Thursday 30 January 2014

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI TAREHE 30/1/2014..

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Mkuya: Serikali itaendelea kukopa

Pia ameelezea sababu  za kuongezeka kwa deni la taifa kuwa ni mikopo iliyopokewa na serikali na ambayo muda wake wa kulipa haujafika kutoka vyanzo vya masharti nafuu ya kibiashara pamoja na malimbikizo ya riba ya deni la nje.
Waziri Mkuya alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana alipozungumza na waandishi wa habari kuelezea utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Fedha.
Alisema hadi kufikia Desemba mwaka jana, deni la taifa lilikuwa limefikia dola bilioni 17.10 sawa na sh trilioni 27.04
Alisema deni hilo linajumuisha deni la nje dola bilioni 12.79 sawa (sh trilioni 20.23) na deni la ndani ni sh trilioni 6.81 ambazo ni sawa na asilimia 25.19 ya deni la taifa.
Kati ya deni la nje la taifa, dola bilioni 10.563 (sh trilioni 16.71) na deni la sekta binafsi ni dola bilioni 2.23 sawa na trilioni  3.52.
Mkuya alisema licha ya deni la taifa kuongezeka kwa kasi nchini lakini mfumuko wa jumla wa bei umeendelea kushuka hadi kufikia asilimia 5.6 Desemba mwaka jana ukilinganisha na asilimia 19.8 zilizofikiwa Desemba mwaka juzi.
“Kupungua kwa mfumuko wa bei kulitokana na sera thabiti za fedha na kibajeti pamoja na kuimarika kwa uzalishaji na usambazaji wa chakula nchini suala hili limekuwa likielezwa kwa kina na Ofisi ya Taifa ya Takwimu  katika taarifa za kila mwezi,” alisema.
Kuhusu matumizi ya mashine za kielektroniki, alisema utaratibu huo utaendelea kutumika kama kawaida na kusimamia vema katika kukusanya kodi ili kuongeza pato la taifa na kupunguza ukwepaji kodi.
“Tulikubaliana na viongozi wa wafanyabiashara  kuwa muda wa kuanza kutumia mashine usogezwe  hadi kufikia tarehe 30, Januari 2014, ili kuwapatia wananchi muda wa kutosha kujiandaa na utekelezaji wa matumizi hayo ya mashine,” alisema Mkuya.

Tanzania Daima

Wednesday 29 January 2014

CCM kuchafuana tu

MALUMBANO ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) yanayoonekana dhahiri kuchagizwa na makundi ya urais yameendelea kushika kasi ndani ya chama hicho.
Baada ya jana Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi, Paul Makonda, kumshambulia Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, kwamba anawatumia watu kusema hovyo kupitia vyombo vya habari juu ya kazi na juhudi zinazofanywa na sekretarieti, kada mwingine, Richad Kiabo, jana aliibuka kuanika majina ya waasisi wa chama cha siasa cha CCJ kilichokufa hata kabla ya kupata usajili.
Makonda alidai Lowassa anafadhili mikakati ya kupingana na juhudi za sekretarieti ya chama hicho na alipongeza kazi zinazofanywa na sekretarieti chini ya Katibu Mkuu, Abdulrahaman Kinana na wasaidizi wake akiwemo Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, akijibu mapigo ya Makonda, Kiabo aliyekuwa mwenyekiti wa CCJ kabla ya kurejea CCM, aliyataja majina 37  na michango  waliyoitoa kwa ajili ya kufanikisha maandamano ya amani ya chama hicho ya kupinga uonevu wa aliyekuwa msajili wa vyama vya siasa nchini wakati huo, John Tendwa.
Kiabo ambaye amekoleza malumbano hayo, alimtaka Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula, kuwachukulia hatua wasaliti hao.
Mbele ya waandishi wa habari, Kiabo aliwataja waasisi hao wa CCJ na fedha walizochangia  kwenye mabano kuwa ni pamoja na  Dk. Harrison Mwakyembe (sh 300,000), Samuel Sitta (sh 500,000), Anne Kilango (sh 400,000), Nape Nnauye (sh 100,000), Paul Makonda (sh 100,000) na James Lembel (sh 400,000) ambao kwa sasa ni miongoni mwa wanachama wa CCM wanaotajwa kuwa na makundi ya urais.
Wengine ni Amina Katemi (sh 300,000), Alex Kisumo (sh 300,000), Baraka Seif (sh 300,000), Sospeter Banigwa (sh 300,000), Saleh Omari (sh 300,000), Sarah Patrick (sh 200,000), Daniel Mwaijojeli (sh 200,000), Dk. Ngonyani (sh 300,000), Elisha Eliya (sh 200,000), Emanuel Magonja (sh 200,000) na Asma Watosha (sh 300,000).
Pia wamo, Kulwa Lulelema (sh 50,000), Hamadi Maduku (sh 100,000), Flavian Nkya (sh 100,000), Gulam kutoka Zanzibar (sh 150,000),  Hamad Ferej (sh 200,000), Ally Harun (sh 50,000), Masudi Kangi (sh 100,000), Gumbo (sh 150,000), Idd Kiriwe (sh 100,000), Innocent Makala (sh 200,000), Jacob Msambya (sh 200,000),  Ishelula (sh 150,000), Kipute (sh 200,000), Joseph Kashindye (sh 200,000) Kamala Ng’ombe (sh 200,000) na Daniel Malongo (sh 50,000).
Kiabo alisema anashangaa kuona ndani ya CCM bado kuna wanachama na viongozi waandamizi wenye kadi mbili, yaani kadi ya CCJ na CCM na wameshindwa mpaka sasa kuzirudisha na hata kukana, ikiwemo kuwaomba radhi wanachama kwa kitendo cha usaliti.
“Nawashangaa baadhi ya wanachama ambao si waaminifu na wasaliti wa chama baadhi yao wameanza harakati za kugombea urais 2015 ili wapewe ridhaa na chama ambacho tayari walikwisha kisaliti, nami nitakishangaa chama wakati ukifika kama kitawakubalia na kuwapitisha kuwa wagombea watu wenye kadi za vyama viwili,” alisema.
Kiabo alisema watu wenye uwezo wa kuwasema viongozi wenzao mara kwa mara na wao wasijisahau kuwa hawana usafi wowote wa kusema na kuwanyoshea vidole wenzao kwa usaliti walioifanyia CCM.
Aidha, alisema wakati CCM ikielekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2015 ni vizuri kikaanza kusafisha nyumba yake ili mamluki waumbuke na wasipewe nafasi ya kugombea wakati ukifika.
Kutoka jijini Morogoro, inaripotiwa kuwa UVCCM Mkoa wa Morogoro  imemtaka Makonda kumwomba radhi Lowassa kwa kauli za kichochezi zinazoweza kukigawa chama.
Kwa mujibu wa taarifa iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii jana, wajumbe hao wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC)  kupitia kundi la vijana, Jonas Nkya na Ramadhani Kimwaga, walisema kauli ya Makonda ni yake binafsi wala haihusiani na UVCCM.
Nkya alisema vijana wa Mkoa wa Morogoro wamehuzunishwa na matamshi ya Makonda akimshutumu Lowassa kuwa hafai kuwa kiongozi wa nchi hii, wala kuwa Amiri Jeshi Mkuu na Mwenyekiti wa CCM  taifa.
Nkya alisema kuwa umoja huo hautaki kuingizwa katika masuala binafsi ambayo yanaweza kusababisha na kuchangia kukigawa chama na jumuiya zake.
Mnyukano wa sasa miongoni mwa makada wa CCM umekuja baada ya Rais Jakaya Kikwete kufanya uteuzi wa Baraza la Mawaziri na kuwarejesha madarakani mawaziri mizigo waliopendekezwa na chama chake watoswe.
Baada ya uteuzi huo, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alitoa kauli ya kuunga mkono uteuzi huo, lakini akisisitiza chama kitaendelea kuwashughulikia mawaziri mizigo na safari hii wataelekeza mapambano hayo ndani ya Bunge na kwenye mabaraza ya halmashauri.
Kauli hiyo ilimuibua mwenyekiti wa zamani wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita, ambaye alimtukana Nape kwamba ameteuliwa kimjombamjomba na hawezi kumchagulia rais majina ya uteuzi.
Kauli ya Guninita ikamuibua Makonda na sasa Kiabo, ambao duru za siasa zinasema wote wanatumiwa kwa malengo ya urais mwaka 2015.

Tanzania Daima

President Obama's 2014 State of the Union Address



Today in America, a teacher spent extra time with a student who needed it, and did her part to lift America’s graduation rate to its highest level in more than three decades. An entrepreneur flipped on the lights in her tech startup, and did her part to add to the more than 8 million new jobs our businesses have created over the past four years. (Applause.) An autoworker fine-tuned some of the best, most fuel-efficient cars in the world,

Mauaji yazidi kutikisa Tarime

Hali ya usalama Tarime imezidi kutoweka baada ya jambazi lisilofahamika likiwa na bunduki ambayo haijafahamika aina yake kuendelea kuua watu kwa risasi hasa wa jinsi ya kiume, ambapo idadi ya waliouawa imefikia saba hadi sasa na inadaiwa huwaua watu na kupotea bila kutambuliwa.
Jambazi hilo lisilofahamika liliua watu hao usiku wa Januari 27, mwaka huu katika maeneo ya Nkende likianza na kumuua Mwendesha Bodaboda, Juma Marwa Mkazi wa Nkende mjini Tarime akiwa anaelekea nyumbani kwake ambaye alikufa akiwa hospitali akipatiwa matibabu.
Mganga wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Tarime, Marco Nega alisema tangu Januari 27 hadi sasa hospitali imeendelea kupokea watu waliouawa na majeruhi ambao wamefanyiwa uchunguzi na kugundulika wakiwa wamejeruhiwa kwa risasi katika sehemu mbalimbali za mwili na kwamba watu wapatao 7 wamekwisha kufa mpaka sasa.
“Tumepokea maiti za watu na majeruhi na tumewafanyia uchunguzi wakagundulika wana majeraha ya risasi sehemu mbalimbali za mwili, ambapo tayari watu saba wamekufa wengine wamekufa wakiwa njiani wakienda kwenye matibabu Musoma, marehemu hadi ni saba,” alisema Nega.
Waliojeruhiwa wakosa huduma ya X-ray
Watu waliojeruhiwa wameshindwa kupatiwa huduma ya X-Ray kutokana na Hospitali ya Wilaya kutokuwa na huduma hiyo kwa muda wa zaidi ya miezi 3 na kusababisha wagonjwa kusafirishwa kwenda Musoma na Mwanza kwa matibabu, ambapo Samweli Richard amekufa akiwa njiani kuelekea Musoma kwenye matibabu ikiwamo huduma hiyo ya X-ray.
Hospitali ya Wilaya yashindwa kutoa huduma
Huduma kwa wagonjwa mbalimbali katika Hospitali ya Wilaya imeshindwa kuendela vilivyo baada ya kupatwa na misiba miwili ya watumishi wawili, ni baada ya waume zao kuuawa na jambazi hilo lisilofahamika.
Awali Januari 26 jambazi hilo lilimuuwa Robert Kisiri (45) mkazi wa Mugabiri ambapo Mstaafu wa JWTZ Zacharia Mwita(58) na Erick Makanya (25)wote wakazi wa Kijiji cha Mogabiri Kata ya Kitare Wilayani Tarime walikutwa wakiwa wameuawa na miili yao ikiwa na majeraha ya risasi mbavuni kushoto na mgongoni.
Pia jambazi hilo liliwajeruhi watu watano kwa risasi ambao ni Mgosi Marwa Mkazi wa Mogabiri, Joseph Richard Mkazi wa Rebu, Gastor Richard Mkazi wa Rebu, Juma Mwita Mkazi wa Mogabiri na Mkandarasi Binafsi wa ujenzi, Mwasi Yomami ambao kati ya hao wawili wamefariki wakati wakipatiwa matibabu.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya, Justus Kamugisha amesema wamemkamata mtu mmoja anayeshukiwa kuwa mhusika wa mauaji ambaye yuko chini ya ulinzi kwa mahojiano na kwamba anazidi kuongeza vikosi vya doria kuimarisha ulinzi na usalama na kuwasaka wahalifu.
Wananchi wacharuka

Matamshi kuhusu ubakaji yakera India


Matamshi ya mwanasiasa mmoja mwanamke nchini India kuhusu ubakaji yamelaaniwa na watu wengi kote nchini humo.
Asha Mirge, ambaye ni mwanachama wa kikundi cha viongozi wanawake serikalini katika jimbo la Maharastra, amesema kuwa wanawake pia wanachangia pakubwa kwa wao wenyewe kubakwa kutokana na mavazi pamoja na wanavyotembea na hata kuzungumza.
Amehoji kwa nini wanawake hutoka nje nyakati za usiku.
Matamshi haya yaliyozua gumzo katika vyombo vya habari kote nchini India, yamesababisha kero kubwa kutoka kwa makundi ya wanaharakati wa maswala ya wanawake na wanasiasa wengine.
Amehoji kwa nini wanawake hutoka nje nyakati za usiku.
Matamshi haya yaliyozua gumzo katika vyombo vya habari kote nchini India, yamesababisha kero kubwa kutoka kwa makundi ya wanaharakati wa maswala ya wanawake na wanasiasa wengine.
Bi Mirge hata hivyo ameomba radhi kwa matamshi yake akisema yametiwa chumvi.
Inda imekuwa ikimbwa na visa vya mara kwa mara vya ubakaji kiasi cha serikali kubuni sharia kali dhidi ya wabakaji.
Ni wiki jana tu ambapo wazee wa kijiji waliamrisha kubakwa kwa mwanamke ambaye alikuwa na uhusianao wa kimapenzi na mwanamume ambaye sio wa kutoka jamii moja naye.

MAKUNGA, KIBANDA, MWIGAMBA WASHINDA KESI YA UCHOCHEZI

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam imetoa hukumu ya kesi ya makala iliyodaiwa kuwa ya uchochezi iliyokuwa inawakabili Meneja Uendeshaji Biashara wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL), Theophil Makunga, Mwenyekiti wa zamani wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba na aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima ambaye sasa ni Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006), Absalom Kibanda ambapo wameibuka kidedea baada ya ushahidi upande wa mashitaka kutojitosheleza.

MFANYABIASHARA AUAWA KWA KUPIGWA RISASI MOMBASA, KENYA


 Mfanyabiashara, Ahmed Bakhshuwein ameuawa kwa kupigwa risasi tatu kichwani akiwa kwenye gari eneo la Malindi, Mombasa karibu na Al-R azaak Stores nchini Kenya.

Maskini Victor Wanyama

HAMU ya mashabiki wa soka Kenya kumuona kiungo Victor Wanyama akiwatesa viungo wa Arsenal imezidi kuwa njia panda kutokana na balaa la majeruhi linalomuandama.
Kiungo huyo wa Kenya anayeichezea Southampton leo Jumanne alitarajiwa kuwa kibaruani kuikabili Arsenal katika mechi ya Ligi Kuu England lakini hali yake bado si nzuri.
Mashabiki wengi wa soka nchini hapa hupenda kumwangalia nyota huyo ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars akiwajibika katika kikosi cha kwanza cha Southampton.
Kutokana na ushabiki wa Ligi Kuu England nchini hapa, Wanyama anazidi kuongeza burudani awapo uwanjani jambo ambalo sasa limeshindikana kwa kuwa nyota huyo ni mgonjwa.
Kocha Msaidizi wa Southampton, Jesus Perez alibainisha kwamba ni mapema mno kwa mchezaji huyo kupona maumivu ya mguu aliyoyapata katika mechi dhidi ya Aston Villa Desemba mwaka jana.
Awali kulikuwa na habari kwamba kiungo huyo angekuwa amepona kwa wakati mwafaka na leo angevaa jezi ya Southampton katika mechi hiyo ngumu dhidi ya Arsenal.
Kwa mujibu wa Perez huenda, Wanyama akawa nje ya uwanja kwa muda mrefu zaidi wakati akiendelea kujiuguza.
Hata hivyo Perez alisema kwamba mchezaji huyo anafanya mazoezi ya kawaida lakini bado hayuko fiti kucheza mechi ya ushindani na kwamba anachohitaji ni mazoezi maalum ya kumuweka katika hali nzuri kushindana uwanjani.
Wanyama alijiunga na Southampton akitokea Celtic, Julai waka jana kwa ada ya Pauni 12.5million na ameichezea timu hiyo mechi 14 kabla ya kuumia.

Nape hajui anapambana na nani CCM

Kati ya vigogo aliokuwa akipambana nao ndani ya CCM ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga na aliyekuwa mkuu wa wilaya kadhaa, Hawa Ng’umbi ambaye ndiye alishinda.
Hata hivyo, Ng’umbi alibwagwa na John Mnyika wa Chadema. Lilikuwa ni pigo kubwa mno kwa CCM na hasa kwa Nape ambaye alishajipambanua kama mpenda mageuzi ndani ya chama.
Alishajiwekea rekodi ya kufichua ufisadi ndani ya chama hicho hasa ule wa ujenzi jengo la Umoja wa Vijana pale Lumumba.
Hapo ndipo zikaanza kusikika tetesi kuwa Nape alitaka kuhamia Chadema, mara wengine wakimhusisha na chama kipya wakati huom cha CCJ (sasa CCK) kilichokuwa kikidaiwa kuanzishwa na baadhi ya vigogo wa CCM wasioridhishwa na mwenendo wa chama hicho tawala.
Lakini CCM nao walionekana kuushtukia mchezo huo. Siku chache kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 mara Nape akafutwa machozi na Rais Jakaya Kikwete alipoteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Masasi. Ilikuwa kama gia ya kumshikilia asije kukimbilia vyama vingine.
Aliishikilia nafasi hiyo hadi mapema Machi, 2011 ambapo CCM ilifanya mabadiliko ya sekretarieti. Hapo Nape akapewa nafasi ya Katibu wa Itikadi na uenezi anayoishika hadi sasa, huku nafasi ya Katibu Mkuu akipewa Wilson Mukama.
Mabadiliko hayo yalikwenda sanjari na mkakati wa kujivua gamba. Hapo mhemko tena wa Nape na viongozi wenzake kukisafisha chama na ufisadi ukaanza pale waliposisitiza kuwa lazima wale wanaochafua sura ya chama wawajibishwe.
Sote ni mashahidi, hadi leo hakuna aliyevuliwa gamba. Chama kinaendelea kusonga mbele na magamba yake.
Juzi juzi tena baada ya sekretarieti ya chama kubadilishwa na Abdulrahman Kinana kuwa Katibu Mkuu, Nape akabebeshwa mzigo la kutaja mawaziri mizigo. Wakawashikia kidedea hadi Kamati Kuu ya CCM ili wahojiwe. Wamehojiwa lakini baadaye wamerejeshwa barazani.
Mara Nape kaibuka tena mbele ya waandishi wa habari akisema eti CCM hakitasita kuchukua hatua kali dhidi ya mawaziri na watendaji wengine watakaoshindwa kurekebisha upungufu unaopigiwa kelele.
Itachukua hatua gani, wakati Mwenyekiti wa chama Rais Kikwete amesharidhika na mizigo yake? Ni kama vile Nape anatamani yeye ndiye angekuwa rais ili awafurumushe mawaziri hao, lakini basi hawezi….!
Hiyo ndiyo CCM. Utamaduni wa kuwajibishana na kufukuzana haupo. Mwenzako akifanya kosa unamezea. Kama Nape anaona kasi yake haiendani na CCM, bora atafute chama kingine ahamie.
Vinginevyo atakuwa anapiga kelele za bure huku wenzake wakiendelea kuchukua vyao mape
 
Mwananchi

Simba yamruhusu Kapombe kusajili Yanga

BEKI Shomari Kapombe, yupo mjini Morogoro akifikiria jinsi ya kurudi katika klabu yake ya AS Cannes ya Ufaransa, lakini uchunguzi umeonyesha kwamba Simba, imebariki nyota huyo kutua Yanga au Azam FC endapo zitafikia makubaliano na Cannes.
Uchunguzi uliofanywa na Mwanaspoti, umebaini kwamba, kwa mujibu wa mkataba ambao Simba ilisaini na Cannes, wakati akiuzwa kupelekwa kwa Wafaransa hao ni kwamba beki huyo aliuzwa kwa klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili.
Katika mkataba huo, ambao Mwanaspoti imepata sehemu ya nakala yake, uliosainiwa na Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage na Rais wa Cannes, Simba imemruhusu Kapombe kuuzwa kwa klabu  yoyote duniani endapo itafikia dau litakalohitajika, hatua ambayo inatoa fursa kwa klabu za Yanga, Azam FC Ashanti United na hata Galatasaray ya Uturuki kama zikimuhitaji.
Sehemu hiyo ya mkataba huo, inaonyesha kwamba endapo Kapombe atauzwa katika klabu yoyote duniani, Simba itavuna asilimia 40 ya mauzo hayo sambamba na Cannes ambao nao watapata mgawo kama huo, huku wakala wake Denis Kadito anayeishi Uholanzi akipata asilimia 20.
Wakala wa beki huyo, Kadito amezitaka klabu zinazomtaka mchezaji huyo kufuata utaratibu kwa kuzungumza na Cannes au yeye lakini kinyume na hapo zinajisumbua.

Mwanasipoti

FURAHA YARUDI MAN UTD, MATA AFUNIKA


Juan Mata ametoa mchango mkubwa lakini cha kukumbukwa zaidi ni pasi yake ya bao la pili lililofungwa na Ashley Young mnamo dakika ya 53.

Kabla ya hapo, Robin van Persie aliyekuwa amerejea akitokea kuuguza majeraha, alifunga mapema bao la kwanza takribani dakika ya 6.

Baadaye van Persie alitoka na nafasi yake kuchukuliwa na Wayne Rooney ambaye pia alikuwa majeruhi!

RWANDA YAZIDI KUMCHOKAZA JAKAYA KIKWETE



BUSARA ya Rais Jakaya Kikwete juu ya kuitaka Serikali ya Rwanda kukaa kwenye meza ya mazungumzo na waasi wa FDLR, imeendelea kutafsiriwa vibaya na baadhi ya wakubwa wa nchi hiyo, ambapo sasa wameanza kumchokonoa kwenye baadhi ya vyombo vya habari, kwa kudai kuwa amekutana kwa siri jijini Dar es Salaam na waasi hao. 

Gazeti la News of Rwanda ambalo linatajwa kuwa mshirika mkubwa wa Serikali ya nchi hiyo, katika toleo lake la Jumapili iliyopita, liliandika kuwa Rais Kikwete amekutana na waanzilishi wa chama cha upinzani nchini humo cha Rwanda National Congress (RNC) na makamanda waandamizi wa waasi wa FDLR.

Habari iliyoandikwa na gazeti hilo, imebainisha kuwa kikao hicho cha Rais Kikwete na watu hao kilifanyika kwenye makazi binafsi ya Rais Kikwete.

Gazeti hilo lilidai kuwa limepata taarifa hizo kutoka kwenye vyanzo vyake vya habari vilivyopo nchini Tanzania, ambapo viliwaeleza kuwa ujumbe huo uliwasili, jijini Dar es Salaam Alhamisi ya wiki iliyopita.

Wameandika kuwa viongozi wa RNC waliokutana na Rais Kikwete ni Mratibu wa chama hicho, Dk. Theogene Rudasingwa na mshauri wake, Condo Gervais.

Katika kikao hicho, News of Rwanda lilidai kuwa kundi la waasi wa FDLR, liliwakilishwa na Katibu Mtendaji wake, Luteni Kanali Wilson Irategeka na Kanali Hamadi ambaye ni kamanda wa operesheni.

Luteni Kanali Irategeka kwa sasa anatajwa kuwa ndiye nembo ya waasi wa Rwanda wa kundi la FDLR na mara kwa mara amekuwa akionekana kwenye mahojiano na vyombo vya habari. 

News of Rwanda liliendelea kuandika kuwa, majina hayo anayotumia Luteni Kanali Irategeka si yake na kwamba jina lake kamili ni Ndagijimana.

Viongozi hao wa FDLR wote wanaishi Washington, nchini Marekani na kwamba wanasafiri kwa kutumia hati za kusafiria za Tanzania.

Hata hivyo, News of Rwanda wameshindwa kuthibitisha madai yao ya pasi za kusafiria za waasi hao kama zimetolewa na Serikali ya Tanzania, au zilipatikana kwa mlango wa nyuma.

Aidha gazeti hili lilikwenda mbali zaidi kwa kudai kuwa Januari 19, mwaka huu, Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Faustin Twagiramungu alikuwa Tanzania kwa shughuli kama iliyofanywa na waasi wa FDLR.

Walidai kuwa hata hivyo aliondoka Tanzania Alhamisi ya wiki iliyopita, kuelekea Lyon, nchini Ufaransa ambako alikuwa aongoze kikao cha kundi lake la kisiasa la RDI na Rwanda RWIZA.

Limedai, Twagiramungu aliondoka kabla ya timu ya RNC haijawasili Dar es Salaam, ingawa Twagiramungu pia alipaswa kuwa pamoja na RNC na FDLR.

News of Rwanda halikuweza kubainisha kilichopelekea Twagiramungu kuamua kukaa mbali na wenzake hao, ingawa walidai kwamba Waziri Mkuu huyo wa zamani hataki kuingia tena katika ndoa ya kisiasa na kundi linalohusisha waanzilishi wanne wa RNC.

Twagiramungu ndiye Waziri Mkuu wa kwanza kushika wadhifa huo mara baada ya kumalizika kwa mauaji ya kimbari, ambapo alishika wadhifa huo kwa kipindi cha mwaka mmoja na baadaye kujiuzulu.

Limebainisha kuwa, Twagiramungu amekuwa na uhusiano mbovu na Dk. Rudasingwa na Kayumba Nyamwasa kutokana na kuwa sababu ya yeye kushindwa kutekeleza majukumu yake na kuamua kuachia ngazi.

Wawili hao wamedaiwa kuwa walikuwa maofisa waandamizi katika nyadhifa kubwa kisiasa na kijeshi nchini Rwanda.

News of Rwanda limebainisha kuwa, Twagiramungu na makundi mengine ya waasi ya Rwanda, yameapa kutoingia katika ushirika wa kisiasa na watu waliokuwa karibu na Serikali, baada ya kutofautiana na utawala wa Rais Kagame. 

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, si mara ya kwanza kwa wawakilishi wa RNC wanaomwakilisha Kayumba Nyamwasa, kukutana na waasi wa FDLR. 

Gazeti hili limezidisha chokochoko kwa kudai kuwa Desemba 20, 2013, Luteni Kanali Wilson Irategeka na Kanali Hamadi walisafiri wakitumia hati ya kusafiria za Tanzania kwenda Msumbiji kwa mazungumzo na wajumbe wa RNC, na kwamba Tanzania imekuwa ikitoa hifadhi kwa waasi wa FDLR. 

Katikati ya mwaka jana, Naibu Kamanda wa FDLR, Jenerali Stanislas Nzeyimana, maarufu kama Izabayo Bigaruka, alitangazwa kuwa yupo Tanzania. Lakini wiki kadhaa baadaye, taarifa ziliibuka kuwa ametoweka na kuzua maswali ya sababu za uwepo wake Tanzania.

Katika kuhitimisha chokochoko zao, News of Rwanda liliandika kuwa nchini Tanzania, upinzani haufurahishwi na mwelekeo wa Rais Jakaya Kikwete kuwabeba FDLR, na kwamba Agosti mwaka jana, CHADEMA, ambacho ni chama kikuu cha upinzani Tanzania, kilimtuhumu Rais Kikwete kwa kutokuwa tayari kukutana na wapinzani nyumbani na kuingilia mambo ya ndani ya Rwanda.

“Hakuna dhati yoyote ndani ya taarifa ya Rais Kikwete kuwa Rwanda inapaswa kuzungumza na kundi la wanamgambo wa FDLR, ambalo limekuwapo katika misitu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo tangu 1994,” walimnukuu Dk. Willbrod Slaa, ambaye ni Katibu Mkuu wa CHADEMA

Katika kuhalalisha kile walichokiandika, News of Rwanda liliendelea kumnukuu Dk. Slaa kuwa: “Iweje Rais Kikwete hayuko tayari kujadiliana na upinzani nyumbani na kwamba, Rais Kikwete hajachukua hatua zozote kuhusu wauaji wa mwandishi, Daudi Mwangosi, na kwamba alimshauri (Kikwete) kuchukua hatua za kumwajibisha Kamanda wa Polisi Mkoa Iringa, Michael Kamuhanda badala yake alimpandisha cheo,” walihitimisha nukuu yao.
-Mtanzania