Thursday 8 May 2014

unamkumbuka Monica Lewinsky?



Mwanamke aliyawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na aliyekuwa Rais wa Marekani Bill Clinton na kusababisha Rais kupigiwa kura ya turufu ya kutaka kumwondoa mamlakani.

Wakati wa uhusiano huo Lewisnky alikuwa na umri wa miaka 20. Alikuja katika Ikulu ya White house kupata ujuzi wa kikazi.Lewinsky akiwa na umri wa miaka 40 sasa amevunja kimya chake.

Katika kusimulia yaliyotokea ndani ya Jarida la Vanity nchini Marekani, Lewinsky amesema anajuta sana kuwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Bwana Clinton.

Rais ''alinidhulumu,'' anasema Lewinsky ingawa amesema hakuna aliyemlazimisha kuwa na uhusiano na Clinton kwani wote wawili walikuwa wamekubaliana.Mnamo mwaka 1998, wanachama wa Republican walishindwa kumwondoa mamlakani Clinton kwa misingi kuwa alidanganya kuhusu uhusiano huo.

Swala la Lewisnky limeibuka tena hasa kwa sababu Bi Hillary Clinton anataka kuwania Urais mwaka 2016 na wanarepublican wanataka kulitumia swala hilo dhidi ya azma yake.Bi Lewinsky amesema anatumai kuliondoa madoa jina lake na kwamba anaelewa bado anatambulika sana katika sekta ya utumbuizaji nchini Marekani hususan katika vyombo vya habari na magazetini.

Lewinsky anasema Bwana Clinton alimdhulumu

Amesema katika jarida hilo kuwa:"mimi mwenyewe ninajuta sana kwa kilichotokea kati yangu na aliyekuwa Rais clinton.''

"acha nirejelee hilo, ninajutia sana kwa kilichotokea.''

Bi Lewinsky alipata masaibu punde baada ya taaifa ya uhusiano wake na Clinton kutokea mwaka 1998 , anasema alidharauliwa na kuchukiwa na pia alitumiwa kama kisingizio ili Rais wakati huo aweze kulindwa. ''

''Serikali ya Clinton , washirika wake na vyombo vya habari viliniona mimi kama adui mkubwa, na imesalia kuwa hivyo kwa sababu ya mamlaka iliyokuwepo''Tangu kuacha kazi hiyo, Be Lweinsky amekuwa aliwahi kutengeneza vibeti na kisha kuwa na kipindi cha kuwakutanisha wapenzi katika televisheni.

Bi Lewinsky anasema sababu kuu ya kuvunja kimya chake ni kutaka kijireshea hadhi yake na kuweka katika kaburi ya sahau yote yaliyotokea maishani mwake wakati huo."Labda kwa kuandika kisa changu, ninahisi kama ninaweza kuwasaidia wenzangu wanaopitia katika hali sawa na iliyonikumba hasa ya kudharauliwa,''.

No comments:

Post a Comment