Saturday 26 October 2013

AUNT LULU ATANGAZA KUACHA KUJIUZA

 
MWANADADA Lulu Mathias Semagongo ‘Anti Lulu’ ameibuka na kusema kuwa sasa hawezi kurudia biashara ya kujiuza na kuwataka wanaodhani kuwa bado yuko na tabia hiyo waondoe hisia hizo kwani kwa sasa si Lulu wa zamani tena.  Akizungumza  hivi karibuni, Anti Lulu alisema sasa hivi amejipanga kuyaendesha maisha yake kihalali na kwa kiasi kikubwa amefanikiwa licha ya kuwepo kwa baadhi ya watu wanaotaka kumrudisha nyuma.  “Watu wameniibia dukani kwangu ili kunirudisha nyuma lakini wamenoa, sirudii zama za kujiuza tena. Duka nimeshalijaza, nimenunua kiwanja huko Bunju na muda mrefu nitaanza kujenga.
  “Niwashukuru sana waandishi wa habari kwa kunibadili tabia kwani huenda mpaka leo ningekuwa nafanya mambo ambayo hayana tija kwenye jamii,” alisema Anti Lulu

No comments:

Post a Comment