Wednesday 13 November 2013

Mwaka wa tabu kwa Messi ndani ya Barcelona

Kwa kifupi unaweza kusema huu si mwaka wa Leonel Messi.
Alizoeleka kwa uwezo wake mkubwa wa kufunga na kunyanyasa mabeki, lakini sasa nyota huyo anaandamwa na majeraha.
Uso wake unazungumza yote, nyota huyo anasumbuliwa na tatizo la misuli ambayo sasa yatamfanya kukosa mechi zote zilizobakia kwa mwaka huu.
 Matatizo yote yalianza Aprili 2 kwenye Uwanja wa Parc des Princes walipocheza dhidi ya PSG. Hapo ndipo alipoanza kusumbuliwa na tatizo la misuli.
Alimaliza msimu katika kiwango ambacho si chake na alitegemea baada ya mapumziko wa majira ya joto mambo yangebadilika kwa kuwa Messi hakukuwa na mashindano ya Olimpiki, Kombe la Dunia wala Copa Amerika.
Hata hivyo, Messi kwa mara nyingine alionekana hayuko fiti wakati wa ziara ya Barca barani Asia. Baada ya mechi ya kwanza ya Spanish Super Cup dhidi ya Atletico, ugonjwa wa misuri ukamrudia tena.
 Mwishoni mwa Septemba, mjini Almeria ilitolewa taarifa kwamba Messi bado hayuko fiti. Jumapili iliyopita Messi ameumia tena kwa mara ya nne na sasa mjini Seville na atakaa nje kwa miezi miwili.
 Labda apone kwa haraka kuliko inavyotegemewa, la sivyo nyota huyo wa Argentina ataufunga mwaka huu akiwa na mabao 42 tu.

No comments:

Post a Comment