Sunday 10 November 2013

Maneno ya M/kiti kamati ya uwiano kuhusu alichosema Rais JK kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

EAC viongozi
Baada ya Rais Jakaya Kikwete kuzungumza bungeni 104.4 Dodoma kwamba Tanzania haitojitoa kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki japo viongozi wa nchi tatu ambazo ni Kenya, Uganda na Rwanda wamekua wakikutana mara kadhaa bila kumshirikisha, Kamati ya uwiano imenena.
Mwenyekiti wa kamati ya uwiano ya Mabunge ya kanda ya Afrika Mashariki  Florence Kajuju anakwambia Marais wa mataifa ya kanda hii ni lazima wakutane na wasuluhishe malalamiko yaliyotolewa na Rais Kikwete.
Baada ya kutoa kauli hiyo fupi na nzito, Kajuju amesema kamati yake itasimamia na kuhakikisha zoezi la kuwaweka pamoja tena viongozi hawa na kila kitu kikawekwa kwenye mstari, linafanikiwa.
Namkariri akisema ‘pamoja na kwamba Rais Kikwete amesema nchi yake haitojitoa kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki, kama kuna ishu nyeti kama hii ni lazima tukae kuimaliza ili tuweze kuendelea mbele kwa umoja’
President Jakaya Kikwete kwenye hotuba yake November 7 2013 alisema ‘Unajiuliza maswali mengi mpaka unakosa majibu, wenzetu hawa wamekosa imani na Jumuiya wanataka kuunda yao? au wanaichukia nchi yetu na wameamua kutufanyia vitimbi tutoke, au sijui wanachuki na mimi? nataka niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge kwamba hatuna mpango wa kutoka katika Jumuiya, tupo na tutaendelea kuwepo…. Tanzania haijafanya jambo lolote baya dhidi ya Jumuiya au nchi yoyote Mwananchama, kama kuna ushahidi watuambie tu’

No comments:

Post a Comment