Saturday 18 January 2014

Yanga yamtosa Chuji CAF

Balaa limeendelea kumwandama kiungo Athumani Idd ‘Chuji’ baada ya kutoswa kwenye kikosi cha Yanga kitakachoshiriki Ligi ya Mabingwa msimu huu.
Mabingwa hao wa Tanzania, Yanga wamewasilisha orodha ya wachezaji wake 26 kwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa ajili ya michuano hiyo huku ikiengua jina la Chuji anayetumikia adhabu ya kufungiwa kwa muda usiojulikana kutokana na matendo yake ya utovu wa nidhamu.
Pamoja na Chuji kuandika barua ya kuomba radhi kwa tukio hilo, lakini viongozi wa klabu hiyo hawataki kumsikiliza.
Mmoja wa viongozi wa klabu hiyo alidai kuwa Chuji asahau kurudishwa Yanga kwa sasa.
Katibu Mkuu wa Yanga, Benno Njovu alikitaja kikosi hicho ni makipa Ally Mustapha, Juma Kaseja na Deogratias Munishi wakati wengine ni Salum Telela, David Luhende, Oscar Joshua, Kelvin Yondani, Mbuyu Twite, Didier Kavumbagu, Haruna Niyonzima na Reliants Lusajo.
Wengine ni Jerryson Tegete, Said Bahanuzi, Juma Abdul, Ibrahim Job, Rajab Zahir, Nizar Khalfan, Mrisho Ngassa, Frank Domayo, Hamisi Kiiza, Hussein Javu, Hamis Thabit, Nadir Haroub, Emmanuel Okwi, Hassan Dilunga, Simon Msuva.
Yanga itacheza mechi yake ya kwanza Februari 7 au 9 kwenye Uwanja wa Taifa dhidi ya Komorozine Sports ya Comoro na watarudiana wiki mbili baadaye kwenye visiwa vya Comoro.
Wakati Yanga wakimtema Chuji, wawakilishi wengine wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho, Azam FC wamemwacha kiungo wa kimataifa wa Kenya, Humphrey Mieno katika orodha yao ya wachezaji 25 watakaocheza michuano hiyo.
Meneja wa Azam, Jemedari Said alisema wametuma majina ya wachezaji 25 ambao ni Makipa: Wandwi Jackson, Mwadini Ally na Aishi Manula. Mabeki: Waziri Salum, Aggrey, Nyoni, David Mwantika, Malika Ndeule, Lackson Kakolaki, Himid Mao na Said Moradi.
Viungo: Joseph Kimwaga, Ibrahim Mwaipopo, Kipre Bolou, Salum Aboubakary ‘Sure Boy’, Jabir Aziz, Khamis Mcha, Samir Haji, Muamad Kone na Farid Mussa wakati washambuliaji ni John Bocco, Abdallah Seif, Kipre Tchetche, Gaudence Mwaikimba na Brian Umony.

No comments:

Post a Comment