Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema ameeleza
kushangazwa na hatua ya kamati ya Bunge kukwepa kuzungumzia suala la
kurushwa bomu kwenye mkutano wa chama chake huko Arusha, Julai 15, mwaka
huu.
Akichangia mjadala wa taarifa ya Kamati ya Kudumu
ya Ulinzi na ya Mambo ya Nje, bungeni jana, Lema alisema kamati hizo
ziligusia suala la bomu lililorushwa kwenye Kanisa Katoliki Olasiti,
Arusha na kuachana kuzungumzia lile la mkutano wa Chadema uliofanyika
kwenye Viwanja vya Soweto.
Alisisitiza msimamo wa Chadema kuwa kinao mkanda
wa video unaoonyesha mtu aliyelipua bomu Uwanja wa Soweto na kushangaa
taarifa ya kamati hizo mbili kutokuzungumzia tukio hilo.
Alisema ushahidi huo ungewezesha vyombo vya ulinzi
na usalama kumbaini mtu aliyerusha bomu hilo na kusisitiza kuwa wako
tayari kukabidhi mkanda huo kwa tume huru itakayoundwa na Serikali
kuchunguza tukio hilo.
“Lakini bahati mbaya alikamatwa jambazi kule Nzega
akapigwa ili anitaje mimi ndiye niliyerusha bomu Olasiti na nilipigiwa
simu na mmoja wa ndugu wa jambazi huyo akaniambia kuhusu suala hilo...
Tunao ushahidi nani alitaka kutuua, Serikali iunde tume tupeleke
ushahidi wetu,” alisema.
Bomu katika uwanja huo lililipuka wakati Chadema kikihitimisha kampeni zake za udiwani katika Kata ya Kaloleni.
Mei 5, mwaka huu, watu wasiojulikana walirusha
bomu katika mkusanyiko wa kidini katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu
Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti na kusababisha vifo vya watu
watatu.
mwananchi
mwananchi
No comments:
Post a Comment