Friday 25 October 2013

DANGURO LA MADENTI LAFUMULIWA








 

Wakati watuhumiwa hao wakihenyeshwa na polisi, mmoja wa madenti hao anayesoma Chuo cha IFM, Peter Davis alisema kwa upande wake aliamua kuweka makazi yake ndani ya chumba kimoja cha danguro hilo.Katika utetezi wake, denti huyo alidai kuwa aliamua kuishi hapo kwa kuwa mazingira hayo ni mazuri kwake kwa ajili ya kujisomea.
Mwingine aliyenaswa ndani ya kiwanja hicho cha maasi ni denti aliyejitambulisha kwa jina la Mwanahamisi (hakutaja chuo) ambaye alidai kuwa tangu siku hiyo atauacha uchangudoa na kuapa kuwa akiachiwa huru ataenda kusoma kwa bidii.

Denti mwingine aliyekamatwa katika msala huo alijitambulisha kwa jina moja la Angel ambaye alidai kuwa anasoma chuo kimoja kilichopo Kariakoo, Dar na wengine hawakutaja majina zaidi ya kukiri kuwa ni wanafunzi.
MUUZA KONDOM NAYE MBARONI
Ndani ya gesti hiyo pia alinaswa njemba mmoja aliyekuwa ameweka maskani na kazi yake kubwa ilikuwa kuuza kondom kwa madenti hao ambao humwingizia kipato chapuchapu.
Hata hivyo, jamaa huyo alitiwa mbaroni kwa uchunguzi zaidi.
Mbali na oparesheni hiyo, pia polisi hao waliendeleza msako maeneo mengine ya Buguruni ambapo dadapoa kibao walikamatwa huku mmoja akiangua kilio na kutamani kujiua kuliko mumewe kujua kuwa anauza mwili.

No comments:

Post a Comment