Tuesday 12 November 2013

wanaowania kuwa mwanasoka bora zaidi Afrika


wachezaji Afrika 
Majina ya wanaowania tuzo ya BBC ya mchezaji bora zaidi barani Afrika mwaka wa 2013 yametangazwa rasmi hii leo kupitia kipindi cha kiswahili cha Amka na BBC ambapo shindano hili huwahusisha wachezaji kutoka Africa likiwa limeanzisha miaka kadhaa iliyopita.
Yaya Toure wa Ivory Coast yuko katika orodha hiyo kwa mara ya tano, wengine ni Victor Moses na John Mikel Obi wa Nigeria, Jonathan Pitripia wa Bukina Faso na Pierre- Emerick Aubameyang wa Gabon.
Mshindi atachaguliwa na mashabiki wa soka ambao watapiga kura hadi tarehe 25 Novemba saa tatu usiku saa za Afrika Mashariki so unaweza kupiga kura kwenye tovuti ya bbc au kwa kutuma ujumbe mfupi kupitia namba ifatayo +44 7786 20 20 08
Tuma 1 ili kumpigia kura Pierre-Emerick Aubameyang
Tuma 2 ili kumpigia kura Victor Moses
Tuma 3 ili kumpigia kura John Mikel Obi
Tuma 4 ili kumpigia kura Jonathan Pitroipa
Tuma 5 ili kumpigia kura Yaya Toure

No comments:

Post a Comment