Friday 25 October 2013

Kocha ataka Cannavaro, Morris wapishe vijana














KOCHA wa Zanzibar Heroes, Salum Bausi amesema kuwa amelazimika kuwaacha mabeki Nadir Haroub wa Yanga na Aggrey Morris wa Azam FC kwenye kikosi hicho kutoa nafasi zaidi kwa vijana.
Bausi alitangaza majina ya wachezaji 25 Jumatatu kwa ajili kushiriki michuano ya Kombe la Chalenji itakayofanyika Kenya kuanzia Novemba 27 hadi Desemba 12 mwaka huu.
“Nimeacha wachezaji tisa ambao tulikuwa nao Uganda mwaka jana na kushinda nafasi ya tatu kwa makusudi kabisa, nataka kutengeneza msingi kwa ajili ya soka la vijana, hatuwezi kufika mbali wala kupiga hatua kwenye soka la nchi yetu kama tutaendelea kuwang’ang’ania wachezaji wale wale, kila siku lazima tubadilike na kuweka misingi kuanzia chini,” alisema Bausi.
Kocha huyo alisema kikosi hicho kitaingia kambini rasmi Novemba 15 na kucheza mechi sita kabla ya kuondoka kwenda kushiriki michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment