Saturday 18 January 2014

MWANAMKE ALIYETAPELI KWA AIRTEL MONEY, JELA MIEZI 6.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi
Wilaya ya Nzega mkoani
Tabora, imemhukumu mkazi wa
hapa kwenda jela miezi sita,
kwa kosa la utapeli wa fedha
kwa njia ya mtandao wa Airtel
Money kwa mawakala
mbalimbali wilayani humo.

Akitoa hukumu hiyo, Hakim
Mkazi Mfawidhi, Joseph
Ngomelo, alisema mshitakiwa
Helena Alexandria, atakwenda
jela miezi sita baada ya kukiri
kufanya utapeli huo.

Mshitakiwa huyo alikiri kutapeli
mawakala mbalimbali wa Airtel
Money waliopo Nzega mjini
kwa njia ya mtandao na
kujipatia fedha kwa njia isiyo
halali.

Alisema kifungo cha mama huyo
kitakuwa fundisho kwa
wanawake wangine wenye
tamaa, kwani makosa kama
hayo yakiachiwa yanaweza
kuleta madhara makubwa kwa
jamii.

Awali Mwendesha Mashitaka wa
Polisi Mkaguzi Msaidizi, Melito
Ukongoji, aliiambia Mahakama
hiyo kuwa Januari mosi mwaka
2014, mshitakiwa ambaye ni
mkazi wa Nzega mjini, aliiba
kwa kutumia mtandao wa
Kampuni ya Airtel Money.

Alidai kuwa Hellena alikuwa
akitumia ujumbe mfupi wa
maneno wenye muamala wa
kutoa pesa Sh 40,000 Airtel
Money na kujipatia Sh 40,000
kwa kila wakala kwa nyakati
tofauti.

Akijitetea, mshitakiwa alikiri
kuhusika na tuhuma hizo kwa
nyakati tofauti na kuongeza
kuwa lengo lilikuwa ni kutafuta
fedha za kujikimu kimaisha
kutokana ugumu wa maisha.
Kabla ya kutoa hukumu hiyo
Mwendesha Mashitaka aliiomba
Mahakama hiyo itoe adhabu
kwa mshitakiwa huyo ili iwe
fundisho kwa watu wenye tabia
kama hizo za wizi wa utapeli
kwa njia ya mtandao.

No comments:

Post a Comment