Monday 11 November 2013

Yaliyotikisa mkutano wa 13 wa Bunge

Mkutano wa 13 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliomalizika juzi mjini Dodoma, umeandika historia mpya kutokana kuwapo kwa mambo makuu manne yaliyolipa Bunge hilo sura tofauti na mikutano mingi iliyopita.
Mambo hayo ni pamoja na tukio la nadra la muswada wa Serikali kuungwa mkono na pande zote ndani ya Bunge, kukataliwa kwa mapendekezo ya marekebisho kandamizi  katika Sheria ya Magazeti ya 1976, kuwapo kwa mjadala mpana kuhusu mambo ya dharura na hotuba ya Rais Jakaya Kikwete iliyotoa msimamo kuhusu uanachama wa
Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Hata hivyo, kuna  mambo kadhaa ambayo yamebaki viporo yakisubiri kuingizwa katika ratiba ya mkutano wa 14  uliopangwa kuanza Desemba 13 mwaka huu, ukihamishwa kutoka Februari 2014 ili kupisha Bunge Maalumu la Katiba ambalo litaketi kati ya Januari na Machi, mjini Dodoma.
Mambo hayo ni kujadiliwa kwa Sheria ya Kura ya Maoni ambayo ilifanyiwa marekebisho makubwa, mrejesho wa Kamati Teule ya kuchunguza migogoro baina ya wakulima, wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi.

No comments:

Post a Comment