KIPA mpya wa Simba, Yaw Berko kutoka Ghana ametamka kuwa amekuja
Tanzania ili kuing’arisha Simba kwenye Ligi Kuu Bara na michuano
mingine.
Kipa huyo pia amesisitiza kuwa, Yanga kwake
imebaki historia huku akinukuu maandiko ya Biblia: “Dunia kila kitu
kitapita, na yeye Yanga alipita na kwa sasa imebaki historia, sasa yeye
ni mchezaji wa Simba.’’
Berko, kipa aliyeipa mafanikio Yanga lakini
alimalizana nao na kurudi kwao Ghana msimu uliopita kuichezea klabu yake
ya zamani ya Liberty Professionals. huyo aliyetua nchini juzi Jumamosi
asubuhi ameweka wazi kuwa ataichezea Simba kwa miezi sita tu kulingana
na makubaliano yao lakini hadi jana Jumapili mchana alikuwa bado
hajasaini.
Berko aliliambia Mwanaspoti kuwa amerejea tena
Tanzania kwa lengo moja tu la kuifanya Simba ing’are kwenye mzunguko wa
pili na kuipa ubingwa.
“Nimerudi kuifanya Simba ing’are mzunguko wa pili,
nina uzoefu na ligi ya Tanzania, nawajua wachezaji na sehemu kubwa ya
washambuliaji,’’alisema Berko kipa bora wa Ligi Kuu Bara 2011-2012
alipokuwa Yanga.
Aliongeza: “Naujua ushindani, ninachowaahidi Simba ni kuwa mambo yatakuwa mazuri, tuombeane tuwe wazima kiafya.”
Berko anajiunga Simba ambayo ina makipa wengine, Abel Dhaira, Andrew Ntalla na Abou Hashim.
Kuhusu makipa hao alisema: “Sijui chochote juu ya
makipa hao, vyovyote sawa kwani wao wapo kwa ajili ya Simba na mimi
nimekuja kwa ajili hiyo hiyo, kikubwa ni ushirikiano.
No comments:
Post a Comment