Saturday 16 November 2013

Eto’o alia hujuma Cameroon

STRAIKA wa Cameroon Samuel Eto’o amewashitua wengi baada ya kudai kwamba kuna baadhi ya wachezaji wa timu hiyo hawataki afunge mabao na hivyo walikuwa hawampi pasi katika mechi yao iliyopita ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Tunisia.
Fowadi huyo alisema mara nyingi alikuwa akirudi katika kwenye kiungo kusaka mipira kwa sababu mbele haikuwa haifiki.
“Huu ni ukweli na haukubaliki,” alisema Eto’o katika mkutano wa waandishi wa habari huko Yaounde juzi Alhamisi.
“Wakati mlipokuwa mkiniona kwenye kiungo natafuta mipira ni kwa sababu mbele ilikuwa haiji. Sasa tunakwenda kwenye mechi muhimu Jumapili, nadhani tusahau haya yote yaliyopita na tuungane tuwe kitu kimoja. Tupeane pasi.”
Kocha Volker Finke alisema hakuwa amelitambua tatizo hilo kwenye mechi hiyo ya kwanza iliyomalizika kwa sare ya bila kufunga.

No comments:

Post a Comment