Monday 11 November 2013

SAKATA LA MWINGIRA KUDAIWA KUZAA NA MKE WA MTU, RAIS KIKWETE AINGILIA KATI

JK, aliingilia kati sakata hilo baada ya mume wa mtu, Dk. William T. Morris, kukamatwa na maofisa wa uhamiaji kisha kutakiwa kufukuzwa nchini kutokana na kile kinachodaiwa ni ‘shinikizo la mtu mwenye nguvu’.
Habari ambazo Uwazi limezithibitisha ni kwamba baada ya Dk. Morris kufungua mashtaka akimtuhumu Mwingira kuzaa na mkewe, Dk. Philis Nyimbi, alikamatwa na maofisa wa uhamiaji kisha kupewa hati ya kutimuliwa nchini.
Uwazi limebaini kuwa JK ndiye aliyezuia hati hiyo na mpaka sasa, Dk. Morris, raia wa Liberia, yupo nchini akiendelea na harakati zake za kusaka haki kisheria kuhusiana na madai yake hayo.

No comments:

Post a Comment