Monday 12 May 2014

RAIS KIKWETE ALIPOKUTANA NA WANASOKA WA TANZANIA SAMMATA NA ULIMWENGU WANAOCHEZEA TP MAZEMBE.

Wachezaji wawili wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Alli Samatta na Thomas Ulimwengu ambao wanachezea klabu ya TP Mazembe ya Congo hii leo walipata faraja kubwa ya kutembelewa na mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho kikwete.
Rais Kikwete ambaye yuko katika ziara kubwa nchini Kongo alipata fursa ya kubadilishana mawazo na wanandinga hao majira ya 06.15 mchana ambao wanachezea katika klabu ya bilionea Musa Kitumbi.Rais aliwasili Kinshasa tangu Ijumaa usiku kwa ajili ya ziara rasmi ya masaa 24 katika muktadha wa ushirikiano kati ya DRC na Tanzania ikiwa ni mwaliko wa Rais Kabila na akafanikiwa kukutana na wachezaji hao.Mazungumzo ya Rais Kikwete na wachezaji hao yalichukua takribani robo saa katika Hoteli moja maarufu iitwayo Congo River ambapo aliwatakia kila la kheri wachezaji wake katika mechi ya Jumapili na kuwatakia mafanikio katika kazi yao hiyo ya soka.

Rais Jakaya Kikwete aliwakumbusha Samatta na Ulimwengu kuwa taifa zima linajiona fahari kuwaona wakiwa katika jezi za rangi ya TP Mazembe na Taifa Stars.
Hiyo ni ishara kuwa Rais anawatambua na kuthamini washambuliaji Samatta Mbwana na Thomas Ulimwengu ambao daima wanajitoa katika kila hali bila kujali Jersey.

No comments:

Post a Comment