Saturday 26 October 2013

MFAHAMU MRISHO HALFAN NGASSA.


Jina kamili : Mrisho Khalfani Ngassa

Tarehe ya kuzaliwa : 12 April 1989(age 24)

Mahali alipozaliwa : Dar es Salaam, Tanzania

Urefu : 1.65 m (5 ft 5 in)

Nafasi uwanjani : Winga,mshambuliaji.

Timu anayochezea : Yanga

TIMU ALIZOWAHI ZICHEZEA

2005–2006 Kagera Sugar
2006–2010 Young Africans
2010–2012 Azam
2012–2013→ Simba(mkopo)
2013-→Young Africans

Mwezi April 2009, Ngassa alienda kufanya majaribio na klabu cha ligi kuu ya uingereza West Ham United.

May 21, 2010, Ngassa alijiunga Azam FC kwa ada ya uhamisho $40,000. Akiweka rekodi ya uhamisho wa dau kubwa katika soka la Tanzania.

Mrisho Ngassa aliwahi fanya majaribio Seattle Sounders FC na akaingia uwanjani akitokea benchi dhidi ya Manchester United katika mechi ya kirafiki.

20 May 2013,Ngasa alisaini mkataba wa miaka 2 kuichezea Yanga mabingwa wa Tanzania.


MICHUANO YA KIMATAIFA

Ngasa aliibuka kuwa mfungaji bora wa CECAFA Cup 2009 akifunga magoli 5 akiiwezesha Tanzania kushika nafasi ya nne katika michuano hiyo.

Ngasa ni mchezaji anayeshikilia rekodi ya kuwa na magoli mengi katika timu ya taifa akiwa na magoli 21.

Ngassa ni mtoto wa kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania Khalfan Ngassa.

MAFANIKIO

Akiwa Yanga

*Ubingwa wa ligi kuu:

2007–08, 2008–09

*Tusker Cup: 2007, 2009

TUZO BINAFSI

*. mchezaji bora wa ligi kuu ya Tanzania : 2009–10

*.Mfungaji bora ligi kuu : 2010–11

*.Mfungaji bora CECAFA Cup : 2009

HADI SASA LIGI KUU

*.Kacheza mechi 5 kafunga goli 3 na katoa pasi za magoli 5.

JAMAA ANAJUA BANA.

No comments:

Post a Comment