Tuesday 21 January 2014

Nsajigwa, Bonny waosha Nepal

WATANZANIA wanaocheza soka la kulipwa huko Nepal, Shadrack Nsajigwa, Godfrey Bonny na Pius Kisambale wameonekana kung’ara kutokana na kuiwezesha klabu yao ya Saraswoti Youth Club kupata matokeo mazuri katika mechi tano walizocheza.
Wachezaji hao wote walijiunga kwa pamoja kwenye klabu hiyo katika msimu huu wa Ligi Kuu kimya kimya bila kutaka Watanzania wajue kinachoendelea.
Nsajigwa kabla ya kwenda kucheza soka nchini humo, alikuwa Kocha Mkuu wa Lipuli FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, pia aliwahi kuwa nahodha wa Taifa Stars na Yanga ambayo ilimtema kwa madai kuwa umri umekwenda na kiwango kimeshuka.
Nsajigwa aliwahi kucheza pamoja na wachezaji Bonny na Kisambale katika klabu ya Yanga na Prisons ya Mbeya kuipa mataji tofauti ya ubingwa.
Kisambale kabla ya kwenda huko alikuwa akiichezea Coastal Union ikamtema. Saraswoti hadi sasa imeshinda mechi mbili, sare mbili huku ikifungwa moja pekee.

Mwanasipoti

No comments:

Post a Comment