Thursday 20 March 2014

MAKOSA YA KIBINADAMU YALIIGHALIMU YANGA.

Siku ya jumapili march 9 2014 Dar es Salaam Young African walicheza na Nationa Al Ahly ya Misri huko Misri pia,hadi kipindi cha kwanza kinaisha ubao ulisomeka bila bila na baada ya kipindi cha pili katika dakika ya 72 Al Ahly walipata bao hadi mpira unaisha Yanga sifuri na Al Ahly goli moja na kuzifanya wawe na uwiano wa bao moja kwa moja kwani katika mzunguko wa kwanza Yanga ilishinda goli moja,bao lilofungwa kwa utaalamu kabisa na beki kisiki wa yanga canavaro kwa kichwa malidadi cha kupalaza.

Baada ya mpira kwenysha na uwiano kulingana kwa taratibu za CAF kilifuata ni penati tanotano ambapo yanga walifunga tatu wafungaji ni Canavaro,Okwi na Kavumbagu kwa upande ya waliopoteza ni Joshua,Bahanuzi na Mbuyo Twite na kufanya tutolewe kwa penati 4 kwa 3.

Tuseme ukweli safari hii Yanga walijiandaa kwa asilimia karibu mia moja kuanzia mahitaji kama vile vifaa vya michezo kama jezi na viatu ambavyo vyote kwa pamoja vilikuwa vipya kwa nyunbani na ugenini tena jezi waliochezea Misri ilikuwa ya ubora wa hali ya juu ikiambpatana na fulana za ndani kwa ajili ya kujikinga na baridi katika mji wa Alexandria ambako Simba simba alilala bao 5 kwa moja na timu ya Al Hadoud.Vifaa vingine ni usafiri wa kwenda Misri kwa wakati na ule wa ndani toka Caoiro hadi Alexandria.
Sio hayo tu walijianda malazi na chakula waraabu safari hii hawakupewa nafasi kabisa ya kuhujumu kama walivyozoea kuzifanyia timu mbalimbali wanapokwenda kucheza kwao.Kwa mandalizi haya walipo changanya na mazoezi kuwaweka wachezaji kisaikolojia ndicho kimewapa haya matokeo na kuvujna mwiko wa miaka mingi wa kutokuwafunga waarabu,hongera sana Yanga pamoja na kutolewa mmtupa heshima kubwa ndani na nje ya Tanzania.
Pamoja na pongezi hizo za dhati kutoka moyoni kwangu kuna sehemu nadhani tulikosea na haya ni makosa ya kiubinadamu na sio kumnyoeshea mtu kidole ni bora kujadiri kusudi siku nyingine itaongeza umakini zaidi.Kwa maoni yangu timu iliyocheza mchezo wa kwanza haikustahili kubadilika sana ingawa Nionzima alilipotiwa kuumwa nahisi pia ilimchanganya kocha na kwasababu Ngasa alicheza namba nane na kiukamilifu sana ndiyo maana alimpanga namba nane badala ya Nionzima aliyekuwa mgonjwa.
Waliocheza mchezo wa kwanza ni Dida,Twite,Joshua,Canavaro,Yondani,Domayo,Ngasa,Niyonzima,Kiiza,Msuva/Kavumbagu na Okwi.Kule Misri walianza wote kasoro Niyonzima badala ya ngasa akarudi nane baadaye kutoka na kuingia Chuji na ngasa kutolewa mimi  naona hapa haikuwa sahihi kama Chuji angeingia Ngasa angeenda pembeni alafu Okwi angeingia ndani Kavumbagu angepumzika badala ya ngasa na Ndomayo angechza nane kama kiungo mshambuliaji na Chuji angerudi sita kuwa kiungo mkabaji sikuona pia ulazima wa kumtoa Msuva na kuingia Bahanuzi ambye kwenye ligi achezi mara kwa mara kwa maana hiyo hakuwa fiti kisaikolojia nigawa haina uhusiano na ukosaji wa penati,kwa mawazo yangu mabadiliko yaliyofanyika kipindi cha pili ndiyo yaliigharimu timu kwa kuipunguzia kasi walioanza nayo na kutoa mwanya kwa beki wa kulia kupanda na kutufunga ila isijengwe kuwa ni hujuma haya ni makosa ya kibinadamu na hakuna sababu ya kumlaumu Mtu tunalazimika kuongea haya kwa akiba ya kesho.
Vinginevyo Yanga imeonyehsa umuhimu wa mandalizi na sio kusubiri muijiza na pia napenda kumpa pole Manji aliamua kuwapa wana yanga zawadi kwa kuwatoa warabu lakini bahati aikuangukia kwake pole na pongezi kwa mafanikio hayo.
Tuonane wiki ijayo.Katika gazeti la Dimba la jumapili na Fikira Yakinifu

No comments:

Post a Comment