Friday 25 October 2013

Mfaransa aanika siri za mbaya wa Yanga


KOCHA wa zamani wa Simba, Mfaransa Patrick Liewig, ametoa siri na sababu zilizomfanya ambadili namba mbaya wa Yanga, William Lucia ‘Gallas’ kutoka beki wa kulia hadi kiungo. Pia amesema yeye humfananisha Gallas na Patrick Vieira.
Awali Gallas alikuwa anacheza namba mbili tangu utotoni mwake na wakati mwingine alikuwa beki wa kati. Lakini Mfaransa huyo ndiye aliyembadilisha namba kutoka nafasi hizo hadi kuwa kiungo.
Alisema kutokana na kiwango chake kizuri, alimwamini na kumpa nafasi kucheza mechi mbalimbali na alifanya vizuri.
Lakini msimu huu hakupata nafasi ya kucheza kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya ushindani wa namba kikosini. Hata hivyo mechi ya Jumapili iliyopita dhidi ya Yanga, ni yeye pamoja na Said Ndemla walioingia kipindi cha pili ndiyo waliiokoa Simba hadi kutoka sare ya mabao 3-3.
Gallas na Said Ndemla walichukua nafasi za Abdullhalim Humoud na Haroun Chanongo wakati Simba ikiwa nyuma mabao 3-0. Kuingia kwao kuliipa uhai Simba hadi ikarudisha mabao hayo.
Akizungumza na Mwanaspoti, Liewig alisema: “Gallas ni mzuri kwenye namba mbili, lakini niliamua kumtumia kwenye kiungo kwa sababu ana uwezo wa kipekee wa kufikiri na kuamua kwa haraka, inakuwa rahisi kwake kuwachezesha wenzake.
“Mbali ya uamuzi wa haraka, pia anajiamini. Kijana yule pia anazo kumbukumbu za kutosha, mwagize chochote uwanjani atakufanyia, lakini kama watakuwa wanamwitaji kucheza beki wa pembeni pia ni mzuri katika nafasi hiyo. “Niliuona uwezo wake tangu mapema ndiyo nikachukua uamuzi ule, Gallas kwangu Vieira kwa jinsi anavyocheza.”
Vieira ni mwanasoka mstaafu wa Ufaransa mwenye asili ya Senegal ambaye aliwahi kuwika na klabu za Arsenal, Juventus Inter Milan na Manchester City alikostaafia soka la kiushindani.
Kwa upande wake, Gallas alisema: “Ni kweli zamani nilikuwa nacheza nafasi ya beki wa kulia na kati, Liewig ndiye alinibadilisha hadi kuwa kiungo.”

source Mwanasipoti

No comments:

Post a Comment