Tuesday 4 March 2014

BILIONEA ANASWA KWA UNGA DAR

BILIONEA maarufu jijini Dar es Salaam, Ali Khatibu Haji ‘Shkuba’(44) ambaye alikuwa akisakwa kwa muda mrefu na Kikosi Maalum cha Polisi Tanzania kwa madai ya kujihusisha na biashara haramu ya ‘unga’, amenaswa.

Bilionea Ali Khatibu Haji ‘Shkuba’(44) aliyenaswa na polisi.
Vyanzo vililiambia gazeti hili kwamba, mtuhumiwa huyo alikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar, Februari 23, mwaka huu, saa sita mchana akijianda kwenda nchini Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, mara baada ya Shkuba kukamatwa alisafirishwa usiku huohuo kwenda mkoani Lindi chini ya ulinzi mkali wa polisi ambapo Februari 27, mwaka huu aliunganishwa na watuhumiwa wengine na kufikishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Kusini.
Madawa ya kulevya.
Shkuba ambaye ni mkazi wa Mikocheni, Dar ni mfanyabiashara mwenye maduka ya kubadili fedha (bureau de change) jijini, ana makampuni ya ulinzi na nyumba Mikocheni pia anamiliki magari ya kifahari likiwemo aina ya Jeep lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 150.
Vyanzo hivyo vilisema mtuhumiwa huyo alikuwa akisakwa na kikosi kazi tangu Januari 12, 2012 na inadaiwa kwamba alikimbilia nje ya nchi na kurudi kwa siri na ndipo jeshi hilo liliamua kumuwekea mtego.
Taarifa ziliendelea kusema kuwa, tangu vita ya kuididimiza biashara ya unga ianze nchini, hakuna bilionea aliyewahi kukamatwa zaidi ya mtuhumiwa huyo.

No comments:

Post a Comment