Wednesday 20 November 2013

Picha na taarifa za mauaji yaliyotokea Ilala Dar november 19 2013, maelezo ya dereva Tax na wengine


IMG_0691

Jumanne ya tarehe 19 Nov 2013 asubuhi kupitia power breakfast ya Clouds Fm wakati kipindi kikiendelea nilisikia taarifa ya mtu kushambulia kwa risasi kisha nae kujiua kwa kutumia bastola Ilala Dar es salaam nikaamua kuifatilia ishu kwa undani.
Kwa ufupi, unaambiwa kijana huyu mkazi wa Mwanza alietekeleza mauaji haya alikodi Tax mpaka nje ya geiti la nyumba aliyokuwemo Mwanamke ambae inadaiwa alikua nae kwenye mahusiano ya kimapenzi.
Muda mfupi baada ya kufika nje ya geiti huku akiwa na bastola yake aliyoiandaa na risasi kadhaa, lilitoka gari kwenye ile nyumba likiwa na huyu Mwanamke pamoja na dereva na abiria wengine wawili, ndipo hapo muuaji akaanza kuwafyatulia risasi ovyo.
Dereva wa Tax aliemleta kwenye eneo la tukio anasema muuaji huyu alianza kuongea nae ghafla kuhusu mapenzi, akisisitiza ‘jana nimechat na mpenzi wangu na mpaka sasa hivi nachat nae’ pamoja na kusema hayo maneno hakumwambia Dereva Tax kama atafanya tukio lolote kuhusu mauaji.
IMG_0699
                   Club ya wazee-ilala.
Tukio hilo ambalo kupitia shuhuda aliyekua akiripoti alisema limetokea asubuhi majira ya saa moja nyumba jirani na club ya wazee maeneo ya ilala, nilifika eneo la tukio lilipotokea mkabala na club ya wazee ambapo nilianza kufanya interview na mtu anaefanya usafi pale club ya wazee na pia ni shoe shine wa mitaa ile ambaye alikuepo mwanzo hadi mwisho wa tukio.
IMG_0703
                                                                 Shuhuda.
Maelezo ya shuhuda huyu ni haya ‘ilikua ni saa 1 na nusu wakati tunamalizia kufanya usafi ndo tunatoka nje tukasikia milio ya risasi yani, tuliposogea tukaona mshkaji [muuaji] anazunguka upande wa pili wa mwanamke kwa sababu ile gari ilikua na watu wanne ndani aina ya toyota Surf rangi nyeupe baada ya hapo ikabidi tuangalie kinachoendelea ni nini tukaona mshkaji [muuaji] anaingia ndani, akatoka akarudi tena kwenye gari akaanza kupiga risasi kwa abiria waliokua ndani ya gari.
‘Ndani ya gari kulikua na abiria watatu na dereva mmoja jumla ya watu waliokua kwenye gari walikua wanne tukaona jamaa ameanza kufyatua risasi kwa yule dada aliekua amekaa mbele, baadae akafyatua tena kwa kaka aliyekua pia mbele kisha akafyatua kwa abiria mmoja aliyekuia ndani ya gari’
IMG_0696
           
Nyumba yenye gheti jeusi ndo nyumba waliyokua wakitokea watu walioshambuliwa kwa risasi.
Sikuishia hapo nikaenda nyumba ya tatu kutoka nyumba yaliyotokea mauaji haya ambapo nilimkuta mama aliepiga simu polisi kuwapa taarifa juu ya mauaji na ndiye aliyekua wa kwanza kusambaza habari kwenye vyombo vya habari.
IMG_0697
   
Vipande vya vioo vilivyovunjika kutoka kwenye toyota surf iliyoshambuliwa.
Maelezo ya mama yalikua hivi ‘siwezi kukumbuka ilikua ni asubuhi ya saa ngapi lakini ni kati ya saa 12 na nusu asubuh na saa 1 na nusu asubuhi nikiwa nyumbani kwangu nyumba kama ya tatu kutoka kwenye nyumba ya tukio nilisikia milio ya mlipuko wa risasi ni zaidi ya milipuko mitatu, nikaweza kupiga simu kwa askari polisi bahati nzuri  namba yake ninayo kwenye simu na akaniomba nidrop simu yangu haraka ili aweze kufanya mawasiliano ya radio ya polisi na baada ya hapo mimi nikateremka chini kwenda kuangalia hali halisi ni nini’
‘Nikakuta kuna gari aina toyota hilux Surf ya rangi nafikiri ya Gold mettalic ikiwa na majeruhi watatu-wawili ndani kuna kaka mmoja na dada mmoja kaka akiwa anapumua na dada nae akiwa anapumua na majeruhi watatu alikua kalala kwenye geti La nyumba ya jirani na nyumba ya tukio nae akiwa anapumua’
IMG-20131119-00050

Aliyekua dereva kwenye gari iliyopigwa risasi.
‘Hali halisi ni kwamba majeruhi hawa watatu tulipowakuta bado wanapumua mimi nikapiga tena simu polisi kuuliza kama tunaweza kubeba hiyo miili kwa sababu hatujui taratibu za kipolisi zikoje kwa hiyo tulifanikiwa kuungana pale watu tulikuepo, tukachukua ile miili bahati nzuri tunaanza kuitoa kwenye magari polisi ndio wakawa wanafika’
IMG-20131119-00045
          
Muuaji ambae ni mkazi wa Mwanza aliyeamua kujiua kwa kujipiga risasi kidevuni na ikatokea juu kwenye paji la uso.
Kamanda wa Polisi Ilala amethibitisha kutokea kwa hili tukio na kusema waliofariki kwenye hili tukio ni watatu ambao ni dereva wa gari, mdogo wa dada anaedaiwa kuwa mpenzi wa huyu muuaji na muuaji mwenyewe.
Kuna taarifa nyingine za hili tukio zinafata muda sio mrefu endelea kupita on millardayo.com

No comments:

Post a Comment