Mbunge wa jimbo la Bahi (CCM) Omar Baduel amefikishwa kwa Katibu wa Bunge Dr Kashilila kwa kosa la kuto mlipa mshahara msaidizi wake wa jimbo kwa kipindi chote cha miaka minne,Said Kayumbo amelalamikia ofisi ya bunge na kuomba iingilie kati ili apate mshahara wake kwa miaka yote minne. Said kayumbo alisema mbunge huyo amekua akimpa 20,0000 au 30,000 wakati mshahara wa msaidizi wa mbunge ni 450,000.

Aidha mbunge huyo amekua na kashifa nyingi kama ile ya rushwa ambayo kesi yake inaendelea kisutu,mwezi wa february 2014 alisomewa tuhuma ya kula pesa ya mfuko wa jimbo,mwaka 2009 alifukuzwa uenyekiti wa halmashauri ya bahi kwa tuhumu za kuiba mifuko ya cement ya shirika la world vision kwenye kata yake ya Chipanga pamoja na tuhuma ya kushirikiana na mkurugenzi wa bahi kujihusisha na rushwa.