Sunday 10 November 2013

Al Shabaab: 'Tumeshambulia hoteli


Wapiganaji wa Kiislamu wa Al Shabaab nchini Somali wamesema wao ndio waliotekeleza shambulizi la bomu la kujitoa muhanga nje ya hoteli katika mji mkuu wa Mogadishu nchini Somalia ambapo watu sita waliuawa wakiwemo maafisa wa polisi.

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amelaani shambulio hilo lilitokea nje ya Hotel ya Maka al Mukurama huku akisisitiza kuwa shambulio halitarudisha nyuma jihada kubwa zinazoendelea za kuleta amani na usalama nchini humo.
Kundi hilo la Al Shabaab ambalo lilifurushwa na majeshi ya Somalia yakishirikiana na yale ya Umoja wa Mataifa AMISOM miaka miwili iliyopita wameapa kuendeleza harakati zao za kufanya mashambulizi.
Hapo awali Waziri wa Mambo ya ndani wa Somalia Abdikarim Hussein Guled aliiambia BBC kuwa watu sita waliuawa na wengine 15 kujeruhiwa katika shambulio hilo la kujitoa muhanga.
Mwandishi wa BBC Ibrahim Mohamed Adan ambaye yupo Mogadishu amesema sauti ya mlipuko ulisikika katikati ya mji huo wa Mogadishu.

No comments:

Post a Comment