Sunday 10 November 2013

Diamond awataja mademu zake wanne, lakini anampenda zaidi ni huyu hapa


Mwanaspoti: Tuzungumzie uhusiano wako. Mpenzi wako wa kwanza unamkumbuka? na je uliwahi kumpa shilingi ngapi?
Diamond: Mpenzi wangu wa kwanza kabisa enzi hizo ninajifunza mambo haya sikumbuki vyema jina ila alikuwa anaishi Tandale na mimi pia nilikuwa naishi huko na mama yangu. Sikumbuki kama nimewahi kumhonga maana enzi hizo mimi nilikuwa napewa tu na mama yangu pesa, sikuwa na hela yoyote ya kumpa na ilikuwa ni kwa kipindi kifupi kama miezi minne hivi, hata hivyo tulikuwa tunaibana tu kwa siri nilikuwa mdogo.
Mwanaspoti: Kwanini mliachana?
Diamond: Kwanza nilikuwa sijajua mapenzi ni nini. Hata hivyo haikuwa rasmi na wala nilikuwa sijawa na akili ya kupenda sana na nilikuwa na fikra kwamba ni mchezo tu hivyo tuliachana mapema kwani hata yeye akili yake ilikuwa haijakomaa.
Mwanaspoti: Mpenzi wako uliyekuwa naye kabla ya kuwa staa nasikia uliachana naye baada ya kutoka kimuziki kwa nini?
Diamond: Nilimpenda sana lakini aliniacha kabla ya kutoka. Mpenzi wangu wa kwanza alikuwa anaitwa Sarah Sadick, sijawahi kumuhonga na ndiye mwanamke niliyewahi kumpenda sana. Wakati huo Naseeb Abdul kabla sijawa Diamond nilikuwa nahaha kuhangaika ni vipi nitatoka kimuziki. Msichana huyu ndiye aliyenipa hasira za kufanya muziki kwa bidii zote baada ya kunitema na kuanza kuhangaika na wengine na aliniita majina mengi yasiyo mazuri, kisa sina fedha. Si kwamba nilimuacha bali yeye ndiye aliyeniacha kama zali baada ya wiki kadhaa nikatoka na wimbo Kamwambie, taratibu nikaanza kuwa staa naye akaanza kurudi ila nilishamuondoa moyoni mwangu.
Mwanaspoti: Kwa nini mliachana? Unadhani hakukufaa tena kwa kuwa ulishakuwa staa?
Diamond: Alinisumbua sana kutokana na ugumu wa maisha niliokua nao kwa kipindi cha nyuma hadi kufikia 2009. Nilimpenda sana huwezi amini nilikuwa silali usingizi kwa ajili yake. Nahisi ilitokana na mimi kukosa kazi ndiyo maana ilifikia hatua alinipotezea. Lakini baada ya kupata na kujulikana alinifuata lakini sikutaka tena hata baada ya kuniomba msamaha.
Mwanaspoti: Umewahi kuwa na wanawake wangapi tangu uwe staa?
Diamond: Sikumbuki kwa kweli wapo wengi mno, si unajua tena wapo walionitaka na kunilazimisha nifanye hivyo, lakini idadi kamili siwezi kukumbuka na kila siku nasumbuliwa na hawa wanawake.
Mwanaspoti: Ni wapenzi wangapi ambao umekuwa nao kipindi kirefu na kuwapenda kama wapenzi wako?
Diamond: Nimewahi kuwa na wapenzi wanne katika kipindi chote cha ustaa wangu na sikupenda kubadili ovyo ila wengi wao hawakuweza kutimiza haja ya moyo wangu.
Mwanaspoti: Unaweza kuwataja majina?
Diamond: Ndiyo ila wawili wanafahamika zaidi. Wa kwanza kabisa alikuwa anaitwa Sarah na wa pili alikuwa anaitwa Hawa yule msichana niliyeimba naye katika wimbo ‘Nitarejea’, huyu alizidiwa ujanja na Wema Sepetu ambaye naye alikuja kuondoka kwangu na baadaye nikawa na Penieli Mungilwa.
Mwanaspoti: Mwanamke yupi unahisi ulimpenda kuliko wote?
Diamond: Mwanamke wangu wa kwanza Sarah Sadick huyu aliniingia sana moyoni sijajua ni kwanini. Lakini nahisi huenda kwa kuwa awali alinipenda kweli kwa kuwa wakati huo sikuwa na kitu. Hata hivyo nahisi ilitokana na mimi kutokuwa bize na wakati huo sikufikiria lolote zaidi ya yeye ilitokana na kutokuwa na kazi ya kufanya. Siku hizi sina mapenzi ya kivilee, nawaza zaidi pesa na ninaihangaikia na zaidi ni muziki wangu, hili ndilo la kwanza kabisa linalonifanya niwe bize mapenzi baadaye.
Mwanaspoti: Umeshawahi kutongozwa na wanawake?
Diamond: Ndiyo, wengi sana tena kuna mmoja kati ya wanawake niliowahi kuwa nao alinitongoza yeye mwenyewe ndipo nikawa naye na nilikaa naye katika uhusiano kwa kipindi kirefu tu. Wanaweza kumfikiria mwanamke fulani lakini huwezi amini ukweli ninao mimi mwenyewe na katu hawawezi hata kumhisi. Ninatongozwa sana kwenye mitandao ya kijamii, facebook, whatsapp, Instagram na kwingineko na wapo wasichana ambao wanatafuta namba zangu za simu na kuanza kunisumbua.
Mwanaspoti: Ni mwanamke wa aina gani unataka awe mkeo?
Diamond: Kwanza ninahitaji aijue kazi yangu na ajue kwamba mimi ni mtu maarufu hivyo akubaliane na changamoto mbalimbali atakazokumbana nazo kwa kipindi atakachokuwa ndani ya ndoa, siyo siku mbili anafungasha virago. Pia ajue kwamba nitamsikiliza mama yangu kwanza kabla ya yeye hilo naliweka wazi, yeye ana nafasi yake katika maisha yangu lakini mama yangu nimempa kipaumbele, tatu awe tayari kuishi na mama yangu. Nne awe na akili na mwenye utambuzi na atakayeniongoza katika kazi zangu, sihitaji kuwa na mwanamke golikipa kila siku ategemee kutoka kwangu. Tano awe mzuri, nahitaji mke bwana…yule nitakayeweza kutoka naye out kwenye zulia jekundu, nikapita naye bila tatizo lolote awe mzuri.

Chanzo MWANASPOTI

No comments:

Post a Comment