Wednesday 25 June 2014

Sekretarieti ya Ajira Yazipa Rungu Serikali za Mitaa.


Serikali za mitaa zitaruhusiwa kuanza kuajiri watumishi wa baadhi ya kada za chini katika mwaka wa fedha wa 2014/2015.Akihojiwa katika Maonyesho ya Wiki yaUtumishi wa Umma kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam, Msemaji wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa
Umma, Riziki Abraham, alithibitisha kuwa Sekretarieti hiyo itakasimu sehemu ya madaraka yake ya kuendesha mchakato wajira serikalini kwa serikali za mitaa.
"Sekretarieti ya Ajira imeandaa mpango wa kukasimisha madaraka yake ya kuendesha mchakato wa ajira serikalini kwa baadhi ya kada za chini (operation staff) kwenye mamlaka za Serikali za Mitaa na mchakato huo utaanza mwaka wa fedha 2014/15" alisema.Pia, alisema katika kila nafasi ya kazi inayotangazwa kwa hiyo haizingatii GPA (kiwango cha ufaulu kwa masomo yote ). Alieleza kuwa zipokada, ambazo GPA inazingatiwa ;na zipo
kada ambazo kinachoangaliwa ni ufaulu tu wa kawaida na sifa zilizoainishwa."Zipo baadhi ya kada ambazo masharti yake ni pamoja na kuwa na GPA ya kiwangofulani. Kada ambazo ni lazima GPA kuangaliwa ni kama vile kada za wakufunzi wa vyuo mbalimbali. Kazi nyingine hazina
masharti ya GPA, kinachoangaliwa ni ufaulu tu na sifa zilizoainishwa katika tangazo la nafasi za kazi kulingana na kada husika",alisema Riziki.Alitaja moja ya matatizo wanayopata waombaji wa kazi kuwa ni kupotelewa na vyeti vya kitaaluma. Alisema waombaji wa kazi ambao wamepata tatizo hilo, wanachopaswa kufanya ni kuripoti kwenye mamlaka husika, alikokuwa amepata cheti hicho ili apewe mwongozo wa kufanya na kutangaza kupotelewa kwa cheti au vyeti kwenye chombo cha habari (gazeti)."Ikithibitika hivyo mamlaka husika kwa mfano Baraza la Mitihani wana utaratibu wa kuwasiliana na Sekretarieti ya Ajira kwa kutoa majina ya watu waliopoteza vyeti nahatimaye huruhusiwa kufanya usaili"
alisema.

No comments:

Post a Comment