Thursday, 8 May 2014

Rished Bade ateuliwa kuwa Kamishna Mkuu Mpya TRA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana
Rished BADE kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Kulingana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, uteuzi huu umaanza tarehe 06 Mei,
2014. Bwana BADE anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bwana Harry KITILYA ambaye alistaafu
tarehe 14 Desemba,2013.
Kabla ya uteuzi huo, Bwana BADE alikuwa Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
tangu Septemba,2012 na baadaye kukaimu nafasi ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania tangu Bwana Kitilya alipostaafu.
Kabla ya kujiunga na Mamlaka ya Mapato Tanzania, Bwana Rished BADE amewahi kufanya kazi
katika maeneo mbalimbali yaliyompa ujuzi na weledi mkubwa kwenye mambo ya fedha na mapato
kama ifuatavyo:-
Oktoba, 1995 – Mei, 2000 – Mkaguzi wa Benki za Biashara, Benki Kuu ya Tanzania.
Juni, 2000 – Juni, 2001 – Credit Manager, Akiba Commercial Bank.
Juni, 2001 – Septemba,2001 – Chief Financial Officer, Akiba Banking Corporation.
Septemba, 2001 – Machi, 2006 – Chief Operating Oficer, Barclays Bank (Uganda).
Januari, 2007 – Desemba, 2009 – Chief Executive Officer, Barclays Bank (Tanzania)
Desemba, 2009 – 2012 – Chief Financial Officer, (East and West Africa Cluster) Barclays Bank
Plc Emerging Markets.
Novemba, 2010 – Septemba, 2012 – Chief Executive Officer, Tanzania Mortgage Refinance
Company.
Bwana Rished BADE ana Shahada ya Kwanza ya Bachelor of Commerce and Management ya Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam (1995); Shahada ya Master of Commerce in Banking and Finance ya Chuo
Kikuu cha Sydney (1999), na ni Certified Public Accountant (CPA).
Katika kumteua kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Mheshimiwa Rais anaimani kubwa kwa elimu, uzoefu na weledi alionao, Bwana Rished Bade kwa kushirikiana nawatumishi wenzake, atatoa mchango mkubwa kwa Taifa kwa kuzidi kuimarisha Mamlaka hiyo na
kuboresha utendaji wake na hivyo kuongeza mapato ya Serikali kwa faida ya Taifa.
Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu - Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment