Wednesday 20 November 2013

Kocha mpya Simba huyu hapa

SIMBA imemtangaza kocha wake mpya kuwa ni Zdravok Logarusic, raia wa Croatia.
Awali ilielezwa kocha mpya kuwa ni Robert ‘Bobby’ Williamson ambaye baadaye iligundulika ni uongo mtupu baada ya gazeti hili kufanya naye mahojiano jijini Nairobi.
Lakini jana uongozi wa Simba umemtangaza rasmi Logarusic ikiwa ni dakika chache baada ya kuwatimua Abdallah Kibadeni na msaidizi wake, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ anayejulikana kwa maneno mengi.
Kaimu Mwenyekiti wa Simba, Joseph Itang’are ‘Mzee Kinesi’, amesema kocha Selemani Matola ndiye atashirikiana na Logarusic kukinoa kikosi hicho.
“Kocha mpya atawasili nchini Desemba Mosi na ataanza kasi siku inayofuatia,” alisema Mzee Kinesi.
Logarusic aliyekuwa kocha mkuu wa Gor Mahia ya Kenya na kocha bora wa Kenya kwa msimu wa 2011-12, atasaini mkataba siku atakayowasili.
Kuhusiana na kufutwa kazi, Kibadeni alisema jana amekuwa akisikia tu taarifa hizo.
“Nasikia tu, sijapata lolote kiofisi kutoka kwa uongozi. Lakini wakinieleza basi sawa, sitakuwa na cha kufanya,” alisema.

No comments:

Post a Comment