Thursday 20 March 2014

MAKATO HAYA BADO NI KIZUNGUMKUTI KWA TIMU

HAYA MAKATO YANAZIHUMIZA TIMU


MECHI ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Al Ahly kutoka Misri iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishonimwa wiki imeingiza sh. 448,414,000.Mapato hayo yametokana na watazamaji 50,202 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa viingilio vya sh. 7,000, sh. 13,000, sh.25,000 na sh. 35,000.
Mgawo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 68,402,135.59, gharama za kuchapa tiketi ni sh. 10,343,219, waamuzi na kamishna sh. 14,665,930 na matangazo sh. 15,679,000. Uwanja sh.50,898,557.31, gharama za mchezo sh. 33,932,371.54, Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF)/Shirikisho la Mpirawa Miguu Afrika (CAF) sh.33,932,371.54 wakati Yanga ilipata mgawo wa sh.220,560,415.01.Hii ni kwa mujibu wa Taarifa kutoka TFF.
Kabla ya kile nilichotaka kukisemea leo labda nigusie kidogo juu ya mapato yaliyopatikana haiendani na uhalisia wa washabiki waliongia uwanjani siku hiyo pamoja takwimu zunu kuonesha ni watu 52,202 ndiyo walioingia uwanjani ni zaidi ya idadi hiyo kwani uwanja ulijaa hadi kwenye viunga na vikorido yaani njia za kupita kwa maana hiyo watu walikuwa zaidi ya idadi mlioitaja mategemeo ya wadau waliowengi mapato yangefikia millioni 6 kwa uchache wake na hii ndiyo maana wadau wanasisitiza Tiketi za electronic ndiyo dawa lakini yaelekea wenye mpira wao hawapo tayari kwa kuwa wamezoea kujinemesha na kuongeza magari ya kisasa na majumba ya kisasa hapa mjini,wanajulikana na wanachokifanya kinajulikana tatizo ni watu tumekuwa waoga kuambiana ukweli.
Malinzi wewe fuatilia kwa ukaribu sana utwajua tu ndani ya shirikisho hilo wapo watu aina ya mchwa ila kama hutapenda kuwa sehemu ya mchwa hao wadau wanawajua kwa majina na matendo yao.
Kwani mashabiki wamechoka kuibiwa na wana mpangowa kuanzisha umoja wao ikiwezekana wagomee kuingia uwanjani kwa shinikizo la kuziba mianya ya wizi sambamba na kuborehsa mfumo wa kielectronic mapema iwezekanavyo,na chama ndiyo suluhisha la sauti ya pamoja ya washabiki bila kuasili ushabiki wao wa timu husika.
Leo napenda kuanzisha mjadala kwa wadao wa soka juu ya mgawanyo wa mapato japo minya ya wizi ni mkubwa bado hata mgawanyo wake kiukweli unaziumiza sana timu tena timu zetu kiujumla ni maskini ingawa umasikini mwingine pia ni watokutumia Rasilimali vizuri hasa Rasilimali watu na majengo kwa baadhi ya timu kwa zile kongwe.
Mfano halisi mchezo wa juzi kati ya timu Yanga na National Al Ahly ya Misri jumla ya mapato ni sh 448,414,000 wakati Yanga ilipata mgawo wa sh.220,560,415.01 ambao nu nusu ya mapato yote kwangu mimi nafikri si halali ukilinganisha na gharama za mandalizi ya mchezo kwa timu husika.Makato ya ongezeko la Thamani yaani VAT sina nalo mataizo hata kidogo kwani ni swala la kisheria.Kwa gharama hizi zingine zingine ni sawa ila kiwangu kilichotumika pia chatutia shaka na gharama zingine hazikustahili kabisha kwa mfano katika mchezo wa Yanga mgao wa waamuzi na kamishna sh. 14,665,930,hizi zote za nini kwani hawaulipwa na CAF,FIFA TFF kutegemia michzo inaandaliwa na nani kwa mfano ligi kuu ni TFF ndiye anawajibika kuwalipa waamuzi na makamishna sasa hizi milioni 14 za kazi gani kwa waamuzi,ninachojua mimi nchi husika inatakiwa iwaandalie sehemu ya kulala na hayo malipo wanalipa wenyewe ila tu jukumu la usafiri wa ndani na gharama zake ndiyo litahihusu timu au nchi husika sasa hizi million zote ndizo zitumike kuwatoa Airport hadi Hotelini na kuwatoa Hotelini hadi uwanja wa Taifa na kuwarudisha Hotelini na hatimaye uwanja wa ndege?Pia tufanya tumewakarimu kama jadi ya watanzania kwa lengo la kuwafanya labda wachezeshe Fair Play na hilo ni jukumu lao na ndiyo miko ya waamuzi wote ulimwenguni au basi upendeleo nao sijawahi kuona Tanzania imenufaika nao zaidi ya mara zote wenyeji ndio ubebwa hii ni kwa mtazamo wangu wa kiufundi kwa michezo mbalimbali ya kimataifa ningetoa mifano lakini si lengo langu kwa leo bado hicho kiasi ni kikubwa kwa huduma ya watu wanne kwa muda wa siku moja au mbili siamini kama kuna hoteli inalipiwa zaidi ya million mbili kwa siku angalia Yanga iliwandalia million 16 kwa hoteli mojwapo ni nzuri na ya kisasa kwa timu ya Al Ahly kwa watu zaidi ya 25 na kwa zaidi ya siku 4 jamani nini hizo million 14 kwa watu wanne kwa siku mbili ni bora mkatoa mchanganua kila mdau aelewe na kujenga uwazi wa mapato zaidi.
Gharama za matangazo sh. 15,679,000,hapa napo panahitaji ufafanuzi zaidi haya ni matangazo ya uwanjani tu au kuna mengineyo?wadau wanaomba kujua ni matangazo gani hayo ambayo TFF mmeingia gharama yote hiyo na kama mlipata idhini ya Viongozi wa Yanga au mnatumia mnawaonesha mchanganuo?Hizi nazo wadau wana masdhaka nazo lisiwe likawa dilisha la kujipatia kipato kwa wajanja wachache.
Gharama za kuchapa tiketi ni sh. 10,343,219, mana yake tiketi moja ni zaidi ya sh.1700 kwa kugawanya hiyo pea kwa watu 60,000 waliotegemewa kuingia uwanjani inga hali halisi ya uwanja ni watu 57,000 waliokaa kwenye viti nayo kwa tiketi zile nafikiri ni kubwa zaidi.Gharama za Uwanja sh. 50,898,557.31,jamani kwa lipi?kama ni kwa asilimia pia naona si sawa lazima kuwa na kiwango kwamba pesa ikizidi kiasi fulani makato yake yawe fixed huku ni kuiumiza timu hapa napo makato yatazamwe upya hasa kwa uwanja wa Taifa unaogharamiwa na Serikali kwa kiasi kikubwa wakati mwingine pia ni fundisho kwa timu kujenga uwanja wao hata hivyo bado ukweli unabaki kuwa pesa iliyochukuliwa na uwanja ni kubwa mno.
Gharama za mchezo sh. 33,932,371.54 hizi nazo kuna maswali mengi ya kujiuliza hii million 33 iligharamia nini ni zile sambusa na soda wanazokunywa na kula wageni wa heshima pale jukwaani au ulinzi na usalama wakati viti vimeng'olewa na kutupwa bila kuwakamata wahusika na gharama zije zibebeshwe timu husika?au chupa zilizotupwa uwanjani bila kumksamata mhusika? iwangawa siwezi kuwabeza wamna usalama ila hgarama ya million 33 wadau wanataka kuzijua kwa mchanganuo halisi pia tukumbuke jukumu la usa;lama ni la Serikali kuhakikisha usalama unakuwepo kwa mtu mmojammoja au kikundi na hatimaye wanamichezo wote wanapokuwepo uwanjani.
Ipo mifano mingi tu hata kwa michezo ya ndani kwa uchache wake ebu angalia mapato na timu zilipata nini,


MECHI za Ligi Kuu Bara zilizohusisha Yanga na Simba na kuchezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam za hivi kribuni zilingiza Sh101 milioni.
Yanga ambayo ilicheza Ruvu Shooting iliingiza Sh68.4 milioni kutokana na mashabiki 11,972 kuingia uwanjani.
Katika mechi hiyo kila klabu ilipata mgawo wa Sh15,687,488 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa kutokana na mapato hayo ni Sh 10.4 milioni. Gharama za tiketi ni Sh3.8 milioni na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ilipata Sh 4.8 milioni wakati uwanja ulipata Sh8.1 milioni.
Gharama za mchezo zilikuwa Sh4.8 milioni wakati Mfuko wa Maendeleo ya soka (FDF) Sh2.4 milioni. Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA) na Chama cha Soka Pwani (COREFA) kila kimoja kilipata Sh945,110.
Simba na JKT Ruvu iliyochezwa juzi Jumapili na kushuhudiwa na watazamaji 5,850 iliingiza Sh32.7 milioni kwa viingilio vya Sh5,000, Sh 15,000 na Sh20,000. VAT iliyolipwa ni Sh4.9 milioni.
Kila klabu ilipata mgawo wa Sh7.4 milioni, tiketi ni Sh2.5 milioni huku gharama za mechi zikiwa Sh 2.2 milioni. Uwanja ulipata Sh3.7 milioni wakati TPLB walipata Sh2.2 milioni. Mgawo mwingine ni FDF Sh1.1 milioni na DRFA Sh881,376.
Ebu angalia hapa bodi ya ligi inapata mgao wakati ni kamati moja wapo iliopo chini ya TFF ni maamuzi yake huwa ni ya TFF kwa nini mzigo huo uwende kwa timu shiriki?na ni nani anakagua mahesabu yake?wakati huohuo kuna mfuko wa maendeleo wa soka ambao nao upo chini ya TFF na mgao wa TFF upo pale pale haya makato ni sehemu ya kuchangia timu kuwa masikini kila siku.

Kuna sababu TFF na vyama shirikishi nikiwa na maana vyama vya mpira wa miguu vya mikoa badala ya kuzidi kumkamua ng'ombe maziwa mweye njaa kali na hawana msaada wowote kumwokoa.Ni vizuri kuboresha utoaji wa tiketi na kuaachana na mfumo wa vishina ambao wezi wamejificha humo najua jitihada zipo ila ongezeni kasi.

Yangu ni hayo tukutane wiki ijayo katika Gazeti la Dimba makala ya Fikra Yakinifu kila Jumapili.

No comments:

Post a Comment