Uruguay ilifunga bao la ushindi katika dakika za mwisho na kuwabandua washindi mara nne wa kombe la dunia Italia .
Hata hivyo habari kuu kutoka katika mechi hii ilikuwa ni kashfa nyingine ya tukio la Luiz Suarez ‘kung’ata’ Italia walitoka uwanjani wakiwa na ghadhabu kutokana na waliyoshuhudia kabla yao kuondolewa katika kombe la Dunia la pili bila kupita kutoka mechi za makundi- kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 1966.
Kocha wa Italia Cesare Prendelli alisema kabla ya mchezo kuwa ilikuwa “mechi muhimu sana katika taaluma yake kandanda” na baada ya kushindwa akapendekeza kujiuzulu.
Mechi hii ilikuwa na hamaki na hasira ndani na nje ya uwanja.
Italia ilikuwa ikihitaji sare tu ili kufuzu. Katika mfumo wa 3-5-2, Italia walikosa mshikamano, mbio na walihatarisha lango lao kila wakati. Lakini iwapo mfumo wao ulitekelezwa ili kuzuia ushambulizi wa Uruguay, mfumo huo ulisaidia.
Andrea Pirlo alimlazimu mlindalango wa Uruguay Fernando Muslera kuondoa mkwaju wake uliotokana na mpira wa adhabu na kuugongesha mlingoti, huku mshambulizi Ciro Immobile akipiga mkwaju nje ya lango.
Edinson Cavani alitaka kuzawadiwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 50 baada ya kuangushwa na Andrea Barzagli, lakini refarii akapuuzilia mbali.
Refarii huyo raiya wa Mexico hata hivyo angebadili mchezo muda mfupi baadae wakati alipomwonyesha Marchisio kadi nyekundu baada ya kiungo huyo wa kati wa Juventus kumchezea vibaya Arevalo katikati mwa uwanja.
Marchisio alinyanyua mguu na kumgonga kiungo huyo wa Uruguay gotini.
Utata zaidi ulizuka wakati Suarez na Chiellini walipokumbana katika maeneo ya penalti zikiwa zimesalia dakika tisa kwa mechi kukamilika.
Beki huyo wa Italia alilalamika wakati huo huo kwa refarii kwamba alikuwa ameng’atwa na akajaribu kumwonyesha alama.
Wakati wachezaji wa Italia walipokuwa wakiendelea kulalamika, Uruguay wakapata kona.
Suarez alipiga pasi nzuri naye Godin akafunga bao hilo la ushindi.
Itali walijaribu kila wawezalo ili kupata bao, hadi mlindalango Buffon kujaribu kutafuta bao kutokana na kona waliyopata waitaliano dakika za mwisho, lakini upande wake Oscar Tabarez ukawadhibiti.
Hata hivyo huenda mechi hii isikumbukwe sana. Macho yote, kwa mara nyingine yatamwelekea Suarez.
No comments:
Post a Comment