Thursday, 15 May 2014

POLISI WAMGUNDUA KINARA WA MTANDAO WA WIZI KATIKA MABENKI JIJINI D’SALAAM NI HUYU HAPA

 Jeshi la Polisi Kanda Maalum D’Salaam limefanikiwa kumbaini mtuhumiwa mhimu ambaye ni kinara wa mtandao wa wizi katika mabenki ambaye anajulikana kwa jina la RONALD S/O MOLLEL umri miaka 37, mfanyabishara na mkazi wa Kimara Bonyokwa Jijini D’salaam.
        
Mtuhumiwa huyu amekimbilia mafichoni mara baada ya tukio la ujambazi katika Tawi la Benki ya Barclays  Kinondoni lililotokea tarehe 15/4/2014 ambapo majambazi walifanikiwa kupora kiasi kikubwa cha fedha T.Shs.390,220,000/= , USD 55,000/= na EURO 2150/=.  Aidha sasa imefahamika kwamba mtuhumiwa huyu ni mume wa mtuhumiwa wa kwanza katika tukio la Barclays Benki aitwaye ALUNE D/O KASILILIKA @ ALUNE D/O MOLLEL , miaka 28,  Mkazi wa Kimara Bonyokwa ambaye ni Meneja wa Benki Tawi la Barclays Kinondoni.

Mtuhumiwa Mollel anatafutwa kwa kila hali kwa vile yeye ndiye alikuwa kinara wa kupanga tukio hilo la Barclays na mara baada ya tukio ametoroka na kiasi kikubwa cha fedha hizo zilizoibiwa.Zipo taarifa za kuaminika kuwa mtuhumiwa huyu amekuwa akipanga na kushiriki kikamilifu katika matukio mbali mbali ya uhalifu mkubwa ikiwa ni pamoja na kuongoza vikundi vya majambazi vilivyowahi kupora katika mabenki mbali mbali katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.  Mtuhumiwa huyo ni hatari kwani ana mtandao na watumishi muhimu katika matawi mbali mbali ya mabenki kwa lengo la kufanikisha uhalifu katika mabenki hayo.

Polisi limelazimika kutoa picha yake hadharani kwa kutumia dhana ya ulinzi shirikishi ili mtuhumiwa huyu akionekana akamatwe na taarifa zitolewe katika kituo chochote cha Polisi ikiwa ni lengo la polisi kupambana na uhalifu katika dhamira ya kuzuia uhalifu, kulinda maisha na mali za wananchi. 

Zawadi nono ya fedha taslim itatolewa kwa siri kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa mtuhumiwa huyu.  Pamoja na maelezo hayo mtuhumiwa mwenyewe sasa anapewa fulsa ya kujisalimisha katika kituo chochote cha polisi kabla ya kukamatwa kwa njia nyingine.

Mtoto aanguka toka orofa ya 11 anusurika.



Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja amenusurika kifo baada ya kuanguka kutoka orofa ya 11 ya jengo moja mjini Minnesota Marekani.

Vyombo vya habari katika jimbo hilo vimeripoti kuwa Musa Dayib, amevunjika mkono mara mbili na kwa sasa anapumua kwa usaidizi wa mashine japo madaktari wanamtarajia kuishi.Musa aliteleza katikati ya mianya inayozingira sebule yao katika orofa ya 11 ya mjengo huo wenye nyumba na makazi ya watu.

Muuguzi mkuu katika zahanati aliyolazwa amesema kuwa Musa anatarajiwa kuishi baada ya kuanguka katika eneo lisilo kavu sana.Jamaa na marafiki wa familia hiyo ya kisomali wamepigwa na butwaa kutokana na tukio hilo.

Tukio hilo lilizua mjadala kama ni muujiza au la kuwa amenusurika kifo lakini watafiti wameelezea kuwa mtoto ananafasi nzuri zaidi ya kuishi hata baada ya kuanguka ama kupatwa na janga lolote lile kwani mwili wao bado ni mwororo na mifupa ya mtoto huwa bado ni laini kinyume na mtu mzima ambaye tayari mifupa yake ni kavu na mwili wake ni mkubwa na mzito.

Abdirizak Bihi alisimulia muujiza huo kwa gazeti la The Star-Tribune .

"baada ya kushuhudia yaliyotendeka hapa ninahofia usalama wa wazazi wa mtoto ambao hadi kufikia sasa wamepigwa na bumbuazi hawazungumzi na yeyote."Dakta Tina Slusher, aliyemhudumia mtoto Musa, alisema hakuna vile mtu mzima angenusurika baada ya kuanguka umbali kama huo.

Haya ni mambo ya dunia,Mwanamke kunyongwa kwa kuolewa na mkristu Sudan.



Mahakama nchini Sudan imemhukumu kifo mwanamke mmoja anayedaiwa kubadili dini yake na kuolewa na mwanamume mkristo.

Daktari Mariam Yahya Ibrahim Ishag, ambaye babake ni muisilamu alishitakiwa kwa kosa la kuasi dini pamoja na kufanya zinaa kwa kuolewa na mwanamume mkristo , kitu ambacho dini ya kiisilamu imeharamisha kwa wanawake.

Mariam mwenye umri wa miaka 27 pia ni mjamzito na pia atapata adhabu ya mijeledi miamoja kwa kosa la zinaa. Maafisa wakuu wanasema kuwa icha ya Mariam kulelewa kwa njia ya kikristo yeye bado ni muisilamu kwa sababu hiyo ndiyo dini ya babake. Kwa kawaida wanawake waisilamu hawaruhusiwi kuolewa na wanaume wakristo ingawa wanaume waisilamu wanaruhusiwa kuwaoa wanawake wakristo.

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International linasema kuwa Bi Ishag alilelewa kama Mkristo muorthodoxi kwa sababu babake hakuwepo naye maishani mwake.

Kesi ya Ibrahim ni ya kwanza ya aina yake kusikika nchini Sudan , kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu, wamelaani uamuzi huo wa mahakama na kuitaka serikali ya Sudan kuheshimu haki na uhuru wa watu kuabudu.

Maafisa wa balozi za mataifa ya magharibi pia wamekemea vikali kesi hiyo na kuelezea asiwasi wao kuihusu.Maafisa hao wamewataka maafisa wa sheria nchini humo kuangalia kesi hiyo upya na kuhakikisha kuwa Mariam anatendewa haki.

Waziri wa mawasiliano amesema kuwa sio Sudan peke yake ambako sheria za kiisilamu zinafuatwa na ambako sio sawa kwa mtu kubadili dini yake, hali hiyo pia ipo nchini Saudi Arabia na katika nchi zingine zinazofuata sheria za kiisilamu.

Serikali ya Rais Omar al-Bashir inakabiliwa na changamoto nyingi za kiuchumi na kisiasa hasa baada ya kujitenga na Sudan Kusini ambako mafuta yake yalikuwa yanatoka mwaka 2011.

Onyo kwa wanaotuma ujumbe wa ngono Kenya

Kumtumia mtu ujumbe wenye picha za watu walio uchi na zenye mada ya ngono nchini Kenya kunaweza kukuweka mashakani.
Maafisa wakuu wanasema kuwa yeyote atakeyepatikana na hatiaatafungwa jela kifungo cha miezi mitatu kwenda chini.
Afisaa mkuu kutoka tume ya kitaifa ya mawasiliano, Christopher Wambua ameambia vyombo vya habari nchini humo kwamba watu wenye tabia hiyo ya kutuma ujumbe wa kingono pamoja na picha zenye watu walio uchi watatozwa hadi shilingi elfu hamsini za Kenya au dola miatano na themanini na nane kama faini au kufungwa jela..
Onyo hilo litawaandamana hasa wale walio na uzoefu wa kutumiana ujumbe kama huo kupitia kwa simu ya mkononi au kwenye internet.
Kwa mujibu wa taarifa za serikali, kiwango ambacho watu hutumiana ujumbe wenye mada ya ngono pamoja na picha za watu walio uchi, zao wenyewe au za mtu mwingine kwa simu zao za, smartphone ilipanda hadi asilimia sitini.sexting

Tuesday, 13 May 2014

YANGA SC, TWITE AONGEZA MKATABA

Mlinzi kiraka wa timu ya Young Africans Mbuyu Junior Twite leo ameongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia klabu ya Yanga baada ya kufikia makubaliano na uongozi na kupata majibu ya Shirikisho la Soka nchini TFF juu ya idadi ya wachezaji wa kimataifa kwa msimu ujao 2014/2015.
Usajili wa Twite umefanyika leo makao makuu ya klabu ya Yanga chini ya Katibu Mkuu Bw Beno Njovu ambapo mchezaji amesema ataendelea kujitolea kwa uwezo wake kuisaidia timu yake ya Yanga.
Katibu Mkuu wa Young Africans Beno Njovu amesema wameingia mkataba wa mwaka mmoja na Twite baada ya pande zote kukubaliana, hivyo kuanzia sasa Twite ataendelea kuwa mchezaji wetu kwa msimu ujao wa 2014/2015 na kusisitiza kuwa usajili ndio umeanza sasa.
Akiongea mara baada ya kuweka sahihi kwenye mkataba wake mpya Twite amesema anajisikia furaha kuendelea kuwa mchezaji wa Yanga, kwani anafurahia maisha ya Jangwani, wapenzi, washabiki, viongozi na wachezaji ni marafiki/ndugu ndani na nje ya Uwanja.
Aidha Twite amesema Yanga ni miongoni mwa timu kubwa barani Afrika, zenye washabiki na waachama wengi hivyo wangu ni fahari kuendelea kuitumika timu hii ambayo tangu kujiunga nayo nimekua nikijtoa kwa moyo wangu wote kusaka mafanikio.
Mbuyu Twite amekua ni mchezaji wa Young Africans kwa kipindi cha miaka miwili tangu Julai 2012 alposajiliwa huku katika kipindi hicho chote akiwa ni mchezaji wa kikosi cha kwanza ambapo msimu uliopita aliweza kuisadia timu yake kutwaa Ubingwa wa Lig Kuu ya Vodacom na msimu huu kushika nafasi ya pili.

Monday, 12 May 2014

RAIS KIKWETE ALIPOKUTANA NA WANASOKA WA TANZANIA SAMMATA NA ULIMWENGU WANAOCHEZEA TP MAZEMBE.

Wachezaji wawili wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Alli Samatta na Thomas Ulimwengu ambao wanachezea klabu ya TP Mazembe ya Congo hii leo walipata faraja kubwa ya kutembelewa na mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho kikwete.
Rais Kikwete ambaye yuko katika ziara kubwa nchini Kongo alipata fursa ya kubadilishana mawazo na wanandinga hao majira ya 06.15 mchana ambao wanachezea katika klabu ya bilionea Musa Kitumbi.Rais aliwasili Kinshasa tangu Ijumaa usiku kwa ajili ya ziara rasmi ya masaa 24 katika muktadha wa ushirikiano kati ya DRC na Tanzania ikiwa ni mwaliko wa Rais Kabila na akafanikiwa kukutana na wachezaji hao.Mazungumzo ya Rais Kikwete na wachezaji hao yalichukua takribani robo saa katika Hoteli moja maarufu iitwayo Congo River ambapo aliwatakia kila la kheri wachezaji wake katika mechi ya Jumapili na kuwatakia mafanikio katika kazi yao hiyo ya soka.

Rais Jakaya Kikwete aliwakumbusha Samatta na Ulimwengu kuwa taifa zima linajiona fahari kuwaona wakiwa katika jezi za rangi ya TP Mazembe na Taifa Stars.
Hiyo ni ishara kuwa Rais anawatambua na kuthamini washambuliaji Samatta Mbwana na Thomas Ulimwengu ambao daima wanajitoa katika kila hali bila kujali Jersey.

Kikosi cha Ghana:Kuelekea Brazil 2014


Goalkeepers: Fatau Dauda (Orlando Pirates), Adam Kwarasey (Stromsgodset), Stephen Adams (Aduana Stars).
Defenders: Samuel Inkoom (Platanias), Daniel Opare (Standard Liege), Harrison Afful (Esperance), Jeffrey Schlupp (Leicester), John Boye (Rennes), Jonathan Mensah (Evian), Jerry Akaminko (Kisehirspor), Rashid Sumalia (Mamelodi Sundowns).
Midfielders: Michael Essien (AC Milan), Sulley Muntari (AC Milan), Rabiu Mohammed (Kuban Krasnodar), Kwadwo Asamoah (Juventus), Emmanuel Agyemang-Badu (Udinese), Afriyie Acquah (Parma), Christian Atsu (Vitesse), Albert Adomah (Middlesbrough), Andre Ayew (Marseille), Mubarak Wakaso (Rubin Kazan).
Strikers: Asamoah Gyan (Al Ain), Kevin-Prince Boateng (Schalke 04), Abdul Majeed Waris (Valenciennes), Jordan Ayew (Sochaux), David Accam (Helsingborg).

SOMA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA WALIOMALIZA MWAKA 2014 WANAOTAKIWA KURIPOTI JKT JUNI 01, 2014

PAMOJA BLOG: SOMA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA WALIOMALIZA MWAKA 2014 WANAOTAKIWA KURIPOTI JKT JUNI 01, 2014

WINGEREZA WATAJA KIKOSI KOMBE LA DUNIA 2014 BRAZIL


Goalkeepers: Joe Hart (Manchester City), Fraser Forster (Celtic), Ben Foster (West Brom)
Defenders: Glen Johnson (Liverpool), Phil Jones (Manchster United), Phil Jagielka (Everton), Gary Cahill (Chelsea), Chris Smalling (Manchester United), Luke Shaw (Southampton), Leighton Baines (Everton), Steven Gerrard (Liverpool), Frank Lampard (Chelsea), Jordan Henderson (Liverpool), Ross Barkley (Everton), Jack Wilshere (Arsenal), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal), Raheem Sterling (Liverpool), Adam Lallana (Southampton), James Milner (Manchester City)
Forwards: Daniel Sturridge (Liverpool), Wayne Rooney (Manchester United), Danny Welbeck (Manchester United), Rickie Lambert (Southampton)

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii


Dengue: Unayohitaji Kujua
Dengue ni ugonjwa unaoleta homa kwa muda wa siku 2 hadi 7 na huambatana na dalili zifuatazo:
- Kuumwa kwa macho.
- Kuumwa kwa kichwa.
- Maumivu ya misuli na viungo.
- Kutokwa na damu (katika fizi au pua).
- Kukwaruzika kwa urahisi.
Huduma ya nyumbani kwa homa ya Dengue ni:
- Pata vinywaji kwa wingi mfano maji, juisi au chai.
- Tumia dawa za maumivu kupunguza homa.
- Usitumie dawa ya "Aspirin" ama "Ibuprofen"
Nenda hospitali haraka unapoona moja ya dalili za tahadhari. Dalili za tahadhari za kuangalia baada ya homa kuondoka:
- Maumivu makali ya tumbo.
- Kutapika mfululizo.
- Kutokwa damu.
- Ngozi kupauka na kuwa baridi.
- Kudhoofika kwa mwili, usingizi mzito.
- Kizunguzungu, kuzimia.
- Kupumua kwa shida.

Mmiliki wa clippers aomba radhi

Mmiliki wa klabu ya mpira wa vikapu ya Los Angeles Clippers, Donald Sterling, ameomba radhi kwa matamshi yake ya kibaguzi.
Shirikisho la mchezo huo nchini Marekani lilimpiga marufuku maisha.
Bwana Sterling aliambia kituo cha televisheni cha American TV kuwa alifanya kosa kubwa sana ambalo hata hajui anavyoweza kulirekebisha.
Katika mahojiano yatakayopeperushwa leo, itakuwa kauli ya kwanza ya Sterling tangu kutokea kakanda nambayo alikuwa anamkarpia mpenzi wake kumtaka akome kujihusisha na watu weusi.

MASTAA KUMFIKISHA MAHAKAMANI,AKIKUTWA NA HATIA KUFUNGWA MIAKA MITANO.


KIMENUKA! Komediani aliyebahatika kuwa maarufu Bongo, Mujuni Silvery 'Mpoki' yuko njiani kupandishwa kizimbani kufuatia mastaa waliodai aliwadhalilisha usiku wa Tuzo za Kili kucharuka na kwenda kwa mwanasheria wao.Kwa mujibu wa chanzo makini, mastaa wanaodaiwa kutinga kwa mwanasheria na kuandikisha maelezo ni hawa wafuatao: Mkurugenzi wa Aset Club inayomiliki Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Asha Baraka, mtangazaji wa runinga, Maimartha Jesse, Meneja wa Wema Sepetu, Martin Kadinda na staa wa filamu za Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’.Wengine ni Mbongo Fleva na mtangazaji, Vanessa Mdee, Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, Aisha Ramadhani ‘Mashauzi’, Maria Sarungi na DJ Bonny Love.

WADAI KUDHALILISHWA BILA KUPEWA NAFASI
Chanzo kilisema kwamba siku ya Tuzo za Kili, Mpoki akiwa MC wa shughuli hiyo, aliwadhalilisha kwa kutangaza ndani ya hadhara iliyohudhuria kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar, mambo ambayo wenyewe “Kule kwa mwanasheria wao, wote walidai kuwa, siku ile Mlimani City, Mpoki alikuwa akitangaza mambo yao, mengine ya siri, mengine si ya kweli, mengine ya udhalilishaji bila wao kupewa nafasi ya kujitetea kama mnavyofanya magazetini.

“Wenyewe wanajua Mpoki hakutumwa na Kili kusema maneno yale bali aliamua yeye kama yeye tu. Ndiyo maana wameamua kushughulika na Mpoki na si mwingine,” kilisema chanzo hicho.hawakupata nafasi ya kujitetea (balansi).

MADAI YAO YA MSINGI
Chanzo kiliendelea kutiririka kwamba madai ya msingi ya mastaa hao  kisheria ni kudhalilishwa, kuzushiwa na kuchafuliwa mbele za watu, jambo ambalo liliwapa usumbufu mbele za jamaa zao, wakiwemo watoto na ndugu wengine waliokuwa wakifuatilia sherehe za utoaji wa tuzo hizo kubwa kuliko zote Afrika Mashariki.

KASHFA ZENYEWE KWA UFUPI
Ili gazeti hili lisijiingize kwenye malalamiko ya mastaa hao linayaandika maneno hayo kwa ufupi sana lakini yenye kueleweka.

MAI; aliambiwa amezipiga jeki nido ilhali ana mtoto.

ASHA; aliambiwa kwa usiku huo alipendeza sana (make up) lakini akionekana kesho yake anaweza kupewa shikamoo kwa mabadiliko ya mwonekano.

RAY; aliambiwa siku hizi amebadilika rangi, si kama zamani. Pia Mpoki alimwambia amesikia ameachana na Johari na yuko na Chuchu Hans.

KADINDA; alimwambia anamuona anakwenda kumpa tuzo shemeji yake (Diamond)...
WEMA; alimuuliza ni kwa nini kila siku kwenye Instagram anatupia picha akiwa anakula mayai tu, anataka watu wamwelewe vipi!

VANESSA; alimwambia afanye mazoezi ya kutembela viatu vyenye visigino (na mengine ambayo si vyema kuyaandika hapa).

WIKIENDA LAWASAKA   
Baada ya madai hayo, gazeti hili liliwasaka mastaa hao mmojammoja ili kusikia ukweli wa madai hayo.
Ijumaa Wikienda lilianza kwa kumsaka Kadinda juzi ambapo simu yake haikuwa ikipatikana hewani kama alivyozoeleka.

Kwa upande wake Ray alikiri kuwepo kwa uwezekano wa kumshitaki kwa kuwa ni kweli alimdhalilisha mbele ya kadamnasi.

Naye Mai alipotafutwa aliwaka akidai kuwa alichokifanya Mpoki hakikuwa sahihi kisheria hivyo jambo hilo lipo.
Kwa upande wake, Isha Mashauzi alisema kuwa labda wenzake wameamua kumshtaki Mpoki lakini hawakuwa wamemjulisha. Mastaa wengine ambao simu zao ziliita bila kupokelewa ni Asha Baraka, Vanessa, Wema na DJ Bonny Love.

MSIKIE MPOKI
Mpoki alipopigiwa simu na kuelezwa kuhusu malalamiko ya mastaa hao, katika hali ya kushangaza alisema hakumbuki nini kilitokea siku hiyo.

“Kusema ule ukweli mimi sikumbuki chochote kile kilichotokea siku ile, we  nitajie majina ya hao watu niwapigie halafu baadaye ndiyo tutaongea,” alisema Mpoki akiweka sharti hilo wakati yeye ndiye aliyekuwa akiwananga jukwaani.

AKIKUTWA NA HATIA KISHERIA
Kwa mujibu wa mwanasheria mmoja (jina tunalo) aliyezungumza nasi, endapo Mpoki akipanda mahakamani na kukutwa na hatia, anaweza kufungwa kifungo cha miaka 5 jela au faini kulingana na uzito wa udhalilishaji huo kwa mujibu wa walalamikaji.

Boko Haram Releases New Video Showing Abducted School Girls

BOKO HARAM WATOA MASHARTI KUWAACHIA WASICHANA WA KINIGERIA ZAIDI YA 2000 WALIOWATEKA.


Kiongozi wa kundi la Boko Haram Abubakar Shekahu amesema kuwa atawaachilia huru wasichana waliotekwa nyara iwapo tu wapiganaji wa kundi hilo wanaozuiliwa na serikali ya Nigeria wataachiliwa huru.
Katika kanda mpya iliyotolewa na kundi hilo, kiongozi huyo, amesema kuwa wasichana hao waliweza kusilimu katika kipindi cha wiki nne zilizopita tangu watekwe nyara.
Kanda hiyo inaonyesha zaidi ya wanawake miamoja wakiwa wamevalia hijabu na kuswali. Abubaka Shekau anasema kuwa wanawake hao ni wasichana waliotekwa nyara na kundi hilo.

Mradi wa reli mpya watiwa saini Nairobi.


Waziri Mkuu wa Uchina, Li Keqiang, na viongozi wa Afrika Mashariki wametia saini rasmi makubaliano ya kujenga njia mpya ya reli itayounganisha mji wa Kenya wenye bandari, Mombasa, hadi Nairobi, Rwanda na Sudan Kusini.
Waziri Mkuu wa Uchina yuko mjini Nairobi akiwa katika ziara ya Afrika.
Njia hiyo ya reli ya upana unaotumika kawaida duniani itagharimu mabilioni ya dola, na itachukua nafasi ya njia ya reli ya sasa ambayo ni nyembamba na ilijengwa zama za ukoloni wa Uingereza.
Sehemu ya kwanza ya reli itajengwa na kampuni za Uchina - jambo lilozusha malalamiko kwamba kampuni nyengine hazikuruhusiwa kushiriki katika kuomba kandarasi.

Chris Brown aongezwa muda jela


Mwanamuziki wa Marekani Chris Brown atasalia jela kwa siku nyingine 131 baada ya kukiri kukiuka amri ya mahakama kuhusu kifungo cha nje alichokuwa amepewa na mahakama.

Muimbaji huyo wa muziki wa mtindo wa R&B alikiri mahakamani mjini Los Angeles mnamo siku ya Ijumaa kuwa alitenda uhalifu mjini Washington Oktoba mwaka jana.Jaji alimuhukumu kifungo cha siku 365 jela ingawa alimpongeza kwa kuhudumia siku 234 katika kituo cha kupata ushauri nasaha.

Brown amekuwa chini ya aungalizi wa mahakama tangu mwaka 2009 alipokiri kumpiga mwanamuziki mwenza na ambaye alikuwa mpenzi wake wakati huo,Rihanna.Mshindi huyo wa tuzo la Grammy amekuwa kizuizini tangu mwezi Machi alipokamatwa kwa kukiuka amri ya mahakama iliyomweka ndani ya kituo cha ushauri nasaha pamoja na jela.

Kifungo alichopata kuongezewa siku kinahusiana na kisa cha ugomvi kilichotokea mjini DC mwaka jana.Brown anakabiliwa na mashitaka ya kumchapa mwanamume mmoja nje ya hoteli moja mjini Washington

Thursday, 8 May 2014

YANGA KUFANYA MABADILIKO YA KATIBA JUNI MOSI.


Uongozi wa klabu ya Young Africans Sports Club umeitisha mkutano mkuu
wa wanachama wa mabadiliko ya Katiba ili wanachama waweze kutoa maamuzi kwenye baadhi ya vipengele vilivyoongezwa kabla ya kuelekea kwenye mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa viongozi.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu mitaa ya Twiga/Jangwani, Katibu Mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu amesema wamefikia kuitisha mkutano huo wa mabadiliko ya Katiba ili wanachama wapate fursa ya kupitisha baadhi ya vipengele kabla ya kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.
"Tumekua na mawasiliano na TFF juu ya kuongezwa baadhi ya vipengele kwenye Katiba yetu kabla ya kufanya uchaguzi mkuu wa viongozi, baada ya hapo ni nafasi kwa wanachama wa Yanga sasa kukutana na kuweza kupitisha hivyo vipengele vitakavyoongezwa kwenye Katiba Mpya" alsiema Beno.
Aidha Beno amesema wanachama wakishapitisha/kukubaliana juu ya hivyo vipengele ndipo uoungozi utawasilisha mapendekezo hayo kwa TFF ambayo ikishayabariki, yatapelekewa kwa Msajili nae akiyapitisha ndipo itakua tayari ni Katiba halali ambayo itatumika kwwenye uchaguzi mkuu.
"Nawaomba wanachama wa Yanga wajitokeze kwa wingi kwenye mkutano wa mabadiliko juni mosi 2014 ili waweze kupitisha hivyo vipengele ambavyo vitapelekea kuwa na Katiba Mpya itakayotumika kwa shughuli za kila siku za klabu ya Yanga SC" aliongea Beno.

Majanga Yanga KOCHA HANS AAGA YANGA!



Hans Van Der Pluijm kocha mkuu wa timu ya Young Africans leo amewaaga rasmi wachezaji wake, viongozi, wapenzi na wanachama baada ya kumalizaa wake wa miezi sita na sasa anakwenda kujiunga na timu Al Shoalah FC iliyopo Ligi Kuu nchini Saudi Arabia.

Kocha huyo mdachi ambaye ameiongoza Young Africans kwa kipindi cha miezi mitano amesema anashukuru kwa sapoti aliyokua akiipata kutoka kwa wachezaji, viongozi, wapenzi na wanachama wa timu hii kwa kipindi chote alipokuwa nchini Tanzania.

"Najua wengi itawashangaza kuona naondoka lakini ukweli ni kwamba niikua na hiyo deal hata hata kabla ya kuja Yanga, nilikua na makubaliano na timu ya Al Shoalah FCmakubaliano ambayo yanaanza mwezi ujao hivyo nilikubaliana na viongozi wa Yanga kuja kufanya kazi kwa kipindi cha miezi sita tu, nashukuru tumefanya kazi salama na baada ya mkataba huo kuisha nipo tayari kurudi kuja kufanya kazi Tanzania" alisema Hans

Naipenda Yanga SC, nimejaza fomu kuomba uanachama hivyo mimi ni sehemu ya Yanga na katika usajili ujao nitawasaidia kuleta wachezaji wazuri ambao wataisaidia timu kwenye msimu ujao kwa Ligi ya Vodacom na mashindao ya Kimataifa.

Kocha Hans anaondoka leo nakwenda Ghana kisha baadae atakwenda nchini Saudu Arabia tayari kwa kujiandaa na maandalizi ya msimu ujao katika timu yangu hiyo ambayo nitaitumikia kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Kuhusu usajili kocha mkuu ameshakabidhi ripoti yake ya kiufundi jana, viongozi wanaifanyia kazi kisha baadae itawekwa wazi.

Yanga sasa nimfumo mpya wa kisasa (digital)

Klabu ya Young Africans imeeingia makubaliano na Benki ya Posta nchini
juu ya mabadiliko ya utengenezaji wa kadi za wanachama kutoka kwenye mfumo wa zamani (analogy) kwenda kwenye mfumo mpya wa kisasa (digital) ambapo sasa wanachama wake watakua wakitumia kadi zenye mfumo wa ATM.

Mkurugenzi Masoko wa Benki ya Posta nchini Bw. Deo Kwiyukwa amesema wamefikia makubaliano hayo baada ya kukaa na viongozi na kuona njia hiyo itaisaidia klabu kuongeza mapatao kwani wigo wake wa kuandikisha wanachama utakua ni mkubwa kwa nchi nzima na kwa muda mfupi.

"Badala ya wanachama kuja Dar es salaam makao makuu kujaza fomu za uanachama watakua wanaweza kufanya hivyo popote walipo kwa kwenda ofisi za Benki ya Posta na kujaza fomu hizo na baadae kupewa kadi ya uanachama" alisema Deo.

Gharama za kujiunga na uanchama zitabakia zile zile Tshs 15,000/=, na ada ya mwaka elfu Tshs 12,000/= ambapo mwanachama wa Yanga atapata kadi ya TPB yenye logo ya timu yake ambayo pia ataitumia kwenye shughuli za kibenkI kwa huduma ya kuweka na kutoa fedha.

Naye Makaumu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Clement Sanga amesema anaishukuru Benki ya Posta kwa kuweza kufikia makubalianao hayo, kwa kutumia mfumo huu wa kisasa tutaweza kujua idadi ya wachama wetu walio hai kwa wepesi zaidi na taarifa zetu zitaweza kuwafikia wanachama kwa uharaka zaidi.

Uzinduzi rasmi wa kadi mpaya za uanachama utafanyika tarehe 16.05.2014 kwenye hoteli ya Hyatt Kempsinki eneo la Posta (zamani Kilimanjaro Hotel) na mara baada ya uzinduzi moja kwa moja zoezi la kuhamisha wanachama kutoka kwenye mfumo wa analogy kwenda digital utaanza.

unamkumbuka Monica Lewinsky?



Mwanamke aliyawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na aliyekuwa Rais wa Marekani Bill Clinton na kusababisha Rais kupigiwa kura ya turufu ya kutaka kumwondoa mamlakani.

Wakati wa uhusiano huo Lewisnky alikuwa na umri wa miaka 20. Alikuja katika Ikulu ya White house kupata ujuzi wa kikazi.Lewinsky akiwa na umri wa miaka 40 sasa amevunja kimya chake.

Katika kusimulia yaliyotokea ndani ya Jarida la Vanity nchini Marekani, Lewinsky amesema anajuta sana kuwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Bwana Clinton.

Rais ''alinidhulumu,'' anasema Lewinsky ingawa amesema hakuna aliyemlazimisha kuwa na uhusiano na Clinton kwani wote wawili walikuwa wamekubaliana.Mnamo mwaka 1998, wanachama wa Republican walishindwa kumwondoa mamlakani Clinton kwa misingi kuwa alidanganya kuhusu uhusiano huo.

Swala la Lewisnky limeibuka tena hasa kwa sababu Bi Hillary Clinton anataka kuwania Urais mwaka 2016 na wanarepublican wanataka kulitumia swala hilo dhidi ya azma yake.Bi Lewinsky amesema anatumai kuliondoa madoa jina lake na kwamba anaelewa bado anatambulika sana katika sekta ya utumbuizaji nchini Marekani hususan katika vyombo vya habari na magazetini.

Lewinsky anasema Bwana Clinton alimdhulumu

Amesema katika jarida hilo kuwa:"mimi mwenyewe ninajuta sana kwa kilichotokea kati yangu na aliyekuwa Rais clinton.''

"acha nirejelee hilo, ninajutia sana kwa kilichotokea.''

Bi Lewinsky alipata masaibu punde baada ya taaifa ya uhusiano wake na Clinton kutokea mwaka 1998 , anasema alidharauliwa na kuchukiwa na pia alitumiwa kama kisingizio ili Rais wakati huo aweze kulindwa. ''

''Serikali ya Clinton , washirika wake na vyombo vya habari viliniona mimi kama adui mkubwa, na imesalia kuwa hivyo kwa sababu ya mamlaka iliyokuwepo''Tangu kuacha kazi hiyo, Be Lweinsky amekuwa aliwahi kutengeneza vibeti na kisha kuwa na kipindi cha kuwakutanisha wapenzi katika televisheni.

Bi Lewinsky anasema sababu kuu ya kuvunja kimya chake ni kutaka kijireshea hadhi yake na kuweka katika kaburi ya sahau yote yaliyotokea maishani mwake wakati huo."Labda kwa kuandika kisa changu, ninahisi kama ninaweza kuwasaidia wenzangu wanaopitia katika hali sawa na iliyonikumba hasa ya kudharauliwa,''.

MAHABUSU AVUA NGUO NA KUNG'ANG'ANIA BENDERA YA TAIFA


MAHABUSU wawili kati ya sita wanaotuhumiwa kwa kesi za mauaji,
wameleta kizaazaa baada ya kujaribu kutoroka na kukimbilia kwenye mlingoti wa Bendera ya Taifa nakuing'ang'ania kisha kuvua nguo na mmoja wao kubaki mtupu.

Tukio hilo limetokea leo majira ya saa 4:00 asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza, wakati mahabusu hao walipofikishwa kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi zao, lakini ghafla walipofika kwenye viwanja vya mahakama hiyo walitimua mbiyo kuelekea kwenye mlingoti wa Bendera hiyo ya Taifa na kuvua nguo.

Wananchi waliokuwa katika viwanja vya mahakamani hapo waliachwa midomo wazi na hali ya mshangao, mara baada ya mmoja kati ya hao wawili wakifanikiwa kuufikia mlingoti huo na kuvua nguo kisha kuanza kupiga kelele kwa kupaza sauti kudai haki itendeke.

Tukio hilo pia lilishuhudiwa na watumishi wa Mahakama ya Wilaya, Mahakama ya Mwanzo, Mamlaka ya Maji Safi na Majitaka ya jijini hapa (MWAUWASA), Askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), na taasisi zingine zilizo jirani na majengo ya mahakamani hapo na wananchi waliokuwa wakisubilia kesi zao kutajwa.

Mahabusu hao sita waliojaribu kutoroka na kuishia kudhibitiwa vyombo vya dola, walitajwa kwa majina kuwa ni Thobiasi Warioba (35), aliyeamua kuvua nguo zote na kubaki mtupu eneo la mlingoti wa Bendera ya Taifa, ambaye anakabiliwa na kesi ya mauaji Na. 32/2012.

Watuhumiwa wengine waliojaribu kutoroka ni Hamis Ramadani (30), Anthony Petro (35), Marwa Mwita (38), na Chacha Wangwe (35), na mwingine ambaye hakufahamika majina yake mara moja, wote wanakabiliwa na kesi ya Jinai Na. 215/2013  na walikamatwa tangu mwaka 2011.

Wakiwa katika viwanja vya mahakama hiyo baada ya kudhibitiwa na askari polisi, mmoja wa mahabusu hao walisikika wakisema: “Haiwezekani, tangu mwaka 2011 tulipokamatwa hadi sasa kesi zetu hazijasikilizwa. Wengine tumebambikiziwa kesi.  “Tunaomba haki zetu, polisi mnatuonea, vyombo vya habari tunaomba mtusaidie  tumekaa muda mrefu bila kusikilizwa na hatujui hatma yetu tangu 2011 tulipo kamatwa tumechoka kukaa mahabusu, tunaomba kesi zetu zisikilizwe”.

Baada ya malalamiko yao, ndipo askari  mmoja aliyejitambulisha kuwa ni Inspekta Henry akiwa na wenzake sita waliokuwa wakiwadhibiti wasikimbie na kuwahoji kuhusiana na madai yao, huku askari hao wakiwataka kuondoka katika mlingoti huo na kumtaka Warioba avae nguo ili waweze kuingia mahakamani.

“Pamoja na maamuzi yenu haya, lakini mtambue mnavunja sheria na hili ni kosa jingine la jinai, hivyo ni vema mkaondoka kwenye mlingoti huu na kuingia mahakamani. Malalamiko yenu tumeyasikia na yatashughulikiwa,” alisema Inspekta Henry.

Mmoja wa maofisa waandamizi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, ambaye alikataa kutajwa jina lake, alidai ushahidi wa kesi za watuhumiwa hao bado haujakamilika, na kwamba kesi zao haziwezi kusikilizwa na mahakama ya wilaya kwani haina uwezo na badala yake zitatajwa tu kisha kuhamishiwa Mahakama Kuu.

“Bado hiyo ni Criminal Case (kesi ya mauaji) au PI Case hivyo Mahakama Kuu haiwezi kuzungumzia hilo kwa sasa kwa kuwa utaratibu wa mahakama kuu ikisha kuwa tayari huitwa ‘Criminary Session Case’, ambapo sasa hupangiwa namba ya kesi na Jaji wa kuisikiliza,”  alisema.

Hizi ndiyo tabia za watu ambao hupandishwa vyeo . | Hisia za Mwananchi

Hizi ndiyo tabia za watu ambao hupandishwa vyeo . | Hisia za Mwananchi

Usain Bolt asaka viatu vyake

Mwanariadha Usain Bolt hana raha, anatafuta viatu vyake vilivyoibwa.
Mwanariadha huyo bingwa wa Olympic wa mbio fupi sasa ameeingia kwenye akaunti yake ya mtandao wake wa twitter ulio na zaidi ya mashabiki millioni 3 wanaomfuatilia, akisihi 'jamani najua si tumarafiiki.., aliyeonea viatu vyangu au aliyenavyo tafadhali uvirudishe'!
Viatu hivyo vya michezo rangi ya chungwa chapa cha Puma ,alivyowiweka saini yake vinagharimu pauni za Uingereza elfu ishirini.
Majajusi wa Scotland Yard wanasema viliibwa wiki iliyopia mtaa wa Craydon huko London maeneo ya viwandani vilipokuwa vimeekwa kama maonyesho.
Pia nao wanasihi atakaekuwa na fununu yoyote kuvihusu apige ripoti polisi.
Picha za viatu hivyo alivyovaa Usain alipotwaa ushindi zimezagaa mitandaoni, na sasa anaweka saini pair nyengine atakayoipelekea huko Uingereza.
Wadadisi wanasema itabidi ulinzi wa viatu hivyo uimarishwe zaidi.

Rished Bade ateuliwa kuwa Kamishna Mkuu Mpya TRA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana
Rished BADE kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Kulingana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, uteuzi huu umaanza tarehe 06 Mei,
2014. Bwana BADE anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bwana Harry KITILYA ambaye alistaafu
tarehe 14 Desemba,2013.
Kabla ya uteuzi huo, Bwana BADE alikuwa Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
tangu Septemba,2012 na baadaye kukaimu nafasi ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania tangu Bwana Kitilya alipostaafu.
Kabla ya kujiunga na Mamlaka ya Mapato Tanzania, Bwana Rished BADE amewahi kufanya kazi
katika maeneo mbalimbali yaliyompa ujuzi na weledi mkubwa kwenye mambo ya fedha na mapato
kama ifuatavyo:-
Oktoba, 1995 – Mei, 2000 – Mkaguzi wa Benki za Biashara, Benki Kuu ya Tanzania.
Juni, 2000 – Juni, 2001 – Credit Manager, Akiba Commercial Bank.
Juni, 2001 – Septemba,2001 – Chief Financial Officer, Akiba Banking Corporation.
Septemba, 2001 – Machi, 2006 – Chief Operating Oficer, Barclays Bank (Uganda).
Januari, 2007 – Desemba, 2009 – Chief Executive Officer, Barclays Bank (Tanzania)
Desemba, 2009 – 2012 – Chief Financial Officer, (East and West Africa Cluster) Barclays Bank
Plc Emerging Markets.
Novemba, 2010 – Septemba, 2012 – Chief Executive Officer, Tanzania Mortgage Refinance
Company.
Bwana Rished BADE ana Shahada ya Kwanza ya Bachelor of Commerce and Management ya Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam (1995); Shahada ya Master of Commerce in Banking and Finance ya Chuo
Kikuu cha Sydney (1999), na ni Certified Public Accountant (CPA).
Katika kumteua kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Mheshimiwa Rais anaimani kubwa kwa elimu, uzoefu na weledi alionao, Bwana Rished Bade kwa kushirikiana nawatumishi wenzake, atatoa mchango mkubwa kwa Taifa kwa kuzidi kuimarisha Mamlaka hiyo na
kuboresha utendaji wake na hivyo kuongeza mapato ya Serikali kwa faida ya Taifa.
Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu - Dar es Salaam.

Tuesday, 6 May 2014

Aina 10 za wanaume wa kuepuka kuwa na mahusiano nao hawa hapa…!


5. Mwanaume anayependa kutukuzwa kama mfalme:

Unaweza kukutana na mwanaume aliyejipachika kibandiko ufalme ambaye anapenda sana kuhudumiwa kama mfalme. Yaani anataka afanyiwe kila kitu, na hajishughulishi kukusaidia kazi hata zile zinazotakiwa zifanywe na mwanaume, yeye kazi yake ni kukaa sebuleni na kuangalia TV au kusoma vitabu au magazeti huku akiagiza kila kitu asogezewe miguuni. Hawezi hata kunyanyuka kufuata kitu anachotaka na badala yake ni kuamrisha aletewe. Mwanaume wa aina hii ni wa kuepukwa kwani mwanamke kukubali kuwa na uhusiano na mwanaume mwenye tabia za kupenda kutukuzwa kama mfalme ni kutaka kuishi kwa msongo wa mawazo na jakamoyo na hivyo kufupisha umri wako wa kuishi hapa duniani. Kinga ni bora kuliko tiba, ukikutana na mwanaume wa aina hii chapa lapa hakufai..



6. Mwanaume mwenye utititri wa watoto kila kona:
Mwanaume kuwa na watoto nje ya ndoa si jambo la kushangaza siku hizi, lakini pale unapokutana na mvulana mwenye umri wa miaka 25 lakini ana watoto watatu kwa mama tofauti, mh! hapo sikushauri ujiingize kwenye uhusiano na mwanaume huyo. Hata hivyo si lazima awe na miaka 25 tu hata mwanaume mwenye umri mkubwa zaidi ya huo halafu ana watoto watatu au hata wanne au zaidi kutoka kwa mama tofauti ni wa kuepuka. Hivi atakupa sababu gani zilizomfanya akawa na watoto kwa mama tofauti kila kona ya mtaa mpaka umuelewe! Kuwa na mahusiano na mwanaume aina hiyo ni kukaribisha shari nyumbani kwako maana kila siku utapata wageni wanaokuja kudai hela za matumizi kutoka kwa mumeo tena wengine watakuja kishari hasa na kukuharibia siku. Mh mh! sikushauri mwanamke, sepa zako, bado nafasi unayo ya kumpata mwanaume mwingine mwadilifu.



7. Mwanaume anayejipenda mwenyewe:

Mwanaume anayejipenda mwenyewe ni kizungumkuti kingine ambacho wanawake wanapaswa kujiepusha nacho. Utakuta mwanaume anajipenda mwenyewe hakuna anachojali kuhusu mwenzi wake zaidi ya kujijali yeye mwenyewe. Wanaume wenye tabia hii ya kujipenda wenyewe, huwa wana kawaida ya kujijali wao wenyewe. Wanataka wavae nguo nzuri za thamani ili wao wapendeze na si wenzi wao. Swala la kumjali mwenzi wake halipo katika vichwa vya wanaume wa aina hii kabisa. Mwanamke sikushauri uingie katika moto huu.



8.Mwanaume bahili:
Unakutana na mwanaume mtoko wa kwanza tu anakuchagulia aina ya chakula au kinywaji kwa kuangalia bei rahisi na wakati wa kulipa anahesabia hela yake mfukoni, huyo ni janga. Utakapoingia katika uhusiano na mwanaume wa aina hii atakusumbua sana na pia katika kupanga bajeti nyumbani usishangae akihesabu finyango za nyama au vipande vya samaki jikoni. Sikushauri mwanamke, we ingia mitini hakufai huyo........



9.Mwanaume chapombe mlevi kupindukia:
Hakuna ubaya mtu kunywa pombe, hasa kama unajua kiwango chako cha unywaji, lakini kuwa na uhusiano na mwanaume mlevi anayekunywa pombe kupindukia kila siku non stop 24/7 huyo hafai. Mwanaume wa aina hii ndio wale wanaosema kunywa pombe watoto wakitembea uchi atajua mama yao. Hata siku moja hawezi kuzungumzia maendeleo kwa ustawi wa familia, kwake utakuwa ni msamiati mgumu.



10. Mwanaume mwenye kisirani na asiyeweza kumuuwa nyoka akafa :

Mwanaume mwenye kisirani ni ngumu sana kuishi naye. Mwanaume mwenye kisirani na anayependa kuweka vitu rohoni na asiyeweza kusamehe ni janga. kuishi na mwanaume wa aina hii ni sawa na kuishi na explosive material ambayo yakipata joto tu hulipuka. Mwanaume umetoka naye mtoko wa kwanza na kwa bahati mbaya mhudumu wa mghahawa akasau kitu katika vitu mlivyoagiza akagomba kupita kiasi na kuwakusanya mameneja wote wa mghahawa akiwemo mpishi mkuu akilalamika. Na kama hiyo haitoshi mtaondoka hapo mghahawani njia nzima kambeba kichwani mhudumu yule masikini aliyeghafilika mpaka mwisho wa safari yenu na huenda akalala naye kichwani. Mwanaume huyo hafai kama gome la mgomba lisilofaa kwa dawa ya miti shamba wala kuni, labda kwa kufungia ugoro. Huyo mpishe ajiendee zake hakufai......



1. Mwanaume Kicheche:
Hakuna mwanamke anayependa kuchezewa na wanaume, labda tu kama anafanya hivyo katika juhudi zake za kujikwamua kiuchumi, lakini pale mwanamke anapokuwa katika harakati za kutafuta mwanaume ambaye kama mambo yakiwa mazuri wafunge ndoa, ni vyema akajiepusha na wanaume vicheche wanaotongoza wanawake kwa lengo la kustarehe na kumaliza matamanio yao ya ngono. wakati mwingine mwanaume mwenye tabia ya kuchezea wanawake anaweza kumfuata mwanamke ambaye ametamani mwili wake na kujifanya eti amebadilika na kuwa mtakatifu. Anaweza kujiweka katika mazingira yanayoonyesha kwamba amebadilika ili kumvuta mwanamke. Shituka mwanamke, jasiri haachi asili atakutumia kama condom na kisha kukutupilia mbali. Wanaume wenye tabia hizo ni vigumu kubadilika. Inahitaji subira ya hali ya juu kujiridhisha kama kweli amebadilika au anazuga ili apate anachokitaka.



2. Mwanaume asiye na kazi na asiyejishughulisha:

Mwaume asiye na kazi na asiyejishughulisha ni mzigo usio na mwenyewe. Mwanaume asiyejishughulisha eti kwa sababu hajapata kazi huyo hana malengo. Kukubali kuwa na uhusiano na mwnaaume wa aina hiyo ni sawa na kuishi na mtu mfu anayetembea (dead alive), labda tu kama atakupa sababu inayoingia akilini kuhusu kutokuwa kwake na kazi na kutojishughulisha kwake. Kama atakuwa ni mtu wa kulalamika tu kwamba hakuna ajira na haonyeshi dalili zozote za kuhangaika kutafuta hata vibarua ili kujikimu eti kwa sababu ni msomi na badala yake anageuka kuwa ombaomba kwa ndugu zake na marafiki zake Nawashauri wanawake muwaepuke wanaume wa aina hii kwani hawafai wanataka kulelewa. Kama amekuona unafanya kazi au una vibishara vyako vinavyokuingizia shilingi mbili tatu zinazokufanya uishi vizuri hapa mjini jua kwamba hicho ndicho kilichomvuta kwako, ukikubali umekwisha maana atakukamua hadi tone la mwisho kisha ahamie kwa mwingine, si kilichomleta kwako hakipo, sasa awe na wewe kwa lipi....



3. Mwanaume asiyejiamini:
Kukubali kuwa na mahusiano na mwanaume asiyejiamini ni sawa na kuishi na bomu ndani ya nyumba. Mwanaume asiyejihisi kuwa yuko salama na mwenye mashaka muda mwingi kuhusu uhusiano wenu, hutawaliwa na wivu wa ajabu ambao licha ya kukuletea fedheha kwa ndugu, jamaa na marafiki zako, lakini pia anaweza kukudhuru au hata kukutoa roho siku moja. Wanaume wasiojiamini mara nyingi ni watu wa kujitilia mashaka kuhusu hali zao za kipato na uwezo wao katika tendo. Kuwa na mahusiano na mwanaume asiejiamini inabidi uishi kwa akili na uchague maneno ya kuzungumza kila uwapo naye, kwani kila neno utakalotamka litatafutiwa tafsiri na kitakachofuata ni tafrani, sasa tabu yote ya nini..... Tupa kule hafai kwa mchuzi wala kwa kulumangia...



4.Mtoto wa mama:

Inawezekana mwanaume akalazimika kuishi nyumbani kwao kwa muda baada ya kumaliza masomo au amepoteza ajira na akawa bado hajapata ajira au hajapata shughuli ya maana itakayomwezesha kujitegemea, hii inakubalika. Hata hivyo kama mwanamke anakutana na mwanaume ambaye anaishi na wazazi wake na haonyeshi dalili za kutafuta kazi au shughuli yenye kipato itakayomwezesha kuondoka hapo kwao na kujitegemea, usije ukajiingiza katika uhusiano na mwanaume wa aina hiyo, itakula kwako, huyo ashakuwa kupe na tegemezi, utakuwa ni mzigo wako na atakuganda kama luba na kupoteza bahati ya kukutana na wanaume wenye mwelekeo wa maisha.





Monday, 5 May 2014

KAMA ULIKOSA HII NDIO LIST YA WASHINDI WA TUZO ZA KILIMANJARO TANZANIA MUSIC AWARDS (KTMA).


1. WIMBO BORA WENYE VIONJO VYA ASILI YA TANZANIA - Bora Mchawi, Dar Bongo Massive
2. MSANII BORA CHIPUKIZI ANAYEIBUKA - Young Killer
3. WIMBO BORA WA ZOUK - Yahaya, Lady Jaydee
4. WIMBO BORA WA AFRO POP - Number One, Diamond Platnumz
5. WIMBO BORA WA RAGGA / DANCEHALL - Nishai Chibwa Ft Juru
6. WIMBO BORA WA RAGGAE - Niwe na wewe, Dabo
7.WIMBO BORA WA TAARAB - Wasiwasi wako, Mzee Yusuf
8. KIKUNDI CHA MWAKA CHA TAARAB - Jahazi Modern Taarab
9. MWIMBAJI BORA WA KIKE TAARAB - Isha Ramadhani
10. MWIMBAJI BORA WA KIUME TAARAB - Mzee Yusuf
11. WIMBO BORA WA KISWAHILI BENDI - Ushamba mzigo, Mashujaa Band
12. MWIMBAJI BORA WA KIKE BENDI - Luiza Mbutu
13. MWIMBAJI BORA WA KIUME BENDI - Jose Mara
14. RAPA BORA WA MWAKA BENDI - Furguson
15. BENDI YA MWAKA - Mashujaa Band
16. MWIMBAJI BORA WA KIKE, KIZAZI KIPYA - Lady Jaydee
17. MWIMBAJI BORA WA KIUME, KIZAZI KIPYA - Diamond
18. KIKUNDI CHA MWAKA CHA KIZAZI KIPYA - Weusi
19. WIMBO BORA WA RNB - Closer, Vanessa Mdee
20. WIMBO BORA WA HIP HOP - Nje ya Box, Nick wa Pili Ft Joh Makini & Gnako
21. MSANII BORA WA HIP HOP - Fid Q
22. WIMBO BORA WA KUSHIRIKISHA / KUSHIRIKIANA - Muziki Gani, Nay wa Mitego ft Diamond
23. WIMBO BORA WA AFRIKA MASHARIKI - Tubonge, Jose Chameleone
24. MTUNZI BORA WA MWAKA TAARAB - Mzee Yusuf
25. MTUNZI BORA WA MWAKA BENDI - Christian Bella
26. MTUNZI BORA WA MWAKA KIZAZI KIPYA - Diamond
27. MTUNZI BORA WA MWAKA HIP HOP - Fid Q
28. MTAYARISHAJI BORA WA NYIMBO WA MWAKA, TAARAB - Enrico
29. MTAYARISHAJI BORA WA NYIMBO WA MWAKA, BENDI - Amoroso
30. MTAYARISHAJI BORA WA NYIMBO WA MWAKA, KIZAZI KIPYA - Man Water, CombinationSound
31. HALL OF FAME, INDIVIDUAL - Hassan BItchuka
32. HALL OF FAME, INSTITUTION - Masoud Masoud
33. VIDEO BORA YA MUZIKI YA MWAKA - Number One, Diamond
34.WIMBO WA MWAKA - Number One. Diamond
35. MTUMBUIZAJI BORA WA KIKE WA MUZIKI - Isha Ramadhani
36. MTUMBUIZAJI BORA WA KIUME WA MUZIKI - Diamond


Friday, 2 May 2014

Kuelekea kombe la Dunia Makahaba kufanyiwa malipo ya ngono benki.



DUNIA imeshavua nguo na sasa kilichobaki ni ufirauni. Atakayekwenda kushuhudia fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil atakumbana na mabadiliko makubwa ya maisha ya kidunia nchini humo.
Wanawake malaya nchini humo wamekubaliana na benki za nchini humo kupata malipo kutoka kwa wateja wao kupitia kadi maalumu za malipo za wateja hao, Credit Card. Wamepewa mashine maalumu za kuwatoza wateja wao ambao hawana fedha mfukoni lakini wanazo katika kadi zao za benki.

Wanawake katika mji wa Belo Horizonte uliopo maili 270 kutoka katika Mji Mkuu wa Brazil, Rio de Janeiro wamefurahishwa na kaulimbiu ya mtindo huo wa malipo ambao umepachikwa jina la “Furahia sasa, lipia baadaye”.

Cida Vieira, malaya wa kundi la makahaba linalofahamika kama Aprosmig, ambaye pia ni Rais wa Chama cha Malaya katika jimbo la Minas Gerais alidai kwamba kwa sasa hakutakuwa na kukabana koo dhidi ya wateja ambao hawana pesa mifukoni lakini wanazo katika akaunti zao.

“Wateja wanaotaka kuendelea na starehe zao lakini hawana pesa taslimu mifukoni, wanaweza kuendelea kula raha bila ya kuingiliwa,” alisema Cida ambaye ni malaya maarufu wa maeneo hayo.

Kwa mujibu wa kundi hilo, wamedai kwamba malipo ya kupitia kadi yanaleta usalama kwa mteja na vilevile taarifa za matumizi ya mteja hazitaeleza sababu hasa za matumizi yake katika pesa zilizotoka kwenda kwa malaya.

Wajifunza Kiingereza

Wakati michuano hiyo ikiwa imebakisha siku chache kuanza huku ligi mbalimbali barani Ulaya zikiwa zinafikia ukingoni, baadhi ya malaya wameanza kujifunza lugha ya Kiingereza kwa ajili ya kunasa wateja ambao hawafahamu lugha ya Kireno.

Tangu mwaka jana, malaya hao wa Brazil wamekuwa wakijiunga katika madarasa mbalimbali ya Kiingereza nchini humo kwa ajili ya kujifunza lugha hiyo ambayo itawarahisishia majadiliano na wateja wao wanaotumia lugha ya Kiingereza.

“Hii ni muhimu kwa heshima ya ya kazi hii. Wanawake wanapaswa kujadiliana bei na mteja na kujitetea wenyewe,” aliongeza Cida. Umalaya umehalalishwa nchini Brazil na wanawake nchini humo wanatazamia mapato makubwa wakati wa Kombe la Dunia.

Kundi hilo la malaya pia linatazamia kujifunza lugha mbalimbali wakiwa darasani kama vile Kihispaniola, Kiitaliano, Kifaransa na hata Kireno kwa malaya ambao wamezamia nchini humo, lakini hawaifahamu lugha hiyo inayotumiwa zaidi na Wabrazili.
Mpaka Juni mwaka jana, Vieira anadai malaya 20 walikuwa wamejiunga katika madarasa hayo, lakini alikuwa anatazamia kuwa malaya wengine 300 wangejiunga katika kundi lao lenye malaya 4,000.

Waingereza waonywa na polisi wao

Polisi nchini Uingereza imewaonya mashabiki wa soka nchini humo kuwa Polisi wa Brazil wanawasubiri kwa hamu mashabiki ambao watafanya ngono na watoto wadogo nchini humo kwa ajili ya kuwapeleka jela.

Mashabiki hao wa England wameambiwa kuwa watazamie vifungo vya gerezani nchini Brazil au Uingereza kwa kufanya ngono na watoto wadogo ambao wamekuwa tatizo kubwa katika nchi hiyo ya Amerika Kusini.

Ripoti kutoka Brazil zinadai kuwa watoto wenye umri mdogo hata wa kufikia miaka 11 huwa wanavaa nguo ambazo zinawafanya waonekane wakubwa kwa ajili ya kufanya biashara ya ngono. Ni marufuku nchini humo kulipia huduma ya ngono kwa msichana mwenye umri chini ya miaka 17.

Michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu, pamoja na ile ya Olimpiki miaka miwili ijayo inatazamiwa kufichua kwa kiasi kikubwa tatizo hili na polisi pamoja na vyombo vya dola nchini humo vimejipanga kuchukua hatua madhubuti.

Brazil inashika nafasi ya pili nyuma ya Thailand kwa biashara ya ngono kwa watoto.

“Watoto wa Brazil wanaweza kuathirika kwa kiasi kikubwa na biashara ya ngono na wanaweza kujibadilisha hili waonekane wakubwa kuliko umri wao halisi,” alisema Johnny Gwynne, ambaye ni mkubwa kitengo cha kuzuia masuala hayo.

Uhalifu wa ngono unatajwa kuwa wa pili kwa ukubwa nchini humo huku waathirika wakubwa wakiwa watoto wenye umri kati ya miaka 10 hadi 14. Zaidi ya wageni 600,000 wanatazamiwa kuhudhuria fainali za Kombe la Dunia nchini humo ambalo linatazamiwa kuanza Juni 12.


Mwananchi.

VIDEO: WEUSI--GERE (Official Video) - BongoSwaggz.Com | Udaku,Mapenzi,Burudani n.k

VIDEO: WEUSI--GERE (Official Video) - BongoSwaggz.Com | Udaku,Mapenzi,Burudani n.k

Magazeti ya leo May 02 2014 Udaku, Michezo na Hardnews


.


.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.