.
Kwa sasa bado Bakhresa anaendelea kutanua wigo wa biashara katika kuweza kufikia nchi nyingi zaidi duniani. Hata hivyo anaamini kwamba bidhaa zake bado hazijatosheleza soko la ndani . Bado anazitizama fursa zilizopo katika soko la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Hivyo basi anajitahidi katika kuboresha bidhaa zake zaidi ili kuhakikisha zinakuwa na ubora unaotakiwa na hatimaye kushikilia soko la kitaifa na kimataifa.
Pia anatoa ushauri kwa Watanzania, hususani vijana, wajitahidi kufikili vizuri na kutazama fursa zilizopo nchini kwa kuanzisha miradi mbalimbali ambayo itawainua wao kiuchumi , ili hatimaye kuondokana na umaskini unaolikabili taifa letu.

KAMA UNAPENDA KUSHIRIKI SHINDANO LA BIG BROTHER MWAKA HUU BASI HII INAKUHUSU ILI UJUE UTARATIBU NA LINI NA WAPI UENDE.

Kampuni ya MultiChoice Africa inayoandaa mashindano ya Big Brother Africa imetangaza tarehe ya usaili wa shindano hilo mwaka huu katika nchi mbalimbali za Afrika.
Waandaaji hao wameitaja nchi ya Rwanda mwaka huu kuwa miongoni mwa nchi zitakazokuwa na washiriki katika shindano hilo mwaka huu ambapo mshindi ataondoka na kibunda cha $300,00.
Nchi zitakazoshiriki mwaka huu ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Afrika Kusini, Sierra Leone, Nigeria, Botwasana, Malawi, Namibia, Ghana, Zimbabwe na Ethiopia.
Kwa Tanzania, usaili utafanyika July 11 na July 12 jijini Dar es Salaam (New Africa Hotel).
Ni muda wa kuona sarakasi nyingine na kuibua mengi mapya yakiwemo mahusiano ambayo mengine huwa na nguvu hata baada ya kumalizika kwa shindano hilo.
Mwaka jana mshiriki wa Namibia, Dillish Mathews aliibuka mshindi wa msimu huo ulipewa jina la The Chase.
KWA KUPATA STORY NA MAPICHA ZAIDI BOFYA HAPA
-tanzanianewz

Saturday 14 June 2014

Madhara ya simu za mkononi katika uzazi kwa wanaume.

Tumekua tukisikia mUda mrefu kuhusu madhara ya simu kwa uzazi wa mwanaume. nimeona ni-copy na ku-paste habari hii ya leo kama ilivyo nisije ongeza neno.

Carrying a mobile phone could significantly affect a man's fertility, scientists have suggested
Radiation from the phones could cut the number of sperm a man has by a third, researchers from the University of Szeged, Hungary, said.The research, presented to the European Society of Human Reproduction and Embryology (ESHRE) meeting in Berlin, studied over 200 men.

But other experts have criticised their research, saying it did not take any other aspects of the men's lives into account.The Hungarian study is the first to look at how electromagnetic radiation from mobiles could affect sperm.

The men who had their phone on standby throughout the day had about a third less sperm than those who did not. High numbers were found to be swimming abnormally, reducing the chances of fertilisation.

The researchers say their findings suggest that mobiles do have a "negative effect" on male sperm and fertility.But other experts at the ESHRE conference said the Hungarian study did not allow for other factors which could have affected the men's fertility.

Professor Hans Evers, the former chairman of the European Society of Human Reproduction, said it "raises more questions than it answers".Other factorsHe said the study had not taken into account the "many potential confounding factors which could have skewed the results".

These could include whether the men who had affected sperm came from a different social class or age range than those who did not.It was also unclear whether the men were carrying their phones in their trouser pockets, close to their bodies, or in briefcases away from them.

He said: "These factors would have a considerable effect on the outcome of the research."Professor Evers added: "Mobile phones are related to a certain lifestyle and they may be related to stress, to a heavily occupied business man rushing around from one office to another, having a lot of concerns in the life; there's all kind of things."

And it is known that this decreases sperm counts and if you compare that to farmers living in the open air, on the land and not carrying a mobile phone at all you can explain the difference by completely other ways than the use of a mobile phone.

"He said the only way to get a clearer picture would be for scientists to carry out a study which was carefully designed only to look at the effect of mobile phones on sperm.

Heavy use of mobile phones may damage men's fertility,

A study has suggested.Researchers found those men who used a phone for four hours or more a day had fewer sperm and those they had moved less well and were of poorer quality.


The Ohio study involving 364 men was presented to the American Society for Reproductive Medicine in New Orleans.But a UK expert said it was unlikely the phones were to blame, as they were in use and not near the testes, and it may be being sedentary was the cause.

If you are holding [the phone] up to your head to speak a lot, it makes no sense that it is having a direct effect on your testesDr Allan Pacey, British Fertility SocietyThe team from the Cleveland Clinic Foundation in Ohio tested the sperm of 364 men who were being treated at fertility clinics in Mumbai, India, with their partners.

It was found that the heaviest users, those who used their phones for more than four hours a day had the lowest average sperm counts, at 50 million per millilitre (ml) and the least healthy sperm.

Men who used their phones for between two and four hours a day averaged sperm counts of 69 million per ml and had moderately healthy sperm.Those who said they did not use mobile phones at all had the highest average sperm counts, of 86 million per ml, and their sperm was of the highest quality seen.

'Used without thinking twice'Dr Ashok Agarwal, who led the research, told the New Orleans conference the study did not prove mobiles damaged fertility, but said it showed more research was warranted."There was a significant decrease in the most important measures of sperm health and that should definitely be reflected in a decrease in fertility, which is seen worldwide.

"People use mobile phones without thinking twice what the consequences might be."It is just like using a toothbrush, but mobiles could be having a devastating effect on fertility."It still has to be proved, but it could be having a huge impact because mobiles are so much part of lives.

"He suggested radiation from mobile phones might harm sperm by damaging DNA, affecting the cells in the testes which produce testosterone or the tubes where sperm is produced.

But a British expert cast doubt on the suggested link between mobile phone use and infertility in the men studied.Dr Allan Pacey, senior lecturer in andrology at the University of Sheffield, said: "This is a good study, but I don't think it tackles the issue.

"If you're using your phone for four hours a day, presumably it is out of your pocket for longer."That raises a big question: how is it that testicular damage is supposed to occur?"Dr Pacey, who is honorary secretary of the British Fertility Society, added: "If you are holding it up to your head to speak a lot, it makes no sense that it is having a direct effect on your testes.

"He added that people who use phones for longer might be more sedentary, more stressed or eat more junk food, which might be more likely explanations for the link found in the study.

HAYA NDIYO WAMETUMWA WAYAFANYE VIONI?

TUANGAZE BONGO: WAKUBWA TU, VIDEO YA WAKE ZA WATU AKIUZA URODA KAT...: Hivi karibuni kituo cha K24 cha nairobi kilibaini kile ambacho watu wengi kiliwaacha mdomo wazi kuwa, wapo wake za watu wanaofanya shughu...

Friday 13 June 2014

Timu za Afrika kufungua kampeini, leo Cameroon.

Baada ya kushuhudia mechi ya kwanza ya fainali ya kombe la dunia la mwaka huu huko Brazil,mamilioni ya mashabiki kutoka bara Afrika hii leo watafungua macho na kupaza sauti zao wawakilishi wa kwanza wa Afrika The Indomitable lions wa Cameroon ikitoana kijasho na Mexico katika mechi ya pili ya kundi A. Timu hizi zimewahi kukutana mara moja pekee kabla ya hii leo.Mexico ilishinda mechi hiyo ya kujipima nguvu kwa bao moja kwa nunge.
Mechi hiyo ilichezwa huko L.Angeles Marekani mwaka wa 1993 ,lakini hii leo hii haitategemea historia wala ukweli kuwa Mexico haijawahji kuishinda timu yeyote ya Afrika katika kombe la dunia ,la dakika tisini katika uwanja wa Arena das Dunas,ulioko Natal ndizo zitakazoamua yupi kati yao ni kidedea.

Kocha wa Mexico Miguel Herrera atakuwa bila ya mshambulizi nyota Javier Hernandez kutokana na kuwa hajafunga bao lolote katika mechi tisa.Kocha huyo atawategemea Giovani dos Santos na Oribe Peralta katika safu ya ushambulizi huku akitarajia Guillermo Ochoa kulinda lango lake.
Kwa upande wao Cameroon ambao walifanya mgomo wa marupurupu kabla ya kuabiri ndege ya Brazil ,nyota wao Samuel Etoo anatarajiwa kuanza katika mechi hii licha ya kuwa hayuko timamu kiafya.
The indomitable Lions walifuzu kwa mashindano haya baada ya FIFA kubatilisha matokeo ya kichapo mikononi mwa Togo.

Kocha Volker Finke anakabiliwa na changamoto ya mshikamano wa timu yake iliyowasili Brazil siku nne tu zilizopita baada ya mgomo huo wa marupurupu.Timu yake ndiyo yenye kushikilia rekodi ya kushindwa mara nyingi kuliko timu zote.Cameroon imepoteza mechi 24 na kushinda mechi moja pekee kati ya 13 ilizoshiriki.
Cameroon iliilaza Saudi Arabia bao 1-0 mwaka wa 2002.Katika mashindano haya Camerooon imemshirikisha mchezaji mchanga zaidi katika kikosi chao Fabrice Olinga mwenye umri wa miaka 18.

 Uhispania vs Uholanzi

 Mechi nyengine itakayokuwa ikitazamiwa na mamilioni ya mashabiki kote duniani ni Mabingwa watetezi wa kombe la dunia Uhispania .
Mabingwa hao huko Afrika Kusini mwaka wa 2010 wanafungua kampeini yao dhidi ya Uholanzi katika Arena Fonte Nova, Salvador.
Mechi hii itakuwa kumbukumbu ya fainali miaka minne iliyopita lakini Kocha wa Uhispania Vicente del Bosque hana sababu ya kuwa na wasiwasi kwani anajivunia kikosi dhabiti kinachosheheni mabingwa wa dunia mabingwa wa kombe la Ulaya na mabingwa wa taji la bara Uropa.
kati ya mechi kumi walizochuana Uhispania imeishinda Uholanzi mara tano na ikashindwa mara nne.
Kocha mpya wa Manchester United na Uholanzi Louis van Gaal anamtegemea nyota wa united Robin van Persie Wesley Sneijder na Dirk Kuyt kudhibiti tikitaka ya wahispania.
Bila shaka ukitaka kutizama janja na janjaure basi kaa kitako usubiri mechi hii.
Mechi ya mwisho hii leo itakuwa ya baina ya Chile na Australia.
Kinyume na mechi baina ya Uhispania na Uholanzi itakayoshuhudia tiki taka mechi baina ya chile na Australia inatarajiwa kuwa ya kasi na nguvu kutokana na mifumo ya timu hizo mbili.

 Chile dhidi ya Australia

Australia haijawahi kushinda mechi yeyote ya kombe la dunia wala alama yeyote ila ile waliojinyakulia mwaka wa 1974 walipotoka sare ya suluhu bin suluhu dhidi ya CHILE
'The Socceroos' wameshindwa na Chile katika mechi zao zote za kujipima nguvu.
Australia ambayo inaorodheshwa katika nafasi ya 62 katika orodha ya timu bora na shirikisho la soka duniani FIFA, ndiyo timu ya chini kabisa katika orodha hiyo ya FIFA inayoshiriki katika mashindano haya huko Brazil.
Kwa upande wao Chile wamewahi kushinda mechi mbili pekee kati ya 17 walizocheza za kombe la dunia.
Chile ilizilaza Honduras na Switzerland huko Afrika kusini mwaka wa 2010.
Wanamtegemea nyota wao Arturo Vidal kuwafungia mabao .
Australia kwa upande wao wanawategemea Mark Bresciano na Tim Cahill kusonga mbele katika hatua ya makundi

Timu ya soka ya Kenya kwenda Brazil.

ais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameizawadi kwa kuifadhili timu ya taifa ya soka Harambe Stars ziara ya kwenda Brazil kutazama michuano ya kombe la dunia.Hafla ya kuikabidhi rasmi ufadhili huo timu hiyo, ilifanyika katika ikulu ya Rais Ijumaa ambapo wachezaji kumi na moja wa timu hiyo walikabidhiwa vyeti vya usafiri kwenda Brazil.Mmoja wa wachezaji hao alifurahi sana na kusema kuwa hatua ya Rais Kenyatta kwao imetimiza ndoto yao. Rais atagharamia tiketi za timu hiyo kutazama michuano, malazi na usafiri ingawa haijulikani ni mechi zipi watakazotazama.

Mmoja wa wachezaji hao alifurahi sana na kusema kuwa hatua ya Rais Kenyatta kwao imetimiza ndoto yao. Rais atagharamia tiketi za timu hiyo kutazama michuano, malazi na usafiri ingawa haijulikani ni mechi zipi watakazotazama.

Kitendo cha Rais bila shaka ni jambo la kutaka kuwatia motisha wachezaji wa timu ya taifa ambao hivi karibuni waliicharaza Djibouti mabao mawili kwa moja katika duru ya kwanza ya michuano ya kuwania kombe la taifa bingwa Afrika baadaye mwakani.

Hatua ya Rais Kenyatta imewashangaza watu wengi sana nchini Kenya kwa kuwa timu ya taifa ya Kenya haikuwahi kufuzu kushiriki michuano hiyo, sasa wengi wanahoji hatua yake itasaidia nini?

Soka ya Kenya imekuwa ikikumbwa na changamoto si haba, usimamizi duni na wachezaji kukosa motisha ya kufanya vyema kwa ajili ya usimamizi huo mbaya.

Kenyatta na mkewe mama wa kwanza wa taifa Margaret Kenyatta wamewafadhili vijana hao kwa kima cha dola elfu arobaini. Akitoa ufadhili huo Kenyatta amesema lengo lake hasa ni kuwapa matumaini na motisha ya kuweza kuinua mchezo wa soka nchini Kenya.

Pia ni kama ishara ya kuthamini wachezaji hao ambao hivi karibuni walishinda kombe la Cecafa.

Kenyatta mwenyewe hatakwenda na kikosi hicho bali amewaasa vijana hao kuwa mabalozi wema wa Kenya nchini Brazil.

Ufadhili huu unakuja miezi sita baada ya Kenyatta kukubali kumlipa mshahara wa kocha wa timu hiyo kwa miakja miotano ijayo.

Kenya haijawahi kufuzu kwa michuano ya kombe la dunia lakini ziara hii kwa vijana wa Harambee Stars itawafungua macho huku wakiwa na azma ya kufuzu kwa michuano ya taifa bingwa Afrika mwaka 2015 baada ya kufuzu kwa duru ya pili na kujiandaa kuchuana na Lesotho tarehe 18 Julai.

Wednesday 11 June 2014

Wasifu Dr Wilbroad Peter Slaa,Katibu mkuu CHADEMA

Wilbroad Peter Slaa Amezaliwa Tarehe 29/10/1948, Alipata Elimu Ktk Shule Ya Kanisa Catholic Ya Dun'gunyi Seminary O Level 1966-1969, Baadae Akajiunga Na Shule Ya Kanisa Itwayo Itaga Seminary A-Level 1970-1971, Baadae Akapata Cheti Cha Masomo Ya Upadre Ya Philosophy Mwaka 1973 Ktk Shule Ya Kibosho Seminary, Na Tena Akapata Cheti Cha Masomo Ya Upadre Ya Theology Mwaka 1977 Kipalapala Seminary, Akaenda Kusoma Catholic Church Law Ktk Chuo Cha St Urban University Rome Italy Mwaka 1977-1981, Baada Ya Hapo Akateuliwa Padre Jimbo La Mbulu