Tuesday 17 June 2014

WIZI SIMBA NA YANGA HUU HAPA

Jamii ya wanayanga inampenda sana mtu huyu kwa sababu yuko tayari hata kufilisika kwa ajili ya Yanga. Ni wazi Yanga ikibeba ubingwa yeye hufarijika sana kwa sababu yeye ni Yanga na Yanga ni yeye! Kinachonipa kizunguzungu kuhusu mtu huyu ni kufanya mkakati Yanga ifungwe mabao mengi na Simba ili kiongozi fulani afukuzwe! Kumbe kwa mtu huyu nani anaongoza Yanga ni jambo lenye umuhimu mkubwa mno linapolinganishwa na mafanikio ya timu! Cha kusisimua anapewa hadhi kubwa mtu huyo kwa jinsi alivyopanga "kumuondoa kiongozi wa YANGA ANAYOIPENDA SANA" kwa kipigo kikubwa kwa YANGA ANAYOIPENDA SANA!
Jamii ya wanasimba inawapenda sana watu hawa kwa sababu wako tayari hata kufilisika kwa ajili ya Simba. Ni wazi Simba ikibeba ubingwa wao hufarijika sana kwa sababu wao ni Simba na Simba ni wao! Kinachonipa kizunguzungu kuhusu watu hawa ni kufanya mkakati Simba ifungwe fungwe mechi nyingi za ligi kuu, ikiwezekana ishuke daraja ili kiongozi fulani aonekane hafai! Kumbe kwa watu hawa nani anaongoza Simba ni jambo lenye umuhimu mkubwa mno linapolinganishwa na mafanikio ya timu! Waafrika bwana, tuko zaidi ya bogus! Jamani Yanga na Simba, siku hizi hakuna mapinduzi, hata mkimhujumu kiongozi kwa kuifanya TIMU MNAYOIPENDA SANA IHARIBU VIBAYA SANA kiongozi huyo mtakuwa naye tu mpaka amalize muda wake. Mtapigwa weeeeeee lakini yupo tu.
Naiona mikakati hii dhidi ya viongozi wanaochukiwa ndani ya Yanga na Simba kama mume kukorofishana na mkewe KIPENZI halafu anawatafuta wahuni, anawalipa pesa nyingi wambake mkewe KIPENZI kisha kumwambia "umelala na wahuni vichochoroni,umepoteza sifa za kuwa mke wangu". Sijui hii imekaaje hii.

No comments:

Post a Comment