Friday 29 November 2013

UFOO AAPA KIAPO CHA SIRI

http://api.ning.com/files/l8tah2vExAULAoDSzOz1POhNbFKkIlgOZXJ4VWhoq1BOrsbduXn5KOa8PS-UMuYpB5x9hzTnqBWYoqUT4vf-HOtIG9zyEfL3/UFOOSARO1.jpg?width=404 
Ufoo Saro.


SIKU chache baada ya Mtangazaji wa Runinga ya ITV, Ufoo Saro kuruhusiwa hospitalini alipokuwa amelazwa baada ya kudaiwa kupigwa risasi na mzazi mwenzake, marehemu Anther Mushi, ameibuka na kula kiapo cha siri.
Ufoo Saro akiwa hospitali baada ya kupigwa risasi na mzazi mwenzake, marehemu Anther Mushi.
Ufoo ambaye alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, katika tukio la yeye kupigwa risasi, alimpoteza mama yake mzazi aitwaye Anastazia Saro aliyedaiwa kuuawa na marehemu Mushi aliyejiua kwa risasi.
Akizungumza na gazeti hili Ufoo alisema, kamwe hawezi kusema kilichokuwa kikiwagombanisha yeye na marehemu Mushi mpaka siku ya mwisho wa uhai wake.

“Siwezi kuzungumzia kabisa chanzo wala ugomvi wetu mimi na marehemu Mushi. Hiyo itakuwa siri yangu,” alisema Ufoo.
Katika mahojiano na gazeti hili, mtangazaji huyo alipoulizwa kuhusu msimamo wake wa uhusiano baada ya kupona kabisa alisema, hawezi kujiingiza tena kwenye mapenzi kwa sasa.
“Sitaki kabisa kusikia juu ya mapenzi, siwezi kuliweka suala hilo akilini tena,” alijibu kwa kifupi kwa sauti ya chini lakini yenye mkazo.

TAARIFA YA SAMSON MWIGAMBA KWA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU WARAKA WA MKAKATI WA MABADILIKO 2013

Jumatano, 27 Novemba 2013
Jana katika taarifa kwa waandishi wa habari, Mhe. Tundu Lissu na Mhe. John Mnyika waliudanganya umma kuhusu waraka unaohusu Mkakati wa Mabadiliko 2013. Katika maelezo yao waheshimiwa hawa, pamoja na mambo mengine, walidai kuwa waraka uliosambazwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari ni feki. Ukweli ni kwamba:


  1. Ninathibitisha kwamba waraka uliosambazwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii ni sahihi neno kwa neno kama nilivyousoma katika magazeti ya HabariLeo, Jamhuri na Rai, pamoja na nakala iliyopo Jamii Forum. Ili kuthibitisha kwamba waraka ule ndio wenyewe, nawatumieni ‘soft copy’ kutoka kwenye kompyuta mpakato (laptop) yangu ambako ndiko ulikoibwa na viongozi wa chama baada ya kunipora kwa nguvu laptop yangu Oktoba 25 na kukaa nayo hadi jioni ya Oktoba 28. Naomba kila mtu asome neno kwa neno waraka ninaowapa leo halafu afananishe na ule uliopo kwenye magazeti na kwenye mtandao ili mjiridhishe kama kweli sio wenyewe. Kama Lissu na wenzake wana mpango wa kuuchakachua waraka huu wamekwama!
  2. Waraka huu si wa uhaini wala mapinduzi wala usaliti kama inavyodaiwa na akina Lissu. Huu ni waraka wa kusaka ushindi katika uchaguzi halali ndani ya chama ambao ulikuwa ufanyike Desemba 2013, na ambao sasa umesogezwa mbele.
  3. Napenda ijulikane kwamba wakati wa uchaguzi si jambo la ajabu kuwa kwa wanachama kuwaunga mkono wagombea tofauti. Nimekuwa karibu na Mwenyekiti Mbowe kwa miaka mingi na ninajua kwamba yeye naye anao mkakati tena unaohusisha mbinu haramu za kuhakikisha anammaliza Zitto na yeye kupita bila kupingwa kwenye uchaguzi huo. Wanaoshiriki mkakati wake ni pamoja na Lema, Lissu na wakurugenzi kadhaa waliopo makao makuu.
  4. Waraka huu ulipaswa kuwa siri ndani ya watu watatu tu (M1, M2 na M3) na haikutarajiwa kwamba ungevuja kwa jamii. Bahati mbaya viongozi wa chama baada ya kuunasa waraka huu kutoka kwenye komputa yangu mpakato (laptop), na baada ya kikao cha Kamati Kuu, waliamua, kwa jazba na bila kutumia busara ya kiuongozi, kuusambaza waraka huo kwenye vyombo vya habari kwa lengo la kuwakomoa na kuwadhalilisha waandaji. Sasa baaada ya kugundua madhara ya waraka huo machoni pa jamii wameamua kuukana. Ni ajabu kwamba wanaukana waraka ambao waliusambaza wenyewe.
  5. Nasisitiza kwamba mambo yaliyopo kwenye waraka ni bayana na dhahiri. Sibahatishi kwa sababu mimi nimefanya kazi makao makuu kama Mhasibu Mkuu hadi Mwezi Aprili 2012. Ni kwa kutambua uozo uliopo katika uongozi wa chama makao makuu niliona umuhimu wa kubadilisha uongozi kwa njia za kidemokrasia ili tukiokoe chama na hatukuwa na nia wala sababu za kuanika haya yote kwenye umma. Kwa sababu za chuki na kukosa busara za kiuongozi huyo anayeitwa Mwanasheria Mkuu akawashauri viongozi wetu kijinga wauanike waraka mbele ya macho ya watanzania. Wangekuwa na akili na busara baada ya yote haya kutokea wangejiuzulu au kuitisha uchaguzi mara moja.
  6. Tunatambua kwamba viongozi wetu wanamchukia Mheshimiwa Zitto Kabwe kwa siku nyingi sana na wametamani kumfukuza siku nyingi. Hata hivyo, ninawashauri watafute sababu nzuri za kumfukuza uongozi na hata uanachama kwa sababu yeye hahusiki na waraka wetu wa Mkakati wa Mabadiliko 2013 hata chembe, pamoja na kwamba yeye ndiye alikuwa na bado ndiye mlengwa mkuu, kama atakubali.



Samson Mwigamba (M3)
Arusha
Jumatano, 27 Novemba 2013.

Saturday 23 November 2013

BABU SEYA ALIA DUNIA HAINA HURUMA


Hukumu iliyokaziwa na Mahakama ya Rufaa, Dar es Salaam, juzi (Alhamisi), ikipigilia msumari adhabu ya kifungo cha maisha jela dhidi ya mwanamuzi mkongwe nchini, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’, imesababisha maumivu makali kwa wahusika.
                                 Mwanamuziki Nguza Viking na mwanaye Johnson Nguza 'Papii Kocha'.
Uthibitisho wa hilo unatokana na kauli ya Babu Seya, aliyoitamka mahakamani akimnong’oneza Papii Kocha, akisema: “Kweli hii dunia haina huruma, hukumu hii imeniuma sana kuliko zote ambazo zimetangulia.”
Akizungumza kwa upole kwa sauti ya majonzi, huku sura yake ikionesha dhahiri kutokuwa  na furaha, Babu Seya aliendelea: “Kinachoniuma zaidi ni wewe, nakusikitikia sana, wewe ni kijana mdogo ambaye ulipaswa kuwepo uraiani ukitimiza ndoto zako na ukiisadia nchi yako.
...Akiwa katika huzuni na majonzi makubwa.
“Ndoto zako zimeishia hapa. Tumejitahidi sana kukwepa hiki kifungo lakini imeshindikana, wewe unajua.”
Hata hivyo, wakati akitoka nje ya ukumbi wa mahakama, Babu Seya alimweleza mwandishi wetu: “Hili jambo sijalifanya, nitaendelea kupambana mpaka mwisho.”

NI HUKUMU YA MWISHO
Msajili Mwandamizi wa Mahakama, Zahra Mruma, akisoma hukumu  hiyo alisema: “Ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka ambao ni Jamhuri, umeendelea kuwa na nguvu, kwa hiyo vipengele vya utetezi vilivyowasilishwa na mawakili wa utetezi vimekosa nguvu ya kutengua hukumu ya awali.”
...Ndugu na jamaa wakiangua kilio baada ya hukumu.
Zahra, alisoma hukumu hiyo kwa niaba ya jopo la majaji watatu ambao waliipitia upya hukumu hiyo, baada ya mawakili wa utetezi, Mabere Marando na Gabriel Mjele, kuomba Mahakama ya Rufaa ifanye mapitio ya mwisho, baada ya kutokuzikubali zote zilizotangulia.
Mawakili wa upande wa utetezi, walitaka mapitio hayo yafanyike kwa hoja kwamba haiingii akilini kwa Babu Seya na mwanaye kushiriki tendo la mapenzi kwa pamoja, tena kwenye nyumba wanayoishi.
Hoja hiyo ilishibishwa na maelezo kuwa Babu Seya na Papii ni Waafrika, kwa hiyo kitamaduni haiwezekani kushiriki mapenzi kwa pamoja.
Utetezi mwingine ni kuwa nyumba ya tukio ni ya kifamilia, kwa hiyo isingekuwa rahisi kwa tendo husika kutendeka, maana wengi wangekuwa wanashuhudia.

KESI YA MSINGI
Babu Seya na Papii, walishtakiwa na baadaye kukutwa na hatia ya kuwabaka, kuwalawiti na kuwaambukiza Virusi Vya Ukimwi, watoto nane, wenye umri wa kati ya miaka saba na sita.
Mahakama ilielezwa kuwa Babu Seya alikuwa akiwaita watoto hao na kuwanunulia pipi kisha kuwaingiza ndani ambako waliwaingilia kwa zamu na baada ya kitendo, waliwapa mgao wa kati ya shilingi 100 na 150.
Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani kwa mara ya kwanza mwaka 2003 na mwaka 2004, hukumu ilitolewa, ikiwatia hatiani Babu Seya na wanaye watatu na kuwahukumu kwenda jela maisha.
Watoto wengine wawili wa Babu Seya, waliokuwemo kwenye kesi hiyo ni Francis Nguza na Nguza Mbangu ‘Nguza Mashine’ aliyekuwa mpiga drum wa Bendi ya FM Academia, mpaka wakati anaingizwa kwenye mashtaka.
Mwaka 2005, rufaa ya kwanza ilisomwa ambayo ilikazia hukumu ya awali lakini Februari 2010, Mbangu na Francis waliachiwa huru baada ya kuonekana hawana hatia, huku Babu Seya na Papii, ikipitishwa na Mahakama ya Rufaa kwamba waendelee na kifungo cha maisha jela.

MAJAJI WALIVYOTOA HUKUMU
Zahra, alisema jopo la majaji watatu, Nathalia Kimaro, Salum Masati na Mbarouk Salim Mbarouk, lilichambua hoja za utetezi na kuona hazina nguvu, kwa hiyo wakajiridhisha kuwa Babu Seya na Papii, wanastahili kuendelea na adhabu ya kifungo cha maisha jela.
Hukumu hiyo, ilikuwa ni ya rufaa ya nne, lakini imeshindikana kwa kuwaondoa Babu Seya kwenye kifungo.

MAWAKILI WASALIMU AMRI
Mmoja wa  mawakili wa utetezi, Mjele, alisema kuwa hukumu hiyo ndiyo ya mwisho na kwamba wao hawana njia nyingine ya kukata rufaa kisheria.
“Hatuna njia nyingine, hapa ndiyo mwisho,” alisema Mjele na kuongeza: “Labda tusubiri msamaha wa rais kwa sababu ni yeye pekee mwenye mamlaka ya kutengua hii adhabu.”

RAIS AZIDI KUTUPIWA MZIGO
Watu kadhaa waliohudhuria mahakamani juzi, waliungana na Wakili Mjele kwamba kesi hiyo iachwe mikononi mwa rais kwa sababu ndiye mwenye nafasi ya kufanya lolote katika kesi hiyo kama anavyoruhusiwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Mahakama imefanya kazi yake, mawakili wa utetezi wamejitahidi lakini imeshindikana, sasa hatutakiwi kuijadili sana hukumu, badala yake tumuachie rais kwa sababu ndiye mwenye mamlaka,” alisema Fredrick Mwaluwanda wa Kinyerezi.
Mosha Kabogo alisema: “Katika hukumu hii, kila mmoja anaweza kuwa na hisia zake, jambo la msingi ni kumuacha rais afanye anachoona kinafaa. Uzuri ni kwamba siyo rais wa sasa peke yake, kwani hata ye yote anayekuja, anaweza kutumia mamlaka yake kikatiba kuwaachia huru au kuwapunguzia adhabu.”

WANAMUZIKI WAANDAA UJUMBE KWA RAIS
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Abdul Sykes ‘Dully Sykes’, alisema mahakamani hapo kuwa anakusudia kuitisha kongamano la wanamuziki halafu watafanya mkutano na waandishi wa habari kumuomba rais awaachie huru Babu Seya na Papii.
“Hili suala linauma sana, hatuwezi kukaa kimya tukiwaacha wanamuziki wetu nyota wakienda na maji. Lazima tufanye kitu na tutakachofanya  ni kujikusanya na kuandaa mkutano wa waandishi wa habari ambao tutautumia kutuma ujumbe kwa mheshimiwa rais,” alisema Dully.

PAPII NI WA KUMJADILI KIDOGO
Papii Kocha, wakati alipoingia kwenye mashtaka hayo, alikuwa ni kijana mdogo ambaye nyota yake kwenye muziki ilikuwa inang’ara kwa kiwango cha juu sana nchini Tanzania.
Alifanya vizuri sana akiwa na Bendi ya FM Academia na Tot Plus kabla ya kutoka na albamu yake binafsi iliyokuwa na nyimbo nyingi kama vile Salima, Fanta na Seya ambayo uliimbwa mithili ya wimbo wa taifa.
Alitabiriwa kwamba angeweza kuendelea kufanya vizuri kutokana na uwezo aliokuwa nao lakini nyota yake ilizimwa na kesi hiyo.
Kwa upande wa Babu Seya, ni nguli aliyejenga jina na heshima kubwa nchini kupitia muziki wake, huku akipigiwa mfano kama mpiga solo bora kabisa, lakini historia yake imehitimishwa kwa kifungo cha maisha jela.

Jeraha lamzonga Andre Ayew


Mwanakandanda wa timu ya taifa ya Ghana Andre Ayew hataweza kucheza kwa takriban kipindi cha majuma manane baada ya kutegua goti.
Kijana huyo wa umri wa miaka 23 aliumia goti lake wakati wa pambano la mkondo wa pili dhidi ya Misri katika kinyang'anyiro cha nafasi za fainali ya kombe la dunia siku ya jumaanne.
Klabu yake ya Marseille ya Ufaransa ilisema katika wavuti wake kwamba Ayew alipimwa na Klabu yake ya Marseille ya Ufaransa ilisema katika wavuti wake kwamba Ayew alipimwa na madaktari na kupatikana ametegua goti lake na atafanyiwa operesheni siku ya Jumaatatu.
Hili ni pigo kubwa kwa Ayew, ambae amekua akitamba katika michezo ya hivi karibuni na akifunga mabao manne katika michuano tisa aliyokwishacheza.
Ghana ilipoteza mechi ya mjini Cairo 2-1 lakini ikafaulu kucheza katika michuano ya fainali ya kombe la dunia nchini Brazil hapo mwakani kw akuibuka na ushindi wa jumla ya mabao7-3.

Friday 22 November 2013

Ismail Aden Rage amerudi bongo apata mapokezi makubwa


DSC_0023
Mwenyekiti wa klabu ya Simba Ismail Aden Rage amewasili Dar es salaam Tanzania leo akitokea Sudan ambapo alipokelewa na baadhi ya Wanachama wa Simba kwenye Uwanja wa ndege wa mwalimu JK.Nyerere.
Waandishi wengi walikua na maswali mengi kuhusu yeye kusimamishwa kuwa Mwenyekiti wa Simba lakini akayapangua kwa kusema kesho mchana ndio atazungumza na Waandishi kuhusu kila kitu ila sentensi moja iliyonyakwa na millardayo.com ni ‘taarifa za kusimamishwa Uwenyekiti sijazipata ndio kwanza nakusikia wewe, ninachojua mimi bado ni Mwenyekiti wa Club ya Simba’
‘Nimefurahi kwa mapokezi mazuri ambayo yameonyesha imani ya Wanachama kwangu mimi, mimi kama Mwenyekiti nitatoa tamko langu rasmi kesho mchana makao makuu ya Club ya Simba, sasa hivi siwezi manake rafiki yangu mpenzi Zitto kabwe ameondolewa kwenye Unaibu katibu mkuu na mimi sijafurahia kwa hiyo siko kwenye mood ya kuongea’ – Aden Rage
Alipoulizwa kama ana taarifa za kocha mpya Simba na pia kikao hicho atakifanyiaje Makao Makuu wakati ameondolewa kwenye Uwenyekiti, Rage kasema swala la kocha atalizungumza kesho ila hilo la kufanyia mkutano na Waandishi wa habari makao makuu ya Simba, waandishi wasiwe na wasiwasi kwani yeye ndio Mwenyekiti.
rage
Kuhusu kikao kilichofanyika na kumuondoa kwenye nafasi ya Uwenyekiti, Ismail Aden Rage amesema kikao kilichofanyika sio halali manake ukisoma katiba ya Simba, FIFA na CUF katika aya zote hakuna aya inayosema kamati ya utendaji ina mamlaka ya kumsimamisha Rais au Mwenyekiti.
DSC_0005
            Baadhi ya Wanachama wa Simba wakicheza wakati wa mapokezi.

ZITTO KABWE, DK.KITILA MKUMBO NA SAMSON MWIGAMBA WAVULIWA VYEO VYAO VYOTE CHADEMA



Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe.
Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe, Dk. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba wamevuliwa vyeo vyao vyote baada ya kuhusika na waraka wa mkakati wa siri wa kukipasua chama unaojulikana kama 'Waraka wa Ushindi' ambao umevunja katiba za chama hicho, kupandikiza chuki za kidini, majungu na kukashifu viongozi wa chama.
Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Mhe. Tundu Lissu akieleza maazimio ya Kamati Kuu ya Chadema kwa wanahabari (hawapo pichani).
SABABU ZA ZITTO, DK. KITILA NA MWIGAMBA KUVULIWA VYEO VYAO
Mhe. Tundu Lissu amesema kuwa Kamati Kuu imenasa waraka huo wa mkakati wa siri wa kukipasua chama vipande vipande unaohusisha watu wanne ambao ni Zitto Kabwe, Dk. Kitila Mkumbo, Samson Mwigamba na mtu mwingine ambaye hajajulikana.
Anasema lugha iliyotumika katika waraka huo ni ya siri ambapo kuna mtu anaitwa MM ambaye ni Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe, M1 ni Dk. Kitila Mkumbo, M2 hajajulikana na Dk. Mkumbo alikana kumfahamu kabisa M2 na M3 ni Samson Mwigamba.
Waraka huo uliojulikana kama Waraka wa Ushindi unavunja katiba ya chama kwa sababu umepandikiza chuki za kidini, majungu na kukashifu viongozi wa chama kinyume na katiba ya CHADEMA.
Tuhuma zote zilizoko katika waraka huo hazijawahi kuwasilishwa kwenye kikao chochote halali cha chama kinyume na matakwa na masharti ya katiba ya chama.
Anaongeza kuwa hakuna taasisi yoyote inayoweza kupuuza wala kuvumilia mambo haya yaliyopo kwenye waraka huo kwani umewatukana sana viongozi wa chama.
Anasema matusi hayo ni ya muda mrefu na viongozi wakuu wamekuwa wakiyavumilia kwa muda mrefu lakini yalivumiliwa kwa lengo la kuwapa nafasi wanamtandao hao kujirekebisha.
Kamati Kuu imeamua kuwavua nyadhifa zao zote watu wote waliotajwa katika waraka huo ambao ni Zitto Kabwe, Dk. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba.
Pia Kamati Kuu imeunda kamati ya kuchunguza na kufuatilia mhusika mwingine M2 ambaye anadaiwa ni Mtumishi wa Makao Makuu ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi yake.
Kamati Kuu imeagiza wahusika wote waandikiwe barua za kujieleza ni kwa nini wasivuliwe uanachama kwa makosa hayo makubwa waliyofanya.
Pia Kamati Kuu imeagiza mchakato wa kumvua Zitto nafasi yake ya Unaibu wa Kambi ya Upinzani Bungeni.
Lissu anasema Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe na Dk. Kitila Mkumbo waliomba kujiuzulu nyadhifa zao zote baada ya waraka wao kukamatwa lakini Kamati Kuu iliwakatalia baada ya kuona kuwa kukubaliana na maombi yao hayo ilikuwa ni kama kuwaacha wajiuzulu kwa heshima ambayo hawaistahili hata kidogo.
Kamati Kuu pia imeazimia kuusambaza waraka huo kwenye vyombo mbalimbali vya habari ili Watanzania waone na kujua ukweli.
Lissu amemalizia kwa kuwaomba Watanzania na wanachama wote wa CHADEMA nchi nzima wasife moyo na waendelee kukijenga chama na nchi yao.

WARAKA ULIOWAVUA VYEO ZITTO, DK KITILA NA MWIGAMBA HUU HAPA

Zitto Kabwe.
MKAKATI WA MABADILIKO 2013
UTANGULIZI:
Taasisi tunayoizungumzia ilisajiliwa rasmi mwezi January 1993 na tokea wakati huo imeongozwa na wakuu wa taasisi wapatao wawili na aliyepo kwa sasa ni wa tatu. Wa kwanza aliongoza kwa miaka mitano tangu wakati huo 1993 hadi 1998 na kumwachia aliyefuata ambaye naye aliongoza kwa miaka mitano hadi mwanzoni mwa 2004 na kumwachia aliyepo sasa. Huyu aliyepo aliongoza kwa miaka mitano tangu mwaka 2004 hadi 2009 na kisha akachaguliwa tena mwaka 2009 kwa kipindi cha pili.
Tunapenda kwa hatua ya mwanzo kabisa kutambua juhudi za wakuu wetu wote waliopita walizozifanya katika kuhakikisha taasisi yetu inakua kwa kutumia uwezo wote waliokuwa nao na katika mazingira yaliyowakabili. Mwaka 1995 chini ya mkuu wa kwanza tulipata wawakilishi watatu kwenye chombo chetu kikuu cha uwakilishi. Mwaka 2000 chini ya mkuu wa pili tukapata wawakilishi wanne pamoja na wa nyongeza mmoja na kufanya idadi kuwa watano. Mwaka 2005 chini ya mkuu wa tatu ambaye ndiye aliyepo hivi sasa, tulipata wawakilishi watano na wa nyongeza sita jumla wakawa 11. 2010 chini ya mkuu huyu huyu wawakilishi wakaongezeka na kuwa 23 na wa nyongeza 25 na kufanya idadi kuwa 48 kabla ya kupata mwingine mwaka jana na kufanya sasa wawe 49.
Dk. Kitila Mkumbo.
Tunapopongeza juhudi zao hizi tunahitaji pia kuwapongeza wakuu wetu wawili wa kwanza ambao kimsingi waliweka msingi mzuri sana wa kutong’ang’ania madaraka na badala yake kuachia mapema na kumwachia mwingine kidemokrasia bila vurugu. Hawakuwa madikteta na tunawapongeza sana. Walijitahidi sana kutokuwa wapenda madaraka na kimsingi walituwekea utamaduni ambao walitaka wote tuufuate na kujenga taasisi imara inayojali demokrasia na haki ya kila mwana taasisi. Ni kwa msingi huo waliamua kuandika kabisa katika mwongozo wetu kwamba kiongozi yeyote katika ngazi yoyote ya kuchaguliwa atakapogombea na kushinda ataongoza kwa kipindi kimoja cha miaka mitano na kisha ataweza kugombea na kuongoza kwa kipindi cha pili cha miaka mitano baada yapo hawezi kugombea tena katika nafasi ile ile aliyoitumikia kwa vipindi viwili. Ili kuonyesha kwamba walimaanisha kile walichokisema, wote wawili hawakuwahi kukaa madarakani kwa vipindi viwili vilivyoruhusiwa katika mwongozo bali wote wawili walikaa kipindi kimoja kimoja tu.
Samson Mwigamba.
Lakini kuna matatizo yameanza kujitokeza na tusipochukua hatua haraka huko mbele tunaweza kupata shida kubwa. Tunapenda kuainisha matatizo hayo kwa uchache kama ifuatavyo:

Wakati tukiufanyia mwongozo wetu mabadiliko mwaka 2006 hatukugusa kipengele kinachomzuia kiongozi kuongoza kwenye nafasi moja kwa zaidi ya vipindi viwili vya miaka mitano mitano. Lakini wakati mwongozo unachapwa chini ya uongozi uliopo, kipengele hicho kiliondolewa kinyemela. Mambo yanayotokea hivi leo yanaonyesha dhahiri kipengele hicho kiliondolewa kwa makusudi kwa maslahi na kwa faida ya viongozi waliopo madarakani kwa sasa. Hiki kinaweza kuchukuliwa kama kitendo kidogo lakini kama viongozi wetu wanaweza kutokuwa waaminifu katika jambo kama hili, ni dhahiri hawawezi kuaminika na wanaweza kufanya mambo mengine makubwa na yenye athari zisizomithirika kwa taasisi yetu.

Ni dhahiri kwamba uongozi uliopo umeishiwa mbinu na kuakisi jambo la msingi sana ambalo waasisi wetu waliliona tangu mwanzo na kuamua kuweka kipengele cha ukomo wa uongozi kwenye mwongozo wetu. Kuchoka kwa uongozi wetu kunaonekana dhahiri katika mipango na mikakati ya taasisi ya miaka kadhaa. Mfano mwaka 2008 uongozi ulianzisha mkakati wa operesheni samaki mkubwa (maarufu kama Oparesheni Sangara). Huo ulifanyiwa kazi katika mikoa kadhaa na hatimaye ikafa kimya kimya. Baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kulianzishwa matembezi ya maandamano ambayo nayo yalikuwa yakipeleka ujumbe kwa watu na yalipangwa kufanyika mikoa yote na wilaya zote.

Kumbukumbu zetu zinaonyesha kwamba yalikuwa yakianzia makao makuu ya mkoa na kwenda kwenye wilaya zote. Lakini kumbukumbu hizo zinaonyesha kwamba yalifanyika Mwanza, Musoma, Shinyanga, Kagera na mikoa ya Nyanda za Juu kusini (Mbeya, Iringa, Njombe na Rukwa) kisha nayo yakafa kifo cha mende. Kisha mwaka 2012 ikaanzishwa operation ya mabadiliko maarufu kama Movement for Change (M4C). Hiyo ilikuwa inakwenda kwenye mikoa na timu kama nne hivi ambazo kwa ujumla zilitathmini hali ya mtandao na uongozi wa taasisi, kuhamasisha umma kwa njia ya mikutano ya hadhara, kuingiza wanachama na kusimika uongozi na hatimaye kufanya mafunzo kwa viongozi. Hiyo ikafanyika Mtwara na Lindi, Morogoro na kisha ikaenda kufia Iringa. Mwaka huu viongozi wetu wamekuja na ugatuaji madaraka kutoka makao makuu ya taasisi na kupeleka madaraka kwenye kanda mbalimbali. Mkakati huu ulikufa kabla ya kuanza pale viongozi wakuu walipobadilisha maazimio ya kikao kikuu na kutekeleza matakwa yao ikiwa ni pamoja na kuleta suala la viongozi wa muda kwa muda mrefu badala ya kuajiri maofisa na wakahakikisha wanaweka watu wao kwenye uongozi wa muda. Kitendo hiki kwa peke yake, cha kufeli kwa kila mkakati unaoletwa na viongozi wetu katika hatua za utekelezaji unaofanywa na wao wenyewe waleta mkakati, ni kiashiria tosha kwamba uongozi uliopo umechoka.

Performance yetu kwenye chaguzi ndogo nayo ni ishara kwamba mabadiliko yanahitajika. Tangu uongozi huu uingie madarakani, kumefanyika chaguzi ndogo 8 za wawakilishi kwenye chombo kikuu, kati ya hizo tumeshinda 2 tu sawa na asilimia 25. Aidha baada ya mwaka 2010 kumefanyika chaguzi kadhaa za wawakilishi kwenye halmashauri. Mwezi Oktoba 2011, mwezi wa4 2012, mwezi Septemba 2012 na mwezi Juni 2013. Kote performance yetu imekuwa poor kupindukia. Mfano mwezi wa Juni 2013 tumepata viti 6 kati ya 22 (27%) na mwezi Septemba 2012 tulipata viti 7 kati ya 29 (24%). Ni dhahiri mabadiliko yanahitajika kwa kuwa wakuu waliopo wanatumia mbinu zile zile na kupata matokeo yale yale. Tunahitaji mbinu mpya. Kwa kifupi, ushindi ambao tumekuwa tukiupata katika chaguzi ndogo haulingani na ukubwa wa hamasa kwa taasisi yetu iliyopo mitaani. Hii ni kwa sababu tumekuwa tukitumia mbinu hizohizo katika kila chaguzi. Aidha, tu wepesi mno wa kuridhika na kujisifu kwa mafanikio madogo badala ya kukaa chini na kutafakari kwa kina mahala tunapojikwaa.

Matumizi ya fedha za taasisi. Hakuna mtu anayejua hivi sasa fedha za chama zinatumikaje zaidi ya kakikundi ka watu watatu yaani mkuu kabisa, mtendaji mkuu na mkuu wa fedha kwenye taasisi yetu. Maamuzi ya vikao hayaheshimiki tena na mabwana hawa. Baada ya uchaguzi wa 2010 vikao halali vilielekeza kiasi na aina ya fedha ambazo hazitaguswa bali zitunzwe kwenye akaunti maalum kwa ajili ya uchaguzi wa 2015. Lakini leo si tu akaunti hiyo haina fedha bali hakuna akaunti yoyote yenye fedha. Watu watatu ndo wanaamua fedha zitumikeje. Mfano mwingine ni maamuzi ya kikao cha juu mno cha hivi karibuni kilichoamua kwamba kiasi cha fedha inayotoka serikalini kipelekwe kwenye mikoa na wilaya na kiasi kingine kipelekwe kwenye kanda. Leo ni mwezi wa tano maamuzi hayo hayajatekelezwa. Lakini kuna michango ya watu binafsi kama yule mtanzania mwenye asili ya kihindi, hizo nazo hazijulikani zimechukuliwa lini kwa mfumo gani, zikatunzwa wapi na hatimaye zimetumikaje. Hapo hatujataja fedha zinazopatikana kutoka kwenye fundraising events mbalimbali kama ile ya Dar es salaam na Mwanza. Hizo nazo hazijawahi kuonekana na walioendesha hizo fundraising, uaminifu wao kwenye masuala ya fedha ni questionable.

Taarifa za fedha. Tokea baada ya uchaguzi wa 2010 mpaka leo, hakuna kikao chochote kilichowahi kupokea na kujadili hadi mwisho ripoti ya mapato na matumizi ya fedha za taasisi. Kila kikao agenda hiyo inarushwa kiaina. Wanaojua mchezo huo ni watu watatu tu tuliowataja hapo juu na malengo ya kurusha hiyo agenda kila wakati na kukwepesha isijadiliwe pia wanayajua wao. Ni dhahiri tukiendelea na hawa watu tutafika 2015 tukiwa hatuna pesa hata ya kuweka mawakala kwenye vituo na tutapigwa tukiwa tumesimama. Kwa kiasi kikubwa mkuu aliyepo anatengeneza mazingira yaleyale ya mwaka 2005 na 2010 ya kutaka chama kiwe hakina hela ili ikifika wakati wa uchaguzi kimpigie magoti. Kisha atatoa pesa bila kumbukumbu zozote na mara baada ya uchaguzi anapeleka lundo la deni na kudai alipwe hela aliyekikopesha chama wakati wa uchaguzi. Alifanya hivyo katika chaguzi za 2005 na 2010. Wakati wote wa kampeni za mwaka 2010, kwa mfano, taasisi yetu ilihangaika sana kwa kukosa hata hela ya kununua maji kwa wajumbe wa ngome. Lakini ajabu ni kwamba baada ya uchaguzi mkuu wa taasisi na baadhi wa wapambe wake walilete deni kubwa la takribani shililingi milioni mia tano akiadi kuwa walikikopesha chama. Taasisi imewalipa pesa zote hizi kwa muda mwaka mmoja. Sasa anatengeneza mazingira hayohayo kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2015.

Mipango ya kukipatia chama mapato ya ziada kutoka nje ya chama. Wakuu waliopo hawana hata ndoto ya namna ya kupata fedha za ziada. Wanachokijua ni kukusanya ‘sadaka’ kwenye mikutano ya hadhara na kuwapatia kazi watu wanaoonekana kuwa matapeli eti waendeshe harambee za kuchangisha fedha kwa njia ya matukio. Mawazo mazuri kama lile la kuanzisha kampuni la uwekezaji la taasisi yetu litakalowekeza kwenye miradi mbalimbali, halijawahi kufanyiwa kazi, na hivyo uanzishaji wa miradi mbalimbali ya kuiingizia taasisi fedha imebaki ndoto ya mchana. Hatuwezi kufika hata siku moja bila fedha. Hata uchaguzi wa wenzetu wa hapa jirani juzi juzi wakuu wetu ingawa walishiriki lakini hawaonekani kama wamejifunza chochote.

Njia haramu za kubaki madarakani. Ili kuhakikisha wakuu wanabaki madarakani, wameanzisha vikundi vikundi ndani ya taasisi yetu. Siku hizi ni rahisi sana kuambiwa kwenye taasisi yetu eti huyu ni wa boss na huyu ni wa dogo. Na wale walio wa boss kwa kuwa boss ndo anashikilia raslimali za taasisi anatumia mfumo haramu kuwaneemesha watu wake kwa kutumia raslimali za taasisi na kuwakandamiza wote wanaoonekana wanapishana naye kimtazamo. Jambo hili limewaibua wachumia tumbo, wapenda madaraka, na vibaraka lukuki wanaokwenda kujipendekeza kwa wakuu wa taasisi kwa malengo ya kujinufaisha binafsi. Katika kufanya hivyo vibaraka hao wamekuwa wakiwaendea wakuu wa taasisi na kuwajaza maneno mabaya dhidi ya viongozi wenzao na kuzidi kuwafarakanisha viongozi wa juu.

Kuna mchezo umeanzishwa na wakuu wa taasisi unaitwa ulinzi wa chama uliogawanyika katika makundi mawili yaani visible na invisible. Visible ni ule unaoonekana ambao uko chini ya kikosi chetu chekundu ambacho kinajulikana kwa kila mtu lakini invisible wanajulikana kwa mkuu wa taasisi na mtendaji mkuu peke yake. Wanafanya kazi kwa maelekezo ya wakubwa hao wawili na hawajulikani kwa viongozi wengine wa juu. Ni hawa hawa ambao wanatumika vibaya pale wanapoleta taarifa za kiintelijensia ambazo zinawahusisha viongozi wasiopendwa na wakuu na usaliti dhidi ya taasisi. Hakuna kamati maalum inayowathibitisha maaintelijensia hao bali wakuu wenyewe wanawachukua wanaowataka. Ni katika mfumo huu wa kipuuzi mida eight amekuwa akitumika vibaya kwa kumshambulia mtendaji mkuu msaidizi hadharani kwa kutumia mitandao ya kijamii na wakuu wanafurahia na kumlipa pesa.

Udhaifu wa utendaji wa mtendaji mkuu. Mtendaji mkuu ni dhaifu mno na ni mara nyingi sana tumeshuhudia mkuu wa taasisi akifanya mambo ya kiutendaji kinyume na utaratibu kama vile yeye mwenyewe kuja kwenye kamati ya makatibu na wakurugenzi na kupangua mipango yao na ku-inject ya kwake na mtendaji mkuu kuadopt tu kana kwamba yeye hawezi kupanga mambo ya kiutendaji, hata tunapokuwa kwenye operesheni maalum tumeshuhudia mkuu wa taasisi ndo akipanga watendaji, posho zao na hata kusimamia matumizi ya pesa na shughuli mbalimbali za kiutendaji. Udhaifu wa mtendaji mkuu ni udhaifu wa mkuu wa taasisi kwa kuwa amemteua yeye mara mbili tena mara ya pili alileta jina moja mbele ya Baraza la juu kuonyesha kwamba aliridhika na utendaji wake kiasi cha kutotaka kumpambanisha na mwingine. Lakini baada ya kumpendekeza mara ya pili ndipo tumeshuhudia yeye kuingilia kati mara nyingi sana mambo ya kiutendaji kana kwamba anamfichia aibu mtendaji wake. Swali kwa nini alimteua tena? Jibu lake litakuwa rahisi tu kwamba ni kwa sababu mtendaji huyu ni passivekwa kila takwa la mkuu wake.

Matumizi mabaya ya madaraka yanayoweza kuhusishwa na ufisadi. Taasisi yetu inayo kamati ya tenda ambayo iko chini ya kamati ya makatibu na wakurugenzi. Lakini uzoefu unaonyesha kwamba kamati hii haifanyi kazi imezimwa kimya kimya na wajumbe wote wa kamati ya tenda kwa kuwa ni wachumia tumbo wanaojigonga kwa wakuu, wamekubali kuzimwa. Leo ikidaiwa kamati hiyo ilete nyaraka za mchakato wa manunuzi ya magari, pikipiki, vifaa vya kueneza taasisi, set ya televisheni iliyofungwa ofisini kwa mtendaji mkuu, hawana. Manunuzi haya yote yote yanafanywa na wakuu hasa hasa mkuu wa taasisi bila utaratibu wowote jambo ambalo ni hatari na linarahisisha matendo ya kifisadi. Bila aibu, mkuu wa taasisi ndio amekuwa mnunuzi wa vifaa vyote vya chama nje ya nchi kwa bei anayoijua mwenyewe na ambaye haihojiwi popote. Huu ni mfano wa wazi wa mgongano wa kimaslahi jambo ambalo ni hatari kwa kiongozi mkubwa wa taasisi kama yetu inayojitambulisha katika kupinga vitendo vya ufisadi na uvunjifu wa maadili ya uongozi kwa ujumla.

Makubaliano ya kifisadi na mtu binafsi anayeuza vifaa vya kueneza taasisi. Hakuna kikao chochote cha juu kilichojadili ama kilichowahi hata kupewa taarifa tu kwamba sasa kuna mtu binafsi kapewa tenda ya kuuza vifaa vya taasisi na taasisi inanufaika vipi na mauzo hayo na kwa nini vifaa muhimu vya taasisi vinauzwa. Jambo hili linajulikana kwa wakuu tu.

Mifumo ya uteuzi wa maofisa wa makao makuu ya taasisi imevurugwa na siku hizi wakuu wa taasisi hasa mtendaji mkuu anateua na kutimua ofisa anavyotaka na mara nyingi bila hata kamati ya makatibu na wakurugenzi kujua. Mambo haya yanafanyika mbele ya macho na masikio ya mkuu wa taasisi jambo ambalo linazidi kuthibitisha kwamba mkuu na mtendaji mkuu wanajuana na wanafanya kwa kulindana.

NANI TUMUUNGE MKONO KUCHUKUA NAFASI YA MKUU:
Baada ya utangulizi huo unaoonyesha kinagaubaga kwamba tunahitaji mabadiliko, hatua iliyofuata ilikuwa ni kuangalia nani anaweza kuleta mabadiliko tunayohitaji. Ni vema ikazingatiwa kwamba mtu ambaye tungemuunga mkono lazima awe ni mtu mwenye uwezo mkubwa kuliko tunayetaka kumtoa. Awe ana qualities za kiuongozi na zaidi sana awe na uwezo wa kupambana na mkuu aliyeko. Tukileta mtu asiyefahamika sana kwenye mifumo ya taasisi yetu hata kama angekuwa mzuri kiasi gani hatachagulika na mkuu aliyeko atarudi kwa urahisi na kuendelea kuididimiza taasisi.

Katika kuchunguza ndani ya taasisi tuliridhika kwamba mtendaji mkuu msaidizi ana sifa zote tulizozitaja hapo juu ingawa kila mwanadamu ana udhaifu wake. Ni dhahiri pia kwamba udhaifu wa mtendaji mkuu msaidizi unarekebika kuliko wa mkuu aliyepo. Kwa ujumla mtendaji mkuu:

Ni kiongozi anayeweza kuongoza taasisi bila kujenga makundi akijali zaidi kazi ya taasisi kuliko maslahi binafsi.
Ameonyesha kwa vitendo kwamba hana maslahi binafsi kwa kuwa tumeshuhudia akifanya kazi nyingi za taasisi bila kudai malipo kwa njia ya posho ama vinginevyo.

Anaheshimika na viongozi wa ndani na nje ya taasisi jambo ambalo ni la muhimu sana kwa ustawi wa taasisi na kwa yeye kuwa mkuu wa taasisi tunatarajia wakubwa wengi sana kutoka nje ya taasisi yetu kuiamini na hata kujiunga nasi katika kuhakikisha tunafanikisha lengo la taasisi.

Ni msomi wa kiwango cha juu na mwenye uwezo mkubwa katika kuchanganua mambo ya kiuchumi, kisiasa, kijamii, kimichezo, nk jambo ambalo ni muhimu sana kwa kuwa ni hatari kuwa na kiongozi asiye na ujuzi wa kutosha kwenye masuala kama hayo.
Ndani ya taasisi anakubalika kwa makundi yote ya vijana, wazee na akina mama.

Uongozi wa sasa wa taasisi yetu umefanya tuonekana kwamba taasisi yetu ipo kwa ajili ya kuvuruga amani ya nchi. Yote hii ni kwa sababu tumekuwa hatuna mbinu mpya za mapambano zinabadilikabadilika zaidi ya maandamano ya kila mara. Kwa kuzingatia utamaduni wa watanzania wa kupenda amani, kuna haja ya kufuta hii taswira na njia rahisi ni kubadilisha uongozi wa taasisi haraka iwezekanavyo.

Uelewa wake wa mambo ya kiuchumi ni muhimu sana kwa taasisi kwa sasa. Tunahitaji kuja na vyanzo vipya vya mapato ikiwa tunahitaji kufanikiwa. Mkuu aliyepo si kwamba ameishiwa bali hana mbinu za maana za kuiimarisha taasisi kimapato kwa ajili ya malengo yake ya mbele.

Exposure kubwa na kukubalika katika siasa za kimataifa. Tunahitaji kiongozi ambaye anazifahamu siasa za kimataifa na anayeweza kuungwa mkono na viongozi wengi wa kimataifa. Ni hatari kutegemea utaweza kufanikisha malengo kama ya taasisi yetu bila mpango kabambe wa kuungwa mkono na jumuia ya kimataifa. Mpaka hivi sasa hakuna mpango wowote wala hata mchakato wa maana kuwa connected na jumuia ya kimataifa. Kiongozi wetu mkuu wa sasa yupo ‘too local’ na hana mawasiliano yeyote ya maana na viongozi wengine katika kanda na kimataifa. Ndio maana mkuu huyo na mtendaji wake mkuu wamekuwa hawaonekani katika matukio makubwa ya kimataifa. Hata katika kutoa maoni katika mambo makubwa ya kitaifa na kimataifa viongozi hawa hawapo. Kwa kifupi kwa sababu ya aina ya viongozi tulio nao, nafasi ya taasisi yetu katika nyanja za kimataifa haipo!

Aina na staili ya uongozi wa sasa wa taasisi yetu ni kina kwamba nchi hii haipo hadi taasisi yetu itakapochukua dola. Yaani tunafanya mambo kama kwamba tutaanza upya kabisa tukichukua dola. Ni kwa sababu tumegombana na kila mtu katika utawala wan chi, vikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama. Ukweli ni kwamba tutavihitaji vyombo hivi kabla na baada ya kuingia madarakani na ni ndoto kudhani kwamba tutakabidhiwa nchi kwa kugombana na kila mtu. Ni kwa sababu ya mtazamo kama huu ndio maana wakuu wetu wa sasa hawaonekani kabisa katika shughuli za kitaifa kama vile sherehe za uhuru wan chi, n.k.

Uwezo wa kuwaunganisha wasomi wa kada mbalimbali, wafanyabiashara wakubwa, watumishi wa umma na sekta binafsi, nk katika kupata muunganiko wa mawazo na kutoka na sera murua zinazogusa kila sekta. Hili la kuwashirikisha litaenda sambamba na kutoa elimu kwa wote waelewe na watuunge mkono. Tunasema hivi kwa kuwa watu wa kada mbalimbali hawajaelewa sera zetu juu ya mambo yanayowahusu mfano wafanyabiashara wakubwa, wawekezaji, wakulima, watumishi, wanafunzi,nk na hivyo hawajawa tayari kutuunga mkono. Kile kinachofanywa wakati wa uchaguzi kwa njia ya ilani ya uchaguzi na elimu kutolewa kwa njia ya kampeni majukwaani hakitoshi. Tunahitaji watu wajue tumeunda think tank kwa ajili hiyo na baadaye wajue nini kimetokana na think tank hiyo ili wajadili na kutoa maoni na hatimaye tutoke na kitu kinachokubalikwa na wananchi wote. Na tuna imani hilo tunayempendekeza ana uwezo nalo.

Kubwa zaidi ni kwamba alishaiangalia taasisi yetu na kuona mambo yanayohitaji mabadiliko na kujiangalia yeye na kuridhika kwamba ataweza kuleta mabadiliko tunayoyahitaji na ndipo mwaka 2009 aliamua kujitosa kuutafuta ukuu wa taasisi yetu kabla ya kuombwa kumwachia aliyepo.

SWOT ANALYSIS:
Kwa kutumia uchambuzi huu hapa chini wa uimara, udhaifu, fursa na vitisho ama vikwazo dhidi ya mtu tunayempendekeza, utaweza kutuonyesha kama tunayempendekeza ataweza kushinda vita iliyo mbele yetu. Kama SWOT inavyotaka, tutaangalia sifa njema alizonazo tunayemtaka ambao ndio uimara wake, tutaangalia pia udhaifu wake, tutaangalia fursa alizonazo na mwisho tutazingatia vitisho ama vikwazo vilivyopo. Ni muhimu tukaeleza kwamba katika SWOT analysis tunajikita kwa mambo yanayohusika moja kwa moja na uwezekano wa tunayemtaka, kuchaguliwa. Kwa hiyo kwa mfano utakuta kwamba katika sehemu hii hatutazungumzia sifa njema alizonazo tunayemtaka kama kiongozi lakini sifa hizo zikawa hazina ushawishi wa kuwafanya wajumbe wa kikao cha uchaguzi kumchagua.

Uimara wa tunayemtaka:
Ingawa si mmoja wa waasisi wa taasisi yetu, lakini ni mwana taasisi mkongwe akiwa amejiunga na taasisi yetu miaka miwili tu tangu ianzishwe na mwaka mmoja tangu isajiliwe rasmi na serikali.

Zaidi ya kuwa mwanataasisi mkongwe, hajawahi kujiunga na taasisi nyingine hapo kabla. Alijiunga na taasisi hii kabla hata haijajulikana kwa watu na alibaki kuwa mwana taasisi mwaminifu hata pale taasisi zingine zilipoonekana kuwa imara na maarufu zaidi ya hii.

Kutokana na vipengele ‘a’ na ‘b’ hapo juu, hakuna mtu hata mmoja anayeweza kusema mtu huyu alikuja kwenye taasisi yetu kwa ajili ya kutafuta maslahi kama vile uwakilishi kwenye chombo chetu kikuu cha uwakilishi hapa nchini.

Ni mvumilivu sana. Katika jitahada za wakuu waliopo kuhakikisha wanaendelea kukalia viti vyao, wamejitahidi sana kumpaka matope lakini amevumilia. Mahali ambapo wengine wangeshakata tamaa na kuhama taasisi, yeye alibaki kuvumilia mpaka imefikia wana taasisi wa ngazi za chini waliokuwa wanadanganywa kwamba mtu huyu ni msaliti, wameanza sasa kushtuka.
Ana historia nzuri ya utendaji uliotukuka ndani na nje ya chombo cha uwakilishi.

Ana uwezo mkubwa wa uelewa wa mambo mbalimbali ya uchumi, jamii, utamaduni, michezo, nk. Uwezo wake unachagizwa si tu na elimu yake ya darasani bali pia vipaji na akili ya kuzaliwa.

Ni mzalendo wa hali ya juu anayeipenda nchi yake kwa moyo wa dhati. Amethibitisha hilo kwa namna anavyolitetea taifa letu katika medani za kimataifa na jinsi anavyolipigania ndani dhidi ya mafisadi na wasiolitakia mema taifa letu. Ni mwakilishi pekee aliyekuwa tayari kukosa mishahara ya miezi kadhaa kwa kuamua kusimamia ukweli kwamba kuna ufisadi ulifanyika mpaka akasimamishwa uwakilishi wake kwa mikutano kadhaa ya chombo chetu cha uwakilishi.

Katika kuzidi kuonyesha alivyo mzalendo tunaweza kusema hapa kwamba ni kiongozi pekee kutoka upande huu ambaye ameonekana sana kwenye mambo ya kitaifa kwa mfano kulipigania taifa letu katika mambo ya kimchezo, kutumia gharama zake kwenda nje ya nchi na kujifunza mambo mbalimbali yanayoweza kulisaidia taifa katika sekta nyeti kama mafuta, gesi na madini, nk bila kusahau kwamba amekuwa ndiye mwakilishi pekee aliyeongoza katika kuibua kashfa nyingi na nzito za ubadhirifu ndani ya serikali hata kufikia mawaziri kadhaa kufukuzwa kazi.

Mambo hayo tuliyoyataja kwenye vipengele ‘e’, ‘f’, ‘g’ na ‘h’ yamemfanya kuwa kiongozi wa kwanza kuwa maarufu sana katika taasisi yetu aliyewapiku hata viongozi wa serikali kwa umaarufu. Hii ya umaarufu ni sifa muhimu sana linapokuja suala la uchaguzi.

Uwezo wake wa kujieleza kwa kujenga hoja pale anapopewa nafasi. Hata pale anapokuwa amepakwa sana matope na wenzake, anapopewa nafasi ya kujieleza huweza kuwashawishi watu wengi wanaomsikiliza. Hii itamsaidia sana siku ya kujieleza mbele ya kikao cha uchaguzi ambapo ataweza kupangua hoja zote dhaifu za kumpaka matope.

Ana uwezo wa kuchangamana na makundi yote ambapo vijana humwona kama mwenzao, wanawake humwona kama mtetezi wao wakati wazee humwona kama kijana mwenye busara anayeweza kuelekeza kama kiongozi.

Ana mahusiano mema na mazuri na viongozi wa ngazi za chini kutokana na ziara nyingi alizozifanya na kukutana na viongozi wa ngazi za chini akiwa katika kuijenga taasisi hii. Mahusiano haya mazuri yanachagizwa na jinsi anavyotumia muda wa kuongea na viongozi wa ngazi za chini kuzungumza kwa lugha ya upole na kuelekeza viongozi wenzake bila kuwaonyesha dharau.

Si mtu wa kujipenda nafsi na katika kupambana umaskini wa watu badala ya umaskini wake, alifikia kuzikataa posho wanazolipwa wawakilishi wakati wakitekeleza majukumu ambayo kwayo wanalipwa na kuiomba ofisi ya chombo hicho kuzipeleka posho hizo kwa watu maskini.

Ana limu nzuri sana aliyoipata katika vyuo vinavyoeleweka kitaifa na kimataifa
Ni kijana na hii ni taswira njema kwa sababu taasisi yetu inaungwa mkono sana na vijana

Udhaifu wa tunayemtaka:
Maneno yake mara nyingine hayazingatii anayazungumza katika mazingira gani na hivyo kuwasha masikio ya wanataasisi jambo linalompunguzia kukubalika kwake taratibu.

Kama ilivyo kwa maneno, kuna matendo pia ambayo mara nyingine huyafanya bila kuzingatia mazingira na wasikilizaji wake na hivyo kupunguza imani ya wana taasisi kwake.

Hali ya ndoa ya tunayemtaka kutoeleweka msimamo wake

Kuna wakati tunayemtaka hu-respondkwa taharuki kubwa dhidi ya mashambulizi yanayoelekezwa kwake jambo linalomfanya achukue maamuzi yasiyo sahihi kwa wakati huo. Kwa kifupi kuna wakati tunayemtaka huonekana kufanya maamuzi kwaemotion zaidi badala ya kutulia kwanza na kutafakari kwa kina ikiwa ni pamoja na kutafuta ushauri kwa wenzake kabla ya kurespond.

Jambo lililoelezwa katika ‘d’ hapo juu humfanya tunayemtaka wakati mwingine kuonekana ana jazba sana kwa sababu akishataharuki na kuchukua maamuzi akingali kwenye taharuki huwa ni rahisi sana kuonekana anajibu mapigo kwa jazba sana.

Ustahimilivu: yaliyotajwa katika ‘d’ na ‘e’ hapo juu yanaashiria tunayemtaka si mstahimilivu sana sifa ambayo inahitajika sana kwa kiongozi.

Uwazi:
Katika taasisi zetu hizi ni muhimu sana kuepuka kufanya mambo yote wazi wazi hata kama ni mema ama ni haki ya mhusika ama si makosa katika jamii tuliyomo. Kuna mambo ambayo ni haki ya mtu mfano mahusiano binafsi ya kimapenzi, kuwa na marafiki wa damu kutoka upande mwingine wa utawala, nk. Lakini mambo hayo ni muhimu wakati mwingine ama kwa kiwango fulani yakafanywa kwa siri kuepuka mitazamo potofu kwa unaowaongoza.

Fursa alizonazo tunayemtaka:
Utamaduni wa taasisi yetu wa kubadilisha wakuu wa taasisi kila baada ya vipindi vifupi ili kuleta maono mapya kwenye taasisi unampendelea tunayemtaka.

Udhaifu ulioonyeshwa na uongozi uliopo chini ya mpinzani wetu katika kutekeleza program mbalimbali za taasisi nyingi zikiwa zimebuniwa na wao wenyewe, pia ni fursa kwa tunayemtaka.

Udhaifu mkubwa ulioonyeshwa na uongozi uliopo kwenye ugawanyaji wa raslimali za taasisi kama vile fedha za ruzuku, michango mbalimbali ya wahisani na hata vifaa vya uenezi.

Kujitokeza kwa tunayemtaka kutaonekana kama fursa kwa wanataasisi kufanya mabadiliko makubwa na kuua kabisa ile propaganda ya kwamba taasisi yetu ni ya kabila fulani ama eneo fulani kwa kufanya reference kwa uongozi wa taasisi.

Hoja ya uongozi uliopo kushindwa kabisa kusoma taarifa za fedha tokea 2010 ikifahamika kwa wapiga kura inaweza kuwa machinjio kabisa ya uongozi uliopo na kumpa fursa kubwa tunayemtaka.

Imani ambayo wana taasisi wengi wanayo kwake. Utafiti mdogo unaonyesha kwamba bado jina la tunayemtaka linatamkika sana midomoni mwa wanataasisi pale wanapotajwa viongozi wa juu wa taasisi yetu. Hii inaonyesha bado wana taasisi wanayo imani kubwa kwake na kwa hiyo atakapopata fursa ya kupangua matope aliyopakwa atakuwa na nafasi kubwa ya kuchaguliwa.

Mpinzani wetu hana historia nzuri ya utendaji uliotukuka ndani na nje ya chombo cha uwakilishi. Hakuonyesha utendaji wowote wa pekee alipokuwepo kwenye chombo mwaka 2000 -2005 na hata alipopewa uongozi wa upande wetu ndani ya chombo tokea 2010 hadi leo 2013 hajafanya lolote la kutukuka ndani ya chombo hicho.

Mpinzani wetu hana uwezo mkubwa wa uelewa wa mambo mbalimbali ya uchumi, jamii, utamaduni, michezo, nk. Si tuelimu yake ya darasani ni ya magumashi bali pia vipaji na akili ya kuzaliwa havijaonekana katika maisha yake.

Uzalendowampinzani wetu unatia shaka akiwa hajaonyesha lolote la maana katika kulitetea taifa letu kimataifa. Ingawa ameshapata nafasi lukuki ya kwenda nje ya nchi lakini mara zote akifika huko ni kuiponda tu nchi yake. Ingawa anayo majukwaa ya kufanya hivyo akiwa ameshakuwa mwakilishi mara mbili kwenye chombo chetu lakini hatujawahi kumsikia akiibua kashfa mahsusi ya ufisadi na kuisimamia zaidi ya yeye mwenyewe wakati fulani fulani kutuhumiwa kwa ufisadi mfano pale alipokopa kwenye shirika la umma na kugoma kulipa mkopo.

Katika kuzidi kuonyesha uzalendo hafifu wa mpinzani wetu tunaweza kuangalia jinsi ambavyo mpinzani haonekani kwenye mambo ya kitaifa. Hii ni fursa kwa tunayemtaka.

Mpinzani wetu si maarufu akilinganishwa na tunayemtaka na hivyo kumpa fursa zaidi tunayemtaka kumshindani mpinzani wetu kwenye uchaguzi.

Uwezo wa mpinzani wetu wa kujieleza kwa kujenga hoja pale anapopewa nafasi ni mdogo sana.

Mpinzani wetu hajazoea ushindani na changamoto. Ni mtu aliyezaliwa kwenye utajiri na anadhani pesa ni kila kitu. Ukimnyang’anya pesa ukamwambia ashindane kwa hoja hawezi na ndo maana anajaribu sana kuhakikisha anaingia mwenyewe ulingoni bila kupingwa.

Kutokana na tuliyoyasema hapo juu kwenye ‘m’ ni dhahiri kwambapale mpinzani wetu anaporushiwa kombora la kashfa anakuwa mzito kujieleza hata kama anapewa nafasi ya kufanya hivyo na hii ni fursa muhimu kwa tunayemtaka.

Mpinzani wetu ni mgumu sana katika kuchangamana na makundi yote ambapo vijana humwona kama si mwenzao kiumri na kifedha, wanawake humwona kama malaya anayependa kutumia miili yao kujistarehesha wakati wazee humwona kama mtu anayedhalilisha hata nafasi aliyopewa kwa kufanya uhuni waziwazi hata kuvunja ndoa si ya kwake tu bali hata za watu wengine.

Mpinzani wetu hana mahusiano mema na mazuri na viongozi wa ngazi za chini kutokana na dharau nyingi anazozionyesha pale anapokukutana na viongozi wa ngazi za chini akiwa katika kuijenga taasisi hii. Hutumia muda mwingi kuwaponda viongozi wenzake hata kufikia kutamka mara nyingi kwamba kama kiongozi hawezi kujigharamia nauli na malazi ya kutoka mahali fulani kwenda mahali fulani kwa siku kadhaa hafai kuwa kiongozi bila kujali kwamba kuna viongozi wetu wana moyo na taasisi hii na ndo wameifikisha hapa ilipo lakini hawana uwezo wa kifedha na hivyo kauli kama hizo za mkuu huyu huona kama anawadharau kwa kuwa yeye ni tajiri. Hii imemfanya kutopendwa na viongozi wengi wa ngazi ya chini hivi sasa na kutoa fursa ya pekee kwa tunayemtaka.
Mkuu aliyepo amekuwa na mkakati unaoitwa kuondoa watu wa zamani. Jambo hili linawaudhi sana viongozi wa ngazi za chini ambao wanaona kama baada ya kuifikisha taasisi mahali ilipo kwa sasa wanaonekana hawana maana tena. Wengi wamefikia kuapa kwamba kama mwendo ni wa kuwaondoa watu wa zamani basi na yeye ni wa zamani lazima aondoke.

Mpinzani wetu amejionyesha dhahiri kujipenda na kujijali nafsi bila kujali watu wa hali ya chini. Matukio mawili yanamwacha uchi katika hili pale alipolitangazia taifa kwamba wawakilishi wetu wote hawatachukua posho za vikao halafu yeye na wengine wote wanazichukua hadi leo na kumwacha mtendaji msaidizi peke yake. Na la pili linalofanana na hilo ni pale alipotangaza kutotumia gari la serikali ambalo ni la kifahari kisha akalirudia kimya kimya.

Kuwepo muhtasari wa kikao cha wazee ambacho mwaka 2009 kilimshauri tunayemtaka ajitoe na kumwachia mkuu aliyepo na kumtaka mkuu aliyepo kumwachia tunayemtaka katika uchaguzi ujao na wote wakasaini makubaliano hayo, nayo ni fursa muhimu sana kwa tunayemtaka.

Mkuu aliyepo anaamini kwamba ameshamsambaratisha tunayemtaka na hivyo kwa sasa amebweteka na hiyo inatupatia sisi fursa kuendelea kuimarisha mtandao wetu.

Kwa kuwa ni mwislamu. Hii ni fursa katika kupata kuungwa mkono na wanachama waislamu ambao wamekuwa na kigugumizi wakidhani waislamu hawatakiwi katika uongozi wa taasisi yetu.

Elimu ndogo na duni aliyenayo mpinzani wetu ambaye ndiye mkuu wa taasisi yetu kwa sasa. Kwa sasa ni kiongozi pekee katika nchi yetu anayeongoza taasisi kubwa asiye na elimu ya shahada huku taasisi yetu ikiwa inaongoza kwa kuwa na wasomi waliobobea katika kila nyanja. Hii ni kejeli hasa kwetu sisi ambao tumekuwa tukiwasema wenzetu kwamba ‘akili ndogo’ inaongoza akili kubwa. Kimsingi tumekuwa tukijisema kwa kukubali kuongozwa na mtu mwenye akili ndogo.

Mkuu wa sasa kutokuwa na msimamo thabiti katika mambo ya msingi. Rejea swala la maandamano ya kumshinikiza Kawambwa ajiuzulu na kujitoa katika mchakato wa katiba.

Vikwazo dhidi ya tunayemtaka:
Sisi wenyewe tunaoandaa mkakati huu hatuna uhakika kama tunayemtaka yuko tayari na yuko serious na business hii, na kwa hiyo huenda tusifanye kwa nguvu zetu zote ikiwa hatutapata nafasi mapema ya kukutana na mhusika na akatuhakikishia kwamba yuko serious.

Utayari wa mhusika mkuu kutekeleza yale tunayokubaliana. Inapotokea baada ya kukubaliana sisi na yeye akapata ushauri tofauti na ukauona uko more genuine, basi tuwasiliane kwamba nimeshawishika kufanya hivi badala ya vile tulivyokubaliana kwa sababu hizi ama zile. Hii haitatukatisha tamaa tofauti na kama tutakuwa tunapanga hivi halafu yeye anafanya vile bila maelezo yoyote
Kitendo cha mkuu aliyepo kung’ang’ania kuendelea nayo ni kikwazo kwa kuwa baada ya kuwa madarakani kwa miaka yote hiyo lazima amejipatia watu wanaomhusudu ama kumpenda ama kumkubali na kuwepo wengine wanaoogopa tu kwamba mkuu aliyepo akitoka taasisi itakufa hata kama hawana sababu yoyote.

Tunatazamia mkuu aliyepo atafanya vitendo vingi zaidi vya haramu katika kumdhibiti tunayemtaka pale tunapoelekea kwenye uchaguzi wenyewe.

Raslimali za taasisi kutumiwa na viongozi waliopo katika kumsaidia mkuu aliyepo wakati wa kwetu anatumia raslimali zake za mfukoni.

Propaganda chafu zilizokwishapigwa dhidi ya tunayemtaka zimepunguza imani ya wanataasisi kwa tunayemtaka kwa kiasi fulani
Baadhi ya mambo ambayo amekwishayasema ama kuyatenda nayo yameshawapunguzia imani kiasi fulani wanataasisi mbalimbali.
Kutoonekana sana kwenye operations za taasisi yetu pia kumewapa wasiwasi baadhi ya wanataasisi.

Muhtasari wa SWOT analysis unaonyesha kwamba strength na opportunities za tunayemtaka ni nyingi sana zikilinganishwa na weaknesses zake na threats dhidi yake. Aidha ukichambua zaidi utaona kwamba weaknesses za tunayemtaka nirepairable na vikwazo dhidi yake pia ni rahisi kuvikabili na kuvisambaratisha. Tukishamaliza maandalizi ya mkakati huu tukaonana na mhusika mkuu na kumpa ushauri akatulia na kufanya kazi, mkuu aliyepo hatafua dafu. Tunahitaji kutekeleza mkakati huu kwa siri kubwa ili mkuu aliyepo aendelee kubweteka na ndiyo maana hata lugha iliyotumika ni ndani hapa ni ya pekee. Tunahitaji tunayemtaka asionekane kama kuna kitu anafanya na tunafurahi kwamba kuna wakati alitangaza kwamba hana nia ya kugombea tena waliopo wanatosha. Ikitokea vyombo vya habari vikamuuliza tena hiyo ndiyo iwe kauli yake ili kuendelea kumfanya mkuu aliyepo asihangaike na hivyo kuja kummaliza kirahisi. Aidha katika utekelezaji wa mkakati kama tutakavyoeleza hapo baadaye, tunayemtaka atajitenga mbali asionekane hata kuwa karibu na sisi. Vikao vyetu na yeye vitafanyika mara chache sana na mahali pa faragha kupita kiasi ikiwezekana hata nchi jirani.

Mkakati huu hautatakiwa kupatikana kwenye komputa zaidi ya tatu yaani ya mchapaji ambaye ni M3, ya M3 na ya MK mwenyewe. Hata hivyo email zitakazotumika kusafirisha mkakati huu kutoka kwa M3 kwenda kwa M1 hadi kwa MK hazitakuwa zile za kawaida za hao watu bali mpya kabisa zilizofunguliwa kwa makusudi haya tu na kwa majina fictitious. Aidha kila atakayekuwa na mkakati huu kwenye computer yake anatakiwa kuliwekea file hilo password ili hata mtu wa karibu naye anayeweza kufungua computer yake asiweze kulifungua file hilo. Pia email address hazitatolewa kwa sms bali kwa kupiga na kuambiana spelling za address.

MTANDAO WA USHINDI:
Mtandao wa ushindi utakuwa kama ifuatavyo. Kwenye ngazi ya kitaifa tutakuwa na kamati yenye members watatu tu. M1 ndiye atakayekuwa anawasiliana na tunayemtaka ambaye ataitwa MM (Mhusika Mkuu). Tumepanga kwamba kusiwe na mawasiliano mengi kati ya kamati na mhusika mkuu kuepuka tracking ya wapinzani wetu. M1 ni mtu wa karibu na MM kwa hiyo mawasiliano yao hayataweza kutiliwa shaka na mtu yeyote hata wangewasiliana mara nyingi kiasi gani. Hata hivyo, linapokuja suala la mkakati huu tunasihi mawasiliano yawe kwa kuonana uso kwa uso ama kwa simu na si sms. M1 ndiye atakayewasilisha mambo yote yanayotoka kwenye kamati ya kitaifa na endapo kuna haja ya MM kukutana na kamati ya kitaifa, mipango yote ya kikao itafanywa na M1 kwa usiri mkubwa. M2 ni mtu ambaye yuko kwenye ofisi kuu za taasisi yetu wakati M3 ndiye mchapaji wa mkakati huu.

Kamati hii imefanywa kuwa na members wachache sana wenye uelewa mpana wa mambo na wenye elimu nzuri ili kuhakikisha kazi inafanyika kitaalam na kwa uhakika sana. Kamati ya kitaifa itapeleka mapendekezo yake kwaMM na yeye pia ataleta ushauri wake kwa kamati kama mishale inavyoonyesha. Chini ya kamati ya kitaifa kutakuwepo waratibu wa kanda zote kumi watakaojulikana kama MK1 – MK10. Hawa watatafutwa na kusimikwa na kamati ya kitaifa kwa kushauriana na MM kwa utaratibu utakaokubalika na pande zote yaani MM na kamati ya kitaifa. Chini ya waratibu wa kanda kutakuwapo waratibu wa mikoa yote 30 (MMK1 – MMK30) ambao watapatikana kwa utaratibu ule ule wa kuwapata waratibu wa kanda. Isipokuwa pale ambapo inakuwa ngumu, itabidi kamati ya taifa isaidiane na waratibu wa kanda kuwapata waratibu wa mikoa lakini kamati itashauriana na MM kabla ya kuwasimika rasmi hao waratibu wa mikoa.Mtandao utakuwa kama inavyoonyeshwa kwenye mchoro ufuatao:
NAMNA YA KUFANIKISHA MKAKATI:
Kazi itagawanywa katika awamu tatu:
Awamu ya kwanza ni kuanzia sasa mpaka uchaguzi wa ngazi ya matawi utakapoanza. Katika awamu hii kazi ni kuhakikisha kwamba mtandao mzima umekamilika mpaka kwenye ngazi ya mkoa. Kazi nyingine itakayofanyika ni kwa waratibu wa mikoa kuendelea kuspot makada kwenye wilaya na mikoa ambao tayari wana mtazamo tulio nao ama ambao wanaweza kuingiziwa kirahisi mbegu hii ya mabadiliko na wakawa tayari na wana uwezo na sifa za kushinda uongozi kwenye wilaya na mikoa yao bila kusahau sifa ya kuwa waaminifu wenye uwezo wa kutunza siri. Kulingana na muda hii ni kazi inayotakiwa kufanyika sasa lakini kwa uangalifu mkubwa. Ni muhimu kukumbushana hapa kwamba katika awamu hii hakuna anayetakiwa kujua mpango mzima zaidi ya kamati ya kitaifa na MMili kuhakikisha uwezekano wa mkakati wetu mapema kwa wapinzani wetu unakuwa minimized to almost zero.

Awamu ya pili ni kipindi kuanzia uchaguzi wa matawi mpaka uchaguzi wa mikoa unapokamilika. Katika awamu hii tutasaidiana na waratibu wa kanda na mikoa kuhakikisha makada tuliowaspot kwenye wilaya wanapanga safu zao kwenye kata ili kuhakikisha watakaochaguliwa kwenye kata ni watu wao ili waje wawachague kwenye wilaya.Vivyo hivyo kwa makada tuliowaspot kwenye mikoa wahakikishe wanaochaguliwa kwenye wilaya ni wale makada wetu ili nao waje wawachague kwenye mikoa yao. Hapa ndipo kwenye kazi kubwa ya mkakati wetu na hapa ndipo tutakapohitaji kuingia gharama zaidi kwa ajili ya kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa kwa asilimia angalau 80.

Awamu ya tatu ni kuanzia baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa mikoa hadi uchaguzi wa kitaifa utakapoitishwa. Katika kipindi hiki kwa ustadi mkubwa tutakuwa tukiwaandaa makada wetu waliochaguliwa tayari kuja kufanya mabadiliko makubwa kitaifa. Ni wakati huu ambapo tutawaingizia mkakati taratibu lakini kwa ustadi mkubwa tukijikita hasa kwenye kuonyesha kwa nini tunahitaji mabadiliko. Ni katika kipindi hiki ambapo kwa ustadi mkubwa tunaweza kuwaspot wale waliochaguliwa ambao hatukuwaandaa na kuwaingizia pia mbegu ya mabadiliko ili kuwawin na kuwarecruit kwenye mkakati.

Aidha katika awamu zote tatu kazi ya kuianalyze ofisi kuu itakuwa non stop kwa kuzingatia kwamba mabadiliko ya wakurugenzi na maofisa yatakuwa yanatokea na watu nao watakuwa wanabadilika kimtazamo. Analysis ya ofisi kuu ni kuhakikisha tunajua nani na nani wako na sisi na nani na nani wako against na pia nani na nani wanaweza kupandikiziwa mbegu kwa ustadi na wakaungana nasi.
MAHITAJI YA KUFANIKISHA MKAKATI:
Raslimali watu. Tunahitaji watu waaminifu watatu kwenye ngazi ya kitaifa ambao tayari wapo. Tunahitaji watu waaminifu kumi kwenye kanda ambao tutawatafuta na pia waaminifu wengine 30 kwenye mikoa yote thelathini.

Fedha. Tunahitaji fedha kwa ajili ya mawasiliano kati ya wanakamati na wale wa ngazi ya chini. Aidha tunahitaji fedha kwa ajili ya gharama za usafiri pale tutakapohitaji kwenda kwenye kanda na mikoa husika kwa ajili ya kusimika watu hao tunaowahitaji.

MAPENDEKEZO MAHSUSI NA HITIMISHO:
Katika kuhitimisha tunapendekeza mambo mahsusi yafuatayo:

Kuhusu Bajeti:
Tunapendekeza kwamba bajeti ya mkakati huu isipangwe hivi sasa. Ni muhimu tu sote kuelewa kwamba wakati wenzetu wanatumia raslimali za taasisi kujijenga na kutekeleza mkakati wao wa ushindi, sisi tunapaswa kuingia mifukoni. Kwa kila kila mmoja wetu atakuwa budget conscious ili kuepuka matumizi makubwa ya pesa. Hata hivyo, kwa kuzingatia kwamba lazima pesa inahitajika ni muhimu M1 na MM kujaribu kuangalia namna ya kuraise pesa na kushauri. Otherwise, tutakapokuwa tunahitaji kufanya hatua yoyote ama jambo lolote tutakuwa ndo tunapiga hesabu za funds tunazohitaji kwa jambo husika na kuingia katika utekelezaji.

Kuhusu mwenendo wa MM kuanzia sasa:
Ni maoni yetu pia kwamba kuanzia sasa MM aenende katika mwenendo ambao utarahisisha ushindi. Mfano tunapendekeza afanye yafuatayo kuanzia sasa:

Apunguze ukaribu na viongozi wa serikali na wa chama tawala na awe crical zaidi na utendaji wa serikali nje na ndani ya bunge.
Ashiriki kikamilifu katika shughuli za taasisi yetu zikiwamo vikao vyote vinavyomhusu, operesheni mbalimbali, chaguzi ndogo, nk.
Aendelee kushusha ‘nondo’ ndani ya chombo chetu cha uwakilishi na kuendelea kuwa juu ya wawakilishi wengine katika hoja mbalimbali zenye maslahi ya kitaifa.

Ajitahidi kudhibiti jazba hata pale anapokuwa amebambikiziwa tuhuma nzito namna gani. Atulie, ashauriane na wazee ili kuona namna nzuri ya kujibu tuhuma zinazomkera. Tukumbuke kwamba wakati mwingine kukaa kimya ni jibu zuri zaidi kuliko hoja nzito.
Sambamba na ‘iv’ hapo juu, adhibiti sana emotion ili kuhakikisha kila kitu kinachofanywa ama kuzungumzwa kinachomgusa asikimbilie kuongea na vyombo vya habari ama kwenye mitandao ya kijamii bali afuate kile tulichokizungumza kwenye kipengele cha ‘iv’ hapo juu.

Kuhusu mapambano ya kuchafuana kwenye mitandao ya kijamii:
Katika hili sisi hatukuona haja ya kufanya hivyo kwa sababu mbili:
Imani yetu kwamba taasisi yetu ni kubwa kuliko watu kwa hiyo ni muhimu kuzingatia kwamba hatuiui taasisi katika mapambano haya. Tukiendekeza mashambulizi kwa njia ya mitandao ya kijamii hatutakuwa na ngao ya kuwakinga watu wa kawaida (wanataasisi na wasio wanataasisi) dhidi ya kujikuta wakiamini kwamba taasisi hii nayo haina jipya ni sawa tu na ile tunayotaka kuitoa.

Tutakuwa tumeiua taasisi na mkakati huu hautakuwa na maana sana kama lengo ni kufanya mabadiliko ya uongozi wa taasisi tu lakini malengo ya taasisi ya mwaka 2015 yasitimie!

Kujikita kwenye mashambulizi kupitia mitandao ni kuzidi kuwashtua wakuu waliopo kwamba bado tuko serious na mkakati wa kuwatoa na kuwafanya wafanye kazi zaidi huku wakiendelea kumpaka matope MM kwamba ndiye anayerusha makombora hayo kwenye mitandao kwa kusudi la kuhujumu taasisi maana hiyo ndo lugha yao. Hatukatai kwamba wakuu wanajua kabisa kwamba bado MM ana nia ya kumvaa mkuu aliyepo lakini tunajua kwamba kwa sasa wanaamini wamemdhoofisha na hana madhara tena. Ndiyo maana tunataka kutekeleza mkakati wetu kwa siri sana ili wafikiri MM amekata tamaa kumbe ndo anakuja na mkakati mzito zaidi.

Hata hivyo, ni muhimu kukumbushana kwamba wenzetu hawatanyamaza kwa sababu eti sisi tumeacha kuwashambulia kwenye mitandao ya kijamii. Lazima wataendelea! Wataendelea kumchafua MM kwa kupitia wapuuzi kama yule kichaa wa ‘ars’ na kundi lake. Nini tutakuwa tunakifanya sasa? Tutahakikisha tuko busy kupost mambo mema na mazuri yatakayokuwa yakifanywa na MM kila wakati na kuzidi kusambaza sifa zake njema kila inapotokea nafasi. Atakayefanya kazi hiyo ni sisi wengine wala si yeye! Pia tutahakikisha kila post ya kumchafua inapatiwa majibu bila kutumia ID yake inayojulikana. Ni vema aidha akatupatia majibu na sisi kuyapost ama afungue ID mpya kabisa ambazo hazijawahi kuwepo kwenye mitandao halafu ndo awe anazitumia kujibu lakini kwa kuzingatia tuliyokwishayazungumza hapo juu yaani kutofanya kwa emotion na kuepuka jazba lakini pia kushauriana na watu wa karibu kabla ya kutoa majibu kwa jambo lolote linalomhusu.

Kuhusu kamati ya kitaifa (hususan M2 & M3):
Tulikubaliana kwa kauli moja kwamba katika kutekeleza mkakati huu tunahitaji members hawa wawe wametulia kimaisha. Inakuwa vigumu kwa mfano kumtaka member aende mahali fulani kwa makusudi ya mkakati huu wakati hajui familia yake nyumbani anaiacha inakula nini. Tuliona kwamba M3 tayari hana kazi kwa sasa tena kwa kufanyiziwa na wakuu waliopo. Ni katika mwendelezo huo huo tunamwona M2 naye akiwa ukingoni kupigwa nje na kuachwa mtupu na wakuu waliopo katika kile wanachokiita wao reshuffle ya ofisi kuu. Kwa sababu hiyo tukapendekeza kwamba MM kwa kushirikiana na M1 kwa hatua ya kwanza wanaweza kutafuta kiasi cha sh. 2m kila mmoja tukijua kwamba kama members hawa wawili wakisaidiwa milioni mbili mbili wanaweza kuanzisha projects ambazo zitawasustain hata kama hawana ajira. Kwa hatua ya baadaye tutasaidiana kuona kama hawa members wanaweza kusecure good employments mahali, provided hazitawazuia kufanya siasa.

ELIMU:MAUMIVU YA KIFUA (ANGINA PECTORIS)

Maumivu haya zaidi uhusisha moyo na yanapomtokea mtu huchukua muda mfupi na huisha, aina hii ya maumivu kwa lugha nyingine ya kitaalamu huitwa Kilio cha moyo ambapo misuli ya moyo inayowezesha moyo usukume damu inakosa hewa ya oksijeni hivyo inachoka na kufanya kazi kwa kujilazimisha ndiyo maana hali ikizidi kuwa mbaya utajikunja inakulazimu upumzike au ukae chini.
Chanzo cha tatizo
Maumivu haya ya kifua kama tulivyoona hutokana na misuli ya moyo kufanya kazi huku ikikosa hewa ya oksijeni. Kwenye misuli ya moyo kuna  mishipa ya damu inayosambaza damu katika misuli hiyo.
Mishipa hiyo inayoitwa Coronary Artery. Mishipa hii ni midogo kwa hiyo huwa inaziba kutokana na mafuta mengi kuzunguka kwenye damu au ‘Cholesterol’ au kwa Kiswahili ‘lehemu.’ Mafuta haya huganda  ndani ya mishipa ya damu hivyo hupunguza kipenyo cha mshipa wa damu au bomba la kupitisha damu na mwishowe kuziba kabisa. Mishipa hii ikiziba katika upande mmoja wa moyo husababisha upande huo kitofanya kazi vizuri.
Mahitaji ya mzunguko wa oksijeni katika misuli ya moyo huwa makubwa pale unapojishughulisha kwa mazoezi, aidha kukimbia, kutembea harakaharaka au kupanda ngazi au mlima, hapo utajisikia pumzi inapungua na kifua kinauma.
Maumivu ya kifua zaidi huwa upande wa kushoto na wakati mwingine yakielekea mgongoni upande huohuo.
Jinsi tatizo linavyotokea
Kama tulivyoelezea jinsi maumivu yanavyotokea, mgonjwa atagundua kwamba anatatizo hili la Angina endapo siku zote anaishi vizuri tu, hana presha ya kupanda wala kushuka lakini si mtu wa kufanya mazoezi lakini akijishughulisha kwa mazoezi au kupanda ngazi anapata shida hasa kupanda mlima.
Maumivu anayoyapata katika upande huo wa kifua huwa kama vichomi ambapo kitaalamu tunasema ‘constricting, squeezing or choking’ anajihisi kama  ametiwishwa zigo zito kifuani kwake lakini akikaa na kupumzika  yanaacha.
Maumivu haya yana tabia ya kusambaa endapo yatakuwa makali au utakuwa unayavumilia, husambaa upande wa kifua kushoto kuelekea mgongoni na katikati ya kifua na kuhisi kama unakiungulia yaani moto mkali ndani ya kifua.
Mgonjwa pia anaweza kuhisi maumivu katika bega la kushoto au mabega yote.
 Kwahiyo hata ukiwa umekaa tu utahisi mabega yanauma na kifua kinauma katikati na kusambaa hadi mgongoni na mwili kuwa mchovu. Hali ikiwa mbaya maumivu husambaa hadi shingoni na kwenye mataya na kujihisi kila wakati wewe ni mgonjwa na kuhangaika mara upime malaria, Typhoid au uende kwenye masaji.
Hali hii ya uchovu wa mwili na kujihisi mgonjwa kila wakati husababishwa na misuli ya moyo kutopata oksijeni ya kutosha na mara myingi vipimo vingi utakavyofanyiwa utaambiwa huna tatizo lakini wewe bado unaumwa.
Hali hii huongezeka au huendelea hivyo siku hadi siku endapo akili yako itakuwa na msongo wa mawazo.
Maumivu ya kifua na mwili wakati mwingne huwa makali baada ya tendo la  ndoa.
Maumivu makali na uchovu hupungua dakika ishirini baada ya kujitokeza, unatakiwa upate muda wa kupunguza na  kama ulikuwa unafanya mazoezi uache hadi uonane na daktari wako wa uchunguzi na ushauri.

Uchunguzi
Utafanyika katika hospitali za mikoa, vipimo mbalimbali vinavyohusu moyo hufanyika, historia ya tatizo itachukuliwa kwa undani. Chunguza ulaji na unywaji wako na maisha unayoishi.

Athari za tatizo
Tatizo hili linaweza kukusababishia matatizo makubwa ya moyo ambapo upande mmoja wa moyo unaweza kufa au ‘myocardial infaretion’ endapo tatizo litaendelea kwa muda mrefu, vilevile unaweza kukutwa na mauti ghafla kwa shinikizo au mshtuko wa moyo.
‘Heart Attack. Magonjwa haya tutakuja kuyaona hapo baadaye. Tatizo huathiri nguvu za kiume na  kukosesha hamu ya tendo la ndoa.

Ushauri
Endapo unafanya mazoezi halafu unashindwa kutokana na dalili tulizozielezea au unatembea kwa kupandisha kilima au ngazi inakuwa tabu, basi usidharau muone haraka daktari wako kwa uchunguzi. Pia hata ukiona kabla na wakati wa tendo la ndoa unahisi moyo unaenda mbio basi wahi hospitali. Epuka unywaji pombe, ulaji wa vyakula vyenye mafuta na uvutaji wa sigara,
Pendelea kufanya mazoezi, Tatizo ni kubwa  kwa wasiofanya mazoezi, tumia hata nusu saa kwa siku.

GPL

MKE NUSURA ATOLEWE ROHO KISA UNYUMBA!

Sada Majaliwa mkazi wa Temeke Mikoroshini jijini Dar.
Stori: IMELDA MTEMA
MWANAMKE mmoja Sada Majaliwa mkazi wa Temeke Mikoroshini jijini Dar, amedai kunusurika kutolewa roho na mumewe Mohamed Rashid hivi karibuni kwa kosa la kunyimwa unyumba.
Akizungumza na mwandishi wetu, Sada alisema siku ya tukio, mumewe alirudi nyumbani usiku akiwa amelewa na  kudai unyumba kwa nguvu, jambo ambalo hakukubaliana nalo na kusababisha kutokea kasheshe kati yao.
“Siku zote nimekuwa nikimpa unyumba kama kawaida, lakini siku hiyo mwenzangu alirudi akiwa amelewa chakari, sikupendezwa na hali yake ndiyo maana sikutaka kushirikiana naye,” alifafanua Sada.
Mke huyo alisema baada ya kukataa kushiriki tendo hilo, mumewe alianza kumkaba shingoni kwa kutumia mikono yake, lakini alipoona haitoshi akachukua khanga na kuendelea kumkaba nayo.
Sada alidai kwamba hali ilikuwa mbaya na alishindwa kujiokoa kirahisi na kulazimika kumng’ata mumewe mkononi ndipo alipojiokoa huku shingo yake ikiwa imechubuka.
“Baada ya kunikaba na khanga shingoni sikuwa na jinsi ilinibidi nimng’ate ndipo aliponiachia na kupata upenyo wa kutoka nje,” alisema.
Sada alidai baada ya tukio hilo yeye na watoto wake walikimbilia kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, Rehema Bakari kuomba hifadhi wakati akisubiri mwafaka na mumewe.
Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo mume wa Sada amekamatwa na polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.
“Mume wake amekatwa leo (Jumatano iliyopita) lakini nitaendelea kumhifadhi mwanamke huyu hadi pale suala lake litakapopata mwafaka,” alisema mwenyekiti huyo wa serikali ya mtaa.

GLP

P-SQUARE WATUA DAR


Wanamuziki wa kundi la P-Square Peter na Paul baada ya kutua jijini Dar usiku wa kuamkia leo. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkrulu ambao ndio wadhamini wakuu wa onesho lao ambalo limeratibiwa na East Africa Radio na EATV.
 
 Hapa wakifanya mahojiano na kituo cha East Africa TV ambao ndio wenyeji wao.
Mahojiano na picha za hapa na pale zikiendelea.
Vijana wakielekea kupumzika tayari kwa kazi ya kesho

Thursday 21 November 2013

Babu Seya na Papii walivyoyasema kabla ya kurudishwa gerezani.

Ni dhahiri kwamba huu ndio mwisho wa harakati za Mwanamuziki maarufu wa muziki wa dansi Tanzania mwenye asili ya Congo DRC Nguza Viking na mtoto wake Johnson Nguza (Papii kocha) kujinasua kwenye kifungo cha maisha gerezani.
Kwa mara nyingine tena harakati zao za kujitoa kwenye adhabu hiyo zimegonga mwamba baada ya Mahakama ya Rufani kupigia msumari wa mwisho uliozima harakati zao kujinasua baada ya kutupilia mbali maombi yao ya marejeo ya hukumu ya rufaa yake.
hii ni mara ya tatu kwa wafungwa hawa kugonga mwamba baada ya Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam na Mahakama ya Rufani kutupilia mbali rufaa zao kupinga hukumu ya Mahakama ya hakimu mkazi  kisutu iliyowahukumu kifungo cha maisha.
Wafungwa hawa kupitia kwa Wakili Mabere Marando walikua wakiiomba Mahakama ya Rufani ifanye marejeo ya hukumu yake ya February 11 2010 iliyothibitisha adhabu hiyo waliyohukumiwa na Mahakama ya chini na badala yake iwaachie huru lakini Mahakama ya Rufani katika uamuzi wake uliotolewa na Majaji watatu, Nathalia Kimaro, Salum Massati na Mbarouk Mbarouk ilitupilia mbali maombi hayo hivyo waendelee kutumikia kifungo cha maisha gerezani.
Ni uamuzi ambao uliibua machungu sio tu kwa Wafungwa na ndugu zao lakini hata kwa Wakili wao mwingine Gabriel Mnyele aliesema ‘hakuna namna nyingine ya kuwachomoa kwenye adhabu hii isipokua miujiza’
Ndugu na watu wengine waliohudhuria Mahakamani waliendelea kutokwa na machozi ya huzuni pale Wafungwa hawa walipokua wakipandishwa kwenye gari la Magereza kurudishwa kuendelea kutumikia adhabu yao.
Kauli ya Mahakama baada ya kutupilia mbali maombi yao ni ‘Waomba Marejeo hao hawakuwa na hoja ya msingi kwa sababu hoja zilizotolewa sio tu hazikidhi kuifanya Mahakama irejee hukumu hiyo bali pia zilishatolewa wakati wa usikilizwaji wa rufaa na kutolewa uamuzi na kwamba waomba Marejeo hawakuweza kubainisha makosa waliyodai yalijitokeza kwenye hukumu iliyowatia hatiani na hawakuweza kueleza ni jinsi gani yalisababisha haki kutotendeka’
Mahakama hiyo imesema ‘kuhusu upande wa mashtaka kushindwa kuwaita Mahakamani mashahidi wanaoonekana kuwa muhimu kuunga mkono ushahidi wa Watoto, tunasema hoja hiyo haina msingi…. suala la shahidi gani aitwe Mahakamani kuthibitisha kesi ya upande wa mashtaka liko mikononi mwa upande wa mashtaka, zaidi ya yote idadi ya Mashahidi sio hoja ya msingi bali kuaminika kwao’
Wakili Mnyele amesema ‘huu ndio mwisho wa mchakato, kulinganisha na hukumu ilivyokua ni kwamba kunahitajika kuwepo na Mahakama ya juu zaidi ya hii, kungekuwepo na Supreme Court ingeweza kusikiliza na kufikia maamuzi ya haki’
Kwa upande wake, Babu Seya wakati akipelekwa na askari kwenye gari la Magereza alitoa kauli ambayo hakuipa ufafanuzi wowote baada ya kuisema kwamba ‘kwa binadamu ni makosa lakini kwa Mungu hakuna makosa’
Papii Kocha nae wakati anapelekwa kupanda gari arudishwe Magereza alisema ‘sasa tunamuachia tu Rais ndie anaweza kutoa uamuzi wa mwisho’
Babu Seya na wanawe watatu walihukumiwa adhabu ya maisha gerezani na Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu June 25 2004 baada ya kupatikana na hatia ya kuwabaka na kuwalawiti watoto kumi wa kike wenye umri chini ya miaka 10.

Joseph Kony ataka kujisalimisha?


Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya kati inasema inajadiliana na kiongozi aliyetoroka wa waasi kutoka Uganda Joseph Kony.
Msemaji wa serikali ameiambia BBC kwamba Joseph Kony alikuwa katika Jamhuri ya Afrika ya kati, lakini alitaka kuhakikishiwa usalama wake kabla hajajisalimisha.
Marekani imekuwa ikivisaidia vikosi vya Uganda kumsaka Kony.
Kony, ni kiongozi wa kundi la waasi la LRA, na anatakikana na mahakama ya kimataifa ya jinai kwa madai ya uhalifu wa kivita.
Kony, ni kiongozi wa kundi la waasi la LRA, na anatakikana na mahakama ya kimataifa ya jinai kwa madai ya uhalifu wa kivita.
Marekani ilikuwa imeahidi kumtuza dola milioni 3.3 yeyote mwenye taarifa itakayopelekea kukamatwa kwa Kony
Hii ni mara ya kwanza kwa miaka mingi, kwa taarifa kuhusu aliko Kony kutolewa.
Pia mnamo siku ya Jumatano, mjumbe maalum wa muungano wa Afrika kuhusu LRA, Francisco Madeira, aliambia baraza la usalama la umoja wa mataifa, kuwa aliona ripoti kuwa Kony anaugua ugonjwa mbaya sana usiojulikana.
Mnamo mwezi Aprili, jeshi la Uganda lilisitisha msako dhidi ya Kony katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati, likisema kuwa linabiliwa na mashambulizi makali kutoka kwa serikali waasi walipochukua mamlaka baada ya mapinduzi.
Joseph Kony pamoja na wapiganaji wake walio kati ya 200-500, wamekuwa wakipigana dhidi ya serikali ya Uganda kwa zaidi ya miaka 20.

Tajiri Simba awafuata Yondani na Msuva


KIGOGO mmoja mwenye ushawishi mkubwa Simba na anayewania kugombea uongozi mwakani (jina tunalo), ameanza mazungumzo ya faragha na wachezaji wawili wa Yanga.
Wachezaji hao ambao mikataba yao inamalizika ndani ya miezi sita ijayo ni beki kisiki, Kelvin Yondani na winga mwenye kasi, Simon Msuva.
Habari za ndani ambazo Mwanaspoti inazo ni kwamba kiongozi huyo amepanga kuwasainisha wachezaji hao ambao kuanzia mwezi ujao kikanuni watakuwa huru kufanya mazungumzo, kama sehemu ya kampeni zake kwenye uchaguzi huo.
Yondani aliondoka Simba misimu miwili iliyopita na kusababisha madhara kwenye safu ya ulinzi ya Wekundu hao wa Msimbazi kwani wamekuwa wakikosa mbadala makini, ingawa kurejea kwa Joseph Owino na usajili wa Gilbert Kaze vimewapa ahueni.
Mwanaspoti linajua kuwa Yondani na Msuva ingawa wamegoma kukiri lakini wamekuwa wakishawishiwa na kigogo huyo wa Simba na wameelekea kuridhia ndio maana hawajataka kupaparika kufanya mazungumzo mapya na Yanga.
Msuva ambaye alijiunga na Yanga akitokea Moro United iliyoshuka daraja amekuwa kwenye fomu kwa kipindi kirefu na jana Jumatano alisema: “Nimebakiza muda wa miezi sita katika mkataba wangu na Yanga, kisheria sina kipingamizi cha kufanya mazungumzo na timu yoyote kuhusu hatma yangu ya soka, ila bado sijazungumza na Yanga kuhusiana na suala la kuongeza mkataba mpaka sasa, nasubiri kumalizia mkataba wangu na Yanga, endapo watafuata yale ninayoyataka, haitakuwa shida kuendelea kuichezea Yanga, lakini kama itakuwa kinyume, itakuwa tofauti.”
Yondani kwa upande wake alisema mkataba wake unamalizika mwakani mwezi Mei na suala la kuongeza mkataba litatokana na makubaliano baina yake na timu yake ya sasa na hata timu nyingine itakayomuhitaji.
“Mkataba wangu unamalizika baada ya msimu huu, kwa sasa nipo huru kufanya maandalizi ya kazi yangu kwa kufanya mazungumzo na timu zozote, ila kusaini Yanga nahitaji kupata muda wa kutafakari na kama watafuata masharti yangu nitakubaliana nao,” alisema Yondani bila kufafanua ni masharti yapi wala hakukiri kufuatwa na Simba.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Yanga, Abdallah Bin Kleb ambaye mara kadhaa amekuwa akiigaragaza Simba katika vita ya kuwania mchezaji, alisema kuwa hawajafanya mazungumzo na Yondani na Msuva lakini hawana papara kwavile bado ni mali yao mpaka mwisho wa msimu.
“Msuva na Yondani ni wachezaji wetu, bado wana mkataba na sisi na si siri kwa kipindi ambacho wamebakiza tunajipanga kujua tunafanya nini kwao, muda ukifika tutawajulisha, hatuna papara katika usajili, tunachofanya sasa ni kusaka straika wa kigeni kutoka nje,” alisema Bin Kleb kwa kujiamini huku akionyesha kutokuwa na presha ya kuwapoteza wachezaji.
Habari za ndani zinadai kwamba baadhi ya wanachama maarufu wa Simba wameanza mikakati ya chinichini kujipanga kuwania uongozi wa juu klabu hiyo kwenye uchaguzi utakaofanyika baada ya kumalizika kwa ligi mwakani.

Mwaspoti

BREAKING NEWS:BABU SEYA, PAPII KOCHA WASHINDWA TENA, WAREJESHWA JELA MAISHA.Ile hukumu ya rufaa ya mwanamuziki Nguza Viking na mwanaye Johnson Nguza 'Papii Kocha' imewarejesha jela maisha baada ya hoja za serikali za kukazia hukumu kuzidi zile za upande wa utetezi.Babu Seya na Papii Kocha walihukumiwa kifungo cha maisha jela mwaka 2004 baada ya kupatikana na hatia ya kuwanajisi watoto wa Shule ya Msingi, Mashujaa, Sinza jijini Dar ambapo wamekuwa wakikata rufaa mara kwa


BREAKING NEWS:BABU SEYA, PAPII KOCHA WASHINDWA TENA, WAREJESHWA JELA MAISHA.Ile hukumu ya rufaa ya mwanamuziki Nguza Viking na mwanaye Johnson Nguza 'Papii Kocha' imewarejesha jela maisha baada ya hoja za serikali za kukazia hukumu kuzidi zile za upande wa utetezi.Babu Seya na Papii Kocha walihukumiwa kifungo cha maisha jela mwaka 2004 baada ya kupatikana na hatia ya kuwanajisi watoto wa Shule ya Msingi, Mashujaa, Sinza jijini Dar ambapo wamekuwa wakikata rufaa mara kwa

Kutana na picha za kiatu chenye AC.


7
Hydro-Tech ambayo ni kampuni ya Japan ndio imetengeneza hiki kiatu ambacho bei yake ni dola za Kimarekani 75 ambazo ni kama laki moja na 20 za kibongo.
As MobileMag explains, the way these shoes work is a bit different from our conventional understanding of “air conditioning”:
The shoes don’t have a mini air conditioner integrated inside, but rather rely on a new filter technology that releases heat and humidity and allows air to flow, for your feet to feel refreshed and clean
4
1
2

Yanga yatikisa nchi nzima

WATAALAMU wa hesabu wana usemi wao wanaoupenda ‘Namba haziongopi’. Ukirudisha usemi huo kwenye tathimini ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara, lugha nyepesi unayoweza kusema ni kwamba ‘hakuna kama Yanga’.
Sahau kwamba imemaliza ikiwa kileleni na pointi zake 27. Takwimu za Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL), zimethibitisha kwamba Yanga imeongoza takwimu zote kuanzia mapato mpaka idadi ya mashabiki walioingia uwanjani.
Takwimu zilitolewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPL,  Silas Mwakibinga, ni kuwa Yanga imekusanya kiasi cha Sh334.2 milioni katika mechi 13 za mzunguko huo. Katika takwimu hizo, Simba SC ni ya pili kwa kupata Sh304 milioni huku timu iliyopanda daraja msimu huu, Mbeya City, ikiipiku Azam FC kwa kushika nafasi ya tatu kwa kujikusanyia Sh83.8 milioni. Azam imekusanya Sh67.1 milioni.
Nyingine na fedha zilizokusanya katika mabano ni Coastal Union (Sh65. 7 milioni), Mtibwa Sugar (Sh49.9 milioni), Ruvu Shooting (Sh46.1 milioni), Tanzania Prisons (Sh38.1milioni), JKT Ruvu (Sh36.1 milioni), Ashanti United (Sh35.7 milioni), Rhino Rangers (Sh31.1milioni), Mgambo JKT (Sh25.8 milioni), Oljoro JKT (Sh20.8 milioni) na Kagera Sugar (Sh18.5 milioni).
“Huu ni mwanzo tu wa kusimamia ligi na mpaka sasa hatujafikia lengo letu, tunataka kuona kila timu inakuwa na uwiano sawa wa makusanyo na kama kuzidiana, basi iwe kiasi kidogo, tumefurahishwa na mwenendo wa Mbeya City ambao wamefanya mambo makubwa japo wapo katika msimu wa kwanza,” alisema Mwakibinga.
Kwa upande wa mashabiki walioingia viwanjani, Yanga pia imekuwa kinara kwa kuingiza mashabiki wengi katika mechi. Jumla ya mashabiki 107,890 wa timu hiyo wameingia katika mechi na kufuatiwa na Simba ambao wameingiza mashabiki 97,364 mpaka mwisho wa mzunguko huo.
Timu ya Mbeya City imezidi kung’ang’ania nafasi ya tatu na kuendelea kuitambia Azam FC kwa kuingiza mashabiki 43,439 tofauti na Azam ambao mpaka sasa wameingiza mashabiki 30,236.
Nyingine ni Coastal Union (mashabiki 27,880), Mtibwa Sugar (20,794), Rhino Rangers (20,263), Prisons (19,923), Ruvu Shooting (19,000), JKT Ruvu (16,095), Ashanti United (16,093), Mgambo (11,726) na JKT Oljoro (10,430).
Kwa mujibu wa Mwakibinga, jumla ya Sh 2.4 bilioni zimekusanywa katika mzunguko huo wa kwanza. Kiasi hicho ni ongezeko la Sh599. 5 milioni katika mzunguko wa kwanza wa msimu uliopita.
“Hii ni historia na hasa ukizingatia kuwa baadhi ya mechi zimekuwa zikionyeshwa ‘laivu’ katika televisheni na baadhi ya mashabiki kuangalia kupitia luninga zao, lakini bado tumezidi kupata makusanyo makubwa,” aliongeza Mwakibinga.
“Haya ni matokeo mazuri ya kuzinadi mechi za ligi na mfano mzuri mechi ya Yanga na Mbeya City ambayo iliweka historia kwa kuingiza Sh100 milioni na huku tiketi zikiwa zimemalizika kufikia saa 5:00 asubuhi ya siku ya mchezo.”
Kwa upande wa viwanja, Uwanja wa Taifa unaongoza kwa kukusanya fedha nyingi mpaka sasa ambapo kiasi cha Sh1.8 bilioni kimepatikana hapo, kiwango hicho ni sawa na asilimia 75 ya mapato yote ya mzunguko wa kwanza.

Mwanaspoti