Friday 17 January 2014

WANANDOA/WAPENZI...MAUMIVU WAKATI WA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA (DYSPAREU)...SOMA ZAIDI HAPA...

TAFITI za kitabibu zinaonyesha kuwa mwanamke asikiapo maumivu haya anatakiwa kuchukua hatua za haraka bila kuchelewa kabla afya yake ya uzazi haijazorota na kumletea ugumba.

Maumivu wakati wa kushiriki tendo yanaashiria hatari katika afya ya uzazi iwapo yanakuwa na dalili zifuatazo:

i. Iwapo anaumia tangu mwanzo wa tendo mpaka mwisho.
ii. Iwapo anaumia muda mchache au hata saa kadhaa baada ya tendo kukamilika.
iii. Iwapo anapata maumivu chini ya kitovu kushoto na kulia au upande mmoja wakati tendo linaendelea.

iv. Iwapo anapata maumivu ya kiuno kwa nyuma na pia kwenye mapaja wakati wa tendo au baada.
v. Iwapo mwanamke anapata maumivu haya na pia anatokwa na uchafu katika via vyake vya uzazi mithiri ya maziwa ya mtindi au rangi nyingine kama njano, brown, kijani au cream.
vi. Miwasho na fangasi vinashambulia via vyake vya uzazi.

vii. Kubadilika badilika kwa hedhi bila mpangilio maalum, mfano kupata hedhi mara mbili au zaidi katika mwezi mmoja, kukosa hedhi zaidi ya miezi miwili, kupata hedhi kidogo sana au nyingi na nzito kupitiliza na maumivu makali wakati wa hedhi. 

SABABU/ VYANZO VYA TATIZO KWA UFUPI
i. Maambukizi kwenye kuta za uke. Yawezekana ikawa ni maambukizi ya bakteria au fangasi.
ii. Matatizo ya shingo ya kizazi ambayo ndiyo mlango wa kuelekea kwenye mji wa mimba. Mwanaume akimwingilia mwenza wake anaweza gonga sehemu ya shingo ya kizazi [cervix] ambayo inashambuliwa na bakteria au fangasi.

iii. Maambukizi/mashambulizi ya bakteria na fangasi kwenye mfuko wa uzazi, mirija ya uzazi na kwenye vifuko vya mayai ya uzazi.
iv. Kuwa na vimbe kwenye mji wa mimba (fibrods).
v. Kushiriki tendo muda ambao si mwafaka baada ya mwanamke kujifungua au baada ya upasuaji.
vi. Vidonda  kwenye mlango wa via vya uzazi vya mwanamke.
vii. Magonjwa mbalimbali ya ngono [ STDs]
viii. Mimba kutungia nje ya mfuko wa uzazi au mji wa mimba.
ix. Kuanza au kukomaa kwa vimbe kwenye vifuko vya mayai ya uzazi.
x. Kuwa na matatizo ya kibofu cha mkojo na au maambukizi kwenye njia ya mkojo U.T.I

No comments:

Post a Comment