Friday 2 May 2014

Kuelekea kombe la Dunia Makahaba kufanyiwa malipo ya ngono benki.



DUNIA imeshavua nguo na sasa kilichobaki ni ufirauni. Atakayekwenda kushuhudia fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil atakumbana na mabadiliko makubwa ya maisha ya kidunia nchini humo.
Wanawake malaya nchini humo wamekubaliana na benki za nchini humo kupata malipo kutoka kwa wateja wao kupitia kadi maalumu za malipo za wateja hao, Credit Card. Wamepewa mashine maalumu za kuwatoza wateja wao ambao hawana fedha mfukoni lakini wanazo katika kadi zao za benki.

Wanawake katika mji wa Belo Horizonte uliopo maili 270 kutoka katika Mji Mkuu wa Brazil, Rio de Janeiro wamefurahishwa na kaulimbiu ya mtindo huo wa malipo ambao umepachikwa jina la “Furahia sasa, lipia baadaye”.

Cida Vieira, malaya wa kundi la makahaba linalofahamika kama Aprosmig, ambaye pia ni Rais wa Chama cha Malaya katika jimbo la Minas Gerais alidai kwamba kwa sasa hakutakuwa na kukabana koo dhidi ya wateja ambao hawana pesa mifukoni lakini wanazo katika akaunti zao.

“Wateja wanaotaka kuendelea na starehe zao lakini hawana pesa taslimu mifukoni, wanaweza kuendelea kula raha bila ya kuingiliwa,” alisema Cida ambaye ni malaya maarufu wa maeneo hayo.

Kwa mujibu wa kundi hilo, wamedai kwamba malipo ya kupitia kadi yanaleta usalama kwa mteja na vilevile taarifa za matumizi ya mteja hazitaeleza sababu hasa za matumizi yake katika pesa zilizotoka kwenda kwa malaya.

Wajifunza Kiingereza

Wakati michuano hiyo ikiwa imebakisha siku chache kuanza huku ligi mbalimbali barani Ulaya zikiwa zinafikia ukingoni, baadhi ya malaya wameanza kujifunza lugha ya Kiingereza kwa ajili ya kunasa wateja ambao hawafahamu lugha ya Kireno.

Tangu mwaka jana, malaya hao wa Brazil wamekuwa wakijiunga katika madarasa mbalimbali ya Kiingereza nchini humo kwa ajili ya kujifunza lugha hiyo ambayo itawarahisishia majadiliano na wateja wao wanaotumia lugha ya Kiingereza.

“Hii ni muhimu kwa heshima ya ya kazi hii. Wanawake wanapaswa kujadiliana bei na mteja na kujitetea wenyewe,” aliongeza Cida. Umalaya umehalalishwa nchini Brazil na wanawake nchini humo wanatazamia mapato makubwa wakati wa Kombe la Dunia.

Kundi hilo la malaya pia linatazamia kujifunza lugha mbalimbali wakiwa darasani kama vile Kihispaniola, Kiitaliano, Kifaransa na hata Kireno kwa malaya ambao wamezamia nchini humo, lakini hawaifahamu lugha hiyo inayotumiwa zaidi na Wabrazili.
Mpaka Juni mwaka jana, Vieira anadai malaya 20 walikuwa wamejiunga katika madarasa hayo, lakini alikuwa anatazamia kuwa malaya wengine 300 wangejiunga katika kundi lao lenye malaya 4,000.

Waingereza waonywa na polisi wao

Polisi nchini Uingereza imewaonya mashabiki wa soka nchini humo kuwa Polisi wa Brazil wanawasubiri kwa hamu mashabiki ambao watafanya ngono na watoto wadogo nchini humo kwa ajili ya kuwapeleka jela.

Mashabiki hao wa England wameambiwa kuwa watazamie vifungo vya gerezani nchini Brazil au Uingereza kwa kufanya ngono na watoto wadogo ambao wamekuwa tatizo kubwa katika nchi hiyo ya Amerika Kusini.

Ripoti kutoka Brazil zinadai kuwa watoto wenye umri mdogo hata wa kufikia miaka 11 huwa wanavaa nguo ambazo zinawafanya waonekane wakubwa kwa ajili ya kufanya biashara ya ngono. Ni marufuku nchini humo kulipia huduma ya ngono kwa msichana mwenye umri chini ya miaka 17.

Michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu, pamoja na ile ya Olimpiki miaka miwili ijayo inatazamiwa kufichua kwa kiasi kikubwa tatizo hili na polisi pamoja na vyombo vya dola nchini humo vimejipanga kuchukua hatua madhubuti.

Brazil inashika nafasi ya pili nyuma ya Thailand kwa biashara ya ngono kwa watoto.

“Watoto wa Brazil wanaweza kuathirika kwa kiasi kikubwa na biashara ya ngono na wanaweza kujibadilisha hili waonekane wakubwa kuliko umri wao halisi,” alisema Johnny Gwynne, ambaye ni mkubwa kitengo cha kuzuia masuala hayo.

Uhalifu wa ngono unatajwa kuwa wa pili kwa ukubwa nchini humo huku waathirika wakubwa wakiwa watoto wenye umri kati ya miaka 10 hadi 14. Zaidi ya wageni 600,000 wanatazamiwa kuhudhuria fainali za Kombe la Dunia nchini humo ambalo linatazamiwa kuanza Juni 12.


Mwananchi.

No comments:

Post a Comment