Wednesday 22 January 2014

USAJIRI WA OKWI YANGA WAZUIWA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesimamisha usajili wa mshambuliaji Emmanuel Okwi kutoka Uganda katika timu ya Yanga wakati likisubiri ufafanuzi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

TFF imesimamisha usajili Emmanuel Okwi kupata ufafanuzi kuhusu kesi tatu zilizopo FIFA zinamzohusu Okwi, zilizofunguliwa na Simba, Etol Du Sahel na Okwi.

Katika FIFA kuna kesi tatu kuhusiana na suala la mchezaji huyo. Wakati Okwi ameishitaki klabu hiyo FIFA kwa kutomlipa mshahara, Etoile du Sahel imemshitaki mchezaji huyo kwa utoro. Nayo Simba imeishitaki Etoile du Sahel kwa kushindwa kuilipa ada ya mauzo ya mchezaji huyo ambayo ni dola za Marekani 300,000.

No comments:

Post a Comment