Monday 28 October 2013

Uwoya awapasha wanao mwandama


MSANII wa filamu za Bongo aliyetangaza kuikacha kazi hiyo , Irene Uwoya, amesema mali anazomiliki amezinunua kwa pesa zake alizopata wakati akiwa mwigizaji pamoja na zile zinazotokana na biashara zake nyingine.
Ameongeza kuwa ameamua kuweka wazi ukweli huo kutokana na maneno yaliyozagaa kuwa magari anayomiliki amenunuliwa na wanaume ‘wanaomweka mjini’.
“Kwa nini watu hawataki kukubali kuwa kazi ya uigizaji inalipa, yaani sisi tukinunua magari tumehongwa? Yaani wa kuhongwa ni sisi tu na si tasnia nyingine?” alihoji Uwoya.
Aidha Uwoya alisema kuwa kazi ya filamu ukijua kuitumia vizuri kwa kujiwekea malengo na kuitumia vizuri kila senti unayoipata, unaweza kupata mafanikio makubwa.
“Tunaigiza sehemu nyingine ambazo hutaki hata mwanao aone, hii siyo kazi rahisi maana yake ni kwamba kama ukiipatia unaweza kujikuta unaingiza pesa kila siku kwani mwaka mzima uko kazini,” alisema.

No comments:

Post a Comment