Tuesday 12 November 2013

Ni hii alama tu ya hivi vidole vyake imemfanya huyu mchezaji wa Misri kuadhibiwa.


egypt 12

Unaambiwa club ya Al Ahly imemuadhibu mchezaji wake aitwae Ahmed Abdul Zaher kwa kitendo alichofanya cha kuonyesha alama za vidole kama unavyomuona hapo chini ikiwa ni ishara ambayo imekua ikitumiwa na wanaomuunga mkono rais Mohammed Morsi aliepinduliwa July 2013 na kwa sasa anakabiliwa na kesi ya kuchochea mauaji.
Club ya Al Ahly imesema Ahmed Abdul Zaher hatokwenda kwenye michuano ya  Fifa Club World Cup mwezi ujao huko Morocco kutokana na alama ya vidole vinne aliyoionyesha kwenye mechi Jumapili wakati akishagilia goli ambapo pamoja na madai yote hayo, Zaher anasema… yes alinyoosha alama hiyo lakini hakua na maana yoyote au kussuport chochote cha siasa.
Hii ni mara ya pili kwa mchezaji mkubwa wa Egypt kuadhibiwa kwa kuonyesha alama hii ambapo mwezi uliopita mchezaji wa Kung fu Mohammed Youssef aliadhibiwa kwa kufungiwa kutocheza nje wala ndani ya nchi kwa muda wa miaka miwili baada ya kuonyesha alama hiyohiyo.



No comments:

Post a Comment