Stars iliivua Uganda ubingwa wa Chalenji kwa penalti 3-2 katika
mchezo wa robo fainali uliopigwa mjini Mombasa juzi Jumamosi na sasa
itaikabili Kenya kesho Jumanne kwenye mchezo wa nusu fainali.
Kocha huyo alisema aliendelea kuwatumia mastraika
watatu Mrisho Ngassa,Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu kwa muda mrefu
kwa kusudi maalum la kushambulia licha ya Aboubakary Salum kuonyeshwa
kadi nyekundu.
Poulsen alisema; “Niliendelea kuwatumia Ngassa,
Samatta na Ulimwengu kwa muda ili kutunza mashambulizi ambayo yaliipooza
Uganda,ilikuwa ni mechi ngumu na kushambulia ndio kulitusaidia.
“Kuwatoa mabingwa watetezi si kazi rahisi,tumefanya kazi nzuri, timu imecheza vizuri na imefanya Watanzania wanachotaka.
“Tulipoingia lengo ilikuwa ni kufika robo fainali,
tumeingia na tukamtoa bingwa mtetezi kila mmoja sasa atakuwa
akituangalia sisi, tunaingia kwenye nusu fainali kwa ari
ileile,”alisisitiza Poulsen ambaye huenda akamkosa Ngassa na Ulimwengu
kwenye mchezo dhidi ya Kenya baada ya kuumia dhidi ya Uganda.
Ngassa na Ulimwengu waliumia katika mchezo na
Uganda, Ngassa aliumia kifundo cha mguu na kutolewa na nafasi yake
kuchukuliwa na kiungo Athuman Iddi’Chuji’ wakati Ulimwengu aliumia nyama
za paja ingawa aliendelea na mchezo hadi mwisho.
Hatma ya wachezaji hao wawili itajulikana leo
Jumatatu timu hiyo itakapofanya mazoezi mepesi mjini Nairobi ikijiandaa
kwa safari ya saa mbili na nusu kesho Jumanne kuelekea Machakos
itakakopigwa mechi.
No comments:
Post a Comment